Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi...

175
Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana www.africanpastors.org Na Dorothy Almond mwisho na Askofu Francis Ntiruka

Transcript of Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi...

Page 1: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

Ufafanuzi WaAgano Jipya

Yohana

www.africanpastors.org

Na Dorothy Almondmwisho na Askofu Francis Ntiruka

Page 2: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

Kimetolewa na:AFRICAN PASTORS FELLOWSHIP

Station House, Station Approach, AdishamCanterbury, Kent CT3 3JE

United Kingdom

www.africanpastors.org

Ufafanuzi WaAgano Jipya

YohanaDorothy Almond

© African Pastors Fellowship 2010

Page 3: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

DIBAJIAliyeandika kitabu hiki cha ufafanuzi ni Sista Dorothy Almond aliyeishiTanzania kwa miaka 31, na sasa yu Uingereza hali amestaafu. Alikuwamwalimu katika Chuo cha Theologia, Kongwa kwa miaka 16 na katika Shuleya Biblia, Morogoro kwa miaka 6 na katika Shule ya Biblia, Msalato kwamiaka 4.

Mchoraji ni Peter Kasamba. Yeye ni Mwuganda anayeishi huko Kampala.Kwa muda mrefu amechora picha zote kwa vitabu vya APF. Anaongoza piaKwaya ya AYF.

Kitabu hiki chatolewa kwa msaada wa African Pastors Fellowship. Lengo nikuwasaidia watumishi wa Kanisa wanaosoma katika Shule za Biblia naMasomo ya Nyumbani

Page 4: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

.

RAMANI YA PALASTINA WAKATI WA KRISTO

Page 5: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA494

INJILI YA YOHANA

YALIYOMO

UTANGULIZI1. Mwandishi2. Walioandikiwa3. Mahali ilipoandikwa Injili4. Tarehe ya kuandika5. Shabaha ya kuandika6. Mtindo wa Injili7. Tofauti kati yake na Injili tatu zinazowiana

UFAFANUZI1: 1-18 YESU KRISTO - ASILI YAKE na NAFSI YAKE

1: 1-2 Uhusiano wa Neno na Mungu3 Uhusiano wa Neno na Uumbaji4-5, 9 Uhusiano wa Neno na Uzima na Nuru6-8 Uhusiano wa Neno na Yohana Mbatizaji10-13 Uhusiano wa Neno na Ulimwengu na Wanadamu14 Neno alifanyika Mwili15-18 Neno ni bora, amfunua Baba kwa ukamilifu

1:19 - 4:54 MUDA WA WATU KUMFIKIRIA

1: 19-34 Ushuhuda wa Yohana Mbatizaji35-51 Wanafunzi wa Mbatizaji kuelekezwa kwa Kristo

2: 1-12 Arusi huko Kana ya Galilaya13-25 Yesu alitokea kwa mara ya kwanza huko

Yerusalemu na kulitakasa hekalu3: 1-21 Mazungumzo ya Yesu na Nikodemo

22-30 Yohana Mbatizaji amshuhudia Yesu4: 1-42 Yesu azungumza na Mwanamke Msamaria

43-54 Yesu amponya mwana wa diwani

5:1 - 6:7 MUDA WA MABISHANO

5: 1-18 Kumponya kiwete penye birika ya Bethzatha19-29 Madai ya Yesu kuhusu uhusiano wake na Baba30-47 Ushuhuda mbalimbali juu ya Yesu Kristo

Page 6: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA495

6: 1-14 Yesu kuwalisha watu elfu tano15-21 Yesu atembea juu ya maji22-25 Mkutano wamtafuta Yesu26-71 Mazungumzo juu ya Chakula cha Uzima

7:1 - 11:53 MUDA WA MIGONGANO

7: 1- 2 Yaliyotokea kabla ya kuhudhuria Sikukuu3- 9 Kutokuamini kwa ndugu zake10-13 Mkanganyiko wa watu14-19

na 21-24na 33-34 Yesu alijidhihirisha wazi20, 25-32na 35-36 Maitikio ya watu mbalimbali

37-52 Wito maalum wa kumjia7: 53-8: 11 Mwanamke aliyefumaniwa katika kuzini 8: 12-30 Kuwakabili Mafarisayo na kuhojiana nao

31-59 Mazungumzo na Wayahudi waliomwamini9: 1-41 Kumponya mtu aliyezaliwa kipofu10: 1-21 Yesu Mchungaji Mwema

22-42 Mabishano yaliyotokea katika Tao la Sulemani11: 1-53 Yesu alimfufua Lazaro

11:54 - 12:36 UPEO WA MGOGORO

11: 54-57 Yesu alijitenga na kwenda Efraimu12: 1-11 Yesu alirudi mpaka Bethania

12-19 Yesu aliingia Yerusalemu kwa shangwe20-36 Wayunani walitaka kumwona Yesu

12:37 - 17:26 MUDA WA MAONGEZI

12: 37-43 Majumlisho ya huduma ya Yesu kati ya watu44-50 Muhtasari wa Mafundisho ya Yesu

13:1 - 16:33 MAONGEZI NA WANAFUNZI

13: 1-20 Chakula cha mwisho21-30 Kuagana na Msaliti

13: 31-38 Amri mpya14: 1-14 „Mwisho‟ wa waumini

15-31 Kuondoka kwa Yesu na Kuja kwa Roho Mtakatifu15: 1-27 Maongezi juu ya uhusiano wao na Yeye Mzabibu wa kweli

Page 7: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA496

16: 1-33 Maongezi juu ya shida watakazozipata na Huduma ya RohoMtakatifu

17: 1-26 Maongezi ya Yesu na Baba yake

18:1 - 21:25 MUDA WA MATIMIZO

18: 1-11 Kusalitiwa na kukamatwa12-27 Kuhukumiwa na Anasi na Petro kumkana28-40 Kuhojiwa na Pilato

19: 1-16 Pilato alitoa hukumu Yesu afe17-37 Kusulibishwa kwa Bwana Yesu38-42 Kuzikwa kwa Bwana Yesu

20: 1-20 Kufufuka kwa Bwana Yesu21: 1-23 Mambo ya mwisho kuhusu Utume wa Wanafunzi

24-25 Yohana afunga Injili yake

Page 8: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA497

UTANGULIZI(a) MwandishiWataalamu wametoa mawazo mbalimbali. Wengi hufikiri kwamba Injili hiiiliandikwa na Mtume Yohana, Mwana wa Zebedayo na Salome aliyekuwa dadawa Mariamu (Mko.1:19; 16:1; Yn.19:25; Mt.27:56). Mara nyingi aliwekwa pamojana ndugu yake Yakobo na Yesu aliwaita „wana wa ngurumo‟ (Mk.3:17; Lk.9:54).Kwa hiyo kimwili Yohana alikuwa binamu wa Bwana Yesu. Baba yake alikuwa nabiashara ya uvuvi wa samaki, na alikuwa amefanikiwa kiasi cha kuwa na uwezowa kuwaajiri watu. Kabla ya kuitwa na Yesu Yohana na Yakobo walikuwa wavuvi(Mk.1:20).

Yohana alikuwa shahidi wa mengi aliyoyatenda Bwana Yesu na kuyasikia mengialiyosema na kufundisha. Jambo hili limeshuhudiwa kwa jinsi alivyotaja siku hatasaa ya tendo fulani kutokea (1:29, 35, 39, 2:1; 3:24; 4:6,10, 52, 53; 6:22; 7:14;11:6; 12:1; 13:1; 19:14, 31; 20:1,19, 26). Alijua maneno yaliyosemwa na jirani zakipofu (9:8-10). Alijua Yesu alikuwa amechoka (4:6) aliona maji na damu vikitokaubavuni mwake (19:33-45). Alijua jina la yule aliyekatwa sikio pia alijua lilikuwasikio la kuume (18:10). Alimfahamu Kuhani Mkuu (18:15). Aliingia kaburinialipolazwa Yesu (Yn.20:8). Hakutaja jina lake wala jinsi yeye alivyompenda Yesuila alitaja jinsi Yesu alivyompenda (Yn.13:23). Akawa miongoni wa Mitume 12walioitwa na Yesu na mmoja wa wale watatu waliochaguliwa kuwa karibu nayezaidi wakati wa matukio maalumu. Kwa mfano, Yesu alipogeuka sura mlimani;wakati Yesu alipomfufua binti Yairo, na mle katika Bustani ya Gethsemane.Aliegemea kifuani mwake katika Chakula cha mwisho. Mwishowe kabisaalipokuwa akifa Msalabani Yesu alimkabidhi mama yake kwake ili amtunze.

Mwanzoni mwa Kanisa alifanya huduma pamoja na wenzake pale Yerusalemu.Mara kwa mara katika Matendo ya Mitume ametajwa pamoja na Mtume Petro(Mdo:3:1; 4:13; 8:14; Gal.2:9). Baadaye sana, pengine wakati wa Vita kati yaWarumi na Wayahudi, kama B.K.68, alikwenda kuishi Efeso katika Jimbo la AsiaNdogo, na inafikiriwa ni yeye aliyefukuzwa mpaka kisiwa cha Patmo. Penginealikufa mnamo B.K.98.

Kwa sababu ya hayo yote hakuna mwingine miongoni mwa wafuasi wa Yesuambaye alifaa zaidi yake kuziandika habari zake na kuzifasiri. Alikuwa na nafasitele ya kumchunguza Yesu na kuona kwamba hakuwa na makosa wala hitilafu.Pamoja na hayo, kwa kuishi maisha marefu, alijaliwa muda mkubwa wa kuwazakwa makini juu ya yote aliyoona na kuyasikia kwa Bwana wake na kuyahakikishakwa jinsi mambo yalivyotokea katika maisha ya Kanisa baada ya Yesu kuondokana Roho kufika. Mwisho wa maisha yake hakusita kumtangaza Kristo kuwaMungu halisi na Mwanadamu halisi.

Page 9: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA498

Wataalamu wanapochunguza hali ya maandishi ya Injili hiyo wanakubalianakwamba ni andiko lililoandikwa na Myahudi mwenye ufahamu wa nchi yaPalestina, mtu aliyejua jiografia yake vizuri pamoja na kuelewa mila na desturi zawenyeji.

Baadhi ya wataalamu huwaza kwamba mwandishi hakuwa Mtume Yohana ilammoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo piaaliitwa Yohana.

(b) WalioandikiwaHatujui hasa walikuwa akina nani, ila kwa jinsi Yohana alivyoeleza jiografia yaPalestina na desturi za Kiyahudi inaonekana wengi wa wasomaji walikuwaWakristo wa KiMataifa. Pengine ni wale walioishi katika Efeso na makanisa yajirani.

(c) Mahali ilipoandikwa InjiliYafikiriwa na wengi kwamba Yohana alikuwa akiishi Efeso katika Asia Ndogoalipoiandika Injili hiyo. Pengine alifika huko ilipoanza vita kati ya Warumi naWayahudi. Waandishi wa zamani, Eusebio, Origen, Klement wa Iskanderia,Tertuliano, Ireneo, hao wote wametaja Yohana kuwa mwandishi, pia neno hilolaonekana katika Andiko liitwalo Muratorian Fragment.

(d) Tarehe ya kuandikwaHuenda kati ya B.K.80-98 ila siku hizo baadhi ya wataalamu wapenda kuwekatarehe iwe mapema kabla ya B.K.80, au kabla ya Anguko la Yerusalemu (B.K.70)kwa sababu maneno ya Yn.5:2ku. yaelekeza watu kufikiri kwamba Birika laBethzatha penye Mlango wa Kondoo lilikuwa lingaliko wakati wa kuandika.

Pamoja na hayo kipande cha Injili yenye sehemu ya Sura 18 kimepatikana,kipande hicho chafikiriwa kuwa cha mapema sana na kinatangulia nakalanyingine zote zilizoko. Kinaelekeza watu kufikiri kwamba Injili hiyo ilijulikana nakutumika huko Misri katika karne ya pili. Kwa hiyo, kama imekubalika Injiliiliandikwa Efeso, na imeenea mpaka Misri na kujulikana huko, basi wazo lazukakwamba huenda ni vema kuweka tarehe ya kuandika mapema kabla ya hapo.(e) Shabaha ya InjiliYohana ameweka wazi shabaha yake katika Yn.20:31 „ili mpate kuamini (yaanikuendelea kuamini) ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu, na kwakuamini mwe na uzima kwa jina lake‟.

Hakukusudia kuandika historia nzima ya maisha na huduma ya Yesu. Alichaguamambo yaliyotimiza lengo lake na kuweka pamoja habari ya tukio au tendo fulanila Yesu na maelezo ya kiroho, ili umuhimu wake uonekane na shabaha ya Yesukatika kutenda tendo fulani idhihirike. Mara nyingi ni vigumu

Page 10: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA499

kujua mazungumzo fulani yaliishia wapi na maelezo yalianzia wapi. Alitilia mkazotendo la kusadiki, akitumia neno „kusadiki‟ karibu mara mia, na karibu mara zoteni „kitenzi‟ (8:24; 11:42; 12:36, 44; 14:11). Hakutaka watu wasadiki mafundishofulani tu ya Imani ya Kikristo, ila wamwamini Yesu Kristo Mwenyewe ili wapatekushirikiana kibinafsi na Yeye aliye Uzima na kuingia maisha ya uzima na afyaya kiroho, ili wazidi katika kumwamini na kumjua (10:38; 16:12; 17:3). Neno kuuni Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu.

Pamoja na hayo yawezekana Yohana alikuwa akiwaza watu waliokana kwambaYesu ni Mungu halisi na Mwanadamu halisi. Kuelekea mwisho wa karne yakwanza wazushi walizuka ndani na nje ya Kanisa ambao walikana ukweli waYesu kufanyika mwili na wengine waliukana Uungu wake. Mmoja aliyejulikanasana Cerinthus aliishi Efeso wakati huo, yeye alikana kabisa kwamba Yesualifanyika mwili kweli. Pia, yawezekana alilenga wafuasi wa Yohana Mbatizaji,ambao waliendelea kumfuata Yohana. Twajua kwamba Paulo aliwakuta paleEfeso (Mdo.19:3-4). Baadhi yao hawakuwa tayari kumwacha Yohana nakumfuata Kristo. Yohana alianza Injili yake kwa kueleza kwa kirefu habari zaYohana Mbatizaji akionyesha uhusiano kati yake na Yesu na kukaza jinsiambavyo hata Yohana alishuhudia kwamba Yesu alimzidi.

(f) Mtindo wa InjiliYohana hakuandika habari nyingi za matendo na miujiza ya Yesu. Alichaguamambo kadhaa tu na baada ya kuandika habari zake alitoa maelezo ya kirohojuu yake. Si kwamba alibadili habari zenyewe ila aliona vema watu waelewemaana yake katika kumfunua Yesu Kristo kuwa nani. Katika mazungumzo yaYesu pia alitoa maelezo, na kwa jinsi yalivyofumana ni vigumu kujua yapi nimazungumzo ya Yesu na yapi ni maelezo ya Yohana. Neno hilo litakuwa wazitunapoendelea na ufafanuzi. Imeitwa „Injili ya kiroho‟ kwa sababu mwandishiamelenga kutoa maelezo ya kiroho juu ya mambo aliyotaja. Kwa mfano Yesualipomponya mtu aliyezaliwa kipofu Yohana alitoa habari zake ndipo aliendeleakuzungumzia habari ya Yesu kuwa Nuru ya ulimwengu, vilevile Yesualipowalisha watu elfu tano, habari hii ilifuatwa na mazungumzo marefu kuhusuYesu kuwa Chakula cha Uzima.

(g) Tofauti kati yake na Injili tatu zinazowianaInjili hiyo haina habari za mambo makubwa kumhusu Yesu, kama kuzaliwakwake, majaribu yake, kugeuka sura n.k.

Inatoa habari nyingi juu ya huduma ya Yesu katika eneo la Yudea na kuelezamambo yaliyotokea Yesu alipohudhuria Sikukuu za Kiyahudi pale Yerusalemu.Haisemi juu ya huduma yake huko Galilaya kama Injili tatu nyingine zisemavyo.Tofauti nyingine inahusu mafundisho ya Yesu. Katika Injili ya Yohana mafundishohayakutolewa kwa Mifano, kama ilivyokuwa katika Injili tatu, bali yalitolewa kwanjia ya Mazungumzo na Majadiliano ya Yesu.

Page 11: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA500

Katika Injili tatu Ufalme wa Mungu umetajwa sana ila katika Injili ya Yohana,Kristo ndiye kiini cha mambo yote.

Ina habari zisizopatikana katika zile Injili tatu, kwa mfano, Arusi huko Kana,Mazungumzo na Nikodemo na Mwanamke Msamaria, Uponyaji wa mtu kwenyeBirika la Bethzatha, Kuponywa kwa mtu aliyezaliwa kipofu, Kumfufua Lazaro; namafunzo mengi juu ya Roho Mtakatifu.

Ina habari nyingi ndefu za majadiliano kati ya Yesu na viongozi wa Kiyahudi.

Yohana aliweka jambo la Yesu kulitakasa hekalu mwanzoni mwa Huduma yake,na katika Injili tatu jambo hilo limewekwa mwishoni na kuonekana kuwa jambolililowachokoza Wayahudi kumkamata Yesu. Katika Yohana jambolililowachokoza lilikuwa Yesu kumfufua Lazaro.

Katika Injili hiyo miujiza ya Yesu yaitwa Ishara, ishara zilizodhihirisha Nafsi naCheo chake. Hizo ishara ziliashiria Yesu kwa shabaha ya kuwavuta watuwamwamini na kumkubali kibinafsi ili wapate uzima.

Ina misemo saba maalumu ya Bwana Yesu, yenye madai makubwa; kila msemoulianza „Mimi ndimi.......‟(6:35; 8:12; 10:11; 11:25; 14:6; 15:5).

Mwandishi alipotaka kuonyesha uwezo wa ajabu wa Yesu alisisitiza huo uwezokwa kutaja ukubwa wa miujiza; k.m. alimponya mtu kutoka mbali kama kwakuamua tu; alimponya mtu aliyekuwa na shida miaka mingi, miaka 38; alimponyakipofu aliyezaliwa kipofu ambaye hajapata kuona hata kwa siku moja; alimfufuaLazaro aliyekuwa mfu siku nne.

Katika habari zote Injili ya Yohana imesisitiza Yesu Kristo kuwa Mwana waMungu, mwenye umoja na uhusiano wa kipekee na Mungu Baba, uhusiano waukaribu mno (1:18; 20:28).

Yohana ametaja Pasaka tatu na kwa sababu hiyo imefikiriwa Huduma ya Yesuilichukua muda wa kama miaka mitatu. Injili tatu haziweki wazi muda wa Hudumaya Yesu.

MASWALI:1. Taja tofauti kubwa mbalimbali kati ya Injili ya Yohana na Injili tatu

zinazowiana.2. Eleza shabaha ya Yohana katika kuandika Injili hiyo.

Page 12: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA501

UFAFANUZI

Yohana alianza moja kwa moja bila kusema lolote juu ya mwandishi, walahakuwasalimia walioandikiwa, wala hakutaja shabaha ya kuandika mpaka mwishowa Injili. Hakutaja uzushi au makosa yoyote. Ila alisema sana juu ya Yesu Kristoakitangaza kwa nguvu na bila wasiwasi kweli kuu za Yesu Kristo kuhusu asili yakena nafsi yake.

Katika Injili ya Mathayo na Luka waandishi walianza na habari za Yesu kuzaliwaBethlehemu, Mathayo akitangulia kwa kuweka nasaba iliyorudi mpaka Abramu.Luka aliweka nasaba iliyorudi mpaka Adamu. Marko alianza na habari za YohanaMbatizaji. Ila tofauti na hao Yohana alianza kwa kurudi nyuma kabisa kabla yakuwepo kwa kitu chochote, kabla ya wakati na kabla ya mahali, katika umilele nakuwepo kwa Mungu.

1:1-18 YESU KRISTO - ASILI YAKE na NAFSI YAKE

1: 1-2 Uhusiano wa Neno na Munguk.1 „hapo mwanzo kulikuwako Neno‟. Hapo mwanzo ni ukumbusho wa uumbajiwa vitu vyote (Mwa.1:1) na katika Uumbaji jambo kubwa lilikuwa Neno la Mungu,Mungu alisema „iwe nuru, ikawa nuru‟ n.k. (Mwa.1:3, 6, 9, 11, 14, 20, 24, 26).

„Neno‟ ni neno lililotumika sana na wafasalfa wa Kiyunani walipotaka kuelezawazo au akili iliyo nyuma ya ulimwengu. Yohana hakuwa na maana hii. KwakeNeno ni sawa na Mungu, lasema juu ya utendaji wake, Neno ni ukweli mwenyenafsi anayeutegemeza ulimwengu na aliyekuwa sababu na njia ya kuumbwakwake. Tunapotazama Yn.1:1-18 twakuta maneno ya vitenzi 44 na sehemu hiyoyote yasema juu ya Neno, kwa hiyo ni wazi kwamba neno hilo lahusu utendajikuliko dhana au wazo. Katika sehemu hiyo Yohana anasisitiza utendaji wa Kristokabla ya kuzaliwa kwake hapo duniani.

Katika vifungu viwili vya kwanza Yohana amesema mambo makubwa matatu.(a) Kristo ni wa Milele, hana mwanzo, alikuwepo „hapo mwanzo‟ hivyo „alikuwako‟katika umilele, katika muda ule usiopimika uliotangulia „mwanzo‟ kabla ya wakatikupimwa. Kwa sababu hiyo:alikuwapo kabla ya kuwepo kwa mbingu na nchi;alikuwapo kabla ya kuwepo kwa viumbe na vitu;alikuwapo kabla ya kuwepo kwa mahali na wakati.

Twaweza kusema kwamba hakuna Mungu nyuma ya Kristo au hakuwepo Mungukabla ya Yesu Kristo. Maneno kama „kabla‟ „baadaye‟ hayana kazi tunapowazaumilele. (Neno hilo ni kubwa kwa kuwa linagusa jinsi tusomavyo Agano la Kale,kwa sababu Yesu Kristo alikuwa pamoja na Mungu katika yote tunayosoma katikaAgano la Kale).

Page 13: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA502

(b) Kristo ni Nafsi tofauti na Mungu Baba.„alikuwako kwa Mungu‟. Neno „kwa‟ linaonyesha kwamba Yeye ni tofauti naBaba, pamoja na kuonyesha kwamba Yeye yu pamoja na Baba katika uhusianowa kipekee, wa ukaribu kabisa (1 Yoh.1:1-2). Neno „kwa‟ limetumika katikaMarko 6:3 likiwa na maana ya kushirikiana pamoja kama watu walio sawa.

Ndivyo ilivyo kwa Kristo, amemkabili Baba ana kwa ana katika furaha na utimilifuwa ushirikiano, kama aliye nyumbani mwake na mahali pake ndani ya Mungu.Twaona kwamba Yohana hakusema „Mungu alikuwako kwa Mungu‟ bali Nenoalikuwako kwa Mungu, wala hakusema Mungu alikuwako kwa Neno. Mungu niMmoja; Mungu mkamilifu, mtimilifu, Nafsi Tatu, Baba, Mwana, Roho; nafsi zilizotofauti na nafsi zilizo sawa katika Umoja wa kuwa Mungu Mmoja (Yn.10:30;14:9-11). Kwa hiyo Neno ni Mungu, ila Mungu ni zaidi ya Neno. (Iwapo ni vigumukueleza, mfano mmoja wa kutusaidia ni habari ya jua, lililo mwanga, joto, na nuru,vitu vilivyo tofauti ila twajua bila jua hamna mwanga wala joto wala nuru, vyotevyawiana).

(c) Kristo ni Mungu halisi. Katika Kigriki neno „Mungu‟ linatawala sentensi kusudimkazo uwe juu ya Mungu. Yesu ni Mungu si kwamba anayo hali ya Ki- Mungutu. Alikuwa Mungu si alifanywa kuwa. Kwa asili ni Mungu, ni Mungu Mwana (1:18;20:28). Kusoma habari zake ni kusoma maneno na matendo ya Mungu, naYohana anataka tuisome Injili yake katika mwanga huo. Kama jambo hilo si kwelikitabu chake ni kufuru kuu.

Tukumbuke kwamba Yohana alikuwa Myahudi mwenye malezi katika dini yaKiyahudi iliyosisitiza sana kwamba Mungu ni Mmoja (Kum.6:4) hata hivyo,hakusita kumtaja Yesu kuwa Mungu.

Mahali pa Yesu katika „Uungu‟ hapabadiliki. Yeye yu Mungu Mwana daima, nakwa sababu hiyo Yeye ni Neno la mwisho na Ufunuo kamili wa mwisho waMungu, akiwa kati ya Yote yaliyotokea na yatokeayo na yatakayotokea, akishirikiumilele wa Mungu na hali zake za kutokuwa na kikomo wala mipaka.

k.3 Uhusiano wa Neno na UumbajiTabia ya upendo ni kuumba, kwa hiyo, kutokana na ushirikiano wa kipekee waupendo kati ya Mungu na Neno, yaani kati ya Baba na Mwana, ulimwenguulitokea. Yohana aliweka ukweli wa jambo hilo kwa njia ya kuhakikisha „vyotevilifanyika...‟ na kwa njia ya kukana „pasipo Yeye hakikufanyika....‟. Maneno hayoyaziba njia kwa watu kusema kwamba ulimwengu uliumbwa kutokana namata/maada iliyokuwapo. Ndivyo wasemavyo wengine. Pia wasema kwambahiyo mata/maada ilitoa nafasi kwa uovu kutokea, wakitafuta njia ya kueleza asiliya uovu kuwepo ulimwenguni. Mawazo kama hayo yapunguza mamlaka yaMungu juu ya ulimwengu kwa kuwa yadokezea kwamba yuko Mungu na ikomata/maada ya asili. Ni tofauti na ushuhuda wa vifungu hivi.

Page 14: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA503

Yohana alionyesha uhusiano wa Neno na Mungu kiutendaji katika kutokea kwavitu vyote. „vyote vilifanyika kwa (si na) huyo, maana yake, „vilitokea kuwa‟. Vituvyote ni ulimwengu mzima, vitu vya asili, mifumo ya sayari n.k. Badiliko kubwamno lilitokea kutoka „kutokuwepo kwa kitu chochote‟ mpaka „kuwepo kwa vituvyote‟. Katika k.1 Yohana alikaza kuwepo kwa Neno katika umilele uliotanguliakuwepo kwa wakati na mahali na vitu vyote. Hivyo twajifunza kwamba Neno niwa milele, ila uumbaji si wa milele (Kol.1:16; Ebr.1:2, 10; Zab.40:8; Ufu.3:14).Kamwe Yesu hawezi kufikiriwa kuwa „kiumbe‟ hata ikiwa ataitwa „kiumbe chakwanza‟. Neno yaani Yesu ni yule anayeunganisha na kutegemeza vitu vyote, yukati ya kuweko na kuishi kwa vitu vyote. (Tukumbuke kwamba maelezo hayo juuya asili ya uumbaji ni kwa upande wa dini si wa sayansi).

k.4, 5, 9 Uhusiano wa Neno na Uzima na NuruHapo Yohana ametaja matunda ya Utendaji wa Neno katika uumbaji, si kwambani ulimwengu tu uliotokea, bali pia uzima ulitokea ndani yake, ili ulimwengu upatekuendelea kuwepo ukitegemezwa na Neno aliye Uzima na Mtoa Uzima(Mdo.17:8). Halafu Yohana aliendelea kusema kwamba huo uzima ni Nuru,ukumbusho wa Mwanzo 1:3 kwa kuwa kitu cha kwanza kilichoumbwa kilikuwanuru. Kwa hiyo katika mazingira ya vifungu vitatu vya kwanza Uzima na Nuruvyahusika na uumbaji. Twajifunza mambo matatu kwamba 1. Nuru huangazawanadamu; 2. Nuru huangaza katika giza; 3. Giza halikuweza kuizima. Jambohilo lahusika na wanadamu kuumbwa katika mfano na sura ya Mungu.

Kwa sababu Yohana ametumia neno „uzima‟ mara 36 katika Injili hiyo na katikamara hizo ametumia mara 11 katika kutaja „uzima wa milele‟ inaelekea kuwa namaana ya Neno kuwa Uzima na Nuru hivyo ni zaidi ya kuwa uhai wa kawaidawa viumbe hai. Ni uzima wa Mungu na wa Yesu Kristo, ambao wanadamu hupatawanapozaliwa upya na kushiriki katika „uumbaji mpya‟ ambao Mungu alikusudiaalipomtuma Yesu Kristo. Yohana ameunganisha huo uzima na Neno. Neno hasani huo uzima (Yoh.24-26, 40; 6:51, 53; 11:24, 25; 14:6; 1 Yn.5:11, 12). PiaYohana ameweka nuru pamoja na uzima. Ni uzima uletao nuru ya kweli maishanimwa mtu. Yesu ni nuru halisi (Yn.8:12; 17:3) kwa Yesu watu hupata kutambuamaana na shabaha ya kuumbwa na kuishi kwao. Uzima na nuru ni msingi wamaisha ya binadamu. Katika habari za Uumbaji nuru ilikuwa kitu cha kwanzakuumbwa (Mwa.1:3). Upo uhusiano kati ya Neno na Nuru kwa sababu ni tabia yaMungu kujifunua na Neno amemfunua kwa ukamilifu. Baadaye katika Injilimambo hayo mawili yaonekana katika habari za Mtu aliyezaliwa kipofu kupatakuona kwa mara ya kwanza na Lazaro aliyekuwa mfu kwa siku nne kupata kuishitena. Miujiza hiyo ilikuwa ishara za kusimamisha madai ya Yesu kuwa Uzima naNuru. Katika Injili hiyo tumepewa habari za mashindano yaliyotokea kati ya Yesuna viongozi hasa, iliyoashiria vita iliyopo kati ya nuru na giza.

Page 15: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA504

Kwa hiyo twaona maneno hayo yanahusu uzima na nuru ya uumbaji na waMungu kujifunua kwa wanadamu wote katika dhamiri zao na katika kazi zake zauumbaji. Pia yahusu mambo ya wokovu, Yesu ni Uzima na Nuru ya kuwaongozawatu wamfahamu Mungu vizuri. Kutokana na Maisha na Mafundisho ya Yesu nahasa kwa Kifo chake kwa ajili ya wenye dhambi Mungu amefunuliwa kuwaMwenye upendo, Mtakatifu, Mwenye haki, Mwenye rehema, asiyependa mwenyedhambi afe (3:16)

k.5 Hapo Yohana amedokeza jambo ambalo ni hoja kubwa ya Injili. Ulimwenguhaukuwa tayari (wala mpaka sasa hauko tayari) kuupokea huo uzima na hiyokweli, yaani kumpokea Neno ambaye ni Kristo. Wakati wote tangu mwanzo vitaimekuwapo kati ya nuru na giza. Mwisho wa vita hiyo itakuwaje? Yohanaameonyesha mwisho katika maneno „wala giza halikuiweza‟. Nuru italishindagiza, iwapo giza lajitahidi kuizima nuru, halitaweza; Yesu alifufuka kutoka wafubaada ya kuuawa.

k.9 Hapo Yohana ametaja Neno kuwa Nuru halisi, aliye asili ya ufahamu wakiroho kwa kila mtu. Ni nuru safi, yenye ufunuo, isiyomdanganya mtu. Hivyo kilamtu aweza kuwa na ufahamu wa kutosha asiwe na udhuru mbele za Mungu(Rum.1:18ku).

k.6-8 Uhusiano wa Neno na Yohana MbatizajiBaada ya kueleza asili ya Neno kuwa Mungu, na baada ya kuonyesha uhusianowa Neno na Uumbaji, Yohana aliendelea kwa kutaja habari zake kihistoria,alipokuja duniani. Alianza pale walipoanza waandishi wa Injili nyingine tatu kwahabari za Yohana Mbatizaji. Alibainisha kati ya Yesu Kristo na Mbatizaji kwakuweka wazi tofauti kati yao.1. Kristo alikuwa tangu milele, hakuwa na mwanzo, k.1, 2, 9.

Mbatizaji alikuwa na mwanzo, „palitokea mtu‟ k.6,7,8.b) Kristo alikuwa Mungu

Yohana alikuwa mtuc) Neno alikuwa Mungu

Yohana alitumwa na Mungud) Neno alikuwa Nuru halisi

Yohana alikuja ili aishuhudie ile nuru...hakuwa ile nurue) Wote wapate kuamini kwa yeye - Neno ni wa kuaminiwa nakutegemewa. Yohana alikuwa mjumbe wa kuwaelekeza watu kwa Yesu, ambayepeke yake, amestahili kuaminiwa.

Ni ajabu kuona ya kuwa Yohana Mbatizaji amezungumziwa katika utanguliziunaotaja makuu kumhusu Kristo. Yawezekana sababu ni kwamba pale Efesowaliendelea kuwepo wafuasi wa Mbatizaji ambao hawakuwa tayari kumfuataKristo. Twajua walikuwapo Paulo alipofika Efeso na kuhubiri pale kwa mara yakwanza, kama B.K. 54 (Mdo.18:25; 19:3). Hatujui kama waliendelea kuwepo.Yohana alionyesha jinsi Yohana Mbatizaji asivyomfikia Yesu kwa hali zote.

Page 16: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA505

Alisisitiza kazi ya Mbatizaji katika kumshuhudia Kristo. Mbatizaji alikuwa namahali pa maana sana katika maandalio ya Kuja kwa Kristo. Alitumwa na Mungukama wale wa zamani, akina Musa (Kut.3:19ku) Isaya (Isa.6:8) Yeremia(Yer.1:4ku). Kazi yake ilikuwa kutayarisha njia ya Masihi kwa kuliamsha taifa laIsraeli kusudi wawe tayari kumpokea Kristo (1:7) na alipofika aliendeleakumshuhudia vizuri sana. Yohana aliitwa na Mungu Mwenyewe na jinsialivyopata kuzaliwa kwa wazazi waliopita umri wa kumzaa mtoto ilithibitisha witowake na kutumwa kwake. Katika Injili zingine mkazo ulikuwa juu ya Mbatizajikuwatayarisha watu kwa njia ya kuwaita kwenye ubatizo wa toba. Yohana katikaInjili hiyo amesisitiza kazi yake ya ushuhuda (1:7,8,15,19,32,34; 3:26,28; 5:33).Katika mawazo ya Yohana ushuhuda ulikuwa jambo zito, lenye hali ya „kibaraza‟kitu cha kutegemewa katika hukumu. Ushuhuda ulithibitisha ukweli wa madai yaYesu juu ya nafsi yake na cheo chake. Yohana alijitoa kabisa kwa ile kwelialiyoishuhudia.

Pamoja na Mbatizaji kumshuhudia Yesu, Yohana ametaja ushuhuda wa MunguBaba aliyefungamana naye kabisa, kiasi cha kuwa „ampokeaye Mwanahumpokea Baba, asiyempokea Mwana amemkataa Baba‟. Yohana ametajaushuhuda saba: Wa Baba; wa Mwana; wa Roho Mtakatifu; wa Yohana Mbatizaji;wa Maandiko Matakatifu; wa kazi zake; wa mitume, na watu mbalimbali.

1:10-13 Uhusiano wa Neno na Ulimwengu na Wanadamuk.10 Yohana ametumia neno „ulimwengu‟ mara 77 katika Injili hiyo akiwa namaana ya mazingira ya kimwili na kiroho ambayo ndani yake wanadamuwanaishi. Kwa hiyo Neno ahusika na maisha mazima ya wanadamu, akihusishanao kimwili na kiroho, kwa sababu yote mawili huwiana.

Neno aliingia katika mazingira na maisha ya wanadamu na kuishi maishayaliyolingana na maisha yao. Ila Neno si sawa na ulimwengu, si „roho‟ yake. Kwanjia yake ulimwengu ulipata kuwako, kwa hiyo, ni wazi kwamba yeye alikuwa njeyake na kabla yake. Yeye alikuwako „hapo mwanzo‟; ulimwengu ulipopatakuwako. Ulimwengu haukuwako ndipo ulipata kuwako; Neno alikuwako, ndipoakapata kuwako ulimwenguni. Hivyo ana kutokuwako kwake ulimwenguni kwakuwa ni kabla yake na nje yake, pamoja na kuwako ulimwenguni kwa mudaalipokuwa mwanadamu. Ina maana kwamba hafungwi ndani ya ulimwengu.

k.11 Neno alikuja ulimwenguni, si kama mgeni, bali kama mwenyewe, mhusikakabisa, mfano wa mtu ajaye nyumbani kwa jamaa zake na mji wake. Alikuja kwamali yake mwenyewe, mwenye haki na mamlaka juu yake. Ila ajabu ni kwambahakupokelewa kama ilivyopasa apokelewe. Alizaliwa kati ya watu walioitwa tanguzamani za kale ili wafanye maandalio ya kumpokea, watu ambao walimtazamiakwa muda mrefu. Kimwili Yesu alizaliwa Myahudi,

Page 17: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA506

akalelewa Kiyahudi, akafuata mila na desturi za Kiyahudi, aliishi maisha sawa namaisha yao, hata hivyo, hawakumtambua kuwa Mwana wa Mungu, Muumba waona Muumba wa kila mtu na wa kila kitu. Hawakumtambua kuwa timizo la lengo lakuteuliwa kwao. Hawakujua ni Mwokozi wa ulimwengu. Sikitiko ni kwamba zaidiya kumkataa Yeye na madai yake, wakachochea Kuuawa Kwake. Hata YesuMwenyewe alilia kwa ajili yao (Lk.19:41) na Paulo, aliyekuwa Myahudi yeye piaalilia sana kwa ajili yao (Rum.9:1-3).

Ijapokuwa Wayahudi walimkataa, ni vema kutokuwalaumu hao tu, kwa sababu,wanadamu kwa jumla hushiriki tabia hiyo ya uasi, na mpaka leo wengi hawakotayari kumpokea.

k.12 Ila si wote waliomkataa. Kwa neema ya Mungu wengine walimpokea.Kumwamini (k.12) na kumpokea (k.12) na kuzaliwa na Mungu (k.13) ni mamoja.Kuamini ni mkazo mmojawapo kimsingi katika Injili hiyo, ndiyo shabaha yake(20:31). Kuamini kuna maana ya kumpokea na kujitoa kwake Kristo. Haowaliompokea walijaliwa na Mungu kumpokea. Twasoma „aliwapa‟. Aliwapa nini?Aliwapa „uwezo (yaani haki, fadhila, heshima) wa kufanyika watoto wa Mungu‟.Fadhila hiyo ni ya maana sana. Katika ulimwengu wa zamani, hata mpaka leo,jambo la cheo na heshima ni jambo kubwa. Hata tumezoea kusema „si unajuanini, bali unamjua nani‟ kama hii ni njia ya kufanikiwa. Siku zile watumwawalikuwa wengi sana, hawakuwa na haki, wala uhuru, wala matumaini. KatikaInjili walipewa nafasi kibinafsi ya kuingizwa katika familia ya Mungu na kuwawatoto wa Mungu. Hivyo, wengi waliokuwa „si kitu‟ walifanywa kuwa watu wathamani, wapendwa wa Mungu. Nafasi hiyo ilitolewa kwa kila mtu. Kabla ya Injili„wokovu‟ ulipatikana ama kwa wenye akili tu kwa njia ya falsafa, au kwa walewalioingizwa katika dini kwa desturi fulani pengine ya siri, na kwa Wayahudi kwanjia ya kuzaliwa katika taifa hili, ila Ukristo ulitoa nafasi kwa mtu awaye yotealiyekubali kutubu na kumwamini Kristo.

Ina maana kwamba kabla ya kumpokea Kristo watu hawakuwa „watoto halisi waMungu‟. Waliompokea walihamishwa kutoka mauti kwenda uzima (5:24).Walizaliwa na Mungu na kushirikishwa tabia yake (2 Pet.1:4). Shabaha ilikuwawapate kufanana na Baba yao na Mwokozi wao Bwana Yesu, si shabaha yakupata cheo au jina tu.

Katika Agano Jipya Mungu ni Baba wa wote, ila si wote walio watoto wake.Mungu ni Baba katika hali ya kuwa Muumba na Mhifadhi wa wanadamu wote.Kwa sababu ya Anguko la Adamu wanadamu walipoteza „uana‟ wao, waitwawatoto wa hasira (Efe.2:3). Wanadamu hurudishiwa „uana‟ wanapompokeaKristo na kuzaliwa upya kwa Roho Mtakatifu. „wanaomwamini jina lake‟ jina nijumla ya yote yahusikayo na jina hilo, hasa tabia yake. Ni kumkubali Kristo kwadhati jinsi alivyo na jinsi alivyofunuliwa kuwa, na kujikabidhi kwake. Kuamini nizaidi ya kuamini habari kadha juu yake. Hakuna „uana‟ wa Mungu nje ya imanihai katika Kristo.

Page 18: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA507

k.13 „waliozaliwa‟ hakuna neno lingine liwezalo kueleza hali mpya ya mtu maraanapomwamini Kristo. Nia na matakwa yake na maisha yote yaguswa na kuwatofauti na hapo nyuma.„si kwa damu‟ yaani, si kwa kutoka katika ukoo fulani, au kabila fulani. Wayahudiwalitegemea sana kuwa „uzao wa Ibrahimu‟ nao walijivunia mababa wao, akinaMusa, Daudi, n.k.„si kwa mwili‟ kuzaliwa upya hakutokani na jitahada na mbinu za kibinadamu,kwa sababu ndani yetu hamna uwezo wa kuubadilisha utu wetu na kuufanyakuwa upya.„si kwa mtu‟ jambo hilo halipatikani kwa matendo au kazi au nia ya mtu. Hakunaawezaye kumbadili mwingine kwa ndani.

Hakuna kitu, potelea mbali, ni kizuri kiasi gani kiwezacho kufanya na kuletajambo hilo la kuzaliwa upya na kufanyika watoto wa Mungu. Wala hakuna njiayoyote iwezayo kufaulu. Ni mwujiza wa ajabu sana. Neno ambalo Yohanaametumia kwa „kuzaliwa‟ ni lile la mwanaume na uzazi wa kumzaa mtoto.Yohana amesisitiza kwamba jambo hilo latokana na mapenzi ya Mungu, si kwakupenda kwa mtu tu. Neno la kumshukuru Mungu ni kwamba yeye hupendakutuzaa kwa mara ya pili. Hivyo, Yohana amelizungushia boma neno hilo kwakuweka nje lisivyo na kudhihirisha lilivyo.

Uwiano kati ya kuamini na kuzaliwa na Mungu ni fumbo, yote mawili yaendapamoja katika Injili hiyo. Neno „imani‟ husisitiza wajibu kwa upande wa mtu, na„kuzaliwa na Mungu‟ husisitiza utendaji wa Mungu.

k.14 Neno alifanyika MwiliHapo Yohana amefikia upeo wa hoja yake kuhusu Neno. Ameishaonyesha Nenoyaani Yesu kuwa umoja na Mungu, na sasa katika k.14 aonyesha umoja wakena wanadamu. Ilitokea nini ili Neno awe „katika ulimwengu‟? Ilikuwa kwa njia ganiNeno aliye Mungu adhihirika kwa wanadamu, awe mwanadamu na kujihusishana mahitaji ya ubinadamu? Jibu ni „Neno alifanyika mwili‟. Neno lililotajwa katikak.1 na k.2 kuwa kwa Mungu na kuwa Mungu, alifanyika mwili. Alipata hali mpya,asiyokuwa nayo hapo mwanzo. Mungu alijinyenyekeza awe Imanueli, Mungupamoja nasi (Mt.1:23). Ni mwujiza wa ajabu sana upitao uwezo wetu wakuufahamu. Uhusiano wake na ulimwengu ulibadilika. Neno alijieleza kwa njia yakufanyika mwanadamu mwenye nafsi, alionekana, alisema na kusikia, aligusa nakuguswa n.k. Alikuwa mwili na damu kama sisi, alibanwa katika mipaka ya mahalina wakati kama wanadamu wanavyobanwa; Alisikia uchovu, njaa, maumivu n.k.Hivyo aliushiriki ubinadamu wetu huku akiwa Mungu. Ubinadamu wake ulikuwawa kweli vilevile na Uungu wake.

Ndipo Yohana alisema „akakaa kwetu‟ maana ya maneno yaliyotumika ni „alipigahema kwetu‟ ukumbusho wa jinsi Mungu alivyokaa na Waisraeli jangwani. Waowalipiga mahema yao, na Mungu alikuwa na Hema lake katikati yao, Hema laKukutania, iliyoashiria Kuwako Kwake pamoja nao. Utukufu

Page 19: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA508

ulionekana juu ya Hema (Kut.40:34ku). Ijapokuwa Yesu alikaa kwa muda wamiaka kama thelathini tu, hakuwa „njozi‟ wala „ya kuonekana‟ tu, bali aliishimaisha ya kibinadamu kweli. Yesu alipofanyika mwili, Mungu asiyeonekana,asiyeelezeka wala kufasilika, aliletwa karibu na wanadamu ili wapate kumwonana kumfahamu jinsi Mungu Alivyo.

Ndipo Yohana alitoa ushuhuda wake na wa wenzake waliomwona Yesu katikaule muda alipokuwako ulimwenguni. „nasi tukauona utukufu wake, utukufu kamawa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli‟. Yohana nawenzake walimwona kwa muda wa kutosha kumwangalia vizuri nao walitambuakwamba huyo ni yule wa kuwafaa, mwenye kuwapa shabaha ya maana kwamaisha yao. Walimwona wakati wa kufaa na wakati wa kutokufaa, wakatialipopokelewa vizuri na wakati alipokataliwa, wakati alipoishi bila matatizo yakukosa mahitaji na wakati wa kukosa mahitaji. Walimwona katika kila haliiwapatayo wanadamu. Tena walimwona wakati alipojaribiwa kupita wanadamuwajaribiwavyo na katika mambo yasiyo kawaida ya wanadamu kujaribiwa.Walisemaje? Yohana alisema kwa ajili yake mwenyewe na kwa niaba yawenzake „nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana Pekee atokayekwa Baba; amejaa neema na kweli‟ (Ling. na Kut.33:18ku. 34:5ku). Walimtambuakuwa na uhusiano pekee na Mungu. Walimkiri kuwa wa kweli, asiye na hila walauongo ndani yake. Pia walimwona kuwa amejaa neema. Walikirimiwa fadhili nabaraka za Mungu, walisamehewa dhambi zao, walitiwa moyo, walijisikiakupendwa na kuthaminiwa, walifanyiwa vizuri sana kupita ustahili wao. Tenawalijua hayo katika ujuzi wa kibinafsi, katika maisha yao ya kila siku. Kristohakubaki kama itikadi ya dini wala kama dhana au wazo la imani. Yohana alitoaushuhuda juu ya Yesu „nasi tukauona utukufu wake‟. Kwa hiyo, utukufu ni ninihasa? Utukufu ni kuangaza kwa nje tabia njema za ndani, unyenyekevu, upole,kujitoa, kutumika, upendo, n.k. Utukufu si wingi wa mali, wala fahari, wala ukuu,wala mapambo mazuri n.k. La. Utukufu wa mtu huonekana katika tabia zakezinazofanana na zile za Bwana Yesu. Si wote walioutambua utukufu wake. Katika2:11 baada ya ishara ya maji kugeuzwa kuwa divai twasoma kwamba wanafunziwaliuona utukufu wake na kumwamini. Mbeleni katika Injili hiyo Yohanaamesisitiza kwamba huo utukufu ulidhihirika zaidi sana pale Msalabani, mahaliambapo upendo na haki na utakatifu wa Mungu vilidhihirika.

„atokaye kwa Baba‟ Utatu ni wa milele na uhusiano wa Baba na Mwana na Rohoni wa milele, Utatu hauna mwanzo wala mwisho, wala mmoja hapunguimwenzake. Agustino alisema „nionyeshe Baba aliye wa milele, naminitawaonyesha Mwana aliye wa milele‟. Tangu kifungu hicho Yohana hakutumiatena neno „Neno‟ ila alimwita Yesu „Mwana‟ kwa sababu alitaka kusisitizauhusiano na umoja wake na Baba. Mwana ni wa pekee kabisa.

Neno kufanyika Mwili hutia muhuri juu ya uthamani wa ubinadamu wetu.Potelea mbali tumeanguka, tu wenye dhambi, hata hivyo Yesu alithubutu

Page 20: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA509

kuzaliwa mwanadamu, sawa na sisi katika mambo yote isipokuwa dhambi. KatikaNeno kufanyika Mwili twaona Yesu amejihusisha na maisha ya kibinadamu, hasakatika udhaifu wetu (Mt.11:28). Neno kufanyika Mwili ni jibu kwa haja yetu kubwaya wokovu. Kwa sababa wanadamu wote wameanguka hakuna hata mmojaaliyeweza kuokoa. Ni Mungu peke yake awezaye kuwaokoa, ila, kwa sababu niwanadamu ambao wamefanya dhambi lazima matengenezo yafanyike namwanadamu asiyekuwa na dhambi. Kwa sababu hiyo Yesu Kristo aliye Mungukwa asili alifanyika kuwa mwanadamu kwa ajili hiyo. Alikuwa na sifa zotezilizomstahilisha awe mpatanishi kati ya Mungu na sisi. Haikutosha afanyikeMwili tu, ilimpasa afe kwa ajili ya dhambi zetu. Itikio linalofaa kwa Neno kufanyikaMwili ni kumwabudu.

k.15-18 Neno ni bora, amfunua Baba kwa ukamilifu

k.15 Huduma ya Mbatizaji ilikuwa hatua ya mwisho katika maandalio yaukombozi, naye alikuwa shahidi wa kwanza alipotokea Mkombozi Mwenyewe.Mbatizaji aliliamsha taifa la Israeli liwe katika hali ya shauku wakimtazamia „YuleAjaye‟. Walitambua kwamba miaka mingi ya ukimya, wakati walipokosa kusikiasauti za manabii ulikuwa umepita. Yohana alikuwa mwangalifu sana ili watuwasimwaze yeye kuwa Yule, daima alinyosha kidole chake kwa Yesu.

Alisema nini kumhusu Yesu? Alishuhudia kwamba Yesu ni bora kwa sababuanao uwezo wa kutosheleza haja zote za wanadamu. Badala ya Toratiinayowadai watu kufanya zaidi ya uwezo wao wa kuitimiza, Yesu awafanyie watukwa neema na kweli. Ijapokuwa Yohana Mbatizaji alizaliwa kabla yake, Yesuamemtangulia, kwa sababu Yeye ni wa milele, kabla ya „wakati‟ na Yohana ni wa„wakati‟. Pamoja na hayo, Yesu ni bora kwa sababu Yeye ni Mungu aliyefanyikaMwanadamu, Yohana alikuwa mwanadamu tu. Yohana alitumwa na Mungu iliatayarishe njia ya Mwana Wake, Yesu hakusita kuupokea ushuhuda wa Yohana,na baadaye alisisitiza ukuu wake kwa madai mbalimbali yaliyoanza na maneno„Mimi ndimi.......‟

k.16 „katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema‟ „neemana kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo‟. Neema haipungui wakati wowote,haina mpaka, haikatiki. Kwa neema ya Kristo mtu huishi katika ushirikianomwema na Mungu, hana wasiwasi, hufurahia daima wokovu uliompatiamsamaha wa dhambi zake bure, kwa sababu ya Kifo cha Kristo. Huzionja barakatele za Mungu nafsini mwake na kuishi katika tumaini la uzima wa milele. Sikukwa siku muumini hupata neema ya kupambana na jambo lolote limpatalo.Maneno „neema juu ya neema‟ yana maana kihistoria. Hapo nyuma neema yaMungu ilionekana alipofanya agano la Torati na watu wake. Sasa amefanyaAgano Jipya na watu katika Yesu Kristo. Hivyo neema ya Kristo, izidiyo ile yazamani, imekuwa mahali pa ile neema ya Torati, na kwa sababu hiyo ni matimizoyake (Mt.5:17-20).

Page 21: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA510

Yohana alilinganisha Yesu na neema na Musa na Torati. Yesu na neema nakweli zimefungamana kabisa, Yesu ni neema na kweli. Sivyo ilivyo kwa Musa naTorati. Mtu haletwi katika uhusiano na Musa, eti anaishi kwa Torati. Toratihusimama peke yake. Kuishi kwa Torati ni kuishi kwa wasiwasi wa kujiuliza,„katika hili nimefaulu? katika hili nimekosa?‟ leo yawezekana nifaulu mengine,kesho yawezekana nikose? Hamna tumaini la kufaulu yote. Tena Torati ni baridi,haina nafsi, haimhurumii mtu, mtu hasikii kwamba Torati inampenda, kinyumechake mtu husikia kulemewa. Wala Torati haina msamaha, kosa ni kosa, haihojiwi.

k.18 Hapo Yohana amefikia upeo wa maelezo yake kumhusu Neno, Mwana waMungu. Alianza na jambo ambalo Wayahudi wote walifahamu ya kuwa hakunamtu aliyemwona Mungu wakati wowote (Kut.33:20; Hes.12:8). Ila Yesu aliyeMungu Mwana, Mungu aishiye ndani ya Mungu, huyo amemfunua. Amestahilikumfasiri kwa wanadamu kwa sababu Mwenyewe ni Mungu, hivyo anaelewa„Mungu‟, pia katika uhusiano wake na Baba yu karibu naye kabisa, huishi humondani katika „Mungu‟ aliye Baba, Mwana, Roho, kwa masikilizano ya ajabu,maana Mungu ni pendo, hivyo wakabiliana wao kwa wao katika upendo mtimilifu,na Yohana alieleza hali hiyo kwa maneno „aliye katika kifua cha Baba‟. Mungualipomtuma Kristo duniani ni kama alitoa moyo wake. Hata alipokuwa hapaduniani Yesu alikuwemo kifuani mwa Baba, katika hali ya kuwa Mungu Mwana.Alikuwa hapa duniani katika hali ya kuwa Mungu Mwana aliyefanyika mwili. Nivigumu sisi wanadamu kuelewa jinsi hali hiyo ilivyowezekana, lakini ndiyoilivyokuwa. Katika kumfunua Mungu ni dhahiri kwamba twaweza kuutegemeaufunuo huo kwa sababu Yesu aliweza kuleta ripoti kamili na ufafanuzi mzuri juuyake. Neno alilotumia Yohana kwa „kumfunua‟ ni „kumfafanua/kumfasiri‟ (6:46;14:9; Kol.1:15).

MASWALI1. Ni mambo gani makubwa kumhusu Yesu ambayo tunajifunza kutokana na

1:1-18?2. Eleza tofauti kati ya Yohana Mbatizaji na Yesu3. Eleza kwa kutumia maneno yako mwenyewe maana ya 1:12-134. Mwandishi amesisitiza sababu ipi ya Yohana Mbatizaji kutumwa na

Mungu?5. Kwa nini Yesu hawi sawa na manabii na wanaoadhimishwa katika dini

zingine?

Page 22: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA511

1:19 - 4:54 MUDA WA WATU KUMFIKIRIAKatika sehemu hii habari zimeandikwa za matukio kadha wa kadha yaliyomletaYesu mbele za watu ili wapate kumwangalia na kumkubali. Ni kama hayoyamechaguliwa ya kumwakilisha na kutoa nafasi kwa watu kumdhukuru piawasomaji wavutwe kumfikiria vema. Mambo yenyewe ni:a. Ushuhuda wa Yohana Mbatizajib. Wanafunzi wa Mbatizaji kuelekezwa kwa Yesuc. Arusi huko Kana ya Galilayad. Yesu kulitakasa hekalue. Mazungumzo ya Yesu na Nikodemof. Yohana Mbatizaji amshuhudia Yesug. Yesu azungumza na Mwanamke Msamariah. Yesu amponya mwana wa diwani huko Galilaya

1:19-34 a) Ushuhuda wa Yohana Mbatizajik.19-28 Ushuhuda kwa wajumbe rasmi wa KiyahudiHapo nyuma tulipewa habari za utume, lengo, na ujumbe wa Yohana Mbatizaji.Kuanzia k.19 tunaona ushuhuda wake kwa njia ya kuyajibu maswali ya wajumberasmi waliotoka Yerusalemu: k.19 „Wewe u nani?‟ k.21 „U Eliya wewe? k.22 „Unani‟ „tuwape majibu wale waliotupeleka. Wanenaje juu ya nafsi yako?‟. Yohanaalitoka katika jamii ya ukuhani ila hatuna habari kwamba alifanya huduma hiyomwenyewe. Yawezekana ndiyo sababu makuhani walivutwa kujua zaidi juu yake.

Maswali yaliulizwa na akina nani? Hao waliokuja kwake walikuwa Makuhani naWalawi wa Yerusalemu (k.19) na baadhi yao walikuwa Mafarisayo (k.24), hivyowaonekana kuwa kundi rasmi la viongozi wa dini ya Kiyahudi. Ni vematukumbuke ya kwamba wakati huo Wayahudi waliishi chini ya utawala wa Dola laKirumi. Kama ilivyo kawaida ya wakoloni, Warumi walihofu sana waliposikiahabari za kuzuka kwa jambo geni hasa ikiwa mtu au kundi la watu walithubutukuwaamsha wenyeji. Bila shaka Yohana aliwazwa kwa mashaka kwa jinsialivyoliita taifa zima watubu. Mikutano mikubwa ya watu walimwendea. Hivyo,viongozi wa Kiyahudi waliwajibika kumchunguza Yohana na kumhoji, iliwakiulizwa juu yake wataweza kutoa maelezo ya kuridhisha.

Pamoja na hayo Wayahudi wenyewe walikuwa na hamu sana ya kumpata yuleMasihi waliyeahidiwa na Mungu tangu zamani. Walipotawaliwa na utawala wakigeni hamu yao ilizidi. Kwa hiyo, viongozi waliona vema wamchunguze Yohanana kuona kama yeye ndiye yule Masihi au vipi, hasa kwa sababu hakutokea kwajinsi walivyomtazamia wala hakufanya kama walivyotaka. Kwa hiyo, maswali yaoyalilenga jambo hilo.

Katika k.19-20 Mbatizaji alibainisha kati yake na Masihi kwa kukana kabisakuwa Masihi „mimi siye Kristo‟. Kristo (Kiyunani) (Masihi Kiebrania) si jina la

Page 23: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA512

binafsi, ni jina la cheo, maana yake „aliyetiwa mafuta‟ yule aliyetumwa na Mungukuwaokoa watu wake mikononi mwa adui. Walikuwa katika hali ya kufikirikwamba wakati wa Kufika kwa Masihi umekaribia, kwa hiyo, alipotokea mtu aliyetofauti na wenzake mawazo yao yalikwenda kwa Masihi.

Hao wajumbe rasmi waliendelea kumwuliza Yohana maswali, maana badohawajapata jibu lolote la kuwaridhisha. Katika Malaki 4:5 (unabii wa mwishokatika Agano la Kale kumhusu Masihi) ilitajwa kwamba Eliya atatokea kabla yaMasihi kufika. Kwa hiyo, kama Yohana si Masihi yawezekana yeye ni „Eliya‟aliyetabiriwa na Malaki. (Wayahudi walikuwa wamezoea sana kumweka Eliyapamoja na Kristo hata Yesu alipokufa Msalabani walidhani kwamba Eliyaatatokea pale Mt.27:46, 47). Hapo tena Mbatizaji alikana kabisa kuwa huyo Eliya,„mimi siye‟ (k.21). (Twajua kwamba Yesu alisema Mbatizaji ni Eliya Mt.11:14 ilahakuwa na maana kwamba ni yule aliyeishi zamani za kale). Yohana alifananana Eliya na yule nabii aliyetajwa na Malaki, lakini hasa hakuwa Eliya mwenyewe.

Basi, ikiwa Yohana si Masihi, wala Eliya, yawezekana ni „yule nabii‟ aliyetajwa naMusa (Kum.18:15). Musa alikuwa na maana gani aliposema juu ya Mungukumwinua nabii mwingine kama yeye. Alikuwa akimwaza Masihi katika hali yakusisitiza kazi yake mojawapo ya unabii. Kwa kawaida Masihi aliwazwa kuwaMfalme. Hapo tena Mbatizaji hakuwaacha gizani, akajibu La.

Kutokana na majibu ya Yohana na jinsi alivyokana kabisa kuwa si Masihi, auEliya, au yule nabii, basi wakatatanishwa sana, wakataka kujua kwa niniamejitwalia mamlaka ya kuwabatiza watu ikiwa yeye si mmoja wa hao.Wakamwomba ajieleze vizuri na kusema wazi. k.22 „U nani?‟ „Wanenaje juu yanafsi yako?‟. Ndipo Yohana alijihusisha na unabii wa Isaya 40:3 „Mimi ni sauti yamtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana‟. Ametumwa kutayarisha njia yaMasihi. Zamani zile barabara nyingi hazikuwa nzuri, ziliwataabisha wasafiri.Hivyo, wakati wa Mfalme kupitia mahali fulani watu walitumwa kuzitengenenezabarabara. Kazi ya Yohana ilifanana na kazi hiyo, alitumwa kunyosha njia,kutengeneza taifa la Israeli wawe tayari kumpokea Mfalme atakapofika. Alidaikwa unyenyekevu mkubwa kuwa sauti tu, ni bure kujaribu kumshika kama mtufulani na kumweka katika mpango fulani. Hata hivyo, Yohana alidai kuwa yule wakumtangulia Masihi. Yohana aliwabatiza Wayahudi, jambo la kipekee, kwasababu Wayahudi waliwabatiza waongofu, watu wasio Wayahudi, walioigeukiadini yao ya Kiyahudi. Ubatizo wa Yohana ulikuwa ishara ya kuosha dhambi nakuingia maisha mapya, kwa hiyo, Yohana kwa kufanya ubatizo alikuwa amedaikuwa na mamlaka. Nani amempa mamlaka hiyo? maana hakuipata kwao, walahakuomba idhini yao wala hakuomba wamwie radhi. Jambo hilo liliwasumbuaviongozi wa Kiyahudi.

k.26ku Kwa kusudi Yohana alizidi kuwaelekeza wamwaze Kristo si yeye.Aliwashuhudia kwamba ubatizo wake haukuwa mwisho wa mambo, kwa

Page 24: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA513

sababu, Masihi atakayemfuata ataukamilisha kwa kuwabatiza kwa RohoMtakatifu na watu wataguswa kwa nguvu mioyoni mwao. Halafu Mbatizaji akatoasifa kuu kwa Kristo, hali akijidhili sana, kwa kusema kwamba yeye, iwapo nimtangulizi wake, hastahili kuilegeza gidamu ya kiatu chake, kazi ambayo hatawatumwa hawakutakiwa kufanya kwa waalimu wao.

k.29-34 Ushuhuda wa Mbatizaji hadharani mwa watuInaonekana Yohana ameandika jinsi mambo yalivyotokea siku baada ya sikukatika juma moja. Baada ya kuondoka kwa wajumbe rasmi Yohana kwa wazialitoa tangazo rasmi juu ya Yesu akimshuhudia kuwa „Mwana-kondoo wa Mungu,aichukuaye dhambi ya ulimwengu..‟ Kwa mapema sana katika Injili yake Yohanaameweka neno la Msalaba na maana yake mbele ya wasomaji wake. Yesuamekuja ILI awe dhabihu ya kuondoa dhambi za ulimwengu na kufanyaupatanisho kati ya Mungu na wanadamu. „Mwana-kondoo‟ ni ukumbusho wamengi katika Agano la Kale - Mwanzo 22 (Ibrahimu alipomtoa Isaka) Kutoka12 (Kuokolewa Misri na Pasaka) Isaya 53 (Mtumishi ateswaye) na Taratibu zadhabihu mbalimbali. Yesu ni „Mwana-kondoo‟ wa Mungu.Ameandaliwa na Mungu, ametolewa na Mungu, amekuja kutimiza mapenzi yaMungu katika kuokoa ulimwengu na dhambi. „dhambi ya ulimwengu‟ yaanidhambi yote. „achukuaye‟ Yesu ataibeba dhambi na kuiondoa na kuipelekambali. Nafsini mwake Yesu atachukua laana na hatia na hukumu ya Mungu juuya dhambi.

k.30-34 „mtu nyuma yangu‟ Ilikuwa desturi ya Yohana kuuthibitisha Uungu waYesu, ila hakuusahau ubinadamu wake. Pamoja na kuwaleta watu kwenye tobashabaha ya ubatizo wa Yohana ilikuwa Yesu apate kudhihirika, ili watu watubukwa sababu Masihi yu tayari kutokea.

Yohana alipataje kujua Yesu ni Masihi? Alijulishwa na Mungu kwa njia ya kupewaishara ya kumtambua. „sikumjua‟ kwa maneno hayo wengine hufikiri kwambahapo nyuma Yesu na Yohana hawakufahamiana iwapo walikuwa binamu.Yawezekana sababu ni kwamba Yesu alilelewa na kuishi Galilaya na Yohanaaliishi kusini huko Yudea. Pengine wazazi wa Mbatizaji waliomzaa katika uzeewao walikufa na yeye alitunzwa na jamii ya watu walioitwa Waessene walioishijangwani. Wengine hufikiri kwamba walifahamiana kimwili ila Yohana hakuelewakwamba binamu wake ndiye Masihi. Pengine alitaka kubomoa mawazo ya walewaliosema kwamba wamepatana pamoja kuwadanganya watu.

Bila shaka Yohana alisubiri mpaka ishara aliyopewa itimizwe. Yohana hakuandikahabari ya Yesu kubatizwa na Yohana Mbatizaji (taz.Mt.3:13ku. Mk.1:9ku.Lk.3:21ku.) hata hivyo alisisitiza jinsi Mbatizaji alivyomwona kweli kwa machoyake mwenyewe, si katika maono. Alimwona Roho akishuka juu yake kama hua,wakati Mungu Baba alipomshuhudia Yesu kwa maneno „Huyo ni Mwanangu..‟.Kwa njia hiyo „yule Ajaye‟ akajulikana kwa Yohana ndipo

Page 25: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA514

akaweza kumtangaza Yesu wazi na kwa hakika kuwa Mwana wa Mungu, Mteulewake (Isa.42:1). Kwa tangazo rasmi la Yohana njia iliwekwa tayari kwa Yesukuanza huduma yake.

1:35-51 Wanafunzi wa Mbatizaji kuelekezwa kwa Kristok.35-38 Mambo yafuatayo yalitokea katika siku ya 3 na ya 4 ya juma lile.Tumeambiwa jinsi wanafunzi watano wa Yohana walivyoelekezwa kwa Yesu najinsi walivyoitika. Wa kwanza kutajwa ni Andrea, ambaye ametambulishwa kuwa„nduguye Simoni Petro‟, pamoja na mwingine, ambaye afikiriwa kuwa Yohanamwandishi, ila hakulitaja jina lake. Walikuwa wafuasi wa kwanza wa Yesu (k.37).Kwa mara ya pili Mbatizaji alimwona Yesu akitembea karibu, akamtangaza kwahao wawili waliosimama pamoja naye. Alitumia maneno yale yale ya tangazolake la kwanza (k.29) „Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu‟. Hao wawilihawakuridhika kwa kuyasikia maneno hayo tu, walitaka kujua zaidi, hivyowakamfuata Yesu. Yesu alijihusisha nao kwa urahisi, akageuka na kuwauliza„mnatafuta nini?‟. Yesu alitaka watamke wazi mawazo na nia yao. Twaonakwamba Mbatizaji aliwatia moyo wamfuate Yesu, neno linaloshuhudia jinsialivyokubali kwamba huduma ya Yesu itazidi ya kwake. Haikuwa rahisi, maanaangekosa kuwa na wafuasi wazuri, waaminifu. Kiutendaji alifanya sawa naalivyoshuhudia. Katika kuwaambatanisha na Yesu akina Andrea na wenzakehawakumwasi Mbatizaji, hasa walikuwa waaminifu kwake walipofuata maelekezoyake.

k.39-42 Kwa neema Yesu alijifanya kuwa mwepesi wa kupatikana.Walipomwuliza „unakaa wapi? akawaita „Njoni nanyi mtaona‟. Hivyo walipatanafasi ya kuzungumza pamoja naye. Ijapokuwa Yohana hakusema waliongeajuu ya nini, ila kwa jinsi Andrea alivyofanya mbio kumwendea ndugu yake Simonina kusema „Tumemwona Masihi‟ inaonekana kwamba mazungumzo yaoyalihusu madai ya Yesu kuwa Masihi, madai yaliyojengwa juu ya Maandiko.Andrea aliamini kabisa kwamba Yesu ni Masihi, alisikia msukumo wa kumtafutandugu yake na kumleta kwa Yesu. Simoni alikuwa na tabia ya kusema kwaharaka, mtu asiye na msimamo. Yesu alipokutana naye akamtazama kamaanamchunguza kwa ndani ndipo alimwambia kwamba mabadiliko yatatokeakatika tabia yake, atageuka kuwa mtu thabiti, mtu wa kutegemewa, kamamwamba. Yesu akabadili jina lake liwe Kefa (Kiebrania) Petro (Kiyunani) maanayake Jiwe/Mwamba. Ni Yesu atakayemfanya kuwa Mwamba. Maneno„tumemwona Masihi‟ yametatiza wengine, kwa sababu, tunaposoma Injiliinaonekana Mitume walikuwa wazito wa kumwelewa Yesu mpaka baadaye sanakatika huduma yake. Pengine shida yao haikuwa katika kumkubali Yesu kuwaMasihi ila katika kukubali aina ya Umasihi wake alipowafunulia kwamba Yeye niMtumishi Ateswaye na itampasa afe (taz. Mt.16:21ku). Habari ya siku ile ilikaamuda mrefu akilini mwa Yohana hata kiasi cha kukumbuka saa yake (k.39).

Page 26: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA515

k.43-51 Baada ya habari za Andrea, Yohana, na Petro kukutana na Yesu,tunapewa habari jinsi wengine wawili walivyopata kukutana naye. Filipo naNathanaeli. Siku iliyofuata ile ya kuzungumza na Petro Yesu alikuwa tayarikuondoka kusini na kuelekea kaskazini kwenda Galilaya. Twasoma alimwonaFilipo na kumwambia „Nifuate‟. (hatuambiwi mahali walipokuwa). Katika Injili,mara kwa mara Filipo aonekana kama mtu mzito, asiyejua la kufanya (Yn.6:7;12:21; 14:8ku) labda alikuwa na uwezo wa wastani. Alitoka Bethsaida mji waAndrea na Petro.

Filipo alifanana na Andrea katika kumleta mwenzake Nathanaeli kwa Yesu. Kwajinsi alivyosema naye alionyesha ufahamu wa habari za Masihi zilizoandikwakatika Agano la Kale. Nathanaeli aliitikaje ushuhuda wa Filipo? Akamjibu kwakuonyesha dharau kwa mji wa Nazareti „laweza neno jema kutoka Nazareti?‟Alikuwa na mawazo makuu juu ya Masihi, na mawazo hayo hayakumruhusuakubali kwamba Masihi atoka Nazareti. Aliwaza kwamba si mji ufaao kwa Masihikutoka huko. Haukuwa na historia yoyote kuhusu utendaji wa Mungu katikazamani zilizopita. Shida ya Nathanaeli, ambayo ni shida ya watu wengi, nikwamba alikuwa amekomaa katika mawazo yake na alisikia shida mamboyalipotokea tofauti na matazamio yake. Filipo alitumia busara, hakubishana naye,bali akamwita „njoo uone‟. Twaona unyenyekevu wa Yesu katika kukubali kuitwa„mtu wa Nazareti‟. Ijapokuwa alizaliwa katika mji wa Bethlehemu, mwenye sifa yaDaudi, Mfalme Mkuu, tena ni mji uliotabiriwa katika Agano la Kale kuwa MjiAtakapotoka Masihi, Yesu hakuona jambo hilo ni la kushikilia. Alilelewa Nazareti,aliridhika kuitwa Mnazareti.

k.47 Itakuwaje Nathanaeli atakapokutana na Yesu? Yesu alielewa tabia na niaya Nathanaeli. Alijua ni mtu mnyofu, mtu asiye na hila. Mtu mwenye mzigo juu yataifa lake na mwenye tumaini la kupata Masihi. Nathanaeli alijua kwambawametokea wadanganyifu wengi waliodai kuwa Masihi, hakutaka kudanganywa.Nathanaeli alishtuka Yesu alipomfunulia kwamba alijua alikuwa amepumzikawapi na kuwaza nini. Alipokuwa chini ya mtini, hali akifikiri hakuna aliyemwona,kumbe! Yesu alimwona. Licha ya kumwona kimwili, alielewa na mawazo yake.Alijua alikuwa akitakafari habari za Yakobo na ono la ngazi (Mwa.28). Mara mojaNathanaeli akamkiri Yesu kuwa Masihi, Mwana wa Mungu, na Mfalme wa Israeli.Yesu alishinda vipingamizi vyake vyote vya kimawazo kwa kumwambia„nilikuona‟. Ila Yesu hakutaka Nathanaeli aridhike na ufahamu huo juu yake,alimpa changamoto kwamba yeye na wenzake wataona mbingu zimefunguka, namalaika wa Mungu wakikwea na kushuka juu yake. Yesu amekuja ili amfunueMungu kwa ukamilifu na kufanya upatanisho kati yake na wanadamu.Watakapoendelea kuandamana naye wataona ishara zitakazoashiria uwezowake na hasa uhusiano wake wa ukaribu sana na Baba yake. Yesu ni „ngazi‟ yakumleta Mungu karibu na watu na watu karibu na Mungu (Yn.14:6 „Mimi ni Njia....‟).

Page 27: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA516

k.51 Yesu alitanguliza maneno hayo kwa kusema „Amin, amin, nawaambia‟.Alitumia usemi huo sana, kama mara 25. Hasa aliutumia alipotaka kutamka nenokubwa, ukweli wa maana sana. Ni kama kutilia mkazo na uzito, kusudi avuteusikivu wa watu ili wayajali matamko yake. „Mwana wa Adamu‟ ni jina ambaloBwana Yesu alipenda kujiita. Katika Dan.7:13-14 ametajwa „Mwana wa Adamu‟ambaye atatokea mwisho wa dahari. Yeye atapewa mamlaka juu ya mataifa yote.Bila shaka Yesu alikuwa akimwaza huyo alipojitwalia Jina hilo.

Ni Injili ya Yohana tu ambayo ina habari za Nathanaeli. Katika Injili tatu hatajwi,ila mwingine ametajwa, ambaye Yohana hamtaji, jina lake Bartholomayo.Aliwekwa pamoja na Filipo (Mt.10:3; Mk.3:8; Lk.6:4). Kwa hiyo, yafikiriwakwamba hao wawili ni mtu mmoja mwenye majina hayo mawili. Kama sivyo,huenda Nathanaeli hakuitwa kuwa Mtume bali alikuwa katika kundi la wenginewaliomfuata.

MASWALI1. Ni jambo gani lililowatatiza viongozi wa dini walipokwenda kumhoji

Yohana Mbatizaji?2. Mbatizaji alisemaji alipomtangaza Kristo? kwa maneno hayo aliashiria nini

kuhusu Kristo na kazi yake?3. Ni akina nani waliomsikia Mbatizaji alipotangaza hadharani habari za

Kristo? na ilitokea nini kwa upande wao?

2:1-12 Arusi huko Kana ya GalilayaHabari hii ni ya kwanza baada ya Yesu kuondoka kusini, huenda ni siku ya sabakatika mfuatano wa siku zilizotajwa 1:35ku. na ya tatu baada ya Filipo naNathanaeli kuitwa na Yesu. Kana, mji wa Galilaya umetajwa tena 4:46; 21:2.Mwujiza wa kugeuza maji yawe divai ulikuwa wa kwanza na kama tulivyoonakatika utangulizi miujiza kwa Yohana ni ishara za kuashiria nafsi na cheo chaYesu.

k.1-3 Inaonekana arusi hii ilikuwa katika jamaa ya Mariamu kwa sababu yeyepamoja na Yesu na wanafunzi wake (wale watano wa sura ya 1) walialikwa. TenaMariamu alihusika katika maandalio. Katika mila ya Kiyahudi arusi iliendelea kwajuma moja na jambo moja kubwa lilikuwa kuandaa chakula na kinywaji chakutosha kwa wageni wote watakaofika. Kutindikiwa divai kulileta aibu sana,lilihesabiwa tusi na kosa la kutotimiza wajibu wa ukaribishaji wa wageni, hatamara nyingine watu waliwashtaki wahusika barazani.

k.4-6 Mamaye Yesu alifahamu shida iliyokuwapo. Pia, alielewa kwambamwana wake ni tofauti na wengine. Wala si ajabu, kwa sababu, alijua jinsimambo yalivyotokea wakati wa kuzaliwa kwake, na jinsi watu kama walewazee, Simeoni na Ana walivyosema juu yake, pamoja na jinsi mamboyalivyotokea walipokwenda hekaluni alipokuwa na umri wa miaka kumi na

Page 28: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA517

miwili. Alikuwa amemtegemea katika maisha ya nyumbani (yadhaniwa Yusufualikufa mapema na Yesu aliwajibika kuwasaidia). Hayo yote alikuwaameyazingatia kwa muda mrefu. Kwa hiyo, ilipotokea shida ya kutindikiwa divai,hakusita, akamwendea Yesu na kumwambia „Hawana divai‟. Hivyo alionyeshakwamba aliamini kwamba Yesu anao uwezo wa kuwasaidia. Yesu akamjibumamaye kwa maneno baridi na ya fumbo. Katika Kigriki neno „mama‟ ni lile la„mwanamke‟ kwa hiyo, ni kama Yesu alitaka kupunguza „joto‟ katika uhusianowao, kuweka masafa kati yao. Pia, „tuna nini mimi nawe?‟ ni maneno yakumweka mama chini yake. Kwa kimwili ni mama, ila tangu wakati huo wakuanza kwa huduma yake mpaka itakapotimia pale Msalabani, uhusiano waohautakuwapo kama hapo mwanzo (Mt.12:46-50). Hataongozwa na kushauriwana kusukumwa na mama, ila mwongozo utatoka kwa Baba, atafanya mapenziyake tu (5:30; 8:29). Haina maana kwamba mama anataka kupinga mapenzi yaBabake, ila hajaelewa yaliyomo katika mapenzi hayo.

„Saa yangu haijawadia‟ Mara kwa mara katika Injili hiyo twakuta maneno kuhusu„saa‟. Hiyo saa ni saa ipi? Ni saa ya kuitimiza ile kazi ya kuukomboa ulimwengupale Msalabani, kazi ambayo kwa ajili yake alikuja ulimwenguni. Saa hiyo ilizidikukaribia kadiri alivyoendelea na huduma (7:6,8,30; 8:20; 13:1,23,27; 16:32;17:1).

Mama alinyenyekea, hakumjibu, ila katika hali ya kuamini alimwachia Yesuafanye alivyoona kuwa vema. Mariamu akawageukia watumishi na kuwaambia„lolote atakalowaambia, fanyeni‟. Kwa kifupi, mtii Yeye. Katika Agano Jipyatunayo maneno machache ya Mariamu, na maneno hayo aliyosema wakati huoyana maana kwa waumini wote, alisema kama mwumini si kama mama.

k.7-10 Kwa desturi ya Kiyahudi maji yalitunzwa katika mabalasi, kwa kuwawalitumia maji mengi kwa maosho mbalimbali, kwa kutawadha miguu, na kwamatumizi ya kawaida. Katika mabalasi sita maji yalikuwa mengi mno, ya kutoshakwa watu wengi. Ili isiwepo nafasi ya udanganyifu kusudi iwe dhahiri kwambamwujiza ulifanyika kweli Yesu hakufanya lolote ila kuwaagiza watumishi tu.Hatusomi kwamba aliomba, au aliyabariki maji, ila alisema „Jalizeni mabalasimaji‟. Watumishi walijua hakika kwamba mabalasi yote sita yalijaa maji.Walipoteka na kupeleka kwa mkuu wa meza ambaye hakujua lolote la jikoni majiyakawa divai. Ushuhuda wa mkuu wa meza ni muhimu, ni yeye aliyeionja divai,akashuhudia uzuri wake. Tukumbuke kwamba mwandishi Yohana alikuwepo nakuyajua hayo.

Ushuhuda wa mkuu wa meza ulithibitisha kwamba mwujiza umefanyika, mwujizaambao ulizidi matazamio ya wahusika wote. Bila shaka wale wote waliojua hiyoshida walipumua vizuri sana, aibu yao iliondolewa, na wote waliifurahia hiyodivai. Hayo yote yaliashiria uwezo wa Yesu kutosheleza maisha ya wanadamuna kuyajaza na mibaraka yake ya kweli.

Page 29: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA518

Pamoja na hayo twaweza kuutafsiri mwujiza huo kuwa ishara ya kufika kwamwisho wa kuishi chini ya sheria ambayo dini ya Kiyahudi ilisimamia (ambayoimetindika) na mwanzo wa Injili, watu kuishi chini ya neema, katika uhusiano wakibinafsi na Yesu. Injili huleta utoshelevu wa maisha kwa wote wamtiio Yesu.

k.11 Maana kuu ya mwujiza huo ni katika tokeo la wanafunzi wake kumwamini.Kwa kuwepo pamoja naye na kwa kuona uwezo wake wa kubadili maji yawedivai, kwa agizo tu, walianza kuelewa kwamba Huyo ametumwa na Mungu, anaouhusiano wa kipekee na Baba. Imani hii ilihitaji kukua, ila kwa mwujiza huo Yesuameanza kuyathibitisha madai yake ya kuwa Masihi, Mwana wa Mungu. Piaaliwaelekeza mawazo yao ili watambue kwamba Yeye amejaa huruma naatatenda makuu katika hali ya kuwahurumia watu. Mpaka hapa wamemtazamiaMasihi wa siasa atakayewafukuza adui zao Warumi. Polepole, hatua kwa hatua,kwa kushirikiana na Yesu, mawazo yao yalisahihishwa.

k.12 Halafu Yesu, na mama, na ndugu zake, na wanafunzi wake, wote walishukampaka Kapernaumu na kuishi pale kwa muda. Inaonekana kwamba Yesualiweka kituo chake pale (Mt.9:1).

2:13-25 Yesu alitokea kwa mara ya kwanza huko Yerusalemu na kulitakasahekaluk.13-22 Mwandishi ametaja Pasaka tatu au nne (4 ikiwa Sikukuu ya 5:1 ilikuwaPasaka) 2:13; 6:4; 11:55; 12:1; 13:1; 18:28, 39; 19:14). Pengine alikuwa nashabaha ya kuvuta wasomaji wamwone Yesu kama Mkombozi Mkuu aliye MwanaKondoo wa Pasaka, yule wa kuwaokoa watu na dhambi zao (Kum.16:16).

Nabii Malaki alitabiri kwamba Masihi atakuja kwa ghafula kwa hekalu (Mal.3:1-3). Yesu alishuka kutoka Galilaya ili aiadhimishe Sikukuu hiyo kubwa yaWayahudi. Tumeishaona kwamba wanafunzi wake ambao walikuwa wanafunziwa Mbatizaji kabla ya kumfuata Yeye wameanza kumwamini na imani yaoilijengwa walipokuwa huko Kana na kuona ishara ya maji kugeuzwa kuwa divai.Mara kwa mara mwandishi ameonyesha hao „Wayahudi‟ wa kusini kuwa watuwenye uadui juu ya Yesu, wakimwonea shaka na wivu. Hali hizo zilionekana wazikatika habari hii ya Yesu kulitakasa hekalu.

k.14 Ni kitu gani kilichomsukuma Yesu alitakase hekalu? aliona kitu ganikilichomchukiza hata achukue hatua hiyo na kufanya tendo la nguvu na hasiranamna hiyo? Hekalu lilikuwa na sehemu nyingi, lilikuwa na ua mbalimbali, ua wawanawake, ua wa WaMataifa, ua wa makuhani, na jengo lililoitwa Patakatifu paPatakatifu ambapo Kuhani Mkuu peke yake aliruhusiwa kuingia mara moja kwamwaka. Yafikiriwa biashara ya kuuza ng‟ombe n.k. na shughuli ya kuvunja fedhazilifanyika katika ua wa WaMataifa. Yesu alionyesha sababu mojawapo

Page 30: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA519

kwa tendo lake katika maneno „msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumbaya biashara‟. Hekalu lilikuwa mahali pa ibada, si mahali pa biashara. Ilikuwajebiashara ilifanyika katika eneo la hekalu? Kwa upande mmoja biashara hiyoilikuwa msaada na huduma kwa wale waliotoka mbali. Kuleta mnyama wasadaka kutoka mbali mpaka Yerusalemu kuliongeza uzito wa safari. Ikiwa njianimnyama alijeruhiwa au kuugua basi, hakufaa kuwa sadaka, ndipo ikawabidiwanunue mwingine. Kuhusu mambo ya pesa, pesa za kipekee zilitumikahekaluni, na hizo zilipatikana tu pale Yerusalemu. Katika mambo hayo yoteilikuwa rahisi kwa dhuluma kuingia. Mara nyingi wanyama wa watu walikataliwa,kwa hiyo, iliwabidi wanunue kwa hao wauzaji waliokuwapo. Mara nyingi bei zawanyama, na njiwa, zilipanda juu, na waabudu hawakuwa na la kufanyaisipokuwa kuwanunua kwa sababu walitakiwa wawe na mnyama kwa sadaka.Hata katika kuvunja pesa ilikuwa rahisi wadhulumiwe. Yesu hakutaja dhulumakuwa kitu kilichomsukuma alitakase hekalu. Zaidi ya yote Yesu alichukizwa kwakuona mahali pa ibada pamevurugika, mtu atamwabuduje Mungu kwa amani nautulivu kati ya kelele za biashara? Ikiwa hayo yote yalifanyika katika ua laWaMataifa, WaMataifa watasaidiwaje na kuvutwa kumwabudu Mungu wakweli? Watakuwa na dhambi ya ubaguzi wa kabila. Ni kama wakuu wame‟uza‟urithi wao wa kiroho na kufanya hekalu kuwa „soko‟.

k.14ku Tendo la Yesu lilikuwa la nguvu na la hasira. Aliweza kuwatoa watu nawanyama ila hatusomi kwamba aliwaumiza watu au wanyama. Kwa njiwaalionyesha huruma akijua akiwafukuza kwa nguvu wataruka na kupotea. Je!alikasirika vibaya? La, sivyo. Alifanya kwa kusudi, hakuwaka hasira ya haraka,alikuwa amechunguza hali zilizopo. Ipo hasira iliyo dhambi, ipo hasira isiyodhambi. Inategemea kama hasira imetawaliwa, na zaidi ni hasira kwa ajili ya nini.Mara nyingi sisi wanadamu twayakasirikia yale yasiyo haki tuyakasirikie natunakosa kuyakasirikia yale yaliyo haki kuyakasirikia. Vilevile na wivu, upo wivumbaya, na upo wivu mzuri. Wivu wa Yesu ulihusu heshima ya nyumba ya BabaYake, nyumba ya ibada kwa watu wote, nyumba takatifu.

Neno lililowachukiza Wayahudi lilikuwa Yesu kufanya bila ruhusa yao kama mtualiye na mamlaka yake mwenyewe. Aliliita hekalu „nyumba ya Baba yangu‟.Maneno hayo yaliwachokoza Wayahudi kwa sababu kwa maneno hayo Yesualidai kuwa na uhusiano wa kipekee na Mungu na kuwa na mamlaka juu yahekalu kiasi cha kuweza kufanya tendo hilo bila kuomba ruksa wala kuombaradhi kwao. Hivyo alikuwa ametoa changamoto kwao. Wanafunzi walikumbukamaneno ya Maandiko „wivu wa nyumba yako utanila‟ (Zab.69:9). Wayahudihawakuwa tayari kukabili swala la kuhusu kosa lao la kutokumheshimu Mungukatika ibada zao. Ila walitaka wapewe ishara ya kuthibitisha haki na mamlaka yaYesu kwa tendo hilo. (kwa kuomba ishara Je! walimwaza Yesu kuwa nabii?).Ndipo Yesu akaitika kwa kuwapa changamoto nyingine, „Livunjeni hekalu hili,nami katika siku tatu nitalisimamisha‟. Yawezekana alipokuwa akisema manenohayo alijinyoshea kidole mwilini mwake. Hawakumwelewa vizuri, walidhaniamelisemea jengo la hekalu la pale walipo. Wakaona haitawezekana yeye

Page 31: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA520

alibomoe na kulijenga upya, wakamdharau, ila maneno hayo yaliwasumbua sananayo yalikaa katika mawazo yao mpaka wakayataja wakati wa kumhukumu Yesu(Mt.26:6). Wanafunzi hawakuelewa maana ya maneno hayo mpaka Yesualipofufuka ndipo wakaielewa, wakajengwa katika imani yao.

k.21-22 Yohana alifafanua maana ya maneno ya Yesu „livunjeni hekalu hili, namikatika siku tatu nitalisimamisha‟? Katika Kigriki neno „livunjeni‟ lina maana yakulegeza, kufungua, kuachisha. Yeye ndiye Hekalu, nao watalivunjawatakapomwua, ndipo katika siku ya tatu atafufuka kutoka wafu. Yesu alikuwaametazama mbele kwa ibada „katika Roho Mtakatifu‟ ndipo ibada yoteitatengenezwa upya, ikijengwa juu yake na upatanisho wake. (Yn.4:21-24). Ibadayote ya kweli itapitia kwake, „Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima, mtu haji kwaBaba ila kwa mimi‟ (Yn.14:6). Mwili wake utakapovunjwa pale Msalabani dhabihukamili, na ya kutosha, kwa dhambi za ulimwengu wote itakuwa imetolewa nakupokelewa na Baba yake, ndipo haitakuwepo tena haja ya hekalu lao au jengololote au kuhani yeyote, au sadaka yoyote. Ndiyo sababu alipokufa pazia lahekalu lilipasuka kutoka juu, ishara ya kuwa Yesu amepasua njia ya kumwendeaBaba. Mipango yote ya Mungu na mapenzi yake yote, yalikuwa juu yake. Dini yaKiyahudi itakuwa imekwisha, haina kazi tena, hata twaweza kusema ni „mwisho‟wa „dini‟.

k.23-25 Hapo Yohana ametoa habari ya maitikio ya watu kwa huduma ya Yesupale Yerusalemu. Tumeishaona itikio la „Wayahudi‟ kundi la wale waliochukizwana tendo hilo la Yesu. Walikuwapo watu ambao waliunga mkono tendo hilo,walifurahi kwamba Yesu amechukua hatua hiyo ya kurudisha hekalu katika haliya kufaa kwa ibada. Wakati huo wa kuwa kuwapo pale Yerusalemu Yesu alifanyamiujiza mingine ila hatuambiwi ilikuwa ya namna gani. Yohana alisema kwambawatu walimwamini Yesu kwa ajili ya hiyo miujiza. Lakini mwandishi alifafanuazaidi juu ya imani yao na jinsi Yesu alivyoipima. Alisema Yesu „hakujiaminishakwao‟ maana yake hakuona hiyo imani ni imara na ya kutegemewa, ni kamaimani ya juujuu. Itakuwaje atakapowaambia mambo magumu? watafanyajewakati wa wengi kuchukizwa na kumwacha? watasemaje atakapokataakusimikwa kuwa Mfalme wao wa kuwaondoa Warumi? Yesu alikuwa na hekimaya kutokuweka tumaini lake katika watu ambao, kwa ajili ya miujiza,wamemwamini. Alijua wanadamu ni wenye dhambi, mioyo yao ni hafifu, ujuzi huoalipata kutokana na ushirikiano wa ukaribu sana na Babake. Hakuwezakudanganywa na sifa za watu (8:28, 38; 14:10; Yer.17:10). Ijapokuwa hawezikutuamini kwa sababu tu wenye dhambi, hata hivyo, anao mzigo mkubwa juuyetu.

Kujibu kwa fumbo kulimsaidia Yesu aendelee na huduma yake. Hakutakakuwalazimisha watu wamwamini kinyume cha nia yao.

Katika habari hii ya kulitakasa hekalu Yesu alitoa kauli yake juu ya mamlakayake na utume wake na kuonyesha kwamba kwa Kuja Kwake dini ya Kiyahudi

Page 32: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA521

imefikishwa kwenye njia panda. Ama wamkubali afanye marekebisho nakutakasa ibada yao na taifa lao; la, sivyo, watakuta wamefilisika na Munguataweka wengine mahali pao.

MASWALI1. Wanafunzi walijifunza nini juu ya Yesu kutokana na Mwujiza aliofanya pale

Kana?2. Kwa nini Yesu alilitakasa hekalu?3. Yesu alionyesha mamlaka juu ya mambo gani?4. Kwa nini wakuu walichukizwa na maneno „nyumba ya Baba yangu?‟ Kwa

maneno hayo Yesu alionyesha nini?5. Yesu alikuwa na maana gani aliposema „livunjeni hekalu hili, nami katika

siku tatu nitalisimamisha‟?6. Habari hiyo inatufundisha nini kuhusu ibada ya leo?7. Je! Hasira yote ni dhambi? Eleza. Katika vikundi zungumza ni mambo gani

katika Kanisa ambayo mnadhani kwamba Yesu anasikia hasira juu yake.

3: 1-21 Mazungumzo ya Yesu na NikodemoKatika 2:25 Yesu alisema kwamba alifahamu „yaliyomo ndani ya mwanadamu‟.Kuanzia sura ya tatu tunazo habari za mazungumzo yake na watu mbalimbali,Nikodemo, Mwanamke Msamaria, Diwani Mmataifa na Mgonjwa penye Birika.Katika habari hizo twaweza kuona ujuzi huo wa Yesu na jinsi alivyojihusisha nawatu mbalimbali na kuwagusa sana mioyoni mwao.

k.1-2 Nikodemo alikuwa Farisayo mwenye mzigo juu ya Torati na mwangalifusana katika kuyashika maagizo yake. Alikuwa kiongozi katika taifa lake namjumbe katika Sanhedrin, Baraza Kuu la Wayahudi. Afikiriwa kuwa tajiri,alimsaidia Yusufu wakati wa kumzika Yesu, na kwa jinsi alivyotaja mzee katikamazungumzo hayo pengine alikuwa mzee (Yn.7:50; 19:39) Yesu alitazamiakwamba Nikodemo ataelewa mambo aliyoyasema kwa kuwa alikuwa mwalimumashuhuri katika Israeli (k.10).

Alimjia Yesu usiku, mwandishi hakusema sababu yake, kwa hiyo, watu wametoasababu mbalimbali:(a) alitaka kuzungumza na Yesu kwa utulivu bila kuangalia saa wala watu(b) marabi walizoea kusoma na kujadili usiku(c) alihofu jinsi watu watakavyomwazia, haikuwa rahisi kwa mkubwa katika

jamii kumwendea Yesu kwa wazi(d) alitaka kumchunguza Yesu na madai yake kwa siri kabla ya kukata

shauri la kumkubali au kumkataa mbele za watu(e) labda yeye au Yesu au wote wawili walishindwa kupata nafasi nzuri

wakati wa mchana, kwa sababu wote wawili walikuwa watu wa shughuli.Mwandishi Yohana alipenda sana kupambanua kati ya giza na nuru kwahiyo aliona vema ataje kwamba Nikodemo alimjia Yesu usiku.

Page 33: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA522

Alimjia Yesu kwa heshima na adabu akimkiri kuwa Rabi kama yeye. Aliongezakusema kwamba aliamini kwamba Yesu alitoka kwa Mungu kwa sababu yauwezo wake wa kufanya ishara mbalimbali. Alionekana mtu wa kutafakarimambo maana alisema kwamba mtu asingaliweza kuzifanya ishara hizo bilaMungu kuwa pamoja naye (hatujui kama aliziona ishara hizo au amesikia habarizake tu). Sifa hizo zilikuwa za kweli kabisa, ila hatujui kama alikuwa akimpakamafuta, au siyo. Hata hivyo, Nikodemo alikuwa na upungufu katika ufahamuwake juu ya Yesu. Yesu ni zaidi ya mwalimu, ni Masihi na Mwana wa Mungu.

k.3 Yesu akamjibu kwa ajabu na kwa kumshtua. Hakujali sifa alizopewa, ila mojakwa moja, na kwa maneno ya mkato, alimwambia juu ya kuzaliwa kwa mara yapili. Hakuingia mazungumzo ya mzunguko ila aligusa habari za Ufalme waMungu na jinsi mtu atakavyoweza kuutambua na kuuingia. Tena, alitangulizatamko lake kwa maneno ya kutilia mkazo na uzito „Amin, amin‟. Tamko hilolilibomoa tegemeo lote la Nikodemo katika dini yake. „Mtu asipozaliwa mara yapili.....‟ Si kwamba mtu amekataliwa ila mtu hawezi sawa na jinsi kipofuasivyoweza kuliona jua kuchwa na kukwea. Kipofu hakataliwi asilione jua ilahaiwezekani kwa hali yake ya upofu. Ndivyo ilivyo kwa mwanadamu awaye yote,mtu wa dini na mtu asiye na dini, potelea mbali amezaliwa Myahudi au Mmataifa,mweupe au mweusi, mwungwana au mtumwa, tajiri au maskini. Kuzaliwa kwamara ya pili ni sawa na kuzaliwa kwa mtoto mchanga. Mtu huingia katika jamiiya wanadamu kwa njia ya kuzaliwa, lakini hawi mtoto wa Mungu. Vilevile mtuhuingia katika jamii ya Mungu kwa kuzaliwa na Mungu, ahitaji maisha mapyakutoka kwa Roho. Mtoto mchanga anapozaliwa apewa yote yafaayo kwa maishayake mapya kama mwanadamu. Ndivyo ilivyo kwa mtu anayezaliwa kwa mara yapili, apewa yote ili aishi maisha ya kiroho, maisha ya mshiriki wa Ufalme waMungu. Hivyo Yesu alibadili msingi wa mazungumzo yao. Badala ya kumpimaYesu na kumfikiria kuwa nani, swala la maana ni juu ya Nikodemo kufanya nini iliawe tayari kumpokea Masihi.

k.4 Nikodemo alionyesha jinsi alivyoshindwa kuelewa jambo hilo kwa sababualimwuliza Yesu „Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee?‟ „Aweza kuingia tumbonimwa mamaye mara ya pili akazaliwa?‟. Hatujui kama Nikodemo aliwaza kuzaliwakimwili tena au vipi. Iliyo wazi ni kwamba hakuweza kupokea jambo la maishamapya, ni geni kabisa kwake, hakuweza kukubali kwamba yalihitajika (k.7) walahakuliamini (k.12). Kama Myahudi safi alifikiri kwamba mahali pake katika Ufalmewa Mungu palikuwa salama; alizaliwa katika taifa teule, alitahiriwa, alifuatamasharti ya Torati na kutimiza wajibu wake, kwa hiyo, kuambiwa aanze upya,kulimshtua na kumshangaza kabisa.

k.5 Yesu akamjibu kwa kurudia kusema „Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Rohohawezi kuuingia Ufalme wa Mungu‟ akiyatanguliza maneno ya kutilia mkazo„Amin, amin, nakuambia‟. Maneno „kwa maji na kwa Roho‟ yametatiza wengi.Hayahusu ubatizo wa Kikristo kwa sababu wakati wa mazungumzo hayo

Page 34: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA523

huo ubatizo haukujulikana, na ni wazi kwamba Yesu alitazamia Nikodemoatafahamu hilo jambo. Wengine wafikiri kwamba Yesu alimrudisha kwa hudumaya Yohana Mbatizaji aliyebatiza kwa maji, ubatizo wa toba. Jambo hilo lilikuwagumu kwa Nikodemo, maana Wayahudi hawakubatizwa, ila waliwabatizawaongofu, watu wa Mataifa walioigeukia dini yao. Kumwambia Farisayo kwambaalihitaji kutubu na kushuka mpaka Mto Yordani na kuingia majini sawa naMmataifa kulimkwaza. WaMataifa walifikiriwa kuwa wanajisi.

Mambo ambayo Nikodemo aliyafahamu akiwa mwalimu katika Israeli ni mamboya Agano la Kale. Katika Agano la Kale, Nabii Ezekieli alitoa unabii juu yawakati ambapo Mungu atawatakasa watu wake na kuwahuisha na Roho wake.„Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi, nitawatakaseni na uchafuwenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndaniya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu....‟(Eze.36:25-27). Ndipo katika Ezekieli 37 nabii alitabiri juu ya mifupa iliyokaukandipo ikahuishwa. Pamoja na Ezekieli manabii wengine walitabiri mambo kamahayo ((Hes.19:17-19; Zab.51:9-10; Isa.32:15; 44:3-5; 55:1-3; Yer.2:13, 17;Eze.14:7-9; Yoe.2:28-29; Zek.14:8).Yeremia alitaja „moyo mpya‟ (Yer.31:29ku). Manabii walisema juu ya Taifa laIsraeli kutakaswa na kufanywa upya na Nikodemo alikuwa amekosakuyazingatia hivyo. Kwa hiyo, maana ya Yesu ya kuzaliwa kwa maji na kwaRoho ni kwamba kila mtu aingiapo Ufalme wa Mungu lazima atakaswe nakuhuishwa na Roho wa Mungu. Mtu mwenyewe hawezi kujitengeneza nakujiokoa. Kwanza iwe kwamba Mungu amefanya kazi maishani mwake, na kazihiyo itawezekana kwa sababu Yesu atakufa kwa ajili ya wenye dhambi (k.14ku).

k.6 Kwa maneno mepesi ya kufahamika Yesu aliendelea „kilichozaliwa kwa mwilini mwili, na kilichozaliwa kwa Roho ni roho‟. Jambo hilo ni lile lililotajwa haponyuma 1:12-14.

k.7 Yesu alirudia kusisitiza jambo la kuzaliwa kwa mara ya pili kwa kuonyeshakwamba ni jambo lisilo na hoja. „hamna budi‟ - hamna njia nyingine ya kuuingiaUfalme wa Mungu.

k.8 Yesu aliutumia mfano wa upepo na kufananisha Roho na kazi yake naupepo. Matokeo ya kuvuma kwa upepo yaonekana ila upepo wenyewehauonekani, haushikiki wala mwendo wake haujulikani. Upepo ni kitu ambachohatuna madaraka juu yake, ila ni kitu cha kweli. Ijapokuwa hatuelewi upepo, hatahivyo, hatukani kuwepo kwake. Twaona kazi zake hivyo twaukubali kwambaupepo upo. Vivyo hivyo na hali ya mtu aliyezaliwa kwa Roho, twaona kazi yakemaishani mwake.

k.9 Nikodemo alikuwa bado hajaelewa vema. „Yawezaje kuwa mambo hayo?‟yawezekana amefika hatua ya kutaka jambo hilo litimizwe maishani mwake na

Page 35: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA524

swali lake ni kama ombi la kujua kazi ya Roho maishani mwake ili azaliwe maraya pili.

k.10-13 Hapo twaona kama Yesu alimkemea Nikodemo. Ameshangazwa na haliya kutokuelewa kwake kwa sababu alikuwa mwalimu katika Israeli, mtualiyewafundisha wengine, na kwa jinsi alivyosema Yesu inaonekana alikuwamiongoni mwa waalimu mashuhuri. Yesu alisita katika kumwambia zaidi, kamaameshindwa kuelewa mambo ambayo yaweza kuelezwa kwa mifano ya dunia(kama kuzaliwa upya, kwa sababu ni jambo linalotokea hapa duniani) itakuwajeatakapoambiwa mambo yasiyo na mfano wake hapa duniani. Ni Yesu tu aliye naufahamu wa mambo ya mbinguni, Yeye ndiye yule wa kuunganisha mbinguni naduniani, ni Yeye aliyeshuka kutoka mbinguni mwenye ufahamu kamili wakuwafunulia wakaao duniani. Hakuna mwanadamu aliyepanda juu na kujuamambo ya mbinguni, kisha akashuka na kuleta habari zake. Mambo ya mbingunini mambo gani? Pengine ni mpango wa Mungu wa kuukomboa ulimwengu. Yuleanayejua na kuhusika na mpango huo ni Yeye aliyekuwa akisema na Nikodemo!Pia mambo ya baadaye ni yale yatakayotokea Ufalme wa Munguutakapotimizwa, wakati wa mbingu mpya na dunia mpya kutokea. Licha yakufahamu, Nikodemo hakumwamini wala hakumtambua Yesu ni nani.

k.14-15 Ndipo Yesu alitumia Maandiko Matakatifu na habari za Nyoka wa Shabaaliyeinuliwa jangwani wakati wa uasi wa Waisraeli (Hes.21:8ku). Hapo Yesualisemea mambo yake Mwenyewe jinsi atakavyosulibiwa ili kila mtu amwaminiyeawe na uzima wa milele. Waisraeli walipomwasi Mungu, walipatwa na hukumuya kuumwa na nyoka. Watu wakafa (mshahara wa dhambi ni mauti). WakamliliaMungu awaokoe. Mungu akamwagiza Musa afanye nyoka wa shaba na kuiwekajuu ya mti. Halafu watu waliambiwa waitazame hiyo nyoka wa shaba mtini iliwapate kuishi. Ndivyo ilivyotokea. Wale walioliamini neno la Musa na kuitazamanyoka ya shaba walipona. Waliodhihaki, na wale wote waliokataa kuitazama,basi, wakafa. Walioamini waliuthibitisha ukweli wa imani yao walipoitazama hiyonyoka ya shaba. Watu walipona kwa sababu gani? Kwa sababu walimtii Munguna kukubali njia yake ya kuwaokoa, ijapokuwa ilionekana ni upuzi mtupukutazama kitu cha shaba. Kwa neema ya Mungu na uwezo wake, Mungualiwaokoa wale waliotii amri yake. Watu hawakufanya lolote ila kutazama tu.Waliamini na kutii na kwa sababu hizo waliunganishwa na uwezo wa Mungu, nauwezo huo ndio uliowaokoa.

Yesu alikuwa akitabiri Kufa Kwake Msalabani, atakapoinuliwa juu, atafanana nanyoka wa shaba, ndipo kila atakayeweka tumaini lake katika Kifo chakeatashirikishwa uzima wa Kristo (8:28; 12:32-34). Wote ambao hawatakubalikumpokea Kristo watahukumiwa na Mungu kwa dhambi zao. Kwa hiyo ni wazikwamba tangu mwanzo Yesu alijua ni kitu gani kitakachompata mwisho wamaisha yake. Shabaha ya Yesu kuinuliwa juu imeonyeshwa katika maneno yak.15 „ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika Yeye‟. Yeye ni tofautisana na nyoka wa shaba, uzima haukuwemo katika nyoka wa shaba, lakini

Page 36: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA525

uzima wa milele umo katika Yesu (Yn.5.26; 11:25). Kwa hiyo, mtu azaliwa upyakutokana na kazi ya kuokoa Yesu aliyofanya Msalabani, na kwa imani barakayake huletwa maishani mwake. Mtu aweza kushirikishwa huo uzima hata kablaya kufa kwake na kabla ya mwisho wa dunia hii. Ni uzima wa Kristo Aliye Haibaada ya kufa (1 Yn.5:12). (Nyoka wa shaba ilivunjwa na Mfalme Hezekia kwasababu watu wengi waliifukizia uvumba 2 Waf.18:4).

k.16-17 Yawezekana sehemu hiyo ni mafupisho ya mengine yaliyosemwa naYesu, pengine mwandishi Yohana alikuwepo. Wengine wanafikiri ni mawazo yaYohana baada ya mazungumzo ya Yesu na Nikodemo, ila maneno „kwa maana‟ni daraja ya kuyaunganisha yaliyotangulia na haya yafuatayo na kuonyeshakwamba mazungumzo yaliendelea. Kifungu cha 16 kimewasaidia watu wengisana kwa jinsi kinavyofafanua vizuri njia ya kupata uzima wa milele katika lughainayoeleweka. Kwanza kabisa kwa kifungu hicho tumepewa ufunuo wa jinsiMungu anavyoukabili ulimwengu huu na makusudi yake juu yake. Mkazo niupendo wa Mungu. Mungu aliupenda ulimwengu huu na ameuthibitisha upendowake na kuudhihirisha katika tendo kuu la kumtoa Mwana wake pekee ili afe kwaajili ya kuukomboa. Kiasi cha upendo wake kinapimwa kwa kuangalia kipawaalichotoa. Asingaliweza kutoa kipawa cha thamani sana kuliko hicho cha Mwanawake, mpendwa, wa pekee. Jambo hilo linasisitiza kina cha upendo wake.Asingaliweza kuupenda ulimwengu zaidi (Rum.8:32; Efe.3:17-19) Ameukomboaulimwengu kwa gharama kubwa sana, kwanza, kwa upande wake Mwenyewekatika kumkubali Mwana wake mpendwa aje duniani. Pili katika Mwanampendwa kutoa maisha yake mpaka kufa, kifo kikali sana chenye maumivumengi, kifo cha wenye dhambi, kifo cha kuzifidia dhambi za ulimwengu wote, kifocha kubeba dhambi, hatia, na hukumu yake. Ni kwa jinsi hii Mungu aliupendaulimwengu. Hakuupenda ulimwengu kwa sababu ya ukubwa wake na wingi wawatu wake, wala kwa uzuri wake, la! aliupenda kwa sababu ya ubaya wakemkubwa. Shabaha ya kuupenda kiasi hicho ilikuwa amwokoe kila aliye tayarikumpokea Kristo. Kifungu hicho chaweka mbele za wanadamu njia ya kupatamsamaha wa dhambi na uzima wa milele, njia ni ya kumwamini Kristo. Ni kwa kilamtu, haidhuru ni wa kabila au rangi gani, wa tabaka gani, wa hali gani kielimu auvipi. Ila kwa asiyekubali iliyo mbele yake ni kupotea. Kwa hiyo kipawa cha uzimawa milele kimesimama katika upendo wa Mungu.

k.18-21 Atakayempa kisogo Mwana wa Mungu yu gizani, yu chini ya hukumu yaMungu, ni kama mtu aliyelipa kisogo jua, na kivuli chake mwenyewechasababisha atembee katika giza la kutokuamini kwake. Kwa nini haji kwenyenuru, ni kwa sababu matendo yake yamshuhudia kuwa mwenye dhambi asiyetayari kuyaacha matendo yake mabaya. Mtu wa haki na kweli hana hofu yakumkubali na kumfuata Kristo.

Hatuambiwi Nikodemo aliamua nini baada ya mazungumzo hayo ya maanasana kwake, pia, ni ya maana sana kwa wasomaji wote wa Injili hiyo. Twajua

Page 37: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA526

alimtetea Yesu wakati mgumu wa Yesu kupingwa sana (Yn.7:50ku) piaalishirikiana na Yusufu wa Arimathea katika kumzika Yesu akileta marimari na udi(Yn.19:39-40) kwa hiyo, inaonekana aliitika vema, pengine alikuwa mmojawapowa wafuasi wa siri.

3:22-30 Yohana Mbatizaji amshuhudia YesuHapo mwandishi amerudia kuzungumza habari za Mbatizaji na uhusiano wakena Yesu. Wakati huo Yesu alikuwa ameanza huduma yake akihubiri na kuwaitawatu wabatizwe (ling. na 4:2 twasoma wanafunzi walibatiza watu, si Yesu).Hatuambiwi ubatizo huo ulikuwa kwa ajili ya nini, pengine ni kwa walewaliomkubali kuwa Masihi. Pengine ni kuthibitisha huduma ya Mbatizaji ambayealikuwa akiendelea kuwabatiza watu katika eneo la Ainoni karibu na Salimu.Yesu alikuwa mahali pengine katika nchi ya Uyahudi. Pengine ubatizo huouliashiria jambo lililosisitizwa na Yesu kuhusu mwanzo mpya na maisha mapya(taz. 3:5 na habari iliyotajwa katika Ezekieli 36:25-27).

Myahudi mmoja alitokea akibishana na wanafunzi wa Yohana juu ya utakaso.Hatujui neno „utakaso‟ lilihusu ubatizo wa Yohana au maosho mbalimbali yaKiyahudi. Ndipo hao wanafunzi walisema na Yohana juu ya Yesu na jinsiambavyo watu wengi walikuwa wakimwendea. Yawezekana walipata wivukumwona huyo Yesu ametokea na kuwavuta watu zaidi ya Yohana. Jambo hiloliliwasumbua sana wafuasi wa Mbatizaji, lakini Mbatizaji mwenyewe hakuwa nawasiwasi wowote. Yeye aliona ni mpango wa Mungu, kwa mapenzi ya Munguyeye alipewa kuwa mtangulizi wa Masihi si Masihi mwenyewe, na kwa sababuhiyo ilikuwa sawa Yesu achukue nafasi ya mbele kama ilivyokuwa ikitokea. Kwahiyo aliyasahihisha mawazo yao. Aliwakumbusha jinsi ambavyo tangu mwanzoalikuwa amekataa kabisa kuwa Masihi, pamoja na kuwaeleza kazi yake kuwa ileya kutengeneza njia ya Masihi kwa kuwaleta watu kwenye toba. Alichukua kilanafasi ya kumkuza Kristo. Alitumia mfano wa bibi na bwana arusi na rafiki wabwana arusi. Yeye ni huyo rafiki wa bwana arusi, mwenye kazi ya maana sanaya kufanya maandalio ya arusi, kusudi siku ya arusi itakapofika mambo yoteyaende vizuri. Katika siku hiyo rafiki hasikitiki wala hajihurumii bali afurahi sanamaana ni siku ya arusi!! Kwa hiyo yeye Yohana atazidi kupungua na Yesu atazidikuvuta watu. Ukuu na unyenyekevu wa Mbatizaji umeonekana wazi katikamaneno hayo na katika utendaji wake. Bila shaka alijaribiwa kujiinua alipoonawatu walimtaka azidi kuendelea, bila tahadhari angaliweza kuvuruga mpango waMungu na kuleta tatizo kwa Yesu, ila, badala yake, alirahisisha njia ya Yesu kwajinsi alivyofanya kwa furaha. Alipoona watu wanazidi kumwendea Yesualifahamu kwamba amefaulu utume wake, alijisikia kuwa radhi na matokeo hayona furahi yake ilizidi kutimilika. Yeye ni kielelezo chema kwa wote wanaoitwakuwaachia wengine waingie nafasi zao.k.31-36 Maneno hayo ni ya nani? Je! Mbatizaji aliendelea kusema hayo au Je!ni nyongezo ya Yohana mwandishi? Hatujui. Ila hoja ni ileile ya kumhusuMbatizaji na uhusiano wake na Yesu. Kwa nini Yesu ni mkuu kuliko Yohana?Yesu ni mkuu na bora kuliko Mbatizaji kwa sababu ametoka mbinguni, ametoka

Page 38: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA527

kwa Mungu, ni Mungu. Yohana ametoka duniani, ametoka katika wanadamu, yumwanadamu. Kwa hiyo, Neno la Yesu ni bora na lenye nguvu. Ni Neno la MunguMwenyewe, kwa sababu Yesu ameishi katika Mungu na kuelewa yoteyamhusuyo Mungu. Asemayo Yesu, haidhuru ushuhuda wake unapokelewa aukukataliwa, ni ya kweli, yana uhakika. Kumkataa Yesu na ujumbe wake nikumfanya Mungu kuwa mwongo. Wale wote watakaomkubali Yesu na ushuhudawake wamefahamu kwamba Mungu ni mwaminifu kwa Neno na ahadi zake(Rum.3:4; 1 Yoh.5:10).

Manabii walijaliwa Roho kwa kadiri ya kazi au wajibu waliyopewa ila Mungu Babaamempa Yesu Roho bila kipimo na amemkabidhi yote, uwezo na mamlaka. Nenohilo limeonekana katika uwezo wa kuwajalia wamwaminio uzima wa milele. Hapotena upendo wa Baba kwa Mwana umetajwa. Ukombozi wa wanadamuumezaliwa katika upendo uliopo kati ya Baba, Mwana, na Roho. Ndipo Yohanaamerudia jambo kuu la imani. Yesu ndiye sababu kuu ya watu kuokoka aukupotea. Yategemea jinsi kila mtu unavyomfanyia, ama kumpokea, amakumkataa. Maana ya kumwamini ni kumkubali, kujikabidhi kwake, kumruhusuawe na madaraka juu ya maisha, si jambo la kuwaza tu kichwani bali ni jambo lautii wa moyo. Tena linahusu wakati huu wa sasa. Ni sasa mtu anao uzima wamilele au sio, si kitu mtu anachopata wakati wa kufa, kama anazawadiwa kwamaisha yake. Tena ni wakati huo wa sasa ambao wanaomkataa Kristo wanaishichini ya ghadhabu ya Mungu. Kutokuamini ni sawa na uasi kwa sababu Munguawaita watu wamwamini Kristo (1 Yoh.5:12).

MASWALI1. Eleza kwa maneno yako maana ya kuzaliwa kwa maji na kwa Roho.2. Eleza sababu ya Yesu kutumia habari za kuinuliwa kwa nyoka ya shaba?

Kwa habari hii Yesu alikuwa akitabiri jambo gani?3. Ni kwa njia gani mtu hupata uzima wa milele?4. Ikiwa mtu atakuambia kwamba hawezi kusadiki kwamba Mungu anawapenda

wanadamu, eti, kuna misiba na ajali na ugonjwa na vifo vibaya n.k.utamsaidiaje? utamwambia habari za nini kumhakikishia upendo waMungu kwa wanadamu?

5. Kwa nini ni vigumu kuwahurumia watu wasiomwamini Kristo?6. Eleza tabia na hali za Yohana Mbatizaji zilizofaa kwa kazi aliyopewa ya

kutayarisha njia ya Kristo.7. Watumishi wa Kanisa wa leo waweza kujifunza nini kwake?

4:1-42 Yesu azungumza na Mwanamke Msamariak.1-3 Yesu alifahamu kwamba wanafunzi wa Yohana walikuwa na wivu juu yakena hakutaka kuongeza shida yao. Alikata shauri kwenda kaskazini alipofahamukwamba Mafarisayo wamesikia habari zake, hasa habari ya Yeye kuvuta watuwengi kuliko Yohana. Walikuwa na mashaka juu ya Yohana ndipo mashakayalizidi waliposikia habari za Yesu. Wote wawili walifanana katika

Page 39: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA528

kutoa ujumbe kwa mamlaka na nguvu, pia waliwabatiza Wayahudi, jambo lakigeni kwa Wayahudi. Hivyo Yesu aliondoka kusini na kwenda kaskazini.Twajifunza kwamba mashindano hayakubaliki katika utumishi wa Mungu.Twaona Yesu, aliyemzidi Yohana, akajiondoa mahali alipo Yohana mtanguliziwake.

k.2 (lakini Yesu mwenyewe hakubatiza, bali wanafunzi wake) maana yake nikwamba wanafunzi walikuwa wakala wa Yesu, ubatizo ulikuwa wa Yesu ila waowaliufanya kiutendaji. Mtume Paulo alijitenga na kazi za ubatizo, kwa kawaidaaliwaachia wengine wafanye huku yeye alihubiri (1 Kor.1:14-17).

k.4 „alikuwa hana budi kupita katikati ya Samaria‟ Mtu aliyesafiri kutoka kusinihadi kaskazini aliweza kufuata njia ndefu ili asipitie Samaria au apite Samaria nakufupisha safari. Wayahudi wengi walichagua njia ndefu, wakihesabu kupita katiya Wasamaria ni kunajisika. Jambo hilo halikumsumbua Bwana Yesu. Amekujaulimwenguni ili awaokoe wanadamu wote, na kuuondoa „unajisi‟ wa dhambiambao wanadamu wote wanao. Maneno „hana budi‟ yaweza kuwa na maanakwamba Yesu alisikia msukumo wa mapenzi ya Mungu, ila ni vigumu kujua kwahakika kuwa ndiyo maana yake.

(Historia fupi ya Samaria: Wakati wa Yesu Samaria iliunganika na Yudea nakutawaliwa na liwali wa Kirumi. Waashuri walipokamata Samaria (K.K.721)waliwaondoa Waisraeli wote wenye hali njema na kuwaachia walio hafifu nchini,na kuwaleta wageni waishi humo, na hao walioana na Waisraeli waliobaki, hivyowalipoteza usafi wao kwa upande wa utaifa na dini (2 Waf.17- 18). Waisraeliwaliorudi kusini baada ya Uhamisho waliwaangalia hao Wasamaria nakuwahesabu kuwa wa mchanganyiko ambao kwa upande wa dini wameingizamengi yasiyokubalika pamoja na kuwa watu wasio na damu safi ya Kiyahudi.Kama K.K.400 hao Wasamaria walijenga hekalu lao kwenye Mlima Gerizimu.Wakati wa Yesu waliendelea na dini yao iliyojengwa juu ya Vitabu Vitano vyaMusa. Hawakuvipokea vitabu vingine vya Agano la Kale na badala ya kwendaYerusalemu kuabudu pale hekaluni wakati wa Sikukuu waliabudu kwenye hekalulao. Hayo yote yalisababisha uadui kati ya Wayahudi na Wasamaria).

k.5ku Katika safari yake Yesu alifika mji uitwao Sikari kama nusu maili nje ya mjiambapo palikuwapo kisima cha maji kilichokuwapo tangu zamani za kale(Mwa.48:22). Yesu alikuwa amechoka na safari na kusikia kiu. Hivyo alipumzikana wanafunzi walikwenda kutafuta chakula mjini. Ilikuwa wakati wa adhuhuri,wakati wa jua kali. Hapo twauona ukweli wa ubinadamu wake, alifanyika mwilikweli (1:14). Twaweza kufikiri kwamba wanafunzi wangaliteka maji kamawangalikuwapo.

k.7ku Papo hapo akakutana na mwanamke Msamaria. Haikuwa saa ya kawaidaya wanawake kuchota maji, wala kawaida kwa mmoja kuja peke yake.

Page 40: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA529

Yafikiriwa kwamba alikuja saa hiyo ili asikutane na wanawake wenzake kwasababu ya kusikia aibu juu ya maisha yake. Katika hali nyingi alitofautiana naNikodemo. Nikodemo alikuwa mwanaume, yeye mwanamke; Nikodemo alikuwaMyahudi, yeye Mmataifa; Nikodemo alikuwa mwalimu stadi katika Israeli, yeyesiyo (wanawake hawakuelimishwa); Nikodemo alikuwa mtu wa cheo namheshimiwa kati ya watu, yeye siyo. Nikodemo alikuwa Farisayo, mwadilifu, mtuwa kushikilia sana maagizo ya Torati; yeye mwanamke siyo; alikuwa na maishamabovu akiishi kinyume cha maagizo ya Torati. Nikodemo alikuwa na kibalimachoni pa watu, huyo mwanamke alitenganishwa na watu. Nikodemo alikuwatajiri na kutoka katika tabaka ya juu; yeye alikuwa maskini, pengine alitoka katikatabaka ya chini. Nikodemo alimtambua Yesu kuwa mtu wa Mungu, alitafutakuzungumza naye. Huyo mama hakumjali Yesu, alimwona kama msafiri naaliendelea na hali ya kutokumjali mpaka baadaye, baada ya Yesu kuongea nayekwa muda. Kwa hiyo Nikodemo na mwanamke Msamaria walitofautiana kwa halinyingi. Yesu alizungumza na Nikodemo juu ya kuzaliwa kwa maji na Roho. Kwamwanamke Msamaria alizungumza naye juu ya maji ya uzima. Ni mamoja, yotemawili yahusu Ufalme wa Mungu na uzima wa milele. Iwapo tofauti zao zilikuwanyingi na kubwa, hata hivyo, wote wawili walimhitaji Yesu na wokovu wake.

Yesu alijihusisha na mwanamke huyo kwa kumwomba amfadhili na kumpa majiili anywe. Kwa maneno machache Yesu alibomoa ule uadui uliokuwepo kati yaWayahudi na Wasamaria na kiambaza kati ya wanaume na wanawake. Huyomama alishtuka, alipoona kwamba huyo Myahudi amethubutu kumwombamsaada. Haikuwa kawaida Wayahudi washirikiane na WaSamaria, na zaidimwanaume amjali mwanamke. Lakini kwa njia ya kujinyenyekeza na kuombamaji Yesu alipata nafasi ya kuongea na huyu mama. Yesu hakufungwa na milana desturi na ubaguzi wa Wayahudi wenzake.

k.10ku Yesu aliamsha upekuzi wake kwa kumjibu „kama ungaliijua karama yaMungu, naye ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, nayeangalikupa maji yaliyo hai‟. „kama ungalijua...‟ kumbe anayezungumza nayeanacho kitu asichokijua yeye. Tena hajui ni nani anayezungumza naye. Kwamaneno hayo ya kuamsha hamu yake ya kujua, Yesu alitaka kubadili hali yakeya kutokujali na kumfanya amsikilize. Yesu alikuwa na kazi kubwa ya kumletahuyo mama afahamu mambo ya kiroho. Alikuwa akiwaza maji ya kawaida„Bwana, huna kitu cha kutekea, na kisima ni kirefu; basi umeyapata wapi hayomaji yaliyo hai?‟ Ufahamu wake ulikuwa mdogo, hata hivyo, Yesu alikuwa tayarikuendelea na maongezi yake. Yesu alisisitiza tena habari ya maji ya uzima nauzuri wake. Alidai makubwa kuhusu hayo maji, ni maji ya kumtosheleza mtuyenye uwezo wa kukata kiu yake. Maji hayo hayatoki kisimani, bali yatoka Kwake.Ni maji yasiyo na kikomo, yabubujikayo kutoka ndani ya mtu. Yapatikana kwaurahisi, kwa sababu mwenye Maji hayo Yu karibu, ni huyo aliyesema naye. HivyoYesu alijifunua kwa huyo mama kuwa asili ya uzima wa milele, uzima ni kipawachake, ni Yeye Mwenyewe. Kwa maneno hayo Yesu

Page 41: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA530

alikuwa ameamsha nia ya kutaka hayo maji. Huyo mama akamwomba „Nipe .....nisije tena hapa kuteka‟. Lakini hata sasa hajaelewa vizuri, bado angaliakiyafikiria maji ya kimwili, huenda maji mazuri, hai, yanayotembea, yatokayochemchemi, tofauti na maji ya kisima kilichochimbwa. Akayataka, ili asiwe nahaja ya kuja kisimani kila siku.k.16 Hata hivyo, Yesu hakukata tamaa, aliendelea kuongea na huyo mama juuya „maji‟ yake bora. Aliona vema ambane ili atazame maisha yake jinsi yalivyo.Alitaka aone ukame wa maisha yake na haja yake ya maji ya uzima.Akamwambia aende na kumleta mumewe. Akiyataka hayo maji basiajishughulishe, aende mpaka nyumbani na kumleta mume wake. Huyo mamaalipata shida sana, afanye nini, maana yule anayeishi naye si mumewe. Haponyuma amekuwa na waume watano. Hivyo, bila kupenda, na labda kwa uchungu,akamjibu Yesu „sina mume‟. Yawezekana hakupenda huyo Myahudiamchunguze zaidi juu ya maisha yake. Kisha Yesu aliondoa kifuniko kilichofichamaisha yake „huyu uliye naye siye mume wako...kwa maanaumekuwa na waume watano...‟ Kumbe! huyo mgeni anafahamu hata maishayake ya nyumbani na historia yake ya nyuma. Yesu hakuridhiana na dhambi yake„huyu siye...‟ aliweka yote wazi mbele yake. Amekuja ili awaokoe wenye dhambi,hivyo yawapasa watu watazame maisha yao, wakiri dhambi zao na kuzitubu,kisha wamwamini Yesu kama Mwokozi. Kisha huyo mama akamkiri Yesu kuwanabii, akaona afadhali ayabadili mazungumzo, kama Yesu ni nabii borawazungumze mambo ya dini.

k.20ku Alimwuliza Yesu kuhusu ibada na kutaja tofauti kati ya Wayahudi naWasamaria kuhusu mahali pa kuabudu. Yesu akamjibu kwa kubomoa tumaini laWaSamaria katika mipango yao. Alisema wazi kwamba WaSamaria hawakumjuavizuri yule waliyemwabudu kwa sababu ni Wayahudi waliokuwa na ufunuo wakweli juu ya Mungu na ya kwamba wokovu watoka kwao. Ijapokuwa Yesualibomoa tumaini lake lisilo na msingi katika kweli, hata hivyo, akamjenga nakumtumainisha yeye na wanadamu wote kwa kuonyesha kwamba ibada haihusumahali wala wakati, bali ni jambo la moyo na la roho, na msingi ni katika kweli yaMungu Mwenyewe kuwa Roho. Hana hali yoyote ya „kitu‟ au „mwili‟ hafungani nakitu chochote, wala mahali, wala hatawaliwi na wakati. Ni Roho, pia ni Baba, kwahiyo anayo hamu sana ya watu wote kumwabudu katika roho na kweli. „saainakuja, nayo saa ipo‟ Kutokana na kuja kwa Yesu hali mpya imepatikana,mabadiliko makubwa yametokea. Tangu „saa hiyo‟ ya Yesu kusulibiwa nakufufuka na kutukuzwa hamna haja ya mahali maalumu kama Hekalu laYerusalemu au la Gerazimu, wala hamna haja ya mpango maalumu wa sadaka,makuhani, n.k. kwa sababu Kristo Mwenyewe ni Njia, Kweli, na Uzima (14:6).Tangu hapo mtu awaye yote aweza kumfikia Baba kwa njia yake. Tena„imempasa‟ kwa sababu njia halisi imepatikana, hamna nafasi tena kwa njianyingine „mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya Mimi‟. Tofauti kati ya Wayahudi naWaSamaria zaondolewa, hazina maana yoyote tena na muda wa uteule waWayahudi kuwa chombo cha ufufuo wa Mungu umepita. Yesu ni hekalu (2:19-22)naye atatoa Roho (7:38-39; 16:7). Ni ajabu kuona

Page 42: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA531

kwamba Yesu alitoa mafundisho hayo ya juu sana kuhusu Ibada ya Mungu kwamwanamke, aliyekuwa Msamaria, asiyekuwa na maisha mazuri.

k.25 Yesu akatambua kwamba huyo mama ameguswa na mazungumzo hayo,naye yu tayari kuyaitikia. Hakupinga mafundisho yake kuhusu ibada, ila alionakwamba mambo hayo makubwa yamhusu Masihi, ambaye atakapokuja,atadhihirisha yote, kwa hiyo ni vema kumsubiri yeye. Kwa maneno yake twaonakwamba WaSamaria walikuwa wakimtazamia Masihi atakayekuwa kamamwalimu wa kuwafundisha kwa usahihi. Walipokea vitabu vitano vya Musa nakatika Kum.18:15-18 Musa alisema kwamba Mungu atainua nabii mwinginekama yeye. Yesu alikuja ili amfunue Baba kwa ukamilifu, na ajabu ni kwambakwa huyo mama Msamaria pole pole, hatua kwa hatua, alizidi kujifunua kwake.

k.26 Kisha Yesu akajifunua wazi zaidi kuliko alivyojifunua kwa Nikodemo. Bilawasiwasi na bila kusita akakiri kwa huyo mama „Mimi ninayesema nawe ndiye‟.Ni hapo tu Yesu alidai kwa wazi kuwa Masihi isipokuwa mwishoni kabisa mbeleya Kuhani Mkuu baada ya kuapishwa alikiri wazi. Ila katika huduma yake yotealikuwa akidai kwa njia ya ishara zake na kwa jinsi alivyosema katikamazungumzo yake, ila hakutamka wazi kabisa, kama hapo. Kwa nini ajifunuewazi kwa Msamaria wala si kwa Myahudi? Sababu ni kwamba neno „Masihi‟ lilijaamaana ya siasa na vita katika mawazo ya Wayahudi, isingalikuwa busara Yesualitumie, wangalimwelewa vibaya.

4:27ku Wanafunzi walirudi pale kisimani, wakamkuta Yesu na huyo mamawakiongea, wakastaajabu, eti! anazungumza na mwanamke, mwanamkemwenye sifa mbaya, tena Msamaria, ila hawakuthubutu kusema neno. Huyomama akaondoka, akaenda zake mjini, akamshuhudia Yesu kwa ushujaa,akiwaita watu waje kisimani, wamwone huyu mtu, akiwaelekeza kufikiri kwambawatakutana na Masihi. Wengi wakaenda kumwona Yesu. Aliuacha mtungi wakekisimani, labda kwa sababu ya haraka yake ya kumshuhudia Yesu kwa wenzake;pengine alimwachia Yesu maji ya kunywa. Labda twaweza kuona ishara ya yeyekuyaacha mapokeo ya dini kwa ile imani mpya ya „maji hai‟ na „ibada katika Rohona kweli‟. Ni ushuhuda wa mtu aliyekuwepo na kuona mambo hayo. Ni vematuone hatua katika kuongezeka kwa ufahamu wake, kwanza alifikiri Yesu ni mkuukuliko Yakobo (k.12) ndipo nabii (k.19) kisha Masihi (k.29) na WaSamariawalipokutana na Yesu walimfikiria kuwa „Mwokozi wa ulimwengu‟ (k.42). Jambokubwa ni utayari wake wa kumshuhudia Yesu na kuvuta watu kwa Yesu.k.31-34 Yule mama alipoondoka kisimani wanafunzi walimsihi Yesu ale chakulawalichomletea. Hawakuweza kufahamu sababu ya Yeye kutokutaka kula kwasababu walipomwacha alikuwa amechoka sana, na wao wamesumbuka iliwampatie chakula. Kwa jibu la Yesu waliendelea kuwaza chakula cha kimwili,wakifikiri kwamba mtu amemletea chakula, lakini sivyo ilivyokuwa. YawezekanaYesu alikuwa ameshikwa na mawazo mengi akiyazingatia mazungumzo yakena huyo Msamaria. Ndipo alitumia nafasi hii

Page 43: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA532

ya kuulizwa na wanafunzi kuwafundisha juu ya vipaumbele vya maisha yake.Alitamka neno kubwa sana juu ya utume wake na kazi aliyokuja duniani kuifanya.Chakula chake ni kutii mapenzi ya Babake (5:36; 6:38; 8:29) na katikakuzungumza na Msamaria alikuwa akifanya mapenzi ya Babake, basi, katikakufanya hivyo alikuwa akilishwa na kusikia raha nafsini mwake kuliko kulachakula alicholetewa na wanafunzi (Kum.8:3; Mt.4:4 „mtu haishi kwa mkate tu).Ni mapenzi ya Mungu kuleta watu wamfahamu Yeye, na Nafsi Yake, na uhusianowake na Mungu Baba, kusudi wajikabidhi Kwake, wamfuate katika maisha yao,na kushirikiana naye kibinafsi. Katika kuzungumza na huyo mama alikuwaakipanda mbegu, na huyo mama akaenda, akapanda mbegu, na mbegu hizoziliota kwa haraka, na mavuno yalipatikana mara.

k.35-38 Alipoinua macho yake Yesu aliona umati wa WaSamaria wakija Kwake.Alitamani sana wanafunzi wake washirikiane naye katika utume wake, hao naowapande Neno la Mungu na kuvuna matokeo yake ili wazawadiwe katika uzimawa milele, na kuitimiza kazi waliyoitwa kuifanya. Yesu aliona ilikuwa nafasimuhimu iliyotaka haraka. Alitaka wanafunzi watambue kwamba kuvuna kwaokwategemea kazi za waliotangulia, yawezekana Yesu alimwaza YohanaMbatizaji, pamoja na manabii n.k. waliokuwa waaminifu kwa Mungu katika sikuzao. Tena kazi hiyo huhitaji ushirikiano, kila mtu huhitaji mwenzake. Kazi hiihugharimia maisha yote „mmeingia katika taabu yao‟.

k.39ku Kwa nini wale WaSamaria walimwendea Yesu? walikwenda kwa sababuya ushuhuda wa kibinafsi wa huyo mama. Ndipo baada ya Yesu kukaa nao mudawa siku mbili wengi zaidi wakaamini, kwa sababu ya Neno la Yesu. Waliyoyasikiakwa Yesu yaliwahakikishia kwamba Yeye ni Mwokozi wa ulimwengu. Yesualikuwa na mawazo mapana sana, hakufungwa na „Kiyahudi‟ chake, alikuja ili„kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele (3:16) itikio laWaSamaria lilithibitisha neno hilo. Bila shaka WaSamaria walishangazwa nautayari wa Yesu kukaa na kushirikiana nao.

4:43-54 Yesu amponya mwana wa diwani huko Galilayak.43-45 Yesu aliendelea na safari yake ya kwenda Galilaya (4:3). Katika Samariahuduma yake imebarikiwa sana na wengi wa Wasamaria walimwamini. Baada yasiku mbili Yesu akaondoka Samaria na kufika Galilaya na kupokelewa vizuri kwasababu Wagalilaya waliiona miujiza (au walisikia habari zake) aliyoifanyaYerusalemu wakati wa Sikukuu. Maneno ya k.44 ni tatizo, yawezekana yahusuimani ya wengi iliyojengwa juu ya miujiza, haikuwekwa katika Yesu Mwenyewena madai yake ya kuwa Mwana wa Mungu, Masihi. Inaonekana imani yawanafunzi ilikuwa tofauti, ilikuwa katika Yeye Mwenyewe baada ya kuiona ishara(2:23). Yesu alielewa kwamba ilikuwa vigumu kwa watu kumwaza kuwa Masihikwa kuwa alilelewa kati yao, walikuwa wamemfahamu tangu utoto wake, walijuawazazi wake na ndugu zake. Walipoziona ishara walimpokea kama mponyaji namtenda miujiza, ila hawakuwa tayari kumkubali kuwa Masihi. Hali hiyohaikumridhisha Yesu.

Page 44: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA533

k.46ku Yesu akafika Kana ya Galilaya, mahali ambapo wengi walimkumbukakwa mwujiza wa kuyageuza maji kuwa divai katika arusi ya mwenyeji mmoja.Alikutana na diwani mmoja, mtumishi wa Mfalme Herode (yawezekana alikuwaMyahudi) ambaye alishikwa na wasiwasi na huzuni kwa sababu mwana wakealikuwa akiumwa sana huko Kapernaumu (maili 20 mbali na Kana). Inaonekanahuyo mwana alikuwa ameugua kwa muda, na hali yake ikazidi kuwa mbaya,ndipo ikaongezeka kuwa ya hatari sana hata akawa katika hali ya kufa. Diwaniakamjia Yesu na kumsihi aende Kapernaumu na kumponya. Yesu akamjibu kwaukali kana kwamba alikuwa akiyajibu mawazo ya wengi walioko. Hakupendakuombwaombwa afanye miujiza bila watu kufikiri juu ya yeye Mwenyewe kuwanani. Diwani hakulijali hilo jibu la Yesu, hakujitetea, wala hakuudhika. Katikashida zake kubwa mambo hayo kwake si kitu, wakati huo si wakati wamajadiliano bali ni wakati wa utendaji. Mbele yake ni kufa au kuishi kwa mwanawake, kwa hiyo, akarudia kumwomba Yesu aende kwa mwanawe kabla hajafa.

k.50 Ndipo kwa maneno machache mno, ambayo bila shaka yalimshangazadiwani, Yesu akampa changamoto kwa imani yake, Akamwamuru aende, kwasababu mwana wake yu hai. Alibanwa kati ya mawili: akienda kwa kuambiwa tu,anajuaje Yesu atafanya neno? akikataa kwenda ni kama amemkataa yuleambaye amemtumaini kwa msaada. Afanye nini? Aende? asiende? Akakatashauri kuyaamini maneno ya Yesu na kwenda. Yesu hakuwa na haja ya kwendapamoja naye, hakuwa na haja ya kufanya lolote, hata hatusomi kwamba aliombaau kutoa baraka. Alitamka neno tu „enenda‟ na neno hilo lilitosha kabisa. Diwanihakuwa na kitu chochote cha kushikilia au kutegemea ila neno la Yesu.Akalisadiki, akaenda.

Njiani akakutana na watumishi wake waliomwambia kwamba mtoto wake yu hai.Imani yake ilithibitishwa. Alipowauliza watumishi juu ya wakati wa mtoto kuponaaliambiwa ilikuwa „jana, saa saba‟ kumbe! hii ndiyo saa ambayo Yesu alimwagizaaende kwa kuwa mwana wake yu hai. Imani yake ilizidi kukua kutoka kwenyekuwa imani iliyojitokeza kwa sababu ya shida zake, imani iliyosababishwa nakutaka msaada, mpaka kuwa imani ya mtu aliyependa kumwamini nakumshukuru Kristo. Alizidi kumwamini Kristo Mwenyewe kama yule wakuaminika, mwenye uwezo wa kumtunza yeye na familia yake. Kwa kulitii Nenola Yesu aliletwa katika uhusiano wa kibinafsi naye, na ndivyo alivyotafuta Yesu.Hakutaka kufanya miujiza tu, ila alitaka miujiza yake imdhihirishe kuwa Yule waKuaminika kibinafsi. Diwani alijifunza kwamba Neno la Yesu ni sawa na Kuwakokwa Yesu, umbali si kitu. Watu wengi wanaanza na imani isiyo imara, kama imaniya kumwamuru Yesu, kwa mfano, „ukinisaidia kufaulu mtihani nitakuamini‟„ukinijalia kumpata mtoto nitakufuata‟ „ukinipatia kazi nita..‟ Imani ya namna hiyosi nzuri, ni kama rushwa. Kama ni chanzo cha kuamini si vibaya, ila ikibaki hivyoni kama kumfanya Yesu atutumikie sisi na kutupatia matakwa yetu. Yesu niBwana na twajibika kufanya mapenzi yake.

Page 45: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA534

Twajifunza kwamba Yesu aweza kutuhudumia ijapokuwa hatujamwona walahatujakutana naye kimwili. Tu sawa na yule mtoto ambaye hakumwona walakukutana na Yesu, hata hivyo, Yesu alimponya.

5:1 - 6:7 MUDA WA MABISHANOYesu alikuwa ameweka madai ya kuwa Mwana wa Mungu, Masihi, mbele zawatu. Mara kwa mara kwa wazi; mara nyingine yalionekana kwa jinsi rafiki zakewalivyomwita; na mara nyingine yaliashiriwa na miujiza yake. Pamoja na madaijuu ya Nafsi na Cheo chake, Yesu aliwadai wafuasi wake wampe utiifu wao wote,wamwamini na kumtii.

Madai hayo yote yalisababisha agongane na watu mbalimbali, hasa wakatimapenzi yake yaligongana na mapendeleo yao na dhambi zao.

Sura 5 na 6 zinaonyesha jinsi mabishano yalivyozidi kutokea katika majadilianomakali na wakuu kabla hawajazichukua hatua za kumwondoa. Kwa hiyo, kwaupande mmoja alikuwapo Yesu aliyedai kwa haki apewe utiifu wa watu kwasababu ya Nafsi na Cheo chake, pamoja na wale waliomwamini na kumpokea.Kwa upande wa pili walikuwapo wale walioyapinga madai yake, hawakuwa tayarikumwamini na kumpokea, hao walimwaza kama laghai, si mtu wa kweli, nawaliona madai yake hayakuwa kweli.

Mabishano yalisababishwa na matukio mawili; Kuponywa kwa kiwete naKuwalisha watu elfu tano.Tukio la kwanza lilimhusu mtu mmoja tu, aliyesaidiwa kimwili baada ya kuwamlemavu muda mrefu.Tukio la pili lilihusu umati wa watu, watu wenye afya, waliolishwa chakula chamara moja.La kwanza lilitokea Yerusalemu - la pili lilitokea Galilaya.La kwanza lilchokoza Wayahudi na kuamsha uadui wao - la pili liliwafurahishawatu wengi.Yote mawili yalizaa mabishano. Pamoja na habari za matukio Yohana alitoahabari za mafundisho yaliyofuata kila tukio.

MASWALI1. Umejifunza nini kuhusu kujihusisha na watu kutokana na kielelezo cha

Yesu katika kujihusisha na huyo Msamaria?2. Kutokana na jinsi Yesu alivyojihusisha na Nikodemo na huyo Msamaria kwa

njia tofauti, Je! umejifunza nini juu ya kuzungumza na watu unapofanyauinjilisti?

3. „Mungu ni Roho, nao wamwabudo yeye imewapasa kumwabudu katika rohona kweli‟ Maneno hayo ya Bwana Yesu yana mafunzo gani kuhusu ibadazetu? Misingi ya kweli ya ibada ni nini?

4. Umejifunza nini kutokana na habari ya uponyaji wa mwana wa diwani?

Page 46: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA535

5:1-18 Kumponya kiwete penye birika ya Bethzathak.1 Hatujui Sikukuu hiyo ilikuwa ipi. Ilikuwa desturi ya Yesu, kama Myahudi safi,kuzihudhuria.k.2-4 „pana birika‟ kwa maneno hayo inaonekana hiyo birika ilikuwapo wakatiYohana anaandika, ila si lazima tufikiri hivyo. Maelezo kuhusu maji ya birikahayaonekani katika nakala za zamani, pengine yaliingizwa kwa shabaha yakuwasaidia watu kuelewa sababu ya watu wengi kukusanyika pale (manenoyasiyo katika nakala za zamani yamewekwa katika vifungo vya mraba). Maji yabirika yalipata hali ya kipekee, ya kuchemka, yawezekana chemchemiilisababisha hali hiyo, ikiamka halafu kukatika. Pengine habari za malaikaziliingizwa kama njia ya kueleza hali iliyotokea kuhusu maji. Ndipoyalipobubujika, wa kwanza kuingia aliponywa ugonjwa wake.

k.5-9 Kiwete mmoja ambaye kwa muda wa miaka thelathini na minane amekuwamgonjwa alihudhuria pale akitumaini kwamba siku moja atatokea mtu wa kumtiamajini mara baada ya maji kutibuliwa ndipo atapona. Ila katika muda huo wotehakutokea mtu wa kumsaidia, hivyo akaendelea kuja pale, yawezekana alikujamara kwa mara wakati alipodhani maji yatatibuliwa, au alikaa muda mrefu pale,hatujui.

k.6-7 Katika umati wa wale waliokuwapo Yesu alimchagua huyo ili azungumzenaye. Alimwuliza swali la kushangaza „Wataka kuwa mzima?‟. Bila shakamgonjwa yeyote apenda kuwa mzima. Kwa nini Yesu amwulize swali la namnahiyo? Inawezekana Yesu alifahamu kwamba huyo mtu amekaa sana au amekujamara nyingi pale bila kusaidiwa hata amefikia hatua ya kukata tamaa, asiwazetena kuwa mzima. Amebaki pale kama mtazamaji tu si kama mtu mwenyetumaini. Pengine shabaha ya swali ilikuwa kumgusa kwa ndani na kupima kamakweli alitaka kuponywa. Je! yu tayari kwa mabadiliko makubwa yatakapotokeamaishani mwake, yu tayari kwa kuvunjwa kwa mazoea yake, pengine mazoea yakuishi kwa kuombaomba tu. Ni vigumu kujua hasa shabaha ya Yesu ila twawezakufikiri kwamba swali hilo lilimshtua na kuyatibu mawazo yake.

Yesu hakujitambulisha kwake, na huyo kiwete alisikia uhuru wa kumjibu akilaumukwamba amekosa mtu wa kumsaidia. Amefungwa na hali yake na mambo yapale alipo, ulimwengu wake umefupishwa kuwa mdogo sana wa kuona yapalepale tu, mawazo yake yalitawaliwa na jinsi asivyo na msaada. Yesu alitakakuiamsha nia yake pamoja na mwili wake. Ndipo, akamwamuru kwa nguvu„Simama, jitwike godoro lako, uende‟. Yesu alimwamuru na kumwambia wazimambo ya kufanya. Je! si dhihaka kumwagiza mtu asimame, mtu ambaye sasahivi amesema kwamba hana uwezo wowote wala msaada wowote? La, hatakidogo! Si dhihaka bali ni changamoto ili asiendelee kuwaza matatizo yake.Ingawa hakujua ni nani aliyesema naye, aliye mbele yake ni Yesu mwenyemamlaka ambaye kwa neno tu huamuru na jambo latendeka. Kwa njia hiyo imanina nia yake zilichochewa. Kisha akasimama, akajitwika

Page 47: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA536

godoro lake, akaenda. Jambo hilo lilitokea siku ya Sabato. Twajifunza kwambaYesu aweza kukabili shida ya siku nyingi na kuitibu.

Uponyaji huo una maana gani, unaashiria nini kumhusu Yesu? Hatusomikwamba kiwete aliamini, au ya kwamba Yesu alidai amwamini, maana hakumjuani Yesu. Yesu hazuiliwi na hali ya mtu, kama mtu anawaza nini au anatumaininini. Kiwete aliitikia neno la Yesu la kusimama na kwenda. Neno „mara‟ halitumikisana katika Injili hiyo. Huyo mtu alikuwa na shida siku nyingi, alikuwa amepoozamiaka 38, amekosa mtu wa kumsaidia, ila alipoambiwa asimame, basi,akasimama bila kukawia. Yesu alimwambia ajitwike godoro lake aende.

k.10-18 Mabishano yalifuata. Wakuu walikutana na yule aliyeponywa haliamelibeba godoro lake, jambo lisiloruhusiwa siku ya Sabato. Alifanya hivi kwasababu Yesu aliyemponya alimwambia ajitwike godoro lake aende. Amri yasabato ilisemaje? Ilisema „usifanye kazi yoyote....‟ Waalimu wa Kiyahudiwalifafanua amri hii kwa kutoa maelezo mengi juu ya kazi. Waliweka aina 39 za„kazi‟ zisizoruhusiwa na „kubeba kitu‟ ilikuwa mojawapo. Ni mapokeo, kamamwongozo wa kuwasaidia watu. Ila shida ilitokea kwa jinsi walivyozidi mpakakatika maelezo yao, hata mengine yalionekana upuuzi. Pamoja na hayowaliyaweka mapokeo hayo kuwa sawa na Amri Kumi zilizotoka kwa Mungu. Bilashaka wengine walifanya kwa nia safi, wakitaka kuilinda siku ya Sabato isifananena siku nyingine. Ni kama kuliiwekea boma. Kwa sababu ya mabishano mengiyaliyotokea baina ya Yesu na wakuu juu ya Sabato ni rahisi kufahamu mawazoya Bwana Yesu juu yake. Yesu aliona Sabato ni siku ya kutenda kazi za rehema,kama ile ya kumponya kiwete. Ilikuwa siku ya starehe siyo siku ya kutokutendakazi yoyote. Inaonekana alimponya huyo mtu siku ya Sabato kwa kusudi lakuweka wazi msimamo wake na kuonyesha hitilafu katika ufahamu wao juu yashabaha ya Sabato.

Ajabu ni kwamba wakuu hawakutaka kujua jinsi kiwete alivyoponywa ilawalimshtaki juu ya kulibeba godoro lake. Katika kujitetea aliweka lawama juu yayule aliyemponya kwa sababu ni yeye aliyemwambia kulibeba godoro lake. Nivigumu kujua kwa nini amlaumu yule aliyemponya isipokuwa alihofu atashtakiwanao kwa kuvunja Sabato. Walitaka kujua ni nani huyo aliyemponya ila yule mtuhakujua ni nani. Machoni mwao aliyemwambia kuvunja mapokeo yao alikuwahatari kwao kuliko yule aliyeyavunja kwa sababu ya kuambiwa.

k.14 Inaonekana muda ulipita ndipo Yesu alikutana na yule mtu mle hekaluni.Yawezekana alikuwa amemtafuta. Yesu aliona kwamba yule mtu aliwajibikakuiitikia vema neema ya Mungu iliyoonekana katika uponyaji wake. Katikamawazo ya watu wengi walifikiri upo uhusiano kati ya dhambi na ugonjwa. Mtuameugua kwa sababu amefanya dhambi fulani hasa. Lakini haina maanakwamba kila mtu anayeugua ameugua kwa sababu ya kutenda dhambi fulani,ila inawezekana ni hivyo kwa baadhi ya watu, na kwa upande wa huyo

Page 48: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA537

aliyeponywa Yesu ndivyo alivyosema. Yesu akampa changamoto „Angaliaumekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi‟.Jambo lililo baya zaidi, huenda ni hukumu ya mwisho. (Ugonjwa ni laanamojawapo iliyoingia jumuiya ya wanadamu kutokana na Anguko la Wanadamu(Mwa.3)). Yule aliyeponywa alikuwa ameponywa kwa neema ya Mungu, Munguhushirikisha baraka zake hata kwa wale wasiostahili. Hata ikiwa mtu ameponywakimwili siyo kusema ameponywa kiroho.

k.15 Yule mtu alipofahamu ni Yesu aliyemponya akaenda kwa wakuu nakuwapasha habari hiyo. Tukumbuke ya kwamba alikuwa katika hatari yakuhukumiwa nao kwa sababu ameivunja sabato. Mbele yao alikaza uponyajiwake, alitaka wafahamu kwamba yule aliyemwambia ajitwike godoro ni yulealiyemponya.

k.16ku Lakini Wayahudi hawakutaka kumwaza Yesu vizuri, wakamwudhi, kwakuwa ameivunja Sabato! Hatujui walimwudhi kwa njia gani, ila bila shakawalimsema vibaya na kumshtaki mengi. Ila Yesu alikuwa imara, akawakabili,akadai mambo makuu ya kuwakasirisha sana. Alikaza uhusiano wake wakipekee na Baba yake, akimwita „Baba yangu‟. Kwa maneno hayo alidai usawawa asili na Baba, si usawa wa kuwaza mamoja tu. Halafu alisema kwamba Babayake anatenda kazi hata sasa. Alifanya uumbaji katika siku sita na kustarehe sikuya saba, lakini kustarehe siku ya saba siyo kusema kwamba tangu siku ilehakufanya kazi tena. Bado angali akifanya kazi katika hali ya kustarehe,hakuacha uumbaji uendelee tu, mfano wa saa kutiwa ufunguo halafu kuachwakwenda bila kutiwa ufunguo tena, Mungu anautegemeza ulimwengu mpakasasa. Si mvivu, hatoi jasho, hata hivyo, bila Yeye kuendelea na kazi ulimwenguungalikwisha zamani. Ndipo Yesu alisema „nami ninatenda kazi‟. Yeye yu pamojana Baba katika kuutegemeza ulimwengu. Pia Yeye hutenda kazi za rehema hatakatika siku ya Sabato. Kustarehe si sawa na kutokutenda kazi yoyote.Kutokufanya mema ni kutenda dhambi. Kwa hiyo Yesu aliwaletea mawazomapya kuhusu Sabato, na mawazo mapya juu ya Mungu, pamoja na madaimakuu juu ya uhusiano wake na Baba.

k.18 Wayahudi walielewa kabisa aliyosema Yesu juu ya uhusiano wake na Baba.Kwa maneno yake alikuwa amedai kuwa na asili moja na Baba, yu sawa naye.Kwa hiyo, kuna mawili, ama madai yake ni kweli; na kama ni kweli, iliwapasawayajali sana, maana ni makubwa mno. Kama ni madai ya uongo, Yesuamekufuru kufuru kubwa mno, na kwa sababu hiyo alistahili kupigwa mawe nakufa. Washtaki wake hawakuwa na mzigo juu ya ukweli, Yesu kwao alikuwa wahatari sana, kwa hiyo, kwa vyovyote watazidi kumwinda na kutafuta kumnasa iliwapate kesi itakayofaulu juu yake. Ila nguvu ya Yesu ilikuwa katika uwezo wakuyathibitisha madai yake kwa ishara alizozifanya. Waliweza kuyakanushamaneno yake ila hawakuweza kuyakanusha matendo yake. Katika k.16walimwudhi na katika k.18 walizidi kutaka kumwua.

Page 49: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA538

5:19-29 Madai ya Yesu kuhusu uhusiano wake na BabaYesu alifuliza madai yake juu ya uhusiano wake wa kipekee na Baba. Alionyeshaujasiri mkubwa kwa sababu alijua kwamba kwa kufanya hivyo chuki yao itazidikwa vile hawakuwa tayari kuyazingatia madai yake wala kutia maanani miujizayake iliyoyathibitisha madai hayo.

k.19 Alitumia maneno ya kutilia mkazo na uzito kama alivyofanya hapo nyuma„Amin, Amini‟ akisema kwa mamlaka „nawaambia.....‟ Alisema kwamba YeyeMwenyewe hawezi kufanya neno nje ya mapenzi ya Babake. Kwa kudai kuwasawa na Baba hakuwa na maana kwamba Yeye hufanya mambo yakemwenyewe, kama yu huru mbali na Baba. La, hata kidogo, Yeye si Mungu wa pili.Yeye ameambatana na Baba kabisa, hakuna mpaka katika kumtegemea. Yeyeamefungamana kabisa na Baba. Baba ni Mungu aliyemtuma na kumwamuru;Yeye ni Mungu aliyetumwa na kumtii (8:29). Baba ni mfano wake wa kufuatwa;Baba anafanya, na Yeye anafanya anavyoona Baba analitenda. Kwa asili, Yesuni sawa na Baba, kwa upande wa shughuli, Yesu amnyenyekea Baba nakuufuata mfano wake, ila kwa kufanya hivyo isihesabiwe kuwa ishara ya kuwaanao upungufu, la! hana! Ijapokuwa wanawiana sawa, hawabadilishani hali zao.Mwana afanya lile ambalo amwona Baba analitenda, lakini Baba hafanyi lileambalo amwona Mwana analitenda. Kwa sababu Yesu hutenda lile ambalo Babaanalitenda ni dhahiri kwamba Yeye anao Uungu sawa na Baba au asingaliwezakufanya hivyo.

k.20 „Baba ampenda Mwana‟ Mungu si „baridi‟ wala „mwembamba‟ kwa sababuMungu ni upendo budi awe na „nafsi mwenzake‟ wa kumpenda. Pendo halikaipeke yake, lazima liwe na kitu cha kukabili na kupenda. Ndiyo maana Mungu kwaasili ni Baba, Mwana, Roho, wakikabiliana na kushirikiana Nafsi Tatu, MunguMmoja. Katika upendo huo Baba humfunulia Yesu mapenzi yake na Yesu afanyeyale yampendezayo Baba ambayo ameyaona kwa Baba. Katika hali hiyo Yesuatazidi kufanya mambo makubwa hata watu watastaajabu. Ila neno muhimu simakubwa atakayofanya ila ni udhihirisho wa uhusiano wake wa kipekee na Baba.Makubwa ni ishara ya uhusiano huo na thibitisho lake, na yafanyike kwa ajili hiyo.Katika 14:10 yaitwa „kazi za Baba‟. Kwa Mungu na kwa Yesu miujiza ni rahisi, nishughuli ya kawaida tu. Si vigumu kwa mwenye uwezo

k.21 Kazi moja ya Baba ambayo watu wote hukubali kuwa yake ni kuwafufuawafu na kuwahuisha, na Mwana vilevile atawafufua wafu na kuwahuisha. Waliowafu wa kiroho Yesu atawahuisha, kulingana na mapenzi yake pamoja nakuwafufua wafu wa kimwili siku ya mwisho. Wayahudi walifahamu kwambaMungu anao uwezo huo (Kum.32:39; 1 Sam.2:6; 2 Waf.5:7).

k.22-23 Watu walifahamu kwamba ni kazi ya Mungu kuwahukumu watu. MunguMuumbaji anayo madaraka juu ya viumbe vyake wote (Mwa.18:2). Yesu

Page 50: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA539

alisema kwamba Baba amempa Yeye kazi hiyo. Baba atamtumia Yeye(Mdo.17:31). Kwa nini iwe hivyo? Ili watu wamheshimu Yeye sawa na jinsiwanavyomheshimu Baba. Ndipo Yesu aliongeza kusema kwambaasiyemheshimu Yeye amekosa kumheshimu Baba aliyempeleka. Umoja waounadhihirika katika kufungamana katika neno la heshima. Mmoja akiheshimiwandipo mwenzake ameheshimiwa, vilevile, mmoja asipoheshimiwa na mwenzakevilevile amekosa kuheshimiwa. Wako pamoja kwa hali zote. Kwa hiyo ni jambozito kumdharau Yesu, na maneno hayo yalikuwa onyo kali kwa wale ambao haponyuma walimwudhi. Yesu ni zaidi ya balozi wa Mungu.

k.24ku Yesu akarudia kutumia maneno ya kutilia mkazo na uzito „Amin, Amin,nawaambia‟ na alitumia tena katika k.25. Wokovu wa wanadamu unategemeakwamba walipokee Neno lake na kumwamini Yeye aliyempeleka. Baraka nikubwa kwa watu hao, wanapewa uzima wa milele (si watapewa) naohawatahukumiwa kwa ajili ya dhambi zao, kwa sababu wameishatoka mautini nakuingia uzimani. Hapo tena twaona uhusiano wa kipekee kati ya Yesu na Baba,watu wapaswa kulipokea Neno la Yesu, ushuhuda wake juu ya Nafsi yake, nakukubali kwamba ametumwa na Baba. Hilo ni jambo muhimu, linahusu mtu kufaau kuishi milele. Watu ni wafu katika dhambi na Yesu alikuja ili atoe fidia yadhambi zao Msalabani, na kwa sababu hiyo anao uwezo wa kutoa walio wafukatika dhambi na kuwahuisha na kuwapa uzima wake. Maana Baba amempaYeye kuwa na uzima nafasini mwake kama ambavyo Yeye Mwenyewe alio nao(1:4; 1 Yoh.1:2). Mungu hujitegemea, Yu hai milele na milele, hategemei kitukingine chochote kwa uzima wake. Viumbe vyote vingine hupata uzima waokutoka Kwake. Yeye aweza kuwapa, aweza kuutwaa. Vivyo hivyo na Mwana;Yeye yu Hai milele na milele. Kwa neno lake alimponya kiwete, kwa neno lakeawapatia watu uzima wa milele (6:63,68) kwa neno lake watu wapata utakaso(l5:3) na kwa neno lake wahukumiwa (12:48).

k.27 Yesu amepewa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu.Amestahili kuhukumu, kwa sababu ameishi maisha ya mwanadamu, amejaribiwasawa na wanadamu, ameishi bila kufanya dhambi, hivyo amestahili kuhukumu.Ila haitoshi kusema hivi tu, kwa sababu hata sisi tumekuwa wanadamu na kujuamaisha ya kibinadamu. Yesu ni yule aliyetajwa katika Dan.7:10ku. Tena Yeyeameleta ufunuo kamili wa Baba na kwa sababu hiyo amestahili kuwa mhukumuwetu.

k.28-29 Upeo wa mamlaka ya Yesu utaonekana katika siku ya mwisho wakatiambapo wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Wakipenda, wasipende,kila mmoja atafufuka na kwenda ama kwenye uzima wa milele, au kwenyehukumu ya adhabu, kufuatana na jinsi kila mmoja alivyofanya katika maishayake. Yesu ahusika kabisa na mambo ya mwisho. Baba amempa heshima hiyo.

Page 51: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA540

5:30-47 Ushuhuda mbalimbali juu ya Yesu KristoKwa sababu ya ukubwa wa madai ya Yesu udhibitisho ulihitajika. Yesu alikuwana haki gani ya kudai makubwa hayo? Katika sehemu hiyo Yesu alitaja ushuhudambalimbali; wa Kwake Mwenyewe, wa Yohana Mbatizaji; wa kazi zake; wa Babayake; na wa Maandiko.

k.30-31 Ushuhuda wake. Maneno „nikijishuhudia mwenyewe ushuhuda wangusi kweli‟ ina maana kwamba ushuhuda wake usingalisimama mahakamani.Alikuwa ameishasema kwamba hafanyi neno lolote peke yake bila Baba, kwahiyo, hata katika jambo la ushuhuda na mamlaka yake hafanyi peke yake tu.Hakuwa na maana kwamba yale anayosema juu yake Mwenyewe ni uongo, la,siyo, ila akiyadai makubwa kwa kujitegemea tu ni uongo kwa sababu ni kinyumecha alivyosema juu ya kutokufanya neno lolote bila Baba. Hata hivyo alionakwamba anao uwezo wa kutoa ushuhuda bila kujipendelea, ushuhuda wakukubalika kwa kuwa anajifahamu mwenyewe kupita awezavyo mwingine awayeyote kumfahamu (ling.8:14). Pamoja na hayo amefungamana kabisa na Babakekatika kufanya mapenzi ya Yule aliyemtuma. Alifahamu hawataupokea ushuhudawake, kwa hiyo aliendelea kusema juu ya ushuhuda wa Yohana Mbatizaji.

k.32-35 Ushuhuda wa Yohana Mbatizaji. Ulikuwa ushuhuda wa kibinadamu, kwahiyo, haukuwa na mamlaka ya mwisho. Shabaha yake ilikuwa kwa ajili yawasikilizaji wake ili waokolewe (k.34). Hapo nyuma tumepashwa habari zaushuhuda wa Yohana na jinsi alivyomshuhudia Yesu kwa wazi mbele za watu.Hata walipotuma wajumbe rasmi kutoka Yerusalemu na kumhoji, aliwajibu kwakukana kuwa Masihi, na kwa nguvu alimkiri Yesu kuwa Masihi. Alimtangazahadharani kuwa Mwana Kondoo wa kuondoa dhambi za ulimwengu. AlimkuzaYesu sana kwa kusema kwamba Yesu atawabatiza watu kwa Roho Mtakatifu, naya kuwa yeye mwenyewe hakustahili kulegeza gidamu ya viatu vyake. Yesualiwakumbusha kwamba walimfurahia Yohana, waliona ya kwamba amekuwanuru ya kuangaza njia ya Masihi, ila shida yao ilikuwa hawakuwa tayari kuitikiavema ujumbe wake, hawakumpokea Yeye aliyeshuhudiwa na Mbatizaji, hataalipotokea wazi na kufanya ishara za kuuthibitisha ukweli wa Umasihi wake.

k.36 Ushuhuda wa kazi zake. Ushuhuda mkubwa kupita ule wa Yohana Mbatizajiulikuwa kazi alizozifanya, ishara mbalimbali, miujiza ya uwezo mkubwa. Pamojana ishara hizo hata huduma yake yote na utume wake (ambao ndani yake ni Kufana Kufufuka Kwake) alioupokea kwa Baba, vyote viliushuhudia uhusiano wakipekee kati yake na Baba, asili yao ni moja, kazi zao ni moja. Shabaha yakeilikuwa kuthitibisha kwamba alitumwa na Baba, Mungu wao.

k.37-38 Ushuhuda wa Baba yake. Mara tatu Baba alimshuhudia kwa kutoasauti yake kutoka mbinguni. Pale alipobatizwa Baba alisema „Huyu ni Mwanangu,mpendwa wangu, ninayependezwa naye‟ (Mt.3:17; Mk.1:11;

Page 52: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA541

Lk.3:22). Pale mlimani alipogeuka sura Baba alisema „Huyu ni Mwanangu,mpendwa wangu, msikieni Yeye (Mt.17:5; Mk.9:7; Lk.9:35). Mara nyingine baadaya kuingia Yerusalemu kwa shangwe, Baba alisema „Nimelitukuza, naminitalitukuza‟ (Yn.12:28). Umati wa watu hawakuyasikia hayo maneno. Yesualisema „hamkuisikia....(5:37) kwa sababu bila watu kuwa tayari kujaliyanayosemwa hawaisikii ile sauti inayosema. Lakini kwa Yesu Mwenyeweushuhuda wa Baba ulimfariji, ulimtia nguvu na moyo wa kuendelea na hudumayake.

k.39-47 Ushuhuda wa Maandiko. Njia iliyo wazi kwa watu kuhakikishiwa madaiya Yesu ni Maandiko Matakatifu. Yesu alikubali kwamba walipenda kusoma nakutafakari Maandiko na waandishi wao walifanya bidii sana katika kuyafafanua.Waliamini kwamba kwa njia ya Maandiko watapata uzima wa milele, yaaniMungu atawakubali mwisho wa maisha yao hapo duniani. Yesu aliwaambiakwamba kusoma na kutafakari kwao hakuwafaidii, kwa sababu hawakumtafutaKristo ndani ya Maandiko. Mwenye uzima ni Kristo si Maandiko (1:4) na mwenyekutoa uzima ni Kristo (5:21;26) hata hivyo, watu hukutana na Kristo katikaMaandiko. Shida yao ilikuwa kuyachunguza Maandiko hali hawako tayarikumpokea Yeye aliyeshuhudiwa humo. Walikuwa wameishakata shauri lakumkataa (k.40).

Yesu aliendelea kwa kumtaja Musa kuwa yule atakayewashtaki juu ya Maandiko.Kumbe, Musa alikuwa mpenzi wao, waliomtegemea sana. YasemekanaWayahudi wengi walifikiri kwamba Musa alikuwa angali mwombezi wao kwaMungu. Walimheshimu kwa kuwa ni yeye aliyepewa Amri Kumi na kufanyaAgano na Mungu pale Mlima Sinai. Yesu alithubutu kusema kwamba mwokoziwao Musa amekuwa mshtaki na mhukumu wao kwa sababu kama angalikuwahai wakati huo, angalimpokea bila wasiwasi, maana Musa alitabiri kuja kwa nabiimwingine kama yeye, ambaye watu walipaswa kumsikia (Kum.18:15). Musaalifahamu kwamba Torati aliyoileta haikuwa neno la mwisho kutoka kwa Mungu(Ebr.1:1-3) ila iliashiria kuja kwa Kristo (Mt.5:17). Yesu alikuwa utimilifu wa ahadina unabii wa Maandiko, Yeye ni Masihi aliyeahidiwa, na Mtumishi ateswayealiyetajwa na Isaya (Isa.53). Injili ya Yohana ina dondoo nyingi kutoka Agano laKale, zilizomhusu Yesu. Musa na manabii waliandika habari zake, hivyoWayahudi walipaswa kumpokea.

Pamoja na ushuhuda huo upo ushuhuda wa Roho Mtakatifu. Baada ya Yeyekumaliza kazi za ukombozi na kutukuzwa huko juu (7:39; 15:26) ndipo Rohoatatolewa kwa shabaha hasa ya kumshuhudia Kristo (16:8-15) ndipo umati wawafuasi wake watamshuhudia, mmoja mmoja, tangu wale wa kwanza hadinyakati zote (Mdo.1:8).

Shida yao kubwa ilikuwa nini? Mwisho wa mambo yote ni kwamba hawakumtaka.Hata akifanya juu chini hawatabadili mawazo yao. Wao wamezoea kupokeaheshima wao kwa wao, walipenda sifa za wanadamu, wale

Page 53: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA542

waliokubaliana nao na kuwa na malengo sawa na yao. Hawakumpenda Mungukwa moyo, wala hawakuhesabu kwamba kuwa na kibali cha Mungu ni jambomuhimu. Yesu aliona kwamba haikubaki njia ya kuwasaidia, kwa sababuhawakuuweka msingi wa Maandiko kuwa kipimo cha kuamua mambo. Katikaujinga wa maoni yao walizidi kumsukumia mbali, bila kufikiri kwamba ukwelihaupotei, kama Yeye ni Masihi, yule aliyetumwa na Mungu, kwa vyovyoteatadumu, haidhuru wao watakavyomfanyia.

MASWALI1. Eleza tofauti kubwa kati ya Yesu na viongozi inayoonekana katika uponyaji

wa kiwete2. Ni nini iliyokuwa jambo muhimu kwa Yesu?3. Katika sehemu hiyo Yesu alidai mambo makubwa yapi?4. Madai hayo makubwa yana umuhimu gani tunapofikiri juu ya dini zingine?5. Yesu alionyesha ni watu gani na mambo gani yaliyomshuhudia?

6:1-14 Yesu kuwalisha watu elfu tanoNi mwujiza huu tu ulio katika Injili zote, dalili ya kuonyesha kwamba ulihesabiwakuwa wa maana kubwa machoni mwa watungaji wa Injili nne. Katika kuandikahabari zake Yohana ametaja mambo kadha yasiyopatikana katika Injili zingine.Kwa jinsi alivyoandika inaonekana yeye alifikiri kwamba Yesu alitumia nafasi hiikwa kuipima imani ya wanafunzi wake. Yohana hakuandika habari za mamboyaliyotokea Kaisaria Filipi, (Mt.16:13ku; Mk.8:27ku; Lk.9:18ku) wakati wa Yesukuchunguza wanafunzi kuhusu imani yao na kuona wamefikia wapi katikakumwelewa kuwa nani. Wakati huo ulifikiriwa kuwa wakati wa mambo kubadilika.Yesu alikuwa amefika upeo wa kibali chake katika Galilaya; wengi walikuwawamemfuata, ila baada ya mazungumzo juu ya kuwa Chakula cha Uzima, nabaada ya kukataa kushikwa kuwa Mfalme, basi, watu walianza kumwacha.Amefika njia panda katika huduma yake naye alifahamu kwamba wakati umefikawa kuacha umati wa watu wasio na nia safi juu ya mambo ya kiroho, na kuvutamtu mmoja mmoja na kuwafundisha na kuwatayarisha kwa wakati wa kuondokakwake. Yohana ametaja wanne katika wanafunzi wake na kuonyesha itikio lao;Filipo, Andrea, Petro, na Yuda Iskariote. (Yafikiriwa habari hiyo ilitokea karibu nawakati wa mambo ya Kaisaria Filipi Mt.16).

Yohana ametoa habari nyingi za Huduma ya Yesu katika eneo la Yerusalemu naYudea, na Injili tatu zingine zina habari nyingi za Huduma yake Galilaya. Ni katikasura hiyo ya 6 Yohana ameandika habari za mambo yaliyotokea Galilaya.

k.1 Kama wale wa Yudea, Wagalilaya wengi walimfuata Yesu kwa sababu yamiujiza yake. Hapo nyuma Bahari ya Galilaya iliitwa Bahari ya Kinnereti wakatiwa Agano la Kale. Mwaka B.K.20 Mfalme Herode Antipa alijenga Jiji jipya upandewa magharibi wa Bahari na kuliita Tiberia kulingana na jina la Kaisari

Page 54: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA543

Tiberia, ndipo Bahari ilianza kuitwa Bahari ya Tiberia. Yohana ametaja kwambaSikukuu ya Pasaka ilikuwa karibu (Mk.6:39 majani yalikuwa mabichi, nenolinalopatana na wakati kuwa karibu na Pasaka, baada ya mwezi wa Machi naAprili kupita majani yalikauka). Kwa hiyo mwaka umepita tangu Pasaka ileambapo Yesu alilitakasa Hekalu. Inaonekana Yesu alikuwa akitafuta faragha nawanafunzi wake, hivyo akaenda ng‟ambo ya pili ya Bahari na kupanda mlimapamoja nao. Katika Mk.6:33ku. twasoma kwamba alikuwa akiwafundisha watu nakwa sababu hiyo aliona amewajibika kuwalisha. Ndipo akamwuliza Filipo habariza kuwanunulia mkate. Filipo alitoka Bethsaida (1:44) hivyo atajua mahali pakupata chakula kingi kwa hao watu wengi.

k.6 Yohana hapendi tufikiri kwamba Yesu alishindwa kujua la kufanya ila alikuwaakimchunguza Filipo ili apate kujua Filipo alikuwa akiwaza nini juu ya hao watuna jinsi ya kukabili hilo tatizo kubwa na kuwahudumia. Filipo alionyesha ufinyuwa mawazo yake, akamjibu Yesu kwa kutumia hesabu ya pesa. Hakuwa natumaini lolote, maana kwa hesabu zake walihitaji kiasi kikubwa cha fedhaambacho hata kiasi hicho kitawapatia kidogo tu, si mlo. Filipo alikuwa na uhakikakuwa haiwezekani, kiutendaji hakuwa na wazo la kufanya. Halafu Andrea alijitoakumwonyesha Yesu mtoto aliyekuwa na chakula kidogo, labda hicho kitasaidia.Andrea hakuwa na imani kubwa, ila alijitahidi kutafuta msaada. Yesu alitakakuwaingiza wanafunzi wake katika jambo hilo ili asifanye peke yake, iwapo YeyeMwenyewe alijua atakalotenda. Alitaka kuona walikuwa na mzigo gani juu ya haowatu, kama wana huruma au vipi na kama wako tayari kukabili shida za watu?Tukilinganisha habari hizo na zile za Injili zingine ni dhahiri kwamba Yesu alitakawajifunze mambo makubwa kutokana na mwujiza huo. Wajue kwamba kilekidogo walicho nacho Yeye hatakidharau, na ni hicho kidogo walicho nachoatakitumia. Tena ya kuwa kile kidogo kinacholetwa Kwake na kubarikiwa,kitawatosheleza watu. Wakati wote kitapatikana cha kutosha wakiendeleakumtazama Yeye.

k.10ku Idadi ya wanaume imetajwa, huenda kuonyesha kwamba kama Yesuangalitaka kutumia nguvu na kuipindua serikali angaliweza kupata wanajeshi wakufanya hivyo. Ijapokuwa watu walikuwa wengi sana, lakini, alitaka mamboyatendeke kwa utaratibu, watu waketi kwenye majani, ili waone vizuri yoteyaliyotendeka. Inaonekana mikate na samaki viliongezeka wakati Yesualipovitwaa na kuvigawa. Watu hawakuona mikate mingi sana na samaki nyingipale ila ajabu ilitokea kila alipotwaa mkate na samaki. Yesu alitoa shukrani kwaajili yake, hakuvibariki vitu vyenyewe. Yohana alitaka kuonyesha wingi wachakula, kilibaki cha kuwatosha wengine kama wangalitokea, hatakingaliendelea kupatikana kama haja ingalikuwapo. Neema yake hutosha. Katikakuuvunja mkate Yesu aliashiria Kifo chake Msalabani, utafika wakati wa mwiliwake kuvunjwa Msalabani kwa msamaha wa dhambi za walimwengu wote.Ilikuwa desturi ya Kiyahudi kukusanya chakula kilichobaki na Yesu vilevilehakuwaruhusu wayatupe mabaki, chakula ni kitu cha maana sana, si kitu chakudharuliwa.

Page 55: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA544

Mwujiza huo ulikuwa mkubwa sana, Yesu aliwalisha wanaume elfu tano pamojana akina mama na watoto kwa vitu vichache, hata ile mikate si kama yetu ya sikuhizi, ilikuwa midogo, tena samaki si zile kubwa ili zilikuwa kama dagaa. Yesuaweza kufanya madogo yaenea sana. Lilikuwa fundisho kubwa kwa wanafunzikuhusu huduma atakayowaachia kufanya baadaye. Pia ni fundisho kubwa kwamaisha yetu ya kiroho. Filipo alionyeshwa uwezo mkuu wa Yesu uliozidi hesabuzake zote na Andrea alionyeshwa kwamba imani katika Yesu ijapokuwa ni ndogoinafanya kazi. Watu walimwona Yesu kuwa nabii, hatujui kama walimfikiria kuwaMasihi, haieleweki maana yao ya kusema „nabii yule ajaye ulimwenguni‟ (k.14)labda ni yule aliyetajwa na Musa katika Kum.18:15- 19.

6:15-21 Yesu atembea juu ya maji

k.15 Baada ya kuwalisha watu elfu tano Yesu alitambua kwamba watu walitakakumshika na kumtawaza kuwa Mfalme wao. Wakati wa Pasaka watuwalikumbuka sana jinsi walivyotolewa utumwani mwa Misri kwa mkono hodari waMungu chini ya uongozi wa Musa. Walitamani sana wapate „Musa mwingine‟ mtuwa kuwafukuza Warumi ili wajitawale wenyewe tena. Walimwona Yesu awafaasana, maana ilikuwa dhahiri kwamba Mungu alikuwa pamoja naye, alikuwa nauwezo wa kufanya maajabu, kwa hiyo walidhani kwamba watawezakumshawishi apindue serikali ya Kirumi. Ila Yesu hakuja duniani kwa shabaha yakuwaokoa na Warumi bali awatoe katika utawala wa dhambi. Katika hali yamsisimuko Yesu alisikia kujaribiwa sana kama Shetani ameinuka tena nakumshawishi asifuate njia ya Msalaba iliyowekwa na Baba yake. Mwanzonialipoanza huduma yake Shetani alimletea majaribu matatu makali yakumshawishi atumie uwezo wake kwa faida yake mwenyewe na kuwafurahishawatu si kwa kumtii Baba na kufuata utume aliopewa na Baba. Yesu alitambuahila za Shetani zilizofichwa katika hali ya watu kutaka kumshika awe mfalme,akajitenga na watu na wanafunzi, akaenda mlimani ili azungumze na Baba katikamaombi (Mk.6:46) ili apate kushinda jaribu hilo.

Hivyo, Yesu alikuwa peke yake mlimani, na wanafunzi walikuwa peke yao,kwenye ufuko. Wakawa tayari kufunga safari ya kuvuka bahari, ila Yesu alikuwabado hajawafikia. Inaonekana walikuwa wakimtazamia (hajawafikia k.17).Walipotazama hali ya hewa wakaanza kuhofu kwamba wasipoondoka hivikaribuni watapata shida baharini. Baadhi ya wanafunzi walikuwa wavuvi nawalielewa kabisa hali ya hewa na tabia ya Bahari, jinsi dhoruba ilivyowezakutokea ghafla, vilevile jinsi pepo zilivyoweza kuvuma kwa nguvu kabisa, maanaBahari ilikuwa chini ya usawa wa bahari kama futi mia sita. Upepo ulipita kati yamilima, na bahari ilikuwa kama bakuli, basi pepo zilipovuma zilishuka kwa kasikati ya milima na kuichafua bahari. Usiku ulikaribia. Bila shaka baada ya furahaya siku ile ya kumwona Bwana wao akiwalisha watu wengi na msisimuko wao wakutaka kumshika awe Mfalme, walipoa sana walipoona itikio lake. Amewaagawatu, hataki kuwa Mfalme wa dunia hii; pia

Page 56: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA545

amechelewa kuwafikia na hali ya hewa ilileta mashaka; na giza limeanza.Wakakata shauri kuondoka bila Yesu, wakielekea Kapernaumu.

k.18ku Safari ilikuwa ngumu sana, dhoruba ilitokea na upepo mkuu ulivuma nakatika muda wa masaa tisa hivi walikuwa wamepita maili chache tu. Kadiriwalivyochoka kwa kuvuta makasia ndivyo matumaini yao yalivyopoa. Ndipowalishtuka kabisa walipomwona mtu anatembea juu ya bahari iliyochafuka nakuja kwa upesi ingawa upepo ulikuwa mkali, hata angaliweza kuwapita.Wakaogopa sana maana hawakumfahamu. Kisha Yesu akajitambulisha kwao,aliyatumia maneno aliyoyazoea kusema „Ni mimi, msiogope‟ tangu hapo safarihaikuwa ngumu, Yesu aliingia chomboni, alikuwa pamoja nao, na mwujizamwingine ulitokea, wakafika bila kukawia. Yohana hakuandika itikio la wanafunzikwa jambo hilo. Mwujiza huo uliashiria uwezo wa Yesu juu ya uumbaji, namawazo yao juu yake yalipanuka, wakazidi kuutambua Uungu wake na ya kuwaalikuwa Mwana wa Mungu. Walikuwapo alipoyageuza maji yawe divai,walimwona akiwaponya watu mbalimbali, na mwujiza huo ulikuwa hatua nyingineya Yesu kujifunua kwao.

6:22-25 Mkutano wamtafuta YesuWalijua wanafunzi wameondoka peke yao lakini hawakumwona Yesu akiingiamashuani. Waliamua kwenda Kapernaumu katika mashua zingine wakifikirikwamba watamkuta huko. Ndivyo ilivyokuwa, nao walipomwona, wakamwuliza,„Rabi, wewe umekuja lini hapa?‟. Kama kujibu swali lao alianza mazungumzomarefu juu ya Chakula cha Uzima. Inaonekana alilenga vikundi vitatu katikawasikilizaji wake. Alisema na umati wa watu waliokuwapo alipowalisha watu elfutano na mikate michache (k.22-40). Ndipo alisema na Wayahudi (k.41-59)huenda hao walijitokeza katika umati wa watu, ni wale waliozidi kumpinga nakumhoji juu ya madai yake kuwa Chakula cha Uzima, huenda walitoka katikasinagogi la Kapernaumu. Halafu alisema na wanafunzi wake (k.60-71). Katikasehemu ya mwisho tumeambiwa maitikio ya wanafunzi wa Yesu, walewaliomfuata kwa ukaribu.

6:26-71 Mazungumzo juu ya Chakula cha Uzimak.26ku Inaonekana mazungumzo hayo yalifanyika katika sinagogi (k.59) ila siwazi aliingia sinagogi wakati gani, kama hapo au baadaye (k.41). Yesuhakudanganywa na umati wa watu waliomfuata. Akawajibu kwa kusema kwanguvu na kutoboa wazi sababu zao za kumfuata. Walitaka kula bila shida na bilagharama, na kupata Masihi atakayewafukuza Warumi. Ila Yeye si huyo.Aliwakemea wale waliodhani kwamba Ufalme wake hasa unahusu mambo yahapo duniani. Walifanana na Msamaria (4:15). Walitawaliwa na matakwa yakimwili, hawakuwa na nia safi ya kumtambua huyo aliyewalisha ni Mwana waMungu. Hawakuwaza kwamba Yeye aliyewalisha anao uwezo wa kuwashibishana chakula cha kiroho, chakula cha uzima. Chakula cha mwili kilihitajika kwamaisha ya sasa, chahusu muda wa kuishi hapa duniani, ila chakula cha kiroho

Page 57: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA546

ni cha lazima kwa maisha ya kiroho kwa sasa na kwa baadaye. Kwa hiyo, Yesualiwaonya wayashughulikie maisha yao ya kiroho, wasifungwe na mambo yadunia hii tu. Aliwakumbusha kwamba ni Yeye peke yake awezaye kuwapatiashibe ya nafsi na maisha ya kiroho, kwa sababu ni Yeye aliye na kibali chaMungu, Baba yake. Katika kusema hayo Yesu alikuwa amesisitiza shabaha yakuishi kwa wanadamu kunakohusu maisha yao ya kiroho na uhusiano wao naMungu. Wao waliwaza matumbo yao, Yesu aliwaza mioyo yao. k.27 kina (a)katazo: msikitendee kazi chakula chenye kuharibika (b) agizo: tendee chakulakidumucho (c) ahadi: ambacho Mwana wa Adamu atawapa (d) thibitisho: huyondiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani Mungu.

k.28ku Yesu alipotaja „msikitendee kazi.....bali chakula kidumucho..‟ walidhanikwamba walitakiwa kufanya jambo fulani „tufanyaje ili tupate kuzitenda kazi aaMungu?‟. Walifikiri kwamba wanaweza kuitikia changamoto yake kwa kufanya„kazi‟ fulani. Ila kosa lao ni kwamba hawakutambua hicho chakula asemachoYesu ni kipawa kutoka Kwake, na hasa ni Yeye Mwenyewe. Yesu alifafanua hiyo„kazi ya Mungu‟ kuwa kumwamini Yeye Mwenyewe, wayakubali madai yake,wajikabidhi Kwake kibinafsi. Ila wao hawakuwa tayari kufanya hivyo mpakawamepewa ishara nyingine zaidi. Ishara ya kuwalisha na mikate mitano tuhaikuwaridhisha. Kuomba ishara ni itikio lao kwa Yesu kuwafundisha kwamamlaka yake mwenyewe, pia ilikuwa dalili ya kutokuamini kwao, hawatakikuamini. Mawazo yao yalirudi nyuma kwa Musa. Musa aliwalisha maelfu ya watujangwani kwa miaka arobaini kwa njia ya mana iliyoshuka kutoka mbinguni. Kwakuwa Musa alifanya hivi, Yeye atafanya nini kuonyesha kwamba anao uwezosawa au zaidi ya Musa? Akifanya zaidi ya Musa atakuwa na mamlaka zaidi yaMusa. Yesu akawajibu kwa kurekebisha mawazo yao kwa sababu wamemwazaMusa zaidi ya Mungu. Ni Mungu, Baba yake aliyewapa mana, si Musa. Musaaliwajulisha mpango wa kuipata tu. Mana yenyewe haikuwa „mkate wa kweli‟mara walipoingia Kanaani ilikwisha (Yos.5:12). Mungu ametoa „mana‟ ya tofautisana, mana iliyo „chakula cha uzima‟. Yesu Mwenyewe ni hicho chakula chauzima, ametoka mbinguni kwa Mungu, na Yeye huupa ulimwengu uzima. Kwamfano wa chakula ameonyesha uhusiano wa ukaribu sana na Babake. Yesu simwokozi wa mwili tu, wala wa Wayahudi tu (Yeye anaupa ulimwengu uzima).Alikuwa amekataa kuwa huyo aliposhinda majaribu yaliyompata alipokuwajangwani. Akakataa tena kuwa mwokozi wa mwili alipojitenga na wale waliotakakumshika awe Mfalme wao.

k.34 Walifanana na mwanamke Msamaria, walitaka kupewa „kitu‟ mara moja,pale pale. Yesu akaupima ukweli wa nia yao kwa kuwapa changamoto ya kujaKwake, ndipo itaeleweka vizuri kama kweli wanamtaka au siyo.

k.35 Alirudia kutamka „Mimi ndimi chakula cha uzima, yeye ajaye kwanguhataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe‟. Yeye si chakula chakutolewa tena na tena ila haina maana kwamba mtu hana haja ya kuendeleakushirikiana naye daima, kila muumini huhitaji „kumla‟ daima. Hata hivyo kiini

Page 58: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA547

cha „njaa‟ na „kiu‟ zake kimetibiwa, hasikii tena hali ya „utupu‟. Wale ambaohawaoni njaa ni wale wanaokuja Kwake, na wale ambao hawasikii kiu ni walewanaomwamini. Jambo kubwa ni kuja Kwake na kumwamini. Yesu alikuwathabiti sana katika kujua kwa hakika kwamba Yeye anao uwezo wa kushibishanjaa na kiu za kila mwanadamu, Yeye ni shibe ya nafsi ya mwanadamu. k.27Yesu alisema atawapa chakula cha uzima na k.35 alisema kwamba Yeye Ndiyehicho chakula.

k.36 Aliwashtaki Wagalilaya kwamba hawakumwamini. Hapo nyuma alikuwaamewashtaki watu wa Yerusalemu jambo hilo (5:36ku) walikuwa wamemwonakama mwenye uwezo wa kuwalisha mkate na kwa sababu hiyo udadisi waouliamka, pamoja na hamu za kimwili kwa chakula, pamoja na nia ya kumpataMasihi wa kisiasa, ila imani ya kujitoa kwake haikuamka mioyoni mwao.

k.37ku Kama ni hivyo, Je! ina maana kwamba utume wake umeshindikana? La,siyo. Makusudi ya Mungu ya kuokoa watu hayazuiliki. Yesu hakuweka tumainilake katika wanadamu kuitikia vema wito wake, bali aliamini kabisa kwambaBaba atatimiza mapenzi yake, „wote anipao Baba watakuja kwangu‟ na katika utiiwake kwa Baba Yeye kwa upande wake atawalinda hao ili wafikie lengo lakuokolewa kwao ambalo ni kufufuliwa siku ya mwisho na kuingia katika uzima wamilele (k.40). Mungu anafanya kazi katika maitikio ya watu kwa ukombozi waYesu. Tukumbuke kwamba Mwana alikuwepo kwa Baba katika umilele (1:1) nakwa sababu hiyo uchaguzi ni wake pamoja na wa Baba. Ila uchaguzi wa Babahaukanushi lazima ya imani, na haja ya uinjilisti. Baba amempa Mwana hao wakuamini na kwa upande wake Mwana huwalinda mpaka uzima wa milele. Yesualiwaonyesha kwamba ilikuwa mapenzi ya Baba yake kwamba watu wamwaminina kujikabidhi Kwake. Hakuna haja ya kumshawishi Baba awaokoe waumini,wala hakuna haja ya kumshawishi Mwana ayatimize mapenzi ya Babake. Hayoni mapenzi yao tangu milele hadi milele. Kwa hiyo Yesu aliwatumainisha watukusudi waje Kwake kwa sababu hakuna amjiaye atakayekataliwa, wala kupotea.Mwisho wa kila mtu amjiaye ni kufufuliwa na Yesu siku ya mwisho. Ni sawa nawakati wa nyoka kuinuliwa juu jangwani, kila mtu aliyetaka kupona, ilimpasaaitazame nyoka wa shaba kwa imani. Vivyo hivyo wakati huo. Mwana wa Adamuamekuja na kila mtu apaswa kumtazama na kumwamini katika hali ya kujikabidhiKwake, ili awe na uzima wa milele. Kwa sababu ni mapenzi ya milele ya Baba naMwana kuwaokoa wote wamwaminio Mwana. Kwa hiyo jambo la kumtazamaMwana, kukata shauri juu yake, na kumpokea ni la maana sana. Ni juu yaokuzingatia hayo aliyosema kwa makini, kuyatia maanani, na kwa hiari ya kutaka,kumpokea.

Yesu alitaka kuwatia moyo wale waliomtafuta kwa nia safi, alitaka wajuekwamba watapokelewa na kushirikishwa baraka zake. Vilevile alitaka kuwashtuawengine waliodhani kwamba hawana haja ya kumjia wajue kwa uhakikakwamba Yeye huhusika kabisa na wokovu wao, na Mungu Baba ametanguliakatika kuchagua wale wa kumwamini ili ayatikise mawazo ya

Page 59: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA548

kufikiri kwamba Mungu ana deni kwao kwa sababu ya haki yao wenyewe.Wakitiwa mashaka huenda watakuwa tayari kubadili mawazo yao juu Yake.

k.41ku Hapo twakuta upinzani wa Wayahudi. Labda ni kundi tofauti na watu wamkutano, au walitoka katika kundi hilo. Yohana alizoea kutumia neno „Wayahudi‟kwa wapinzani wa Yesu. Hao walikwazwa na maneno ya Yesu. Walifanana nababa zao wa zamani walionung‟unika wakati wa Musa kabla na baada ya kupewamana (Kut.16:2, 8, 9; Hes.11:1ku). Hawakupenda madai yake ya kuwa Chakulacha Uzima kilichoshuka kutoka mbinguni. Kwa maneno hayo alidai kuwa na asilitofauti na wanadamu wengine. Yeye si Mgalilaya mwenzao ingawa amezaliwamiongoni mwao. Ametoka mbinguni, ameshuka kutoka juu kwa Baba. Yesuakajibu manung‟uniko yao kwa kuwarudisha kwenye wazo la k.37 kwa kuliwekajambo hilo kwa upande wa kukana. Katika k.37 alisema kwa upande wa hakika„wote anipao Baba watakuja kwangu‟ na katika k.44 alisema kwa upande wakukana „hakuna mtu awezaye kuja kwangu asipovutwa na Baba aliyenipeleka‟.Ni jambo moja likisemwa kwa njia mbili. Ni Mungu atanguliaye kufanya kazimioyoni mwa watu ili wapate kumpokea Kristo. Kosa lao kubwa ni kwambahawamjui Baba, hawakuvutwa na Baba wala hawakujifunza kwa Baba, kwa hiyohawamjii Yeye. Yesu hakuwa na wasiwasi juu ya kutokuamini kwao, alikuwaradhi kabisa na mpango na mapenzi ya Baba yake, hakutikiswa na hali yao yakutokuamini; alijua kwamba baadhi watamwamini, na baadhi hawatamwamini.Kosa lao kubwa hawakuwa na ujuzi wa kweli wa yule ambaye walimwita Munguwao. Katika manung‟uniko yao hao wapinzani walionyesha dharau kubwa nazaidi walikuwa katika hatari sana ya kuisukumia mbali neema ya Mungu ambayoingaliwafunulia na kuwafundisha na badala yake walijitegemea kwamba kwa njiaya kuzungumza na kujadili mambo ya Mungu wataweza kumfahamu vema.Msingi wa ujuzi wote wa kweli za Mungu ni Yesu Kristo. Manabii wa zamaniwalifundisha watu kwamba Mungu atawafundisha watu mioyoni mwao(Yer.31:31ku. Eze.36:24-26).

Ingawa Yohana amekaza madaraka ya Mungu kuchagua hakuacha kusema juuya upande wa pili kuhusu watu kuwajibika kuitikia vema wito wa Yesu nakumwamini. Yesu aliwaonya wale ambao hawakuitika vema juu ya kutokuaminikwao. Kila wakati alitoa nafasi na kuwaita watu waje Kwake. Yeye alikuwa natofauti sana na ile mana ya zamani. Ijapokuwa ilitoka mbinguni kwa Mungu nakuwa chakula cha kipekee, haikuwa na uwezo wa kufanya watu waishi milele bilakufa. Ila wale watakaompokea Yeye aliye chakula cha uzima watashinda mautinao wataishi milele. Kisha alitoa tamko la maana kubwa akilitanguliza na manenoya kutilia mkazo kama desturi yake ilivyokuwa alipotamka neno muhimu. „Amin,amin, nawaambia...‟ Alisemaje? Alisema kwamba Yeye Ndiye sababu kuu yakuishi kwa mtu, Yeye aleta maana halisi kwa maisha ya kibinadamu, Yeye ndiyemwenye uzima wa milele, na kila amwaminiye yuna uzima wa milele. Kwa asiliametoka mbinguni na shabaha yake ni kumshirikisha kila ampokeaye uzimawake, na mwisho wa kila mtu hutegemea kama amejihusisha naye au siyo. Walewa kumpokea watafufuliwa siku ya mwisho na

Page 60: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA549

kushirikiana naye katika uzima wa milele, wale wasiompokea hawataushirikiuzima wa milele.

k.52ku Ndipo Wayahudi walishindana wao kwa wao juu ya njia ya kuula mwiliwake. Yesu aliongeza „na kuinywa damu yangu‟. Jambo hilo liliwakwaza kwasababu katika Torati walikatazwa wasinywe damu wala wasiile nyama yenyedamu ndani yake. Waliona ni vigumu kuyaelewa maneno jinsi yalivyo kwa hiyowalitatizwa juu ya maana yake. Kuula mwili wake na kuinywa damu yake nikuunganika naye jinsi ambavyo chakula kinavyomezwa na kukolewa na mwili.Waumini wa kweli ni wale wanaomtegemea kwa maisha yao yote, wakimjuakibinafsi na kushirikiana naye kwa njia ya imani na utii. Mfano wake ni jinsi Yeyeanavyomtegemea Baba yake kwa yote, akishirikiana naye kabisa (4:34; 5:19;14:10,11). Alirudia kusema jambo hilo alipotumia mfano wa Yeye kuwa Mzabibuwa kweli na waumini kuwa matawi (15:1ku.). Yesu alirudia kusema ile kweli yak.40 katika k.54 akitumia lugha ya mfano. Twajua ni lugha ya mfano kwa sababukatika k.63 alisema „mwili haufai kitu, maneno hayo niliyowaambia ni roho, tenani uzima‟. Hasa lugha iliyotumika ni ya kidhabihu na inaashiria Kifo chake chaMsalaba ambacho kwa Wayahudi kilikuwa kikwazo kabisa.

Bila shaka maneno juu ya mwili na damu ni ukumbusho wa Ushirika Mtakatifu.Katika Injili hiyo Yohana hakutaja habari ya Yesu kuwaagiza wanafunzi wake juuya Ibada hiyo. Tunastahili tuwaze Ibada hiyo tunaposoma maneno hayo, hatahivyo, ni vema kukumbuka kwamba jambo kubwa lililosisitizwa na Yesu ilikuwaimani, k.40 „kila amtazamaye Mwana na kumwamini Yeye, awe na uzima‟ (3:14),kushiriki Chakula cha Bwana bila mtu kujikabidhi kwake hakutamfaidi.

k.54b (k40b, 44b) „nami nitamfufua siku ya mwisho‟ Hata kula na kunywa pekeyake hakutaleta ufufuo.

k.60-66 Wanafunzi waliotajwa hapo ni wale wengi waliomfuata, walipendakuyasikiliza mafundisho yake na kuona matendo yake makuu. Wengi waowaliona mafundisho yake ni magumu, si magumu ya kufahamu bali magumu yakupokea, walinung‟unika na kukwazwa. Madai ya kuhusu asili yake kuwaameshuka kutoka mbinguni na habari za kuula mwili wake n.k. hayo yoteyaliwakwaza sana. Lakini Yesu aliitikiaje hali yao ya kumkataa? Hakuyapunguzamadai yake, wala hakulainisha wito wake wa kujitoa kabisa. Hata aliongeza uzito,kama wamekwaza na neno la kushuka kutoka mbinguni, itakuwajewatakapomwona akipanda na kurudi mbinguni? Je! si watakwazwa zaidiwatakapomwona ametundikwa Msalabani? Watamwonaje Masihi waoakisulibiwa? Yesu hakushindwa wala kuudhika kwa sababu wengi wa haowaliomsikiliza hawakuwa tayari kujitoa Kwake, alijua hawatadumu kuwawanafunzi. Mwaka mmoja ukipita, itakapofika Pasaka, atatundikwa Msalabani,hali ameachwa peke yake.

Page 61: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA550

Katika k.63 alidokezea kuja kwa Roho baada ya Yeye Kupaa na Kurudi kwaBaba. Yesu alikuwa macho, alijua yote yaliyo mbele yake. Faraja yake ilikuwakatika kujua kwamba Mungu hutangulia na kuwasaidia baadhi ya wasikilizajiwake kuamini, nao watakuwa waaminifu, ndiyo sababu alirudia kutaja tena„hakuna mtu awezaye kuja Kwangu asipokuwa amejaliwa na Baba yangu‟.

k.67-71 Ila Yesu alikuwa na mzigo juu ya Mitume. Alionyesha jinsi alivyoguswasana na kutokuamini kwa wale waliomwacha. Akawageukia wale walioandamananaye kwa karibu na kuwauliza juu ya msimamo wao. Je! walitaka kumwachakama wale wengine? Afadhali wapewe nafasi hii ya kuonyesha utiifu wao.Pengine aliwauliza, si kwa faida yake, bali kwa faida yao, ili wakiri wazi msimamowao. Petro akajibu vizuri sana. Kwa niaba yao alikiri upekee wa Bwana wao,hamna mwingine anayewavuta kama Yeye, wala hawaoni mwingine badala yakeatakayewapa uzima wa milele. Tena alijibu kwa lugha ya kuonyesha kwambaimani yao ni thabiti, wameishakata shauri na wanaendelea kwa uaminifukumtegemea Yeye, maana wamemtumaini kwa uzima wa milele, nawanakusudia kuendelea naye. Kisha Petro alimwambia Yesu jinsi walivyomwona„Wewe ndiwe Mtakatifu wa Mungu‟. Kwa maneno hayo walimweka sawa naMungu, maana ni Mungu peke yake aliye Mtakatifu, wa pekee, tofauti kabisa nawengine wote. Huo ndio uamuzi wao baada ya kuandamana naye kwa muda.Matumaini waliyokuwa nayo walipoanza kumfuata (1:41, 45) yangali yakiendeleakuthibitishwa. Wakati huo walionyesha ujasiri wa kuendelea kumfuata, walijitoaupya kwa Yesu, wakati mgumu wa wengi kumwacha na wakati ambapo Yesuamesema maneno magumu ambayo waliyafahamu kwa shida. Ndipo Yesuakaendelea kwa kuwakumbusha kwamba ni Yeye aliyewachagua, hakupendawajione kuwa bora kuliko wale wengine, wamekuwa walivyo kwa sababu Yeyeamewachagua.

Hata hivyo Yesu alijua mmoja wao hakumfuata kwa moyo ingawa alikuwa pamojanaye kimwili. Alikuwa amejificha na ajabu ni kwamba hakujitokeza wazi nakumwacha Yesu wakati huo wa kupata nafasi nzuri ya kufanya hivyo,asingalikuwa peke yake. Wenzake walikuwa hawajamtambua, wala hata mpakausiku wa mwisho walikuwa bado hawakumtambua ila Yesu alimfahamu tangumwanzo. Yesu hakumchagua ili amsaliti la! alimchagua awe mwanafunzi wakekama wale wengine. Haifikiriwi kwamba angalimchagua kumsaliti. Kwa sababuYesu anajua mioyo ya watu wote alifahamu upo uwezekano wa Yuda kufanyajambo hilo baya. Bila kuitegemea rehema ya Mungu hakuna awezaye kudumukuwa mwaminifu. Haieleweki kwa nini Yuda hakushika nafasi aliyopewa yakuondoka maana alifahamu kwamba Yesu amemgundua na kwa manenoaliyosema Yesu amemjulisha hivyo. Yesu hakutamka jina lake ila alisema „mmojawenu ni shetani‟ maneno ya kuashiria kwamba nyuma ya jambo hilo ni Shetani(13:2, Mk.8:33). Yohana alitaja jina lake na usaliti wake alipoiandika Injili hiyo.

Page 62: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA551

MASWALI1. Unafikiri Yesu alikuwa na shabaha gani alipowashirikisha wanafunzi wake

katika shughuli za kuwalisha watu wengi?2. Walijifunza nini kuhusu huduma yao ya baadaye?3. Kwa nini watu walitaka kumshika Yesu na kumfanya awe Mfalme wao? na

kwa nini Yesu alijitenga nao na kupanda mlimani ili aombe?4. Yesu alikuwa na maana gani aliposema juu ya Yeye kuwa Chakula cha

Uzima?5. Yesu alikuwa na maana gani aliposema „msipoula mwili wake Mwana wa

Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu‟?6. Kwa nini watu wengi walikwazwa na kumwacha Yesu wakati huo?7. Yesu alitoa changamoto gani kwa Mitume? nao waliitikaje?

7:1 - 11:53 MUDA WA MIGONGANO

a) Yaliyotokea kabla ya kuhudhuria Sikukuub) Kutokuamini kwa ndugu zakec) Mkanganyiko wa watud) Yesu alijidhihirisha wazie) Maitikio ya watu mbalimbalif) Wito maalum wa kumjia

Kipengele: Mwanamke aliyefumaniwa katika kuzinig) Kuwakabili Mafarisayo na kuhojiana naoh) Mazungumzo na Wayahudi waliomwaminii) Kumponya mtu aliyezaliwa kipofuj) Mazungumzo juu ya kuwa Mchungaji Mwemak) Mabishano yaliyotokea katika Tao la Sulemanil) Yesu alimfufua Lazaro

Katika sehemu hiyo twaona mambo mawili; jinsi upinzani ulivyozidi na jinsibaadhi ya watu walivyozidi kumwamini Yesu. Wengine walitatizwa sana,hawakujua waamue nini juu ya Yesu; ila wengine walikuwa wamekwisha kukazania zao za kumpinga, walizidi kumsema kwa wazi. Pamoja na hao walikuwapowatu ambao wameishakata shauri la kumpokea Yesu, na imani yao ilizidikuimarika. Katika muda wa mabishano watu walikuwa bado hawajakaza mawazoyao ila katika muda huu wa migongano twaona kwamba watu wamezidi kukazamsimamo wao. Ni wakati wa migongano mingi.

7:1-2 Yaliyotokea kabla ya kuhudhuria Sikukuu

Hapo twaona maneno yanayoonyesha kwamba watu wamekwisha kuamuamsimamo wao, wale wa Yudea na hasa wakuu. Yesu alitambua kwamba haowako tayari kumwua kutokana na uponyaji wa kiwete siku ya Sabato paleYerusalemu (5:18). Kwa hiyo, afadhali ajihadhari na hao, asiende kusini isipokuwakwa kufuata desturi yake ya kuhudhuria Sikukuu. Yeye alifahamu

Page 63: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA552

kwamba ni mapenzi ya Babaye afe kwa dhambi za ulimwengu, ila bado alihitajimuda wa kuwaandaa wanafunzi wake ili waweze kuzieneza habari zake baadaya Yeye kuondoka na kuwaachia kazi hiyo. Kwa wakati huo hawajawa tayari.Hivyo, hawezi kuuawa kabla ya wakati ulioamriwa na Baba ambao ni bado.

Sikukuu ya Vibanda ilikuwa Sikukuu ya kumshukuru Mungu kwa mavuno pamojana kukumbuka kwa shukrani jinsi Mungu alivyowatunza jangwani muda wote wamiaka arobaini kabla ya kuingia Kanaani. Ilikuwa Sikukuu ya furaha sana, watuwalijenga vibanda na kukaa humo kwa siku saba. Wakati huo watu walimtazamiaMasihi kwa hamu, wakifikiri kwamba Yeye atawaongezea mibaraka mingi.Walichinja wanyama wengi, walipiga tarumbeta hekaluni, na kila siku, isipokuwaile ya mwisho, walileta maji kutoka Siloamu. Waliwasha taa kubwa za hekalu.Waliamini kwamba walipoishi jangwani katika mahema Mungu alikuwa kati yaokatika Hema la Kukutania. Kwa wakati huo waliamini Mungu yu pamoja naokatika Hekalu la Yerusalemu.

Hema na Hekalu vilikuwa vivuli tu vya Kuwako kwa Mungu. Vilikuwa ishara yamambo ya baadaye atakapotokea yule atakayekuwa Hekalu halisi, yaani YesuKristo. Yeye ndiye Imanueli, Mungu pamoja nasi, Yeye ndiye Njia, na Kweli, naUzima, na kwa njia yake watu watamjia Baba (14:6). Kwa hiyo mawazo ya watuyalitofautiana na mawazo ya Yesu, kwa sababu walikuwa hawajautambua ukweliwa Yeye kuchukua mahali pa hekalu, hawakumwelewa kuwa „Mungu pamojanasi‟.

Mambo tunayosoma katika sehemu hiyo yote yalitokea kati ya Sikukuu hiyo yaVibanda na Sikukuu ya Pasaka, muda wa kama miezi sita, muda uliotanguliaKuuawa Kwake.

7:3-9 Kutokuamini kwa ndugu zakeVifungu hivi vinaonyesha jinsi ndugu zake wa kimwili walivyomwaza. Hao nduguwafikiriwa kuwa wale waliozaliwa kwa Mariamu na Yusufu baada ya Yesukuzaliwa. Hao walifikiri ni vema ndugu yao Yesu aende Yerusalemu nakujidhihirisha wazi, si vizuri aendelee kujificha, akijitokeza wazi hadharani mbeleya watu wengi wakati wa Sikukuu, na kufanya maajabu, ndipo atafaulu kuwavutawengi kwake. Kwani wamhimize? Tumepewa jibu katika k.5, hawakumwamini, sikwamba hawakuzisadiki zile ishara zake ila hawakumsadiki kuwa Masihialiyetumwa na Mungu, mwenye asili katika Mungu Mwenyewe. Yawezekanawalisema hivi kama jibu lao kwa watu kumwacha Yesu jinsi tulivyosoma katika6:60. Afadhali ndugu yao afufue kampeni yake kwa kwenda kusini na kujitokezawazi huko. Lakini Yesu hakupokea shauri lao. Hakutafuta heshima na ukuu kwaajili yake mwenyewe. Alifahamu kabisa kwamba ametumwa kuukomboaulimwengu kwa njia ya kufa kwa ajili ya dhambi. Aliona wakati wa kuondoka nakujidhihirisha wazi haujaja bado. (Katika k.30 Yohana alisema juu ya wakati wakuutimiza Utume wake, alitumia neno tofauti na hilo la k.8). Akiwahi kufikakwenye Sikukuu wakuu watakuwa na nafasi ya kutosha

Page 64: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA553

kufanya mipango ya kumwondoa, kwa hiyo, atatelemka kusini bila wenginekufahamu mpango wake. Aliwahimiza ndugu zake wamtangulie na kuondoka bilaYeye, maana hao hawachukiwi, hawawindwi, wala hawatauawa. Lakini Yeyesiyo, uhusiano wake na ulimwengu ni tofauti na uhusiano wao na ulimwengu,wao ni wa ulimwengu huu na ulimwengu unawapenda walio wake (15:19). Yeyesi wa ulimwengu huu, Yeye yu kinyume chake, Yeye huushuhudia uovu wake, nakwa sababu hiyo ulimwengu ulimchukia. Yeye yu radhi na mapenzi ya Babayake, na yu tayari kuyatimiza kwa kufuata mipango yake. Yesu alijua kwa hakikakwamba wakati utafika atakapokataliwa na kuuawa, ila mpaka wakati huoatajihadhari na hali za chuki na uadui uliopo. Kwa hiyo, ndugu zake walimtanguliana Yeye akaja baadaye kwa siri.

7:10-13 Mkanganyiko wa watuKwa kawaida Yesu alitazamiwa kwenye Sikukuu ila katika Sikukuu hiyo mashakayalikuwepo kutokana na chuki za wakuu. Hivyo, watu hawakuwa na hakikakwamba atafika. „yuko wapi yule‟ (k.11) maneno hayo yaashiria jinsi Yesualivyojulikana sana hata ilitosha kusema „yule‟.Yohana ameonyesha jinsi watu walivyogawanyika katika mawazo yao juu yake.Walikuwapo „Wayahudi‟ waliomtafuta, yafikiriwa walitaka kumwua (k.1) Nia zaozilikazwa, kwa hiyo walimtafuta, si mara moja tu, ila kila wakati, kusudi wamnasekatika mazungumzo yake, ndipo wapate ushuhuda wa kuleta kesi juu yake. Haliyao ilitawala mawazo ya watu katika siku za kwanza za Sikukuu (k.13).

Halafu wengine walimtetea Yesu, walimwona ni mtu mwema, mtu asiye na dosari(k.12). Kisha walikuwapo wale waliomfikiria kuwa laghai, mtu aliyekuwaakiwadanganya watu (k.12). Kwa hiyo, umati wa wenyeji wa Yerusalemuwalichanganyikiwa, hawakujua wamwazaje huyo Rabi wa Galilaya. Kwa siri watuwalimzungumzia sana wakihisi kama atafika kwenye Sikukuu au siyo. Kila mtualishurutishwa akate shauri juu yake.

7:14-19, 21-24, 33-34 Yesu alijidhihirisha wazik.14-15 Katikati ya Sikukuu Yesu alisafiri mpaka Yerusalemu na inaonekanaalikwenda moja kwa moja mpaka hekaluni, akaanza kufundisha (Mal.1:3:Zek.14). Alifafanua Maandiko akionyesha ufahamu mwingi wa Agano la Kaleingawa hakusoma katika Shule za Marabi. Alifanya bila kuomba ruksa aukuomba radhi. Kwa kufanya hivyo alidai kuwa na mamlaka na haki ya kusikilizwakama Rabi yeyote mwingine. Hakujali jinsi watu walivyomwaza. Hakujisikia kamaamepungukiwa kitu. Hata adui zake walilazimishwa kukiri kwamba alifundishavizuri sawa na wale walioelimishwa katika shule za marabi.

k.16ku Pamoja na kujiinua na kujichukulia mamlaka ya kuthubutu kufundishapale Hekaluni, pia, alijidhili. Alikiri wazi kwamba Yeye mwenyewe hakuwa asiliya mafundisho yake, mafundisho yake na uwezo wake na mamlaka yake

Page 65: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA554

vilitoka kwa Baba yake, yule aliyemtuma. Kwa hiyo, kama ambavyo tumeonamara kwa mara katika Injili hiyo, Yesu alisisitiza uhusiano wake wa kipekee naBaba yake, Yeye ametumwa na Baba, na kuleta ujumbe wa Baba. Ujuzi alio naohutokana na ushirikiano wa ukaribu sana na Baba, anayo nafasi ya kujua mamboya Mungu kwa sababu ametoka ndani ya Mungu. Pia, mamlaka yakeimefungamana na uongozi wa Babaye. Hakufanana na marabi waliotegemeamafundisho na maandiko ya marabi maarufu. Walifundisha kwa kutumiamadondoo mengi ya wenzao. Yesu hakuwa na haja hiyo.

k.17 Neno hilo lilikuwa kubwa na dai lake liliwapa shida wasikilizaji wake. Yesualiwapa njia rahisi ya kuupima ukweli wake. Kwa kufanya mapenzi ya Mungu,watahakikishiwa ukweli wa mafundisho yake. Kwa kawaida, wanadamu wapendakujua kwanza, ndipo kufanya. Lakini Mungu hutaka wafanye kwanza ndipowatajua. Kwa njia hiyo mambo ya Mungu hulindwa, Mungu hawezi kuchezewa,anapatikana kwa aliye na nia safi na lengo la haki. Yeyote atakayejitoa kufanyamapenzi ya Mungu atahakikishiwa ukweli wa imani yake.

k.18 Halafu Yesu alisisitiza ukweli wa mtu asiyetafuta sifa yake mwenyewe balisifa ya yule aliyemtuma. Usafi wa nia yake ulionyeshwa katika Yeye kutafutamapenzi ya Baba yake wakati wote na kumtegemea kwa yote. Twakumbushwamaneno ya Yesu alipotamka „Heri walio na moyo safi, Maana hao watamwonaMungu (Mt.5:8).

k.19ku Ndipo Yesu aliendelea kusema juu ya Musa, na kwa ujasiri aliwashtakikwamba ijapokuwa walimsifu Musa sana kwa sababu aliwapa Torati, ukweli nikwamba hawaitendi. Walikuwa njiani kuvunja amri ya sita kwa sababu walikuwawakitafuta kumwua; aliwauliza waziwazi „Mbona mnatafuta kuniua?‟.

k.21ku Chuki yao ilianza lini, na kwa sababu gani? Ilianza wakati alipomponyakiwete siku ya Sabato (sura 5). Hii ndiyo „kazi moja‟ (si kwamba alifanya moja tu).Yeye aliwashtaki kuwa wavunjaji wa sheria, kwa sababu walitafuta kumwua, nawao waliona kwamba Yeye amekuwa mvunjaji wa sheria kwa kumponya kiwetesiku ya sabato. Alinyosha mawazo yao juu ya tohara. Wao walisema ni Musaaliyewapa tohara, lakini hakuwa Musa, bali Ibrahimu. Wao walizoea kumtahirimtoto siku ya Sabato, kwa sababu ilimpasa mtoto atahiriwe siku ya nanehaidhuru siku hiyo ilikuwa Sabato au siyo. Eti! ikiwa mtoto alikatwa sehemundogo sana ya mwili wake kwa kuhifadhi Agano, siku ya Sabato, Je! Yesu kwakuuponya mwili wa mtu na kumfanya awe mzima katika siku hiyo, amefanya kosagani? Kama kutahiri kulitangulia Sabato katika umuhimu wake; Je! ni sawakuuponya mwili wa mtu siku hiyo? Yesu hakuwa na maana kwamba walivunjaTorati kwa kuwatahiri watoto siku ya saba ila alitaka warekebishe mawazo yaojuu ya uponyaji alioufanya. Yesu hakuwaruhusu wadharau na kuisema vibaya ilekazi njema ya uponyaji. Aliwasihi wapime mambo vizuri na kwa haki, si kwajuujuu. Yesu si adui wa dini yao wala wa Torati yao, ila katika Yeye malengo yadini na Torati yao hutimizwa.

Page 66: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA555

Halafu ilitokea migongano kati ya watu, na hiyo tutaitazama katika fungu lifuatalo.

k.33-34 Kisha Yesu aliwaambia kwamba atakuwa nao kwa muda mfupi ndipoataenda zake kwa yule aliyempeleka, yaani Baba yake, na hapo hawatawezakumpata, hawatamwona, wala hawataweza kufika. Maneno hayoyaliwatatanisha sana.

7:20, 25-32; 35-36 Maitikio ya Watu mbalimbaliWatu walikwazwa na maneno ya Yesu alipowashtaki kwa wazi kwambawalikuwa wakitafuta kumwua. Wakamjibu „Ama, ana pepo!‟ Waliona mwenendowake ni kama mwenye wazimu (10:20) wakijiona kwamba ameonewa nakushikwa na madanganyo ya fahari.

k.25-32 Sehemu hiyo inaonyesha kuchanganyikiwa kwa watu. Jambo la Sabatoliliachwa na badala yake Yohana aliendelea na mazungumzo kumhusu YesuMwenyewe kuwa na asili gani. Watu walishangaa kuuona ujasiri wa Yesualiyeendelea kufundisha hekaluni kila siku. Pia walishangaa kuona kwambawakuu wamenyamaza. Mbona wale waliomtafuta hawakumshika? Hatawalithubutu kusema kwamba inawezekana hata wakuu walijua kwa hakikakwamba Yesu ni Masihi. Ila tatizo ni kwamba wao walifikiri Masihi atatokeaghafula, bila mtu kujua mahali alipotoka, ila Yesu walimfahamu, ametokaNazareti, ameenda kuishi Kapernaumu, hivyo hakuweza kuwa Masihi.

Wakati wa hayo yote kuzungumziwa, Yesu mwenyewe aliendelea kuwafundishawatu. Kwa shauku, akaipaza sauti na kuwaambia „Mimi mnanijua na hukonitokako mnakujua; wala sikuja kwa nafsi yangu; ila yeye aliyenipeleka ni wakweli, msiyemjua ninyi‟. Walijua ametoka Nazareti wa Galilaya, ila hawakujuaametoka mbinguni kwa Mungu, wala hawakuelewa siri ya Nafsi yake kuwaMwana pekee wa Baba. Alirudia kusisitiza uhusiano wake wa ukaribu sana naBaba. „aliyenipeleka ni wa kweli‟ ina maana ya uhalisi wa Mungu, Wayahudiwote waliamini ukweli wa Mungu kuwako ila shida yao ilikuwa hawakuaminiuhalisi wa Yesu kutumwa na huyo Mungu wao. Walizidi kukwazwa na walitakakumshika mara ila walishindwa kufanya lolote kwa sababu watu wengiwalimpenda sana. Hao walivutwa na ishara nyingi alizozifanya, hizoziliyathibitisha madai yake ya kuwa Masihi. Watu waliona hakuna mwingineatakayeweza kumzidi kwa uwezo na ya kuwa yamkini huyo ni Masihi kweli.Mafarisayo hawakupenda watu wazungumzie mambo ya Yesu (k.12-13) nawalipoyasikia mawazo hayo ya mkutano wakawatuma watumishi ili wamkamateYesu wakitaka kumkomesha na kuzuia watu wasiendelee kumfuata.

k.35-36 Hapo Yohana ameandika itikio lao kwa maneno ya Yesu juu yakuondoka na kwenda mahali wasipoweza kumfuata wala kufika. Walihisi kwambaatakwenda na kuwafundisha Wayahudi waliotawanyika kati ya Mataifa,

Page 67: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA556

wale waliotumia lugha ya Kiyunani hata pengine atawafundisha Wayunani pia.Bado wangali wanawaza mambo ya kimwili, walishindwa kuelewa maana yakeya kiroho ya kurudi mbinguni kwa Baba, kule alikotoka.

7:37-52 Wito maalum wa kumjiaSiku ya mwisho ya Sikukuu ilikuwa kubwa, ilihesabiwa kama siku ya kufungaSikukuu zote za mwaka. Kila siku ya Sikukuu maji yaliletwa na makuhani katikachombo cha dhahabu kutoka Birika la Siloamu na kumiminwa madhabahunihuku watu wakiimba maneno ya Isa.12:3 „Kwa furaha mtateka maji katikavisima vya wokovu‟. Walifanya kumbukumbu ya jinsi Mungu alivyokata kiu zaojangwani kwa kuwapatia maji kwa njia ya Musa kuupiga mwamba; mwambaulipigwa na maji yakatoka. Pamoja na kumbukumbu hilo walitazamia mavunowalitumaini kupata mavuno kwa kujaliwa kupata mvua ya kutosha. Hatujui kwahakika walifanya nini siku ya nane, kama siku ya saba au nane ilikuwa yamwisho. Maneno ya Yesu yalikuwa muhimu kabisa yakilingana kabisa naSikukuu hiyo.

Yesu alisimama hadharani mahali ambapo watu waliweza kumwona bila shida,akapaza sauti na kutoa wito maalum ili watu wote wapate nafasi ya kumsikia nakuitika. Alimwita kila mtu mwenye kiu aje Kwake anywe. Badala ya maji ya kimwiliYeye atoa maji ya kiroho, maji ya kweli; badala ya kufuata taratibu fulani, watuwalitakiwa kumjia Yeye, wajihusishe naye kwa njia ya kumwamini kibinafsi ndipowatajua uhalisi wa uwezo wake wa kukata kiu zao, kiu za kiroho na kiu za kimaisha.

Tena katika ujuzi wa maisha watasikia baraka tele zikibubujika ndani yao. (Kamamwamba ulivyopigwa jangwani ndivyo Yesu atakavyopigwa Msalabani, na baadaya Kufa atafufuka na kupaa kwa Baba, kisha Yeye na Baba watatoa RohoMtakatifu). Habari hiyo ilikuwamo katika Maandiko yao ya Agano la Kale. Yatajwakatika Zek.14:8; Yoe.3:18; Eze.47:1ku; Zab.46:4; Halafu Yohana alielezakwamba hilo jambo lilihusu Roho Mtakatifu, (Linganisha na mazungumzo yaYesu na Nikodemo (3:5-7) na mwanamke Msamaria (4:10-15; 23).

Sharti la kwanza kwa mtu kuwa na Roho ndani yake ni kumwamini Kristo katikahali ya kujikabidhi Kwake. Ni jambo la moyo si la akili wala si jambo la hewani,yampasa mtu akate shauri la kumpokea Yesu. Sharti la pili kuhusu Roho nikwamba inampasa Yesu „atukuzwe‟ pale Msalabani ainuliwe juu ya mti, ndipokufufuka kutoka kwa wafu, kisha kupaa na kurudi kwa Baba, ndipo Yeye na Babawatatoa kipawa cha Roho. Siku ya Pentekoste Roho akashuka. Roho hakuwezakufanya kazi yake kwa utimilifu mpaka Yesu aliposulubiwa kwa ajili ya ukomboziwa ulimwengu. Roho atatimiliza Huduma ya Yesu baada ya kufa kwake(Mdo.1:1ku „Yesu aliyeanza..‟). Kwa Yohana mahali pa Yesu kutukuzwa niMsalabani (Yn.17:1ku). Yesu hakuwa na maana kwamba Roho hakufanya

Page 68: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA557

kazi katika manabii na katika Yeye, ila Roho hatafanya kwa utimilifu mpakabaadaye.

k.40ku Watu waliitika wito wa Yesu kwa njia mbalimbali. Baadhi walimkubalikama „nabii yule‟ yule ambaye Musa alisema atakuja (Kum.18:15); bila shakaYesu aliposema juu ya maji walikumbuka jinsi mababa zao walivyopewa majijangwani wakati wa Musa kuupiga mwamba. Wengine walimwona kuwa Masihi„huyu ndiye Kristo‟. Ila imani zao hazikuwa thabiti. Wengine walichanganyikiwajuu ya mahali alipotoka, walifikiri ni Galilaya na unabii ulisema atazaliwaBethlehemu. Ama hawakufahamu habari ya kuzaliwa kwake Bethlehemu auwalitawaliwa na jinsi alivyolelewa na kuishi Nazareti katika eneo la Galilaya.Kutokana na hayo yote matengano yalitokea, na walikuwepo wale waliotakakumkamata; hapo nyuma tulisoma habari zao (k.19,25).

k.45ku Ndipo wale watumishi waliotumwa kumkamata wakarudi kwa wakuu wamakuhani na Mafarisayo bila kumleta Yesu. Walipoulizwa sababu, wakajibukwamba walishindwa kufanya lolote baada ya kumsikiliza. Wakatoa ushuhudawa ajabu „Hajanena kamwe mtu yeyote kama huyu anavyonena‟. Badala yakumkamata Yesu, Yesu alikuwa ameukamata usikivu wao. Hawakushindwa kwasababu ya umati wa watu ila kwa maneno ya mtu mmoja, yule waliyetumwakumshika. Ndani ya ushuhuda wao, Je! kuna dokezo la kuelekeza mawazo kwaUungu wa Yesu, „hajanena kamwe mtu yeyote kama huyo‟. Mafarisayowakawakasirikia na kuwalaumu. Walionyesha chuki na kiburi waliposema „ninyinanyi mmedanganyika? Ni nani katika wakuu amwaminiye, au katikaMafarisayo?‟. Wao walikuwa wakuu, makuhani na Mafarisayo, waliodhanikwamba wanajua mambo. Waliotumwa walikuwa walei, waliodhaniwa kuwahawajui mambo!! Lakini walei wakishikwa na kweli ni vema wakuu wajihadhari!Wakuu walizoea kuwaza akina yahe kuwa watu wasioifahamu Torati walakuitimiza, watu walio chini ya laana ya Mungu.

k.50ku Hapo Nikodemo ametajwa akiwa katika mkutano ulioshughulikia mpangowa kumwondoa Yesu. Bila shaka mazungumzo hayo yalikuwa kwa siri, maanayalihusu kumkamata Yesu na kumshtaki, hata kumwua. Yeye alitaka wafuatebarabara masharti ya Torati katika jambo hilo. Alitaka Yesu apate haki ya kupewanafasi ya kujieleza na kujitetea, kama ilivyosema Torati, kabla hawajachukuahatua nyingine juu yake. Kwa jinsi walivyomjibu walibomoa tumaini lake lakuwavuta wajihoji kwanza. Hawakumjibu juu ya kufuata Torati kwa usahihi ilakwa kumwambia ayachunguze Maandiko kuona kama nabii yeyote alitokaGalilaya. (Yafikiriwa Yona alitoka kaskazini Yon.1:1; 2 Waf.14:25 pia Hosea naNahumu). Mpaka hapo wakuu wameshindwa kumkamata Yesu, askariwaliguswa na maneno yake, kiasi cha kushindwa kumleta; Nikodemoamewasahihisha juu ya utaratibu wa Torati; huku umati wa watu bado wangaliwakimwona Yesu kuwa ama „nabii yule‟ ama „Masihi‟. Yesu Mwenyewe alikuwajasiri na thabiti. Alikuwa ametoa wito maalumu kwa mtu yeyote kumwamini nakumjia, akiwa na uhakika juu ya uwezo wake wa kumpatia kila mtu shibe ya

Page 69: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA558

nafsi yake. Twajifunza kwamba Yesu hutamani kutoa kipawa kikuu na bora chaRoho Mtakatifu. Kuja kwa Roho kumefungamana kabisa na Yesu kutukuzwa.

MASWALI1. Eleza uhusiano wa Yesu na ndugu zake wa kimwili jinsi ulivyoonekana

katika k.3ku.2. Eleza uhusiano wa Yesu na ulimwengu k.7ku.3. Eleza uhusiano wa Yesu na Baba yake4. Eleza tofauti kati ya mafundisho ya Yesu na marabi5. Chuki ya viongozi ilianzia lini? Yesu aliwashtaki nini? na wao walimshtaki

nini?6. Katika siku ya mwisho wa Sikukuu Yesu alitoa wito gani na kutoa ahadi ya

nini?7. Eleza uhusiano kati ya Yesu na Roho Mtakatifu.8. „Hajanena kamwe mtu yeyote kama huyu anavyonena‟ ni akina nani

waliosema maneno hayo, na wakati gani?9. Ni mambo gani yaliyowatatanisha watu hata walichanganyikiwa juu ya Yesu?

7:53-8:11 Mwanamke aliyefumaniwa katika kuziniHabari hii iliyowekwa katika mabano haionekani katika Nakala nyingi za kwanzaziliko za Maandiko. Katika nakala zingine imewekwa mahali pengine, kuelekeamwisho wa Injili hii au baada ya Luka 21:38. Nakala za baadaye zinayo habarihii.

Yafikiriwa kuwa habari iliyotokea kweli, haifanani hata kidogo na hadithi zilizomokatika maandishi ambayo hayakukubalika kuwekwa katika Kanuni ya Vitabu vyaMaandiko Matakatifu. Inapatana kabisa na tabia ya Bwana Yesu na hudumayake. Labda iliwekwa mahali hapo kwa kusudi la kutia nguvu maneno ya 8:15 na8:46 „simhukumu mtu‟ na „nani anishuhudiaye nina dhambi?‟.

Ni hapo tu katika Injili hiyo Waandishi na Mafarisayo wametajwa pamoja. Tukiohilo lilitokea Yesu alipokuwa akifundisha katika Ua la Hekalu, mahali ambapomarabi walikutana na wafuasi wao. Wengi walikuwa wakimjia Yesu ili wamsikilizena kumwuliza maswali. Ndipo, kama kwa ghafula, palitokea kishindo cha kundila wanaume wakija kwa nguvu, wakipita kati ya watu na kufika mbele ya Yesu,hali wamemshika mwanamke. Kwa jinsi mambo yalivyotokea inaonekana jambohilo lilikuwa limepangwa na hao wanaume. Katika hila yao wamemfumania huyumwanamke katika tendo la uzinifu, wamemshika na kumleta kwa Bwana Yesukwa lengo la kumnasa Yesu. Walimweka katikati, mbele za watu, kamakumwaibisha sana, wakitaja kosa lake wazi.

k.5 Kifungu hicho chatoboa wazi nia yao na hila yao. Walifikiri kwamba Yesuatashindwa kupata njia ya kuepukana na hoja yao. Ni kweli wamemkamata

Page 70: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA559

huyo mama katika tendo hilo baya. Tena sheria ya Musa ilisema wazi kwambawenye kutenda dhambi hiyo wauawe ama kwa kupigwa mawe au kwa njianyingine (Law.20:10; Kum.22:22ku). Kwa hiyo, walimbana Yesu kati ya mawili„Musa alituamuru‟ na „nawe wasemaje‟? Tanzi kweli! Atatokaje katika tanzi hilo?Akiamua mwanamke aachiliwe, atakuwa amekwenda kinyume cha Musa nasheria, nao watakuwa wamefaulu kupata shtaki juu yake. Akiisimamia sheria yaMusa watu watapoa na kuona kwamba Yeye si rafiki wa wenye dhambi na waliodhaifu.

k.6 Kwa kifungu hicho twaweza kupima kiasi cha chuki yao kwa Yesu na hila nabidii yao katika kutafuta njia ya kumwondoa. Hawakuwa na mzigo juu ya wokovuwa huyo mama, hawakuwa na mzigo juu ya haki ya kuuondoa uchafu wa mji wao,wala hawakuwa na mzigo juu ya sheria. Walimtumia huyo mama kama chombocha kumtega Yesu. Wako tayari kuua na kuivunja amri ya Musa iliyosema „usiue‟huku wakidai kuwa na mzigo juu ya amri iliyosema „usizini‟. Walikuwa wanafiki.Huyo mama amekuwa kama chambo katika mtego. Waliendelea kumwuliza Yesuna kumsukuma atoe jibu wakifikiri kwa vyovyote atajinasa. Ila machoni mwa Yesuugumu wa mioyo yao ulikuwa dhambi sawa na uzinifu wa huyo mama. Kwa ninihawakumleta mwanaume aliyehusika ili ashiriki aibu na hukumu yake? Je!walikuwa wamemwachilia? Je! alikuwa ametoroka? au vipi? au pengine walikuwawamepatana naye? Walijuaje jinsi watakavyompata huyo mama katika tendo hiloambalo kwa kawaida hufanyika sirini? Sheria ilisema kwamba wote wawiliwahukumiwe (Kum.13:9; 17:7).

k.6bku Yesu alifanyaje? Aliinama, akaandika kwa kidole chake katika nchi. Nikama hakupenda kushiriki aibu ya mambo hayo yaliyotendeka mbele ya watu.Pengine alikuwa amewakasirikia kwa ugumu wa mioyo yao. Hatujui aliandikanini. Watu wamehisi mambo mbalimbali, ila hatujui. Labda kwa kutumia kidolealiashiria mamlaka yake ya kuhukumu (Lk.11:20; Kut.32:16) pamoja na haki yakeya kusamehe (Mt.9:1-8). Ijapo hatujui aliandika nini tunajua kwa hakika manenoaliyosema. Walipozidi kumhoji, akainuka, akawaambia, „Yeye asiye na dhambina awe wa kwanza wa kumtupia jiwe‟ kama isemavyo katika Kum.17:2- 7.Kumbe! kwa njia ya ajabu Yesu akafyatua mtego wao, badala ya Yeye kutegwa,wao walibanwa, ama wakiri kuwa wenye dhambi na kuondoka bila kumpigamawe huyo mama, au wakatae kwamba ni wenye dhambi ndipo wampige mawehuyo mama. Aliwaruhusu wampige kwa mawe ikiwa dhamiri zao ziliwaruhusukufanya hivyo. Kwa sheria ilitakiwa kwamba washtaki wawe wa kwanza kutupiamawe ikiwa hawakuhusika katika kosa lenyewe, tena wawe wamejitahidikulizuia. Kumbe dhamiri zao ziliwashtaki, nao wakaondoka mmoja mmoja. Yesuhakuwa mlegevu kwa Torati kama walivyodhani na kama walivyotaka kumshtakikuwa; alitia maanani dhambi za kila mtu wa pande zote.

Yesu alimfanyia huyo mama kwa adabu, kama mwanadamu mwenye hakisawa na wengine, si kama chambo cha kutumiwa katika mtego. Yesuhakumbana katika tendo lake baya alililotenda hapo nyuma tu, bali aliwaza

Page 71: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA560

maisha yake ya mbele „usitende dhambi tena‟. Badala ya kumpiga kwa mawe,Yesu akamwokoa, hakuja duniani kuhukumu bali kuokoa (3:17; 12:47).Hakusema kwamba tendo lake halikuwa dhambi, alilitaja kuwa dhambi.Alipomsamehe hakuilegeza sheria, bali alikusudia kumtia nguvu ili aiachedhambi, na aanze upya. Hakutaka huyo mama apate madhara huku yulealiyefanya naye ameachiliwa.

k.11 Mwanamke alisema machache tu, hakutoa udhuru wowote kwa dhambiyake, wala hakusema lolote juu ya washtaki wake. Bila shaka alikuwa namshangao mkubwa kwa jinsi Yesu alivyomtendea. Wasio na haki ya kumhukumuwalikuwa wameondoka, mwenye haki ya kumhukumu, Yule asiye na dhambi,alibaki naye, na kwa sababu atatoa fidia ya dhambi, aliachilia haki yake yakumhukumu. Katika hayo yote twaona hekima ya Yesu (Kol.2:3).

8:12-30 Kuwakabili Mafarisayo na kuhojiana naoYesu alikuwa hekaluni katika chumba cha hazina (k.20) na hapo alizungumza naMafarisayo (k.12-30) na Wayahudi waliomwamini (31-59). Katika sehemu hiyoyote Yesu alisisitiza madai yake akijipambanisha na wale wenye msimamo tofautina Yeye kwa kutumia neno „Mimi‟ zaidi ya mara ishirini.

Inaonekana mazungumzo hayo yalitokea wakati wa Sikukuu ya Vibanda (7:2).Yafuata mambo ya sura ya saba tukikubali kwamba 8:1-11 ni kipengele. Jambomoja kubwa katika Sikukuu hiyo lilikuwa kuleta maji kutoka Birika la Siloam kilasiku, ndipo katika siku ya mwisho Yesu alitoa wito maalum kwa kila mwenye kiukuja Kwake na kunywa maji yaliyo hai (7:37ku). Mwanzo wa Sikukuu hiyo taa nnekubwa za dhahabu, zilizokuwamo katika Ua la Wanawake ziliwashwa, watuwalifurahi sana sana, wakiwasha mienge na kucheza na kuimba kwa kumsifuMungu. Mji wa Yerusalemu uliangazwa na nuru ya taa hizo.

Pengine ilikuwa baada ya taa kuzimika mwisho wa Sikukuu Yesu alitoa tamkokubwa la maana sana, alijidai kwa ujasiri na uthabiti kuwa „Nuru ya Ulimwengu‟(si ya Israeli tu). Lakini hakuliachia tamko hilo hewani, bali aliendelea kusemakwamba kama mtu anavyofuata mwanga wa tochi yake, vivyo hivyo, mtu apaswaamfuate Yeye ndipo atakuwa na „nuru ya uzima‟ (1:4,5). Hapo nyuma Yesuamesema kwamba Yeye ni „mkate wa uzima‟ (6:35) na katika Zab.36:9 maji yauzima yametajwa. Bila shaka watu walikumbuka jinsi Mungu alivyowaongozaIsraeli jangwani kwa nguzo ya moto ili wasafiri usiku.

Lakini nuru na giza havipatani, vita ipo kati ya nuru na giza. Yesu ameleta nuru,amekuja kumfunua Mungu kwa ukamilifu, ila watu wamependa giza kuliko nuru,kutokana na kutokujua kwao na dhambi yao (3:19). Kusema „Mimi ndimi‟ alijiwekambali na tofauti na watu wengine wote. Yeye ni Nuru, si kitu alicho nacho, mfanowa mtu aliye na taa, la; Yeye Mwenyewe ndiye Nuru na Kwake watu hupata„nuru‟ kwa kushirikiana naye kibinafsi. Bila kujihusisha naye mtu

Page 72: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA561

hana nuru (1 Yoh.1:5; Mt. 5:14; Flp.2:15). Ni Yesu tu awezaye kumtoa mtu gizani.Katika kushirikiana naye kibinafsi mtu hufunuliwa sababu ya kuumbwa kwake nashabaha ya kuishi kwake na njia za kuishi maisha yake hapo duniani. Huyo mtuaweza kujitambua vizuri na kufahamu mambo ya kiroho.

k.13ku Mafarisayo walibishana naye kuhusu madai hayo, walisema kwambaakijishuhudia, ushuhuda wake haukubaliki kwa sababu mahakamani mtuharuhusiwi kujishuhudia na hata Yesu alikubali ni hivyo (5:31). Ila Yesuhakusema juu ya kujishuhudia bali juu ya Baba kumshuhudia.

k.14 Yesu alisema kwamba ushuhuda wake una haki ya kupokelewa kwasababu ya uwezo wake wa binafsi. Ushuhuda wa mtu mmoja si uongo kwasababu ni wa mtu mmoja, ila kati ya wanadamu hautoshi, ila kama ni Munguanayejishuhudia ushuhuda unatosha kabisa. Kwa kuwa yeye ni Mwana wa Babaaliye na utambuzi kamili wa Nafsi yake na kwa sababu hiyo aweza kujishuhudiavizuri kuliko mwingine yeyote. „Nuru‟ haihitaji ushuhuda, uhalisi wa Nuru ni katikakuwa „nuru‟. Walishindwa kumtambua kwa sababu hawakujua alipotoka, walahawakufahamu anakokwenda, wala Yule aliyemtuma.

k.16ku Akarudia hoja yake ya kila wakati kuhusu uhusiano wake na Baba. Wakomashahidi wawili, Yeye na Baba yake. Tena wote wawili ni Mungu, si wanadamu.Kwa hiyo, hata machoni pa sheria ushuhuda wake unasimama. Hivyo alijiwekajuu sana ya wanadamu.Anao utambuzi mkamilifu juu ya Nafsi yake; ametoka mbinguni kwa Baba,hakuwa na asili katika dunia hii. Shahidi aliye mwanadamu awezajekumshuhudia Mungu, ambaye hakukaa naye wala kumfahamu kwa asili. Yeyealikuwa thabiti, wanadamu huwa na wasiwasi, hawajui wametoka wapi walahawajui wanakwenda wapi bila kufunuliwa na Mungu. Yesu aliweza kusema kwauhakika juu ya Nafsi yake, na ushuhuda wake pamoja na wa Baba ulitoshakabisa kuuhalalisha huo ushuhuda. Shida yao kubwa ni kwamba hawakumjuaYeye wala Baba. Ni ajabu kwa sababu Mafarisayo na wenzao walidai kwambawalimjua Mungu na kuwa walinzi wa ukweli wake. Kumbe walikuwa wageni kwaMungu Hai na kweli zake, ila uzuri ni kwamba waweza kumjua wakimnyenyekeana kumwamini.

k.21ku Ndipo Yesu aliwaambia tena juu ya kuondoka kwake na ya kwambahawataweza kumfuata. Wao walionyesha jinsi walivyokosa kumfahamu, maanawalidhani kwamba atajiua! „Mtanitafuta‟ haina maana kwamba wataendeleakumtafuta Yesu baada ya kumwua, maana watafurahi sana atakapoondolewa,ila kwamba wataendelea kumtazamia Masihi bila kumpata. Yesu aliwaonya juuya kutokuamini kwao na kutokujua kwao. „watakufa katika dhambi zao‟ na hiindiyo sababu hawatamfuata kule anakokwenda. Wasipomwamini Yeye kuwaMwokozi, Mfia dhambi, Masihi, Mtumishi ateswaye (Isa.53) Yule wa kuteswa nakutoa Nafsi yake kuwa fidia ya dhambi, basi watakosa dawa ya kutibu dhambizao na kuwapatia msamaha. Kumkataa Yesu ni kujiweka mahali pagumu sana,

Page 73: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA562

pa giza. Walijivunia kwamba walimfahamu Mungu, kumbe siyo. Yesu atakufakwa ajili ya dhambi; wasipomwamini watakufa katika dhambi.

k.25ku Wakamwuliza wazi „U nani Wewe?‟ Yesu akawajibu kwa kusema tena juuya uhusiano wake na Baba. Jambo hilo ni kubwa na la kwanza kabisa.Wasipomkubali na kumwamini kuwa Mwana wa Baba aliyetumwa nayekuukomboa ulimwengu, watabaki katika hali iyohiyo ya kutokujua na kutokuaminikwao. Wivu wao umewapofusha macho wasimtambue. Kisha Yesu akatamkahabari za Kufa Kwake, watakapomwua ndipo watamfahamu vema. Msalaba ndiomahali pa kumdhihirisha na hapo watu watatengana, wa upande mmoja, wale wakumpokea, na upande wa pili, wale wa kumkataa. Neno hilo linalingana naalivyosema kwa Nikodemo (3:14ku). Yeye na Baba ni mmoja, asili yao ni moja,na utendaji wao ni mmoja. Uaminifu wake kwa Baba umedhihirishwa kwa jinsialivyofanya yote yampendezayo. Alimtii Baba kwa ukunjufu wa moyo. Utii wakeulikuwa msingi wa nguvu na mamlaka yake. Kutokuwa na dhambi ni zaidi yakutokutenda makosa; ni kufanya yampendezayo Baba kwa moyo wote.

Yesu husimama peke yake kwa sababu ya asili yake kuwa Mungu. Ni Yeyealiyekuja kumfunua Mungu, ni Yeye ambaye amefidia dhambi na kutupatanishana Mungu, Yeye peke yake ndiye Njia ya kufika kwa Baba. Hata dini safi yaKiyahudi haikuweza kuwaleta Waisraeli kwa Mungu. Neno hilo ni kubwa katikaulimwengu wa kisasa ambao umekuwa „mdogo‟ kwa sababu ya njia nyingi zamawasiliano yanayowaunganisha wanadamu wa pande zote kwa urahisi. Wengihudhani kwamba kila imani na kila dini ni sawa na kila moja ina kweli fulaniziwezazo kuchangiwa katika ufahamu wetu wa Mungu, lakini sivyo. Yesu pekeyake ni Njia, Kweli, na Uzima na mtu haji kwa Baba ila kwa Yeye (14:6).Majadiliano hayo na Mafarisayo yana nguvu katika majadiliano ya kisasa kuhusuupekee wa Yesu Kristo

8:31-59 Mazungumzo na Wayahudi walioaminik.31-32 Inaonekana hao waliotajwa katika k.30 kuwa walimwamini hawakuwaimara katika imani yao kwa sababu katika mazungumzo yaliyofuata hawakumjibuYesu vizuri. Tena Yesu alisema mambo magumu juu yao, walikuwa watumwa wadhambi (k.34) hawakujali Neno lake (k.37) walikuwa watoto wa Ibilisi (k.44)waongo (k.45) na walitafuta kumwua (k.59).Alianza kusema nao kwa kuwaonya kwamba ni wale wenye kudumu katika nenolake walio wafuasi wa kweli. Iliwapasa kumpa Yeye utiifu wao wote. Wakitiamaanani mafundisho yake watafahamu kweli ambayo itawaweka huru nafsinimwao. Budi waamini ili wafahamu, kwa kawaida wanadamu hupenda kufahamundipo kuamini, ila katika mambo ya kiroho imani hutangulia. Maneno “hiyo kweliitawaweka huri”, yalionyesha kwamba wamekuwa watumwa.

Page 74: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA563

k.33ku Hilo walikataa kwa nguvu. Kwa upande wa kimwili walikuwa watumwa.Historia yao yote ilishuhudia jinsi mataifa mengine walivyowashinda nakuwatawala mara kwa mara. Huenda waliposema „hatujawa watumwa wa mtuwakati wo wote‟ waliwaza uhuru wa kiroho kwa sababu walikuwa watoto waIbrahimu wenye mapendeleo mengi kutoka kwa Mungu. Walijiona kuwa „wanawa ufalme‟ wasiohitaji tabibu (Mk.2:17) watu walio uhuru wasiohitaji ukombozi.Kiburi kiliwapofusha macho wasitambue utumwa wao, na kwa sababu hiyoilimbidi Yesu afafanue maana ya kuwa mtumwa na kuwekwa huru, iliwasiendelee kutegemea kule kuteuliwa na Mungu na kuwa uzao wa Ibrahimu.

k.34 Kwa kutumia maneno ya kutilia mkazo kama ilivyokuwa desturi yakealipotaka kutamka jambo muhimu alifafanua aina ya utumwa aliyokuwaakisemea. Utumwa wa dhambi, utumwa ulio mbaya kuliko utumwa wa kimwili,kutawaliwa na dhambi ni utumwa wa moyoni na utumwa uzaao mauti. Uhuru wakweli ni kutokutawaliwa na dhambi na kutawaliwa na Neno la Mungu. Wayahudihawakupenda hata kidogo kuambiwa kwamba walikuwa watumwa na ya kwambani Yeye tu, aliye na uwezo wa kuwaweka uhuru na dhambi.

k.35 Ndipo Yesu alisema juu ya hali ya watumwa akibainisha kati ya mtumwa namwana. Mwana ana haki katika nyumba ya Baba, ana usalama, ni mrithi, kwahiyo Yesu adumu kuwa mwana, hawezi kukosa kuwa mwana, potelea mbaliwakimwua au vipi. Wayahudi walijiwaza kuwa wana wa Ibrahimu lakini ukweli nikwamba ni watumwa wa dhambi. Kama ni hivyo hawana mahali pa kudumukatika nyumba ya Baba (Mt.3:9; 8:11-12; Mk.12:9). Kuambiwa hivyo kulitikisakabisa imani yao, ila wakimwamini Mwana kwa kweli na kuwekwa huru nayewatakaa nyumbani mwa Baba sawa na Mwana Mwenyewe. Mtu hana uhuruasipofungamana na Mwana.

k.36 Yesu kwa kuwa ni Mwana wa Mungu anayo mamlaka na uwezo wakuwaweka watu huru (3:35) na iliwapasa wajinyenyekeze na kuacha kiburi chaocha kutegemea kuwa watoto wa Ibrahimu na kumpokea Yeye. Yesu alikubalikwamba kimwili walikuwa watoto wa Ibrahimu lakini kiroho sivyo. Kuwa watotowa Ibrahimu kulileta heshima kubwa pamoja na wajibu mkubwa, wajibu wakufanana na Ibrahimu baba yao. Ila swali ni Je! walifanana na Ibrahimu? La! hatakidogo, kinyume chake walitafuta kumwua Masihi, Masihi ambaye Ibrahimualimtazamia kwa hamu sana (8:56; Mwa.18:2ku). Ibrahimu aliwapokea wajumbekutoka kwa Mungu kwa heshima kubwa, lakini wao wanamsukumia mbaliMjumbe Mkuu (Yesu) mwenye habari njema kuliko habari zao. Katika Agano laKale si wote waliozaliwa katika ukoo wa Ibrahimu waliokuwa warithi(Mwa.21:9ku. Rum.2:28ku. 9:7; Gal.4:21-31).

k.38ku Ijapokuwa madai yao ya kuwa watoto wa Ibrahimu yalikuwa uwongo,madai yake ya kuwa Mwana wa Mungu yalikuwa kweli. Kwa nini madai yake nikweli na madai yao ni uwongo? Yeye hufanya kama Baba (3:11-13,34; 5:19ku.6:46). Matendo na mwenendo hudhihirisha ubaba wake, vivyo hivyo kwa

Page 75: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA564

Wayahudi. Kiroho hao si watoto wa Ibrahimu, wala wa Mungu. Hakutaja „baba‟yao mpaka k.44 ila alitoa sababu ya kusema alivyosema, ambayo ni wao kutakakumwua.

k.41ku „Sisi hatukuzaliwa kwa zinaa, sisi tunaye Baba mmoja, yaani, Mungu‟.Kwa nini Wayahudi walijitetea kwa maneno hayo? Pengine walitakakumshambulia Yesu kuhusu jinsi alivyozaliwa kwa njia isiyo kawaida yawanadamu, pengine watu hawakuamini kwamba Yesu alizaliwa na bikira. Auyawezekana walitaka kuepa mashtaka ya uasi, kwa sababu katika Agano la Kale,watu walipomwasi Mungu na kuvunja Agano lake walifananishwa na wazinziwavunjao agano la ndoa. Ilihesabiwa kwamba Mungu alipofanya agano naowalikuwa wamefunga ndoa naye na wakimwacha na kufuata miungu minginewamezini.

k.42ku Yesu alikataa kabisa kuwahesabu kuwa watoto wa Ibrahimu. Wameamuakwamba hawatamwamini, kwa hiyo ni vigumu walisikie neno lake, wamezibamasikio yao ili wasimsikie. Pamoja na hayo Yesu alikataa kwamba licha ya kudaikwamba Ibrahimu ni baba yao, hata Mungu si Baba yao (Kut.4:22; Yer.31:9;Kum.14:1-2). Si kwamba Yesu alisema yaliyosemwa juu yao katika Agano la Kalesi kweli, bali ya kwamba hayo yaliyosemwa hayakuwahusu wao kwa sababu yahali yao ya kiroho. Ni kitu gani ambachokitapima ukweli wa ubaba wao na Ibrahimu na Mungu? Ni kumpenda yulealiyetumwa na Baba.

k.44ku Ndipo kwa ujasiri mkubwa Yesu alisema wazi kwamba baba yao niShetani, iwapo kimwili ni wazao wa Ibrahimu, kwa kiroho sivyo. Tabia yao ni kuuana kusema uwongo na kudanganya sawa na alivyofanya Shetani tangu mwanzo.Shetani ni mwuaji kwa sababu aliingiza taifa zima la wanadamu katika mautialipowashawishi wazazi wetu wa kwanza kumwasi Mungu kwa kutokuaminiNeno la Mungu na badala yake kuyaamini maneno yake. Aliwadanganya kwaahadi za uongo, alimshauri Hawa kwamba atapata uhuru. Mungu alikuwaamewapa uhuru mkubwa, ruhusa ya kula matunda ya miti yote ila mmoja tu, nakatazo hilo lilikuwa kipimo cha kuupima utii wao ambao ulikuwa msingi waushirikiano wao na Mungu, na njia ambayo kwayo utaendelezwa.

k.45 Kwa nini hawakumsadiki? hawakumsadiki kwa sababu amesema iliyokweli!! Ndipo kwa ujasiri aliwauliza swali kubwa kuhusu Yeye mwenyewe kuwabila dhambi? Hao walikuwa adui, hata hivyo hakuogopa kuwauliza wamshuhudiekuwa na dhambi kama anayo. Swali halikuhusu kama walidhani kwamba anayodhambi, hapo nyuma walifikiri amevunja sabato, na ya kuwa amekufuru kwakujiweka sawa na Mungu, ila Je! waweza kumshtaki kwa uhakika mbele zaMungu. Ni dhahiri kwamba hakuna mashtaka yatakayosimama mbele za Mungu,Baba yake. Katika dhamiri yake hakusikia mashtaka yoyote, hakuwa na wasiwasiwowote. Roho yake ilikuwa nyeupe kabisa katika hali ya kuwa na uhusiano waukaribu sana na Baba yake. Katika

Page 76: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA565

weupe kamili wa „kuwako kwa Baba‟ angalisikia kwa upesi hata nukta ya dhambi.Hapo twahakikishiwa utakatifu halisi wa Yesu uliomstahilisha kuwa sadaka kwaajili ya dhambi zetu, kama kondoo asiye na hila wala waa. Bila shaka kamawangaliweza kumshtaki dhambi fulani wangalifurahi kuitaja. Swali la Yesulililofuata lilifungamana na mazungumzo yaliyotangulia. Kama hana dhambi,mbona hawamsadiki? Kama hana kasoro yoyote iliwapasa kumwamini.

k.47 Maneno hayo ni kanuni ya kiroho: walio wa Mungu humsikia Yesu nakufanana naye katika maisha yao na kwa njia hiyo wadhihirika kuwa wamezaliwana Mungu. Kinyume chake wasio wa Mungu hudhihirika kwa njia ya kumkataaYesu na madai yake ya kuongoza maisha yao.

k.48ku Walibaki hawana la kufanya ila kumtusi vibaya na kusema ni Msamaria,na ana pepo. Ilikuwa tusi kubwa kwa Myahudi kuitwa Msamaria, ila Yeye alijibumatusi hayo kwa kusisitiza tena uhusiano wake na Baba na heshima yake kwaBaba, mzigo wake ni kwa heshima ya Baba na kwa ile heshima ambayo Babaanamheshimu daima. Hayo matusi hayakumsumbua, ingawa wamejiinua kiasicha kuamua juu yake, hata hivyo, wako chini ya hukumu ya Baba. Kwa Yesukibali cha Babaye kilikuwa jambo muhimu na la kwanza katika maisha yake.

k.51ku Alizidi kukamilisha madai yake makubwa ya kuwa Mungu Mwana.Alisema kwamba mtu akilishika neno lake atapata uzima wa milele wala hataonamauti milele. Yeye amekuja ulimwenguni ili watu waokolewe (3:16-17). Wayahudiwalijibizana naye wakifikiri kwamba amepita mpaka katika kudai kwamba walewa kumwamini hawataonja mauti. Wao waliwaza mauti ya kimwili na Yesualisemea mauti ya kiroho. Hata Ibrahimu alikufa, hata manabii walikufa, kwa hiyo,huyu anayeifuta mauti ni nani? Je! Yeye ni mkuu kuliko Ibrahimu? Je! Yeye nimkuu kuliko manabii? Wakasema „umejifanya kuwa nani?‟. Lakini Yesuhakujitukuza mwenyewe, zaidi ya watu wote Yesu hakujitegemea balialimtegemea Baba. Alimnyenyekeza na kumtii kabisa na kwa sababu hiyo Babaalimheshimu. Ajabu ni kwamba huyo Baba ndiye yule ambaye Wayahudi walidaikuwa ni Mungu wao. Hivyo Yesu alisisitiza umoja wake na Baba. Umoja wa asili,wa umilele, na kama angalikataa umoja huo angalikuwa mwongo mkubwa kabisa.

k.56ku Kisha aliwaambia kwamba Ibrahimu alifurahi sana kujua Masihi atakuja,na kwa namna fulani, aliiona siku yake. Pengine maana yake ni kwambaalipozaliwa Isaka uwezekano wa kuzaliwa kwa Masihi ulionekana (Mwa.17:17;21:6; 22:18). Ni kwa sababu ya kupata njia ya kumleta Kristo duniani Mungualimwita Ibrahimu atoke Uru ya Wakaldayo, alitengwa na WaMataifa, ili kwa imaniapate kuwa baba wa mataifa mengi, na katika tumaini hili alijenga maisha yake(Ebr.11:10,17-19).

„Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; nayeakaiona, akafurahi‟ Ni vigumu kujua maana halisi ya maneno hayo, ila ni wazi

Page 77: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA566

kwamba katika Kuja kwa Yesu matazamio yote ya wito wa Abramu yalitimizwa.Maneno yaliyowakwaza Wayahudi yalikuwa „siku yangu‟. Ndipo walimaanishakwamba Yesu amedai kuwa hai hata wakati wa Ibrahimu. Ndipo Yesu akadaizaidi kwamba alikuwa hai kabla ya Ibrahimu. „Amin, amin, nawaambia, YeyeIbrahimu asijakuwako, mimi niko‟ (k.24,28). „Mimi Niko‟ ni maneno yanayomhusuMungu Mwenyewe, jinsi alivyojitaja kwa Musa wakati Musa alipotaka kujua ninani aliyemtuma.

Maneno hayo yafanana na mwanzo wa Injili hiyo (1:1,14). Yesu hafungwi katika„wakati‟, hakuna wakati ambapo Mwana hakuwako, aweza kusema wakatiwowote „mimi niko‟. Maneno yahusu kuwako kwake daima, si maneno kuhusunafsi yake tu (Kut.3:14 maneno Mungu aliyoyatumia alipomtuma Musa). Ibrahimualizaliwa, alipata kuwako, ila Yesu yuko hata kabla ya kuzaliwa kwake,amekuwako tangu milele hadi milele. Kwa hiyo Yesu alidai zaidi ya kuwa kablaya Ibrahimu, hasa alidai kuwa Mungu, na ndivyo walivyomaanisha Wayahudi.Basi wakaona amekufuru sana sana; walitaka kumwua pale pale bila kumpelekamahakamani, ila Mungu alimlinda (maana ya neno la Kigriki ni „alifichwa‟).Aliondoka hekaluni, ishara ya kuwaacha katika upofu wa mioyo yao.

MASWALI1. Wakuu walimtumia huyu mwanamke kama chambo mtego. Eleza habarihiyo?2. Yesu alihudumia watu wa pande zote. Eleza ni kwa jinsi gani alivyofanyahivyo.3. Yesu alikuwa na maana gani aliposema „Mimi ndimi nuru ya ulimwengu?hiyo nuru ni ya namna gani, na kwa njia gani mtu atakuwa nayo?4. Wakuu waliona kwamba ushuhuda wa Yesu juu ya kuwa nuru ya ulimwenguhausimami. Kwa nini walidhani hausimami na Yesu alisemaje alipowajibu nakuwaonyesha kwamba ushuhuda wake una haki ya kukubalika?5. Katika majadiliano marefu yaliyofuata neno muhimu kuliko yote ambayo Yesuyo aliyosisitiza lilikuwa nini?6. Eleza maana ya „kuwa mtumwa‟ na „kuwa huru‟ kufuatana na mafundisho yaYesu.7. Yesu alisema wamekuwa „watoto wa Ibilisi‟ kwa sababu gani?8. Kwa nini Wayahudi waliobishana naye walidhani kwamba wako huru?Walimtegemea nani kwa uhuru wao?9. Yesu alidai kuwa mkuu kuliko Ibrahimu. Ni kwa mambo gani Yesu ni mkuukuliko Ibrahimu?

Page 78: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA567

9:1-41 Kumponya mtu aliyezaliwa kipofu

Katika habari hii tunaona maendeleo ya upinzani juu ya Yesu na adui zake.Inadhihirisha maendeleo ya kuamini kwa wengine na kutokuamini kwa wengine.Kipofu ni kielelezo cha kuamini na Mafarisayo na itikio lao ni kielelezo chakutokuamini, walimhoji huyo mtu, ndipo wakamtenga na sinagogi. Ishara hiyoya sita ilionyesha uwezo mkubwa wa Yesu. Jinsi alivyomtendea huyo mtu tangualipoanza kuzungumza naye mpaka baada ya kumponya ni mfano mzuri wajinsi Yesu alivyojihusisha na watu. Tendo hilo lilisababisha watu wamwitikie kwaupya, ama kwa kumkubali, ama kwa kumkataa. Habari imewekwa mara baadaya mazungumzo ya Yesu na Wayahudi katika sura ya nane, mazungumzoyaliyoudhihirisha upofu wao wa kiroho. Wayahudi waliamini kwamba katikaNyakati za Masihi vipofu watapewa uwezo wa kuona (Isa.29:18; 35:5). Twaonauhusiano wa sura hii na ile ya nane Yesu alipojitaja kuwa Nuru ya Ulimwengu,na sura ya saba na Sikukuu ya Vibanda, wakati wa taa kubwa za dhahabukuwashwa.

k.1ku Walipokuwa wakipita njiani Yesu na wanafunzi wake walimkuta mwombajikipofu kando ya njia. Wanafunzi walitatizwa sana na sababu za huyo mtukuzaliwa kipofu (hatuambiwi walipataje kujua alizaliwa kipofu). Kwa niniamezaliwa kipofu? Ni kosa la nani? Ni nani aliyefanya dhambi? Waliona vigumukudhani ya kuwa ni mtu mwenyewe, maana alizaliwa hali hiyo. isipokuwa alifanyadhambi tumboni mwa mama yake, ambao baadhi ya watu waliamini iliwezekana.Kama si yeye pengine ni wazazi wake waliofanya dhambi? Torati ilisema kwamba„Mungu atawapatiliza wana maovu ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nnecha waliomchukia, na kuwarehemu maelfu elfu waliompenda na kuzishika amrizake‟ (Kut.20:5; 34:6, 7).Ilikubalika kwamba upo uhusiano kati ya dhambi na ugonjwa, kutokana na laanajuu ya wanadamu tangu Anguko la Adamu. Biblia haisemi kwamba kila mtuanayeugua au anayezaliwa na kasoro amefanya dhambi, bali magonjwa n.k.yamo ulimwenguni kwa wanadamu kwa jumla. Mara nyingine mtu huugua kwasababu amefanya dhambi, ila sivyo ilivyo kwa kila mtu. Magonjwa na mautiviliingia kwa sababu ya uasi wa wanadamu (Mwa.3:1ku).

k.2 Wanafunzi walitaka kujua Yesu anasemaje juu ya swala hilo. Huyo mtuamekuwa sababu ya hoja ya theologia badala ya kuwa mtu wa kuhurumiwa.Wanafunzi walishindwa kutatua tatizo hilo; iliyobaki ni kwa kipofu kuhudumiwakiutendaji. Kipofu ni wa thamani kuliko majadiliano juu ya sababu za upofu wake.

k.3ku Yesu akajibu kwa kulenga makusudi ya Mungu. Si faida kutazama nyuma,afadhali wafikiri wafanye nini sasa. Yesu alikana kwamba dhambi, ama yake auya wazazi, ilikuwa sababu ya upofu wa huyo mtu. Hali yake ilihitaji matendo simazungumzo. Je! Yesu alipojibu alikuwa na maana kwamba mtu huyo ana shidahiyo kwa kusudi la kumpatia Yeye nafasi ya kumponya? Ni

Page 79: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA568

vigumu kuwaza kwamba Mungu alimruhusu aishi muda mrefu katika dhiki hiyo ilibaadaye amdhihirishie uwezo wake mkuu. „bali kazi za Mungu zidhihirishwendani yake‟ afadhali maneno hayo yamaanisha kwamba hata hali hiyo ngumu yahuyo mtu haikuwa nje ya utawala wa Mungu na kwa sababu hiyo nafasiimepatikana kwa Mungu kufanya kazi njema kwake, si kwamba imekuwepo kwakusudi la mwujiza kufanyika. Mwujiza huo ni tofauti na yote mingine aliyoifanyaYesu, kipofu hakuwa na tumaini lolote, hajapata kuona hata kwa saa moja, walambele hamna tumaini; jinsi alivyozaliwa, na jinsi alivyo sasa, na hata baadayeatakuwa vivyo hivyo; hakuona, haoni, hataona. Hamna tumaini. Ila Yesu niBwana juu ya maisha ya wanadamu, Yeye aweza kupambana na misiba ya watu.

k.4 Yesu alitaja „mwujiza‟ huo kuwa „kazi‟ kwa sababu kwake Yeye na kwaMungu Baba yake si jambo gumu kumpa huyo mtu uwezo wa kuona kwa maraya kwanza. Kwa njia hiyo Mungu atatukuzwa na uhusiano wa ukaribu sana katiya Yesu na Baba utadhihirika wazi tena. Kwa upande wa Yesu, Yeye anao mudamfupi wa kuishi, kwa hiyo kuna hali ya haraka kwa Yeye kufanya kazi zake.„Imetupasa (Yesu na wanafunzi) kufanya kazi zake Yeye aliyenipeleka (Yesu)maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi‟. Ijapokuwa Yesualiwahusisha wanafunzi na Yeye katika kazi alijitofautisha nao katika kutumwa.Alikaza upekee wa kutumwa kwake, pengine kwa sababu ya k.7. Hata hivyo haonao walitumwa kufanya kazi zake. Yesu aliwakumbusha wanafunzi wakekwamba walipaswa kuwa pamoja naye na kutenda kazi ya Mungu maadamu nimchana, maana yake, maadamu nafasi zipo. Wamewajibika kutumika,kuwasaidia wanadamu katika shida zao. Kazi za Injili zina haraka, haziwezikuahirishwa mpaka wakati wa kufaa, wakati wa kufaa ni wakati wote, wasingojempaka hali ya hewa iwe nzuri, mpaka watu wamekuwa tayari kuwapokea. Yesualijua kwamba upinzani uliopo utazidi mpaka watakapomwondoa.

k.5 „Mimi ni nuru ya ulimwengu‟ ni maneno ya kufaa sana katika mazingira yauponyaji wa huyo kipofu. Ila nuru aliyosema Yesu si ya kimwili, bali ya kiroho.Kwa wahusika wote katika habari hiyo itabainika ni akina nani walio na macho yakiroho ya kumtambua Yesu na ni akina nani walio vipofu, wasiowezakumtambua. Haina maana kwamba Yesu aacha kuwa nuru ya ulimwenguatakapoondoka na kurudi kwa Baba. La. Ila kwa muda aliyemo ulimwenguni nuruiliangaza vizuri sana na iliwabidi watu wafanye haraka na kuitika vema (12:35).Muda uliofuata mara baada ya Yesu kuuawa ulikuwa giza zito kwa wafuasi wake.

Yesu alimponya mtu huyo kwa sababu alimhurumia. Yeye mwenyewe hakufaidineno maana alikuwa ameishaonyesha watu uwezo wake mkuu. Katikakumponya siku ya Sabato alijua adui zake watampinga zaidi, ila mzigo wakeulikuwa kwa kipofu mwenyewe.

Page 80: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA569

k.6-7 „Alipokwisha kusema hayo‟ Maneno hayo yanaunganisha maneno ya k.4-5 na tendo la kumponya kipofu linalofuata. Katika k.5 Yesu alisema Yeye ni Nuruya Ulimwengu ndipo aliendelea kuthibitisha hayo kwa kumpa kipofu nuru yakuona kwa mara ya kwanza. Yeye humtii yule aliyemtuma (k.4) huku wengiwamzungukao humpinga Yeye na kuizuia nuru isiangaze maishani mwao. Haponyuma kipofu amekuwa kama kitu cha kuzungumziwa kitheologia, ila kwa Yesuni mtu wa kutendewa kwa rehema za Mungu.

Alimponyaje? Alitema mate na kufanya tope kwa yale mate, akampaka kipofutope kwenye macho na kumwambia aende na kunawa katika birika la Siloamu.Kwa nini atumie tope na mate? Alitumia mate alipomponya kipofu na bubu(Mk.7:33) na kipofu wa Bethsaida (Mk.8:23). Kwa hao wawili alitumia mate tu, ilakwa huyo kipofu alifanya tope na mate yake na kumpaka hilo tope machoni.Hatujui „mate‟ yalikuwa na maana gani na iliashiria nini. Wapagani waliona inahali fulani ya uponyaji. Yawezekana kupakwa hivyo kulimvuta azidi kutazamiauponyaji wake. Kwa kuguswa na kuyasikia maneno alisaidiwa kwa sababuhakuweza kuona kitu. Hapo nyuma kwa wengine Yesu amesema neno tu, mtuameponywa. Kila mtu alitendewa kipekee kufuatana na hali yake na hitaji lake.Kipofu alimtii Yesu, akaenda, akanawa, akarudi hali anaona. Kupakwa topemachoni na kuambiwa „aende‟ kulimsaidia, alipewa jambo la kufanya na nafasiya kumtii Yesu. Kwa vyovyote angalitaka kunawa na kuondoa tope. Topeilimsaidia kumjali Yesu, kwa njia yake Yesu alijihusisha naye kwa ukaribu kabisa.Kwa kumnyenyekea Yesu na kwa kukubali kwenda na kunawa aliponywa.Alipewa tendo la kufanya la kujenga imani yake. Alitumwa kwenye birika laSiloamu, maana yake „Aliyetumwa‟. Kimwili alinawa katika maji ya birika hilo, ilauponyaji wake hasa ulitoka kwa Yule Aliyetumwa na Mungu.

k.8-12 Yesu haonekani tena mpaka k.35; baada ya kumwambia kipofu aendeSiloamu hawakuonana tena mpaka baadaye. Yule aliyeponywa akarudinyumbani kwa jamaa na jirani zake. Bila shaka ni hao waliomsaidia sana haponyuma alipokuwa kipofu. Hivyo walitaka kujua ni kwa njia gani amepata kuona.Wengi walijua ni yeye mwenyewe, ila wachache wakadhani kwamba ni mwinginealiyefanana naye. Kama ni hivyo, swali limebaki kwao, yeye kipofu yuko wapi?Yeye mwenyewe akakiri wazi „Mimi ndiye‟. Ndipo akawaelezea jinsialivyoponywa, kwa maneno rahisi akatoa ushuhuda wake. Tazama maneno yakitenzi „Mtu aitwaye Yesu alifanya tope, akanipaka macho, akaniambia NendaSiloamu ukanawe, basi nikaenda na kunawa, nikapata kuona‟. Ushuhudausiopingwa. Alimtaja Yesu kuwa „mtu‟ bado hajamfahamu kuwa Mwana waMungu na Mwokozi wa ulimwengu. Alipoulizwa Yesu yuko wapi, akashindwakuwaambia, kwa kuwa hata yeye mwenyewe bado hajapata kumwona hawezikumtambulisha kwa wengine.

Page 81: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA570

9:13-34 Mafarisayo walihojiana na kipofu aliyeponywa

k.13-17 Uchunguzi wa kwanza ulifanywa na Mafarisayo. Si wazi ni akina naniwaliompeleka kwa Mafarisayo kama ni wazazi, jirani, au vipi. Wala sababu zakumpeleka hazitajwi. Huenda ilikuwa kupata maoni yao juu ya uponyaji wake,pengine kwa sababu ilifanyika siku ya Sabato. Ni mara ya kwanza kutaja kwambailikuwa Sabato ilipofanyika uponyaji huo. Pengine Mafarisayo walituma watukumleta ili wampeleleze kwa sababu ya tendo hilo kufanyika siku ya Sabato.Walikuwa wakitafuta ushuhuda juu ya Yesu ili wapate kumshtaki. Aliulizwa naMafarisayo jinsi alivyoponywa. Akawajibu kwa kusema kwa ufupi jinsi mamboyalivyotokea, akatoa ushuhuda mkali „na sasa naona‟, jambo lisilopingwa. Bilashaka walidaka habari ya Yesu kutema mate na kufanya tope na kumpakamachoni, wakihesabu kwamba hizo „kazi‟ haziruhusiwi siku ya Sabato.Inawezekana ndiyo sababu mojawapo ya Yesu kutumia njia hii ili atoboe wazikwamba ni halali kufanya „kazi‟ za aina hii za kuhurumia watu (5:1ku).

k.16ku Mafarisayo walitengana wao kwa wao. Baadhi waliona kwamba Yesuhakutoka kwa Mungu kwa sababu ya kutenda „kazi‟ hizo siku ya Sabato ilabaadhi waliona kwamba tendo la kumpa huyo aliyezaliwa kipofu uwezo wa kuonalilitosha kabisa kuonyesha kwamba Yesu ametoka kwa Mungu. Penginewalikuwa wachache waliofikiri hivyo, maana katika mazungumzo yaliyofuatasauti za wapinzani zilizidi. Watu walishurutishwa kuonyesha msimamo waokatika habari hiyo.

k.17 Hata aliyeponywa alilazimika kuonyesha wazi msimamo wake.Wakamwuliza atoe maoni yake, maana yeye ni mhusika kabisa katika habarihiyo, ila Yesu ni kiini chake. Kwa kawaida wasingalipenda kumwuliza „mlei‟ swalala dini, ila walidhani kwamba wakimsumbua na kumtisha yawezekana atasemaneno litakalowasaidia kumshtaki Yesu. Kwa jinsi walivyomsumbua wakamfanyaazidi kulizingatia tendo kuu alilotendewa na Yesu ndipo imani yake ikakua,akapanua mawazo yake juu ya Yesu na kumwona kuwa nabii. Kwa kadiriwalivyomsonga akazidi kumwamini Yesu, na wao walizidi kuhangaika. Alihitajiujasiri kwa kutamka neno hilo maana Mafarisayo waliwatisha watu sana. Hakuwatayari kusukumwa aseme kinyume cha alivyofahamu nafsini mwake. Yeye alizidikusogea kwenye nuru na wapinzani walizidi kupofushwa na hoja zao zakitheologia na chuki yao kwa Yesu.

k.18-23 Wayahudi hawakuwa tayari kuamini ushuhuda wake nao wakahangaikasana katika jitahada zao za kupata njia ya kuukanusha huo mwujiza uliofanyika.Walishindwa kumwogofya aliyeponywa, kwa hiyo, waliamua kwamba watawaulizawazazi wake, ama waseme yeye si mwana wao, au waseme hakuzaliwa kipofu.Hawakuona shida katika kujibu maswali hayo mawili, ila walisita walipoulizwakuhusu jinsi alivyoponywa. Ni vigumu kufikiri kwamba hawakujua ni nanialiyemponya, ila hawakuwa tayari kusema,

Page 82: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA571

kwa hiyo, waliwaambia Wayahudi ni vema wamwulize mwana wao mwenyewekwa kuwa alikuwa mtu mzima mwenye uwezo wa kutoa jibu. Kwa njia hiyowaliutunza uhusiano wao na viongozi wa sinagogi, ila ni dhahiri kwamba mwujizamkubwa umefanyika. Kama ni hivyo iliwapasa kumsifu yule aliyeufanya. Kwa ninihao wazazi wamesita kusema zaidi? kwa nini hawakusimama bega kwa bega namwana wao na kuwa huru kusifu hali yake mpya ya ajabu sana? Sababu nikwamba walijua Wayahudi wameafikiana wao kwa wao kwamba yeyoteatakayemkiri Yesu kuwa Masihi watamtenga na sinagogi. Ila kama tutakavyoonambele mwana wao alikuwa tayari kabisa kutengwa na sinagogi kama ikitokeahivyo (k.34).

9:24-34 Inaonekana Mafarisayo wamepata umoja wa kiasi fulani, ila ni dhahirikwamba hawajafaulu kuitikisa imani ya aliyeponywa, hivyo wakaona vemawahojiane naye tena. Habari tuliyo nayo katika sehemu hiyo inasisimua kweli.Walianza na maneno „Mpe Mungu utukufu‟. Walilenga nini kwa kusema hivyo?Je! walitaka amsifu Mungu kwa uponyaji wake? au pengine amtukuze Mungubadala ya Yesu kwa uponyaji wake? Huenda maana ni ile ya Yoshua 7:19ambayo ni „mbele za Mungu useme iliyo kweli‟ kwa sababu walidhani kwambaamewaficha kweli fulani. Pengine walitaka aseme Yesu ni mwenye dhambi kwasababu amevunja Torati (yaani mapokeo yao). Labda iko habari nyingine ndogoambayo haijatajwa bado.

k.25 Huyo mtu akakiri kwamba yeye si mtaalamu katika mambo hayo ila alijuajambo moja kwa hakika kwamba „mimi nilikuwa kipofu na sasa naona‟. Jambohilo hatalikana, potelea mbali watasema nini, kwa sababu ni kweli.

k.26-29 Ndipo walirudia kumwuliza tena jinsi alivyoponywa. Huyo mtualitambua unafiki wao, ameishajibu maswali yao, kwa nini wamwulize tena,wana sababu gani, wanataka nini? Bila wasiwasi aliwauliza kama walitaka kuwawanafunzi wa Yesu. Ukweli wa uponyaji wake ulimtia nguvu ya kusimama imarana kwa kadiri walivyombana alizidi kumtafakari Yesu kwa makini. Wakakwazwana maneno yake, wakamtukana, bila shaka walikosa amani katika dhamiri zao,kwa sababu huyo mtu amegundua hila yao. Kiini cha jambo lote ni mamlaka yaYesu na ile ya Musa. Wao walikuwa wafuasi wa Musa, ambaye Mungu alisemanaye uso kwa uso na kumpa Torati (Kut.33:11; Hes.12:8). Waliona kwambahakuna uhusiano kati ya Musa na Yesu. Wakamshtaki aliyeponywa kuwa mfuasiwa Yesu. Walikiri kwamba hawakujua Yesu ametoka wapi, walikuwawamechanganyikiwa sana juu yake. Hawakuweza kupatanisha ule ufunuoulioletwa na Musa kwa njia ya Torati na ule ulioletwa na Yesu (1:17-18).

k.30-33 Huyo mtu alizidi kuwa hodari, alishangaa kuona hali yao yakutokustaajabia uponyaji wake na jinsi walivyozidi kumsumbua. Kweli, hakuelewamambo ya theologia kama wao, ila katika ujuzi wa kibinafsi aliweza kuitambuakweli ilivyo juu ya uponyaji wake na ukweli wa yule aliyemponya

Page 83: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA572

kuwa na uhusiano mzuri na Mungu, maana Mungu alisikia maombi yake nakuyajibu. Alisisitiza ukubwa wa mwujiza uliofanyika ambao uliashiria Kuja kwaNyakati za Masihi jinsi Nabii Isaya alivyotabiri (Isa.29:28; 35:5; 42:7). Aliwashindakwa hoja yake, lakini hawakutia maanani maneno yake, wala hawakueleza asiliya uwezo wa Yesu kumponya.

k.34 Kisha wakamghadhibikia na kumtusi vibaya sana, ila katika kumtusi ajabuni kwamba walikuwa wakikiri kwamba alizaliwa kipofu na ya kuwa macho yakeyamefumbuka sasa!! Mambo waliyojitahidi kuyakana. Ndipo wakamtoa nje yasinagogi, jambo ambalo wazazi wake waliepa hapo nyuma kwa sababuhawakuwa tayari kusema kwa wazi yale waliyoyajua.

Twajifunza kwamba ukweli una nguvu kuliko dhana za watu. Aliyeponywa alizidikukua katika nuru, na wakuu walizidi kukwama katika giza. Kwa mwandishiYohana jambo la hukumu linatokea wakati huo huo katika mambo yanayotokea.Sababu kuu ya mtu kuwa katika nuru au kuwa katika giza ni itikio lake kwa Yesu.Haidhuru mtu aanze na ufahamu mdogo ni itikio lake kwa yale yanayompataambalo linazidisha nuru au giza lake.

k.35-38 Yesu aliposikia habari ya kuwa huyo aliyeponywa ametolewa nje yasinagogi basi akamtafuta na kumpa changamoto ya kuongeza imani yake, kwasababu bado alikuwa na ufahamu mdogo. Polepole, hatua kwa hatua, amezidikusogea kwenye nuru. Alianza kwa kusema Yesu ni „mtu‟ (k.11) ndipo akamwonakama ni „nabii‟ (k.17) ndipo akamwona kama „ametoka kwa Mungu‟ (k.33).Walikuwa bado hawajakutana tangu Yesu alipomtuma aende Siloamu nakunawa, hivyo, huyo mtu bado hajamwona Yesu kwa macho yake ya kimwili nahapo kati ameshambuliwa sana na Mafarisayo kuhusu uponyaji wake.Walipokutana, moja kwa moja Yesu alimwuliza „Wewe wamwamini Mwana waMungu‟ (katika nakala za zamani ni „Mwana wa Adamu‟). Akaitika mara kwakuonyesha utayari wake wa kumwamini „Ni nani, Bwana, nipate kumwamini?‟Ndipo Yesu akajifunua Kwake kuwa Ndiye Mwana wa Adamu/Mungu. Kishaakakiri „Naamini, Bwana‟, akamsujudia. na kumpa ile heshima iliyomstahili,amefikia upeo wa imani. „Namwamini‟ maana yake alijikabidhi kwake kibinafsi, siukiri wa kichwa tu. „Umemwona‟ maneno makubwa kwa aliyezaliwa kipofu.Wengi walimwona Yesu (kimwili) kwa muda mrefu lakini hawakumwona kirohowala kuutambua ukweli wa Yesu kuwa Mwana wa Mungu aliyeleta ufunuo kamiliwa Mungu (6:36).

Mwujiza huo umeonyesha matokeo ya kuamini na ya kutokuamini. Kukazanakatika imani kulileta uponyaji wa kuona kimwili pamoja na kuona kiroho. Kipofualianza polepole, akaendelea kukua hatua kwa hatua katika kumwamini Yesuna mwishowe Yesu alipojifunua Kwake kuwa Mwana wa Mungu, akapatathawabu ya imani yake. Kinyume chake kutokuamini kwa Mafarisayo kulianzakatika kutokuelewa maana na shabaha ya kweli ya Musa na Torati pamoja nakukataa kumwona Yesu ni yule aliyetumwa na Mungu Baba. Hivyo walizidi

Page 84: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA573

kupofushwa macho waliposhindwa kukiri kazi ya Mungu katika uponyaji wa huyomtu aliyezaliwa kipofu.

k.39 Hukumu juu ya Mafarisayo: Inaonekana Yesu alikutana na huyoaliyeponywa mahali penye watu na miongoni mwao walikuwepo Mafarisayo.Ndipo Yesu alijumlisha mambo yaliyokuwa yametokea kwa kuunganisha jambola kuona na jambo la hukumu, kuona katika maana ya utambuzi wa ndani, wakiroho. Alisema kwa ujasiri kwamba shabaha ya Kuja Kwake ilikuwa hukumu,hasa Kuja kwake ni hukumu. Katika 3:17 Yesu alisema „Mungu hakumtumaMwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katikayeye‟. Je! si amesema kinyume cha alivyosema katika 3:17. La, siyo. Maanatukisoma 3:18-21 aliendelea kusema juu ya hukumu. Hapo amesema juu yamatokeo yatakayofuata Kuja Kwake, matokeo ambayo aliyafahamu mapemahata kabla ya Kuja Kwake kwamba Kuja Kwake kutasababisha matengano katikawatu. Hasa alikuja kuokoa ila kwa wale wanaomkataa, hukumu itawapata, kwasababu neema ya kuokoa inafunua dhambi, dhambi ambayo mtu apaswakuitubu; asipoitubu basi hamna njia ya kuepa hukumu ya Mungu juu ya dhambiyake. Jinsi mtu anavyojihusisha naye ama kwa kumkubali, ama kwa kumkataa,kunamfanya awe anaona au haoni. Huyo aliyeponywa hakujua mambo ya kiroho,hakuona kiroho, ila kwa kadiri alivyozidi kujiweka upande wa Yesu ndivyoalivyozidi kukua katika ufahamu wa kiroho. Kwa upande wa pili, viongozi wa diniambao walidhani kwamba wanaona kiroho, kwa jinsi walivyozidi kumkataa Yesundivyo walivyozidi kuwa vipofu kiroho. Kila mtu aliwajibika kwa itikio lake. Shidaya Mafarisayo ilikuwa kwamba walidhani kuwa wanaona vizuri sana, hivyo,hawakufaidi nuru iliyoletwa na Yesu.

MASWALI1. Umejifunza nini kutoka kwa habari ya uponyaji wa mtu aliyezaliwa kipofu

(a) kwa upande wa mtu mwenyewe?(b) kwa upande wa wakuu?(c) kwa upande wa Yesu?

2. Ni akina nani walio vipofu hasa? na upofu wao ulisababishwa na nini?

10:1-21 Yesu Mchungaji MwemaUpo uhusiano mkubwa kati ya sura hii na ile iliyotangulia. Katika surailiyotangulia tulipata habari za mtu aliyezaliwa kipofu ambaye Yesu alimponya.Kwa jinsi alivyojihusisha naye Yesu alidhihirishwa kuwa „Mchungaji Mwema‟ nayule mtu kuwa „kondoo aliyeisikia sauti ya huyo Mchungaji Mwema‟. Katika suraya 9 walioona kiroho na walio vipofu kiroho walibainika, na hapo tena katika suraya 10 Yesu alibainisha Huduma yake na wale viongozi waliomsumbua yulekipofu aliyeponywa, pamoja na viongozi wote wa aina yao. Huduma yake ni yaMchungaji Mwema na huduma ya viongozi wa dini ilikuwa ya wevi nawanyang‟anyi; Yeye alitumwa na Baba, wao hawakutumwa na Mungu.

Page 85: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA574

Alionyesha kwamba Yeye alistahili kuwa Mchungaji wa Taifa zima la Israeli.Tukumbuke kwamba katika historia ya Taifa hilo Mfalme aliwajibika kuwaMchungaji pia, kama Daudi alivyokuwa. Ezekieli 34 inatoa habari juu yaWachungaji wa Israeli.

k.1-6 Yesu alianza kwa kusemea Zizi la Kondoo akitumia maneno ya kutiliamkazo kama desturi yake ilivyokuwa alipotamka neno muhimu. Alisisitiza hakiyake ya kuingia katika zizi na kuwachunga kondoo. Yeye ameingia kwa uhalali,amepitia mlangoni, maana yake, ametumwa na Baba, amepewa madaraka naBaba. Kondoo ni mali yake pamoja na kuwa mali ya Baba yake. Viongozi wengiwaliokuwapo wakati huo walikuwa wadanganyifu, hawakutumwa na Baba,walikuwa wamejiingiza na kuuchukulia uongozi bila kibali cha Baba. Dalili yakuwa hawakutumwa na Mungu ilikuwa jinsi walivyowaongoza „kondoo‟ vibaya,hawakuwatunza, hawakuwahifadhi. Alikuwa akiwasemea wale waliomsumbuakipofu aliyeponywa kuhusu jinsi walivyohojiana naye kupita kiasi wakijitahidikumwondoa katika utiifu wake kwa Yesu, kisha wakamtenga na sinagogi.

Tabia ya Mchungaji Mwema ni kukusanya kondoo si kuwasambaza. MchungajiMwema anajua kondoo wake kibinafsi, amwita kila mmoja kwa jina lake.Anawaongoza katika maisha yao akiwatangulia na kupambana na hatari za njianiili wawe salama. Hao kondoo wamfahamu, wanatambua sauti ya Mchungaji wao,sawa na jinsi yule kipofu aliyeitambua. Tena hawaijui wala kuiitikia vema sauti yaviongozi wadanganyifu. Kwa mazungumzo hayo Yesu alikuwa ametumia mfanokutokana na mazoea yao, kwa sababu wachungaji na kondoo walionekanamashambani kila mahali. Kwa upande wa dini Wayahudi walizoea kumwazaMungu kama Mchungaji wao na viongozi pia walihesabiwa wachungaji chini yake(Zab.23; 79:13; 80:1: 95:7; Eze.34:15ku. Isa.40:10ku. Yer.23:1ku. 25:32ku.Zek.11; Isa.56:9-12). Mafarisayo na wakuu wengine katika kumshambulia yulekipofu walikuwa wakitoa changamoto kwa haki ya Yesu kuingia katika zizi lakondoo na kutoa msaada kwa kondoo. Kuwafuata Mafarisayo ni kushika sheria,hasa mapokeo yao, ila kumfuata Yesu ni kujitoa Kwake na kushirikiana nayekibinafsi. Wakuu walikosa kuelewa mithali hiyo iliyowasema (k.6). Hawakuwakondoo zake kwa hiyo ni vigumu waitambue maana ya maneno hayo.

k.7-18 Kristo ni Mlango wa kondoo na Mchungaji MwemaHapo tena Yesu alitumia maneno ya kutilia mkazo alipodai kuwa Mlango waKondoo. „Mimi ndimi‟ ni ukumbusho wa Yeye kuwa Bwana (Kut.3:14). Katika k.2alisema juu ya Mchungaji Mwema kuingia mlangoni, sasa huyo Mchungaji niMlango. Kwa jinsi alivyosema alidokezea kwamba hakuna mlango mwingine(14:6; Zab.118:19-22). Mtu hana budi ampitie Yeye ili apate kuokolewa. Barakaza wokovu ni nini? Baraka kubwa mojawapo ni kulishwa, yaani kupata shibe yanafsi, uzima tele. Alikuwa ameishadokezea jambo hilo alipogeuza maji kuwa divai(2:1ku). Katika kuzungumzia na Mwanamke Msamaria alitaja „maji yabubujikayondani‟ na baada ya kulisha watu zaidi ya elfu tano alitaja Mkate

Page 86: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA575

wa Uzima. Amekuja kwa shabaha ya kuwaokoa na kuwapatia wanadamu uzimatele. Kwake kondoo watendewa kwa neema na kuonja wema wa Mungu. Barakanyingine ya wokovu ni usalama, wanahifadhiwa, wanatunzwa, hawawezikupotoshwa na kudanganywa, mradi waijali sauti ya Mchungaji wao na kumfuatabarabara. Waliokuwa wamepotea wasikia hali ya „kupatikana‟ yaani kuletwanyumbani na kurudishwa zizini (Lk.15:1-6)

„wote walionitangulia ni wevi na wanyang‟anyi‟ hao ni akina nani? Pengine Yesualikuwa akisemea wale viongozi waliokuwapo wakati wake, kama Mafarisayo,Masadukayo, Waandishi, Makuhani, n.k. Wengi wao walitafuta faida zao,hawakuwa na mzigo juu ya watu, hawakusikia uhusiano wa ukaribu nao nakuwapenda na kuwahurumia. Ijapokuwa Yesu alikuwa akisema watu wa zamani,twajua kwamba wengine hawakuwa wabaya, akina Musa, Daudi, Isaya, n.k. haowalikuwa wachungaji wema, ila katika Israeli manabii wa uongo walitokea marakwa mara, pamoja na Masihi wa uongo, ambao Yesu alisema kwambawataendelea kutokea baada yake (Mt.24:5). Wengine waweza kuushirikiuchungaji wa kondoo zake wakitumwa na Yeye (Mt.9:35ku) ila wakijitwaliamadaraka hayo, machoni pa Mungu wamehesabiwa kuwa wevi na wanyang‟anyi(Mt.15:12-14).

k.11ku Yesu aliendelea na mazungumzo yake. Ameishadai kuwa Mlango nakudokezea kwamba Yeye ni Mchungaji. Halafu akadai kuwa Mchungaji Mwemaakitanguliza madai yake na maneno ya kutilia mkazo „Mimi ndimi‟. Akazidikufafanua sifa za Mchungaji Mwema. Sifa kuu kupita zote ni Mchungaji Mwemakuutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. Hapo Yesu alitabiri Kifo chake. Kwakawaida, mchungaji aliishi maisha magumu yaliyomgharimu raha za kukaa nakutulia nyumbani. Mchungaji mzuri alihatarisha maisha yake kwa kuwasalimishakondoo, hata hivyo, ilimbidi aishi wala asife kwa ajili yao, isipokuwa kwa bahatimbaya au ajali au kwa lazima kabisa, kwa sababu akifa kondoo watapotewa namchungaji wao. Ila Yesu ni tofauti, itamlazimu kabisa afe kwa ajili ya kondoo, iliawapatie msamaha wa dhambi na uzima wa milele. Hatakufa kwa bahati mbaya,wala kwa ajali, bali kwa hiari atoa maisha yake, wakati utakapowadia, ndipoatakuwa fidia na dhabihu kwa dhambi za ulimwengu mzima. Kwa hiyo, pamojana kuwa Mchungaji Mwema Yesu ni Mwana Kondoo wa Mungu achukuayedhambi za ulimwengu (1:29).

k.12-13 Hapo Yesu alipambanua kati ya tabia ya mchungaji mwema na mtualiyejifanya kuwa mchungaji, ambaye ni mtu wa mshahara afanyaye kazi hiyokwa faida yake mwenyewe. Huyo mtu wa mshahara aweza kufanya kazi vizurimpaka atakapokutana na shida na hasara kwa ajili yake, ndipo atawaachakondoo zake wapatwe na madhara kwa sababu hana mzigo juu yao, hasikiikama amedaiwa kuwatunza. Huenda huyo mchungaji si mbaya, ila jambo muhimukwake ni mambo yake mwenyewe si mambo ya kondoo. Tabia ya

Page 87: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA576

Yesu ni tofauti, mahitaji ya kondoo hutawala maisha yake Yeye anapendakondoo zake na kuwavuta watu Kwake, upendo wake utaonekana Msalabani(12:32).

k.14 Yesu alisisitiza tena jambo la kuwajua kondoo zake, wao ni mali yake,anawafahamu na wao wanamfahamu. Ni jambo zuri sana maana katikakumwamini Yesu kwa kweli kuna ulinzi wa ajabu, mtu hawezi kudanganywaiwapo Shetani atajitahidi kumpotosha na kumwondoa katika imani ya kweli. Nivema kukumbuka neno hilo na kumshukuru Mungu kwa ajili yake, maana wakowengi ambao wanajitahidi sana kuzipotosha imani za watu, watu ambaowamedanganywa wenyewe, pengine bila kutambua. Yesu alitabiri kwambawadanganyifu wengi watatokea (Mt.24:3ku).

k.15 Huo ujuzi wa Mchungaji kuwajua kondoo zake, na kondoo zake kumjuaYeye ni mfano wa jinsi Baba na Bwana wanavyojuana. Ujuzi uliopo kati ya Yesuna kondoo wake ni mfano wa huo ujuzi uliopo kati ya Baba na Mwana, na nimsingi wake. Kwa hiyo, ni ujuzi wa kipekee, na ni muhimu sana.

k.16 „zizi hili‟ ni Israeli na kondoo wengine ambao Yesu atawaleta kwenye zizi niWaMataifa, ili liwepo kundi moja tu la Wayahudi na WaMataifa. Hao wotewataletwa chini ya uongozi wa Mchungaji Mmoja, nao wampe Yeye utiifu waowote. Maneno „kondoo wengine ninao‟ ni wale ambao ameishapewa na Babatangu milele (6:37,39; 17:6,20ku). Wameitwa „kondoo‟ hata kabla hawajaletwaKwake. Neno la WaMataifa kuokolewa na kupokelewa sawasawa na Wayahudikusudi liwepo kundi moja, liliashiriwa zamani katika Mungu kumwita Ibrahimu(Mwa.12:3) nalo lilisemwa wazi katika Isaya 49:6 na baadaye Yesu aliwatumawanafunzi wake kuhubiri Injili ulimwenguni mwote (Mt.28:18ku. Mdo.1:8).

k.17, 18 Waumini wote ni tuzo la Baba kwa Mwana wake mpendwa kutokana nautayari wake wa kuutoa uhai wake kwa ajili yao. Yesu alikuwa radhi na mapenziya Baba ijapokuwa yalimgharimu sana na kusababisha dhiki zake nyingi. Babaampenda Mwana kwa sababu Mwana anatupenda hata kufa kwa ajili yetu. Hajayetu kubwa ya kupata tiba ya dhambi ilimvuta Yesu aiitikie, na itikio lake lilivutaupendo wa Baba kwa Mwana. Kwa hiyo kuna uwiano kati ya Yesu kufa kwa ajiliyetu na upendo wa Baba kwa Mwana, upendo huo ni msingi wa Kujitoa kwaYesu. Yesu alikuwa na madaraka juu ya uhai wake, na yote aliyoyafanya alitendakwa hiari ya mapenzi. Pamoja na uwezo wa kuutoa uhai wake alikuwa na uwezowa kuutwaa tena. Alijua hakika atafufuka kutoka kwa wafu. Haikuwezekana kifokimshike (Mdo.2:24). Kwa kusema hivi adui zake hawataweza kukifurahia kifochake kama wamemshinda. Vilevile wafuasi wake watajua kwamba Kifo chakeambacho kilitekelezwa na adui zake, Mungu alikuwa amekiruhusu na kukiwekakuwa njia ya wokovu. Yesu alitawala mwenendo wake na mwisho wake. Yeye naBabaye hufanya kwa pamoja. Yesu alifanya kwa hiari. Pilato, Kayafa, wajumbewa Sanhedrin, Yuda Iskariote,

Page 88: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA577

ijapokuwa walihusika kwa kufanya walivyotaka, hawakutawala mambo hayo,Mungu alikuwa juu ya matukio yote.

k.19-21 Wayahudi walionaje mazungumzo hayo ya Yesu alipodai kuwaMchungaji Mwema na kufafanua hali za viongozi waliopaswa kuwa wachungajiwema, ila sivyo walivyo. Walitengana wao kwa wao. Baadhi walisema „ana pepo‟na „ana wazimu‟ hakuna haja ya kumsikiliza. Baadhi walimtetea Yesu kwasababu walikumbuka uponyaji wa yule mtu aliyezaliwa kipofu „Je! pepo awezakuwafumbua macho vipofu?‟ Ila hao hawakuwa tayari kujitoa zaidi kwa Yesu.Kama ambavyo tumeona tangu 7:12 Yesu amekuwa fumbo kwa wengi,wametatanishwa sana naye na kila tendo na kila hotuba vilisababishamajadiliano makali. Hata hivyo, Yesu aliendelea kuwapa changamoto ya kukatashauri juu yake.

10:22-42 Mabishano yaliyotokea katika Ukumbi wa SulemaniMabishano hayo yalitokea hekaluni katika Ukumbi wa Sulemani (huenda Yesualichagua mahali hapo kwa sababu ilikuwa wakati wa baridi). Ilikuwa wakati wakuadhimisha Sikukuu ya Kutabaruku iliyofanyika mwisho wa mwezi waDesemba. Kwa hiyo ni kama miezi mitatu baada ya Sikukuu ya Vibanda (7:2).Sikukuu hiyo haikuamriwa katika Agano la Kale. Ilianzishwa mwaka K.K.164kwa kuadhimisha ushindi wa Yuda Makabayo. Mfalme wa Shamu alinajisihekalu kwa kusimamisha sanamu ya kipagani humo. Jambo hilo liliwachukizasana Wayahudi, na mmoja wao aliinuka na kuwaongoza wengi kupigana naWashamu. Mwishowe wakashinda na Sikukuu iliwekwa kwa kulitakasa hekaluna unajisi, ndipo kila mwaka waliendelea kuiadhimisha Sikukuu hiyo nakukumbuka ushindi wa Yuda Makabayo na wenzake. Wakati kama huoWayahudi walitamani sana kupata Masihi, wa aina ya Yuda Makabayo,atakayepigana na Warumi na kuwaondoa.

k.24 Twaona Wayahudi walimzunguka Yesu na kumbana sana. Walimwulizamoja kwa moja swala kubwa kabisa „Kama wewe ndiwe Kristo utuambiewaziwazi‟. Neno hilo ni kiini cha mahangaiko yao yote. Alikuwa amekiri kuwaMasihi kwa Mwanamke Msamaria (4:26) na kwa wafuasi wake wa karibualizungumzia jambo hilo (Mt.16:13ku) ila kutamka wazi hakufanya. Waliona kamawameachwa hewani, Yesu amedokezea neno hilo bila kulitamka wazi.Hawakutaka kujua kwa kusudi la kumkubali na kumwabudu, la! sivyo, walikuwawakitafuta neno la kumshtaki barazani. Kwa nini Yesu aliwaacha hewani bilakusema wazi „Mimi ni Masihi‟. Ni kwa sababu katika mawazo yao walifikiri nakutaka Masihi wa siasa, mtu wa vita, ili waondolewe chini ya utawala wa Kirumi.Tena Yesu alijua katika wakati huo wa Sikukuu ya kuwakumbuka WaMakabayomawazo hayo yalizuka kwa nguvu. Wakati huo haukufaa hata kidogo alitamkeneno hilo wazi.

k.25 Yesu aliwajibu, ila si moja kwa moja kama walivyotaka. Matendo yotealiyoyafanya pamoja na maneno yake yalimshuhudia kuwa Masihi aliyetumwa

Page 89: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA578

na Baba. Ametenda matendo mengi ya ajabu, kumponya kiwete aliyelemewamiaka 38; mtu aliyezaliwa kipofu; kumfufua binti Yairo, kugeuza maji kuwa divai,kuwalisha watu zaidi ya elfu tano kwa kutumia mikate mitano na visamaki vitano.Alifundisha vizuri sana hata watu waliotumwa kumkamata wakavutiwa namaneno yake. Kila mara alisisitiza kwa nguvu uhusiano wa ukaribu kabisa naBaba. Kwa kutumia maneno „Mimi ndimi...‟ alidai kuwa Bwana Mungu. Wakatiwote alisema wazi kwamba hafanyi neno lolote kwa nafsi yake au kwa mapenziyake tu. Hakujiinua na kujichukulia Cheo hicho cha Umasihi, ila alipewa utumewa kuwa Masihi na Baba, na Baba ni asili ya mambo yake yote. Hivyo, ingawahajatamka wazi kuwa Masihi, hata hivyo, yote aliyotenda na kusemavilimshuhudia kuwa Ndiye Masihi. Katika Injili yote uzi moja unapitia ndani yake,uzi wa uhusiano wake wa ukaribu kabisa na Baba.

k.26 Umasihi wake ni wa kiroho na unatambulikana kiroho kwa wale waliokondoo wake, kwa wale wanaoisikia sauti yake, kwa wale wenye kuona kiroho.Ni dhahiri kwamba hao wasiomsadiki si kondoo wake. Wako wanaoisikia sautiyake, wako wasiosikia sauti yake. Wasiosikia sauti yake hawawi kondoo wake.Walipaswa kuisikia na kuijali. Hayo yote ni chini ya mwavuli wa utawala waMungu, si neno la kushtua kama neno la kigeni, ilitazamiwa kwamba ndivyoitakavyokuwa (6:44; 12:37ku)

k.27-30 Alirudia kusisitiza jambo la kondoo wake kuisikia sauti yake na yeyekuwajua na wao kumfuata. Maneno ya kifungu hicho yana faraja kubwa kwawaumini wote. Yeye huwapa kipawa cha uzima wa milele, uzima wakemwenyewe. Matokeo ya kuwa na uzima wake ni kwamba hawatapotea kamwe,wala hakuna mtu wa kuwapokonya katika mkono wake. Kwa hiyo, mtu asihofukukata shauri la kumfuata Kristo kwa kufikiri kwamba huenda mbeleniatashindwa. Wala asitishwe kwa kuangalia vipingamizi vya wengine; la, sivyo.Wakati huo Yesu alipokuwa akisema maneno hayo Mafarisayo na wenginewalifanya juu chini kumwaibisha na kuwapoza wale waliotaka kumfuata. Jambomuhimu si kwamba mtu awe amemshika Kristo ila Kristo amemshika mtu, Kristoaliye na nguvu kupita wote (mfano wa baba kumshika mtoto si mtoto kumshikaBaba). Tena zaidi ya Kristo kumshika, Baba amshika pia, na ni nani amshindayeMungu Baba, ni nani mwenye nguvu au hekima za kumzidi Yeye. Je! mtu awezakumnyang‟anya Mungu mali yake? Je! mtu aweza kumnyang‟anya Mwanakondoo wake, ambaye kwa ajili yake alimwaga damu yake ili amwokoe? Je!atakunja mikono na kukaa kimya, asifanye lolote, huku mwingine akichukua maliyake? haiwezekani kuwa hivyo. Mwana na Baba ni umoja na katika jambo hilo lakuwatunza kondoo zao Mwana hafanyi peke yake, amtegemea Baba.Alipokaribia Kufa Yesu aliwakabidhi wanafunzi wake kwenye ulinzi wa Babake(17:11). Baba na Mwana ni wa asili moja na utendaji wao wote ni mmoja. Kondooni wa thamani sana, Bwana aliwanunua kwa damu yake mwenyewe. Pamoja nahayo Baba amempa Mwana hao kondoo kama zawadi na hakuna awezayekumshinda Baba. Ukweli wa jambo hilo ulionekana katika habari za yule kipofualiyeponywa.

Page 90: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA579

k.31-39 Uadui wa Wayahudi ulizidi. Katika sehemu iliyotangulia hoja ilihusu Yesukuwa Masihi, na katika sehemu hii hoja yahusu Yesu kuwa Mwana wa Mungu.Hapo nyuma alikuwa amewaelezea kinaganaga tofauti kubwa kati ya MchungajiMwema na wachungaji wa mshahara, na kati ya kondoo wake na wasio kondoowake. Ila neno lililowachokoza zaidi kuliko hilo lilikuwa kusema Yeye na Babakeni wamoja. Waliposikia maneno hayo wakaanza kuokota mawe tayari kumpiga,kulingana na hukumu kwa dhambi hiyo iliyowekwa katika Torati. Machoni paoamekufuru kabisa katika kujifanya mwenyewe kuwa Mungu. Walimwona kuwamwanadamu tu, aliye na asili ya kibinadamu. Ila ukweli ni kwamba „hakujifanya‟kuwa Mungu, alikuwa Mungu aliyefanyika Mwanadamu (Flp.2:5ku) na kamaangalikana jambo hilo angalikuwa mwongo, tena mwongo mkubwa. Angalijifanyaangalistahili kabisa kuuawa. Yesu hakutoroka mara alipoona wameokota mawe,akawauliza ni kwa kazi ipi yaani mwujiza upi wanataka kumpiga kwa mawe?Amefanya miujiza (ishara) nyingi mbalimbali, mikubwa, hata kumfumbua machomtu aliyezaliwa kipofu. Ametoa hotuba za maana sana akitumia maneno „MimiNdimi‟ kwa madai ya kuwa „nuru ya ulimwengu‟; „mkate wa uzima‟ na „maji yauzima‟ n.k. Yesu aliyaunganisha hayo yote pamoja kuwa ushuhuda juu ya asiliyake na kwa kutumwa na Baba na kwa umoja wake na Baba na kwa uhusianowa ukaribu kabisa naye.

Kwa hiyo Yesu aliwapa changamoto „ni kwa kazi ipi mnataka kunipiga kwamawe?‟ Maana kila kazi (mwujiza) ilikuwa ishara ya asili yake na ilitoa ushuhudawa kweli wa kuwasaidia watu wamtambue. Kazi zenyewe zilikuwa njema, zahuruma, za upendo, na za uwezo mkubwa.

Waliepa kusema juu ya kazi zake bali walirudia jambo lililowakwaza kabisa,jambo la kukufuru. Ndipo Yesu akataja Torati na kuwakumbusha maneno yaZab.82:6 akionyesha kwamba hata wao walikubali kuwaita wanadamu „miungu‟.Ni vigumu kujua hao walikuwa akina nani; wengine wamefikiri ni waamuziwaliojulisha watu hukumu za Mungu. Haidhuru ni akina nani, Yesu alitofautishahao wenye asili ya kibindamu na Yeye aliye na asili ya Mungu. Mbona wamwonaamekufuru, huku wanadamu wengine wameitwa „miungu‟ na „wana wa Aliye juu‟?Yeye ni Mungu aliyefanyika Mwili, Yeye ametumwa na Baba, Yeye Babaamemtakasa, yaani ametengwa kipekee kwa ajili ya Utume huo Mbona, basi,asiitwe Mungu? kwa nini wamshtaki kuwa anakufuru? Yeye ni Mwana wa Mungukwa asili, si kwa kuitwa jina hili tu. Twaona Yesu alikuwa na mawazo ya hali yajuu kuhusu Maandiko. Alidondoa katika sehemu ya kawaida tu, hata hivyo,alilihesabu kuwa Neno la Mungu. Kama Yesu hakuwa na asili katika MunguWayahudi walikuwa na haki kabisa ya kumshtaki kuwa amekufuru. Hawakuwa namzigo juu ya kweli; hawakuwa tayari kuzingatia maana ya matendo na manenoyake makuu. Kwa hiyo hata akifanya juu chini kamwe hawatamkubali, kwa kifupi,hawakumtaka. Baadaye atamfufua Lazaro (mfu wa siku nne) kutoka wafu, hatahivyo, hawatamkubali. Wakajaribu tena kumkamata, wakashindwa, hatuambiwiYesu alitokaje? ila twajua kwamba saa yake ilikuwa bado, lakini inakaribia.

Page 91: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA580

k.40-42 Yesu alijitenga nao na kwenda mpaka ng‟ambo ya Yordani, mahalialipofanya kazi Yohana Mbatizaji. Watu wengi walimfuata, hasa walivutwa namambo mawili. Miujiza yake aliyokuwa akiifanya pamoja na kuukumbukaushuhuda wa Yohana Mbatizaji juu yake. Yohana hakufanya miujiza, hata hivyo,wengi walimwendea na kubatizwa naye. Yohana aliwaelekeza kwa yuleatakayekuja, Masihi mwenyewe, alimsifu sana, alisema kwamba atakuwa mkuu,atampita yeye, hata yeye hakustahili kulegeza gidamu ya viatu vyake, na yakwamba itawapasa watu wamwache yeye na kumwandama Yesu. Kwa kawaidaWayahudi hawakuwasifu wale ambao hawakutenda matendo makubwa, hatahivyo, Yohana alikuwa amewagusa sana. Walimpa sifa kubwa „yote aliyoyasemaYohana yalikuwa kweli‟. Wakati huo wengi walimwamini Yesu ila hatujuiwalimwamini kwa dhati au vipi.

MASWALI1. Katika kudai kuwa Mchungaji Mwema Yesu alionyesha tofauti kati yake na

akina nani?2. Yesu aliwaeleza kuwa watu wa tabia gani?3. Eleza tabia za Mchungaji Mwema4. Wema wa Yesu Mchungaji Mwema ulidhihirika katika tendo gani hasa?5. Eleza baraka za kondoo wa Yesu.6. Kwa nini Wayahudi walifikiri Yesu amekufuru?

11: 1-53 Yesu alimfufua LazaroHabari hii ni kubwa sana, ni habari ya ishara ya saba na ya mwisho, aliyoifanyaYesu mbele za watu. Mwujiza huo ulizidi mingine yote iliyotangulia, nauliongoza matukio yaliyofikia upeo katika ishara ya mwisho, Kufa na Kufufukakwa Yesu Mwenyewe. Mwujiza wa kumfufua Lazaro aliyekuwa mfu wa siku nneuliudhihirisha utawala wa Yesu juu ya mauti na matatizo yanayowapatawanadamu kwa jumla. Ulitia muhuri wa hakika juu ya madai yake makubwakuwa Ufufuo na Uzima.

Katika habari hiyo twaona maendeleo ya imani ya Mariamu na Martha. Kisha,matokeo ya mwujiza huo yaliwahimiza viongozi kutekeleza mipango yakumkomesha Yesu ili wasije wakapunguziwa kabisa heshima na madarakamachoni pa watu (11:47). Kwa mwandishi Yohana jambo hilo la Yesu kumfufuaLazaro na kudai kuwa Ufufuo na Uzima lilikuwa sababu kuu ya Kuuawa Kwake.Hivyo, Yesu alifika upeo wa madai yake na viongozi walifika upeo wakutokuamini wakishindwa kumvumilia zaidi.

Ijapokuwa Lazaro alifufuliwa kwa kuwahurumia Mariamu na Martha zaidi ilitoanafasi kwa Yesu kudhihirika kuwa Ndio huo Ufufuo na Uzima (k.25). Kwa tendohilo kuu Yesu alikusudia kuwathibitishia watu kwamba ni mapenzi ya Babake

Page 92: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA581

kuwapa watu Uzima wa Milele, na huo uzima ni Yeye Mwenyewe. Yohanaalisisitiza jinsi Lazaro alivyokuwa mfu siku nne na maozo yalikuwa yameanza.Walio wafu katika dhambi Yesu atawahuisha. Dhambi si bahati mbaya tu, walahitilafu ndogo tu, wala hali ya muda tu itakayotoweka baadaye. La, hata kidogo!Dhambi ni mfano wa mauti, tu wafu katika dhambi.

Tendo hilo lilitokea majira ya baridi, kuelekea mwisho wa maisha ya Yesu.Alikuwa amekwenda ng‟ambo ya Yordani kwa sababu ya uadui wa Wayahudi(10:40) ndipo jambo hilo lilimleta karibu na Yerusalemu kabla ya Pasaka yake yamwisho (12:1). Mwujiza huo ni upeo wa huduma yake na uliyakamilisha madaiyake yote yaliyojengwa juu ya ishara zake ambazo zilidhihirisha uhusiano waukaribu na Babake.

Utengano uliotokea kati ya wenye kuamini na wasioamini ambao ulianzakuonekana wazi hapo nyuma (7:12, 40-44; 8:30, 59; 9:16; 10:19-21) na kukazwabaada ya habari hii. Katika 10:41 tuliona kwamba watu walikuwa hawajausahauujumbe wa Yohana Mbatizaji na kwa ajili yake wengi walimwamini Yesu.11:1-16 Hapo twapewa habari jinsi mambo yalivyotokea. Bethania ilikuwa kusinimashariki ya Yerusalemu, umbali wa maili mbili hivi. Mariamu ametambulishwakuwa yule aliyempaka Yesu marhamu (12:1ku). Katika 19:25- 26; 20:1 Mariamuwengine, tofauti na huyo, wametajwa. Pengine Lazaro hakujulikana sana kwasababu ametambulishwa kwa njia ya dada zake. Tumezoea kufikiri kwamba haowote watatu waliishi pamoja, ila si lazima tufikiri hivi. Katika karamu iliyofanyikabaada ya Lazaro kufufuliwa, yeye ameonekana kama mgeni (Lk.12:2). Penginealikuwa na nyumba yake karibu; ila hatujui kwa hakika.

Jambo la kwanza ni kuugua kwa Lazaro na Yesu alipelekewa habari na dadazake. Walitaka rafiki yao mpendwa apate habari na bila shaka walitazamiaatakuja mara na kumponya. Walipatwa na shida ambayo ni kawaida yawanadamu kupata, watu huugua na watu hufariki dunia, ila umaarufu wa habarihii umetokana na jinsi Yesu alivyofanya, na jinsi alivyoimaanisha. Aliitafsiri kwamaana ya kiroho na kwa kuiweka katika mwanga wa mapenzi na utukufu waMungu.

Dada wa Lazaro walitumaini kabisa kwamba Yesu atakuja mara apatapo habarina bila shaka walimsubiri kwa hamu sana (k.21, 32). Walipompelekea habarihawakumwagiza aje, pengine kwa sababu walijua ni hatari akija kusini. Huendawalikumbuka alimponya mtu kwa mbali, kwa kutamka neno tu (4:43). Walitajashida na kumvuta kwa lugha „yeye umpendaye‟. Yesu alikuwa amezoea kufikanyumbani kwao (Lk.10:38) amejihusisha nao kwa ukaribu, yawezekana ni mahalialipopenda kustarehe alipofika sehemu za Yerusalemu. (Katika Injili nnetumepewa habari chache kuhusu Yesu kuwa na rafiki n.k.).

Page 93: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA582

k.4 Itikio la Yesu lilikuwa la ajabu sana. Alikaa siku mbili zaidi mahalialipokuwapo na katika maelezo yake alitumia maneno ya fumbo „ugonjwa huo siwa mauti, bali kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwahuo‟. Yesu hakuwa na maana kwamba Lazaro hatakufa, ila kufa kwake si nenola mwisho, yatatokea mambo yatakayomtukuza Mungu na kumdhihirisha YeyeMwenyewe kuwa Mwana wa Mungu. Neno muhimu si kuishi kwa mtu, au kufakwa mtu, bali Utukufu wa Mungu. Utukufu wa Mungu ndio lengo kamili na halisila uumbaji wote. Yesu alijua yote yatakayotokea hata kabla hayajatokea. Zaidi yakumsifu Mungu watu watamtukuza Mungu watakapomwona Lazaro anatokakaburini, yu hai, baada ya kuwa mfu siku nne.

(Katika mawazo ya Mwandishi Yohana utukufu wa Mungu utadhihirika zaidi sanapale Msalabani, Yesu atakapokufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu. KumfufuaLazaro ni hatua itakayowachokoza wakuu waitekeleze mipango ya kumwuaYesu).

k.5-6 Itikio la Yesu laweza kufikiriwa kuwa gumu lililokosa kuwaza mahitaji yaLazaro, Martha, na Mariamu, kana kwamba hakuwapenda. Lakini Yohanaamesisitiza kwamba Yesu aliwapenda.

Ijapokuwa itikio lake kwa shida yao lilikuwa vigumu kueleweka, hata hivyoliliongozwa na upendo. Yesu aliwazia sana ni kwa tendo gani na kwa njia ipi imaniyao itakuzwa pamoja na imani ya wanafunzi wake (k.15) maana muda si mudawataachiwa na Yeye, Bwana wao, nao watakabidhiwa Utume mkuu wakuwajulisha walimwengu habari za Kufa na Kufufuka Kwake. Iliyo mbele yakeaende na kumponya Lazaro, au asubiri kifo chake ndipo aende na kumfufua. Je!Yesu alikosa huruma na kufanya vibaya alipowaacha dada zake wahangaikesana, wakiwa na hali ya kumwangalia ndugu yao akizidi kuugua, hukuwakimtazamia Yesu atafika wakati wowote. Kukawia kulikuwa jambo kubwakwao ila kwa Yesu kulikuwa jambo dogo, maana yeye alikuwa na utawala kabisajuu ya mauti, angalikuwa mwanadamu angalifanya kwa haraka, ila kwa sababualikuwa Mungu hakuwa na haja ya kufanya haraka. Hawezi kusukumwa namatakwa ya wanadamu hata yakiwa mazito. Zaidi ya yote alitawaliwa na mapenziya Baba yake, Baba atamwongoza saa ya kwenda Bethania (2:1ku. 7:3ku). Tenakwa kukawia mpaka Lazaro afe na kuwa mfu kweli, haitawezekani mtu asemeYesu alimrudishia fahamu tu.

k.7-8 „twende Uyahudi‟ hakusema „twende Bethania‟ ni ukumbusho kwambawatakapoingia Uyahudi, wanaingia mahali pa hatari, Uyahudi ni mahali wakaapowengi wasiomwamini na wale wanaotaka kumwua. Yesu alikuwa jasiri.Wanafunzi waliogopa kwenda, hawakutaka Yesu aende. Bila shaka kwa jinsiYesu alivyokawia walidhani kwamba Lazaro amepata nafuu na ikiwa ni hivyohakuna haja ya kwenda huko.

Page 94: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA583

k.9-10 Yesu aliwaonyesha kwamba haipo sababu ya kuhofu kwa sababu Yeyeatafanya kazi mpaka saa yake itakapofika, mpaka amemaliza shughuli zotealizokabidhiwa na Baba yake. Baada ya hapo alijua kwamba wanadamuwataruhusiwa kufanya waliyotaka, watamkamata na kumwua. Iliwapasawaandamane naye, wasihofu, watakuwa salama wakiwa pamoja naye, kuwa naYeye ni kuwa na Nuru, wakimwacha basi, watakuwa gizani.

k.11 Ndipo Yesu aliwaeleza kwamba Lazaro amekufa, ila alitumia neno „amelala‟kwa sababu alijua hakika kwamba kitambo kidogo naye atamfufua kutoka kwawafu. Yesu atamwamsha. Si kwamba anatumaini tu litakuwa hivyo, Yesu alijuakwa hakika kwamba itakuwa hivyo, kwa sababu ni kazi yake kuwafufua wafukimwili na kuwahuisha kiroho walio wafu katika dhambi. Tazama jinsialivyojibagua na wanafunzi „rafiki yetu amelala, lakini ninakwenda nipatekumwamsha. Wao waweza kwenda naye, ila ni Yeye tu mwenye uwezo wakumwamsha Lazaro.

k.12-13 Wanafunzi walidaka neno „amelala‟ na kuliwaza kwa kawaida ya„kulala usingizi‟ na walijua kwamba kama Lazaro ametulia na kupata usingizi,basi hali yake ina nafuu, atapona tu. Ni wazi kabisa kwamba walitafuta sababuza kutokwenda. Wayahudi hawakuzoea kuwaza kufa kama ni kulala. Ndiyosababu wanafunzi walikosa kuelewa lugha hiyo.

k.14 Yesu alitoboa wazi kwamba Lazaro amekufa. Alijuaje? hatuambiwi kwambamtu alifika na kumpasha habari. Inaonekana alijua nafsini mwake tu kwa ujuziwake wa kipekee.

k.15-16 „Lazaro amekufa, nami nafurahi‟ bila shaka walishtuka kabisa nakuyashangaa maneno hayo. Mbona mtu akifurahie kifo cha mpendwa wake?Alieleza kwamba alifurahi „kwa ajili yao‟ kwa sababu kwa kumfufua Lazaro waowatajengwa sana sana katika imani yao. Alitaka kuwaelimisha katika imaniinayoshinda mauti, isiyotikiswa au kupozwa na dhiki za wanadamu. Alikuwaakiwaandaa kwa wakati ulio karibu, watakapopata mshtuko mkubwawasioutazamia, wakati wa Kufa Kwake, wakati watakapofiwa na Bwana wao narafiki yao mkubwa. Atakapouawa watahuzunika sana, watapitia katika dhikikubwa, ila watasaidiwa watakapomkumbuka Lazaro na jinsi Yesu alivyomfufua.„twendeni kwake‟ Yesu hakusema „twende kwa maiti‟, Lazaro ni mtu si maiti.

Tomaso, alikuwa mtu ambaye hakusema kwa haraka, tofauti na Simoni Petro,aliuonyesha ujasiri pamoja na utiifu kwa Bwana wake. Alijitoa kwenda pamoja naYesu ijapokuwa alitazamia kwamba watauawa. Aliwashauri wenzake waendepamoja nao. Tumezoea kumwaza Tomaso kuwa mtu wa mashaka, mtu mzito wakuamini, hata hivyo, alikuwa mtu aliyejitoa mia kwa mia kwa Yesu.

k.17ku Bethania ilikuwa karibu sana na Yerusalemu, kwa hiyo Yesu alikuwaakisogea karibu na mahali pa adui zake wengi. Wayahudi wengi walitoka

Page 95: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA584

Yerusalemu na kujiunga na familia hiyo katika huzuni yao, kama ilivyokuwadesturi ya Kiyahudi. Pengine familia hiyo walijulikana sana. Yesu alipofikaBethania siku nne zilikuwa zimepita tangu Lazaro alipofariki dunia, kwa hiyo,halikubaki tumaini lolote juu yake, nje ya Mungu kufanya tendo la ajabu, maanaalikuwa ameanza kuoza. (Nyakati zile watu wengi walifikiri kwamba roho ya mtuilikaa karibu na mfu kwa siku tatu tayari kumrudia, ila ilipofika siku ya nne, naameanza kuoza, ndipo itaenda mbali). Dada zake walikuwa na tumaini kwambaYesu angaliwahi kufika angaliweza kumzuia asife. Wote wawili walisema hivyokwake na ni vigumu kujua kama walikuwa wakimlaumu kiasi fulani kwa kusemahivyo (k.21,32). Wa kwanza kumlaki Yesu njiani alikuwa Martha, tumeishaonatabia yake ni kutenda kuliko kuwaza na Mariamu alikuwa na tabia ya kuwazakuliko kufanya (10:38). Hatujui kama Yesu alikuwa amemwita amlaki njiani iliapate nafasi ya kuzungumza naye faraghani.

k.22ku Kifungu hicho kinatatanisha, Martha alikuwa akitazamia nini kwa manenohayo? Je! aliamini yote yawezekana, hata Lazaro kufufuka kutoka wafu? Labda,ila ilipofika saa ya kuipima imani yake, imani yake ilipungua. Au, pengine, alisematu, kama kumridhisha Yesu. Au, ni kwa sababu amechanganyikiwa sana, maraameshikwa na huzuni, mara na tumaini, na hasa kwa sababu Yesu yupo, hakujuani nini litakalotokea. Tukilinganisha na k.24 na k.39 ni vigumu kufikiri kwambaaliamini Yesu atamfufua Lazaro wakati huo. Yesu aligeuza mawazo yake kwa„ufufuo‟. Martha hakuwa na wasiwasi kuhusu ufufuo wa siku ya mwisho.

k.25 Ndipo Yesu alimfunulia jambo kubwa mno, akisema kwa wazi „Mimi ndimihuo ufufuo, na uzima...‟ Si kama ufufuo na uzima ni vipawa anavyotoa, bali YeyeMwenyewe Ndiye ufufuo na uzima. Hapo nyuma amedokezea jambo hilo(Yn.5:21, 25-29; 6:39-40) pamoja na kudai kuwa Chakula cha Uzima, Maji yaUzima, Mchungaji Mwema wa kuleta uzima tele, na kwa ishara ya kugeuza majikuwa divai aliashiria uzima mpya. Hata mtu akifa kimwili ataishi kwa Yesu. Mautiya mwili si kitu kikubwa, wala si jambo la mwisho, kwa wale wamwaminio Yeye.Kwa muumini mauti ni mlango wa kuingia maisha mapya wa kuuendelezaushirikiano wa ukaribu zaidi na Yesu na Mungu. Hapo duniani twaanzaushirikiano huo tunapompokea Kristo maishani mwetu, na ushirikiano huohauvunjiki wakati wa kufa bali unazidi. Ni uhusiano na ushirikiano usiowezakukatika. Kwa hiyo, Yesu alimpasha Mariamu habari ya nguvu mpya kwa maishaya sasa, pamoja na ahadi ya maisha mazuri zaidi baadaye. „Hatakufa‟ manenohayo yana maana gani - ipo mauti ya kimwili, ipo mauti ya kiroho. Mauti ya pili niya wenye dhambi wanaokufa katika dhambi zao, wakiwa chini ya adhabu yamilele. Yesu ni mshindi wa mauti, ameimeza mauti kama mtu amezavyo kidonge.

Yesu alitoa mafundisho hayo kwa Martha kabla hajamfufua Lazaro, kusudimwujiza wa kumfufua usibaki hewani kama mwujiza tu, bali uwe kwake ishara yautukufu na uwezo mkuu wa Yesu na uhusiano wake na Baba aliyemtuma.

Page 96: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA585

k.26 Yesu alimdai Martha aishuhudie imani yake, alimpa changamoto „Je!unasadiki hayo?‟. Alitaka Martha ajue hayo kibinafsi ili yasiwe dhana au fundishokichwani mwake tu. Akaitika „Naam, Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba .....‟Alisadiki nini? (a) Yesu ni Masihi (b) Yesu ni Mwana wa Mungu (c) Yesu ni yuleajaye ulimwenguni kama Mungu alivyoahidi. Martha alikiri hayo yote kabla yaYesu kumfufua Lazaro.

k.28-32 Mariamu alikuwa ametulia nyumbani hali amezungukwa na Wayahudiwengi waliokuja kuwafariji (k.19). Yesu alitaka kusema naye faraghani, na Marthaalimwita kwa pembeni na kumwambia hivi ili apate nafasi kama alivyopata yeyekushirikiana na Yesu. Kwa sababu hiyo Yesu alikuwa amebaki pale nje yaBethania mahali alipozungumza na Martha. Lakini watu walipomwona Mariamuameondoka nyumbani kwa haraka waliamua kumfuata wakidhani kwambaanakwenda kaburini kulia. Kwa njia hii wengi watakuwa mashahidi wa kuonamwujiza wa Lazaro kutoka kaburini yu hai. Mara alipofika kwa Yesu Mariamuakaanguka miguuni pake na kusema maneno yaleyale aliyosema Martha, daliliya kuwa walikuwa wameongea sana jinsi ambavyo walidhani kwamba mamboyangalikuwa tofauti kama Yesu angaliwahi kufika.

k.33 Ni dhahiri kwamba hakuna aliyewaza kwamba Yesu atamfufua Lazaro. Kwaimani dada zake walifikiri kwamba kama Yesu angalikuwapo ndugu yaoasingalikufa, hata na wengine walielekea kufikiri hivyo (k.37). „Yesu aliuguarohoni, akafadhaika roho yake, akasema, Mmemweka wapi?‟. Yesu alisikia shidakubwa rohoni mwake. Katika Kigriki neno lililotumika kwa „akafadhaika rohoyake‟ ni aliudhika na kukasirika. Ni nini iliyosababisha Yesu ashikwe na hasirakiasi hicho? Kwa kuona huzuni zao Martha na Mariamu kulimfanya awaze sanaubaya wa mauti, utawala wake, kitisho chake, pamoja na asili yake katika uasiwa wanadamu, kutokuamini kwao, pia kumkumbuka yule adui mkuualiyeshawishi wanadamu kumwasi Mungu kwa ahadi ya uongo „hakikahamtakufa‟ (Mwa.3:4ku). Mawazo hayo pamoja na huzuni yake vilimchokoza naroho yake ilijaa hasira na huzuni. Tukumbuke kwamba alitumwa ulimwenguni naBaba ili apambane na maadui hawa wakubwa, dhambi, mauti, Shetani nakuvunja nguvu zao.

k.34 Basi, wakampeleka kaburini ili ashiriki nao pale penye giza na mauti.Walidhani kwamba giza na mauti vinatawala, kumbe Yeye amekuja iliavibatilishe. Alipolijia kaburi alikuja kama mpiga vita shujaa wa kupambana naadui zake, mauti, dhambi, na Shetani. Hapo twapewa kuona moyo wa ndani waYesu katika kutupatia wokovu, hakuja kaburini kwa moyo baridi, wala hakujakama mtu asiyesikia kitu ndani. Alikuja kwa moyo shujaa, uliojaa ghadhabu juuya adui zake. Alihuzunishwa sana alipoona huzuni ya Martha na Mariamu, narafiki zao, hata na wale waliojiunga nao katika kumwombelezea Lazaro.Akaruhusu roho yake ishirikiane nao katika huzuni zao.

Page 97: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA586

k.35-37 „Yesu akalia machozi‟ si kwa fujo wala kwa kelele, wala kwa kukatatamaa kama wengine, maana alijua atamfufua Lazaro. Alijiunga na wanadamukatika huzuni zao na kulia pamoja nao, ila huzuni yake ilitofautiana na huzuniyao. Waliokuwapo walitafsiri kama alilia kwa sababu ya pendo lake kubwa kwaLazaro. Walikumbuka jinsi alivyompa uwezo wa kuona yule aliyezaliwa kipofu nakuuliza kwa nini asingaliweza kumzuia Lazaro asife. Mpaka hapo imani yao nikama kutokuamini kwa sababu inategemea kuyaona maajabu, badohawajamwamini kuwa Mwana pekee wa Baba, mwenye umoja naye.

k.38 Yesu akafika kaburini, hali akiugua tena nafsini mwake. (neno ni lile laKigriki lenye maana ya kukasirika). Hakuja kama mtazamaji tu, alikuja kama yulealiyekuwa amejitoa kabisa kupiga vita na adui mkuu wa wanadamu, yaani mautiiliyopata nguvu yake kwa dhambi (1 Kor.15:26.55ku).

k.39 Ndipo ilipofika dakika kwa Yesu kuuonyesha uwezo wake mkuuakawaamuru waliondoe jiwe. Papo hapo Martha akampinga akimkumbushaYesu kwamba Lazaro amekuwa maiti siku nne na jiwe litakapoondolewa mnukombaya utasikika (imani yake ilikuwa na mpaka). Ila Yesu alikazanaakimkumbusha mawazo aliyomwambia hapo nyuma juu ya kuuona utukufu waMungu. Kisha wakaliondoa jiwe. Bila shaka wote waliokuwepo waliusikia mnukowa maiti. Ndipo Yesu akamshukuru Baba yake kwa kumsikia. Ndipo alifunuashabaha yake juu ya kumshukuru Baba kwa wazi. Lengo lake hasa lilikuwautukufu wa Mungu, ijapokuwa alimhurumia Lazaro na dada zake, zaidi sanaalitaka Baba yake atukuzwe. Baba akitukuzwa, Yeye naye hutukuzwa. Pamojana hayo alitaka kuikuza imani yao ili wamwone kuwa Mwana pekee wa Babamwenye umoja naye, aliyetumwa naye, mwenye utume maalumu wa kuokoaulimwengu. Hivyo alitoa shukrani kwa Baba hata kabla hajalitenda tendo kuu lakumfufua Lazaro. Alikuwa na imani kubwa katika Baba, na aliwaita wotewaliokuwepo wamwamini Yeye kama Yeye alivyomwamini Baba. Kwa hiyo,katika ombi lake twaona mambo manne,i)alimwita Mungu „Baba‟ na alitufundisha sisi kumwita hivyoii)alishuhudia uhusiano wake na Baba usiokatika „wanisikia sikuzote‟iii)ombi lake lilikuwa kwa ajili ya waliokuwapoiv)alitafuta matunda ya imani yao kukua.

k.43 Kwa sauti kuu Yesu alilia „Lazaro, njoo huku nje‟. Maneno kwa mfu wa sikunne ambaye kimwili hasikii, hajui yanayotokea, hatembei, n.k. Ni ishara kwambahata wafu katika dhambi wataisikia sauti yake na kupona. Mapenzi yake, na amriyake, vina nguvu ya kiutendaji. Ni amri kutoka Bwana wa mauti (5:25, 28-29). Nitendo la Mungu aliyeumba kila kitu kwa Neno lake. Mungu akasema „iwe..ikawa‟(Mwa.1:3ku). Twaona Yesu akisema kwa maneno machache sana, kwa Kigriki ni„huku, nje‟.

k.44 Mara Lazaro akatoka hali amefungwa sanda miguuni na mikononi, nausoni amefungwa leso. Alitoka kwa nguvu ya Mungu ndipo walimwondoa

Page 98: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA587

vitambaa vilivyomzuia asitembee, na tangu hapo alikuwa huru kwenda zake.Hana haja ya kubaki pale na kutazamwa na watu na kuridhisha utafiti wao.Iliwapasa watu walizingatie tendo hilo kuu kuwa ishara kuu ya uwezo wa Yesu,lililoashiria asili yake katika Mungu. Lilikuwa limbuko la ufufuo wa mwisho nathibitisho lake. Ikiwa Yesu alimfufua mfu wa siku nne aliyekwisha kupatikana nauharibifu, aweza kuwafufua wote ambao wamekufa siku nyingi zilizopita, ambaowameishaoza na kutoweka. Hatupewi habari nyingine ya Lazaro, jinsi alivyoishina jinsi alivyokufa baadaye. Imetubakia ishara, ishara na hasa iliyoashiriwa naishara ni muhimu kuliko jambo lenyewe.

k.45ku Maitikio mbalimbali: Kama ilivyotokea mara nyingi, watu walitengana kwajinsi walivyoitikia tendo hilo. Wayahudi wengi waliojiunga na Mariamu na Marthakatika msiba wao walimwamini Yesu, ila baadhi yao waliwaendea Mafarisayo nakuwapasha habari ya mambo hayo. Kwa nini waliwaendea hao waliojulikanakuwa na chuki kwa Yesu? Pengine walitaka kuwajulisha habari hiyo ili wawavutekubadili mawazo yao juu ya Yesu na kuanza kumwazia vizuri. Pengine walitakakuwatahadharisha kwamba ni vema waanze kutengeneza mambo kwa sababuyamefikia upeo. Ila kwa jinsi Yohana alivyoandika akiwapambanua na walewaliomwamini Yesu inaonekana walifanya kwa chuki na wivu.

k.47 Ndipo walikuwapo wakuu walioitisha baraza la Sanhedrin na kukata shaurijinsi ya kumfanyia Yesu. Walikutana katika hali ya wasiwasi mwingi. Yesu alikuwaakizidi kufanya miujiza, tena mikubwa, isiyokanikana. Zaidi ya yote wengi walizidikuandamana naye, jambo lililowaumiza sana. Wivu uliwashika sana kiasi chakuwapofusha akili zao. Wakakosa kutia maanani neno la kweli, hawakuwa tayarikuzingatia ishara zake na maana yake, kwa kuwa hawakumtaka.

„Warumi watakuja na kutuondolea mahali petu na taifa letu‟. Waliogopa kwambawatu watainuka na kufanya fujo wakitaka kuipindua serikali, ndipo Warumiwatakuja na kuwaondoa katika vyeo vyao na kuweka wageni mahali pao katikautawala. Hasa kwa kusema mahali petu na taifa letu‟ ni wazi kwamba waliwazavyeo na heshima zao. Walihofu kwamba watapoteza mamlaka ya kuongoza taifachini ya Warumi, hata pengine kuondolewa uongozi wa hekalu na mambo yake.(Dola ya Kirumi iliwaachia nafasi kubwa kuongoza mambo yao ya Kiyahudi,walipewa mapendeleo mengi, hasa kwa upande wa dini).

Ndipo Kuhani Mkuu Kayafa akatoa maoni yake. Kwanza kwa adabu mbayaaliwaambia wenzake kwamba hawakujua lolote. Yeye aliona kwamba njia rahisini kuepa shida na kutunza hali zilizopo. Kwa hiyo, ni lazima Yesu afe ili taifalisalimike. Hakujali kama ni haki Yesu afe, ingawa hakufanya kosa la kustahiliauawe, hilo si neno, bora taifa zima lipone, huyo naye alikuwa akiwaza cheochake pamoja na vyeo vya wenzake. Mwandishi Yohana aliona ya kuwa iwapo

Page 99: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA588

Kayafa alisema neno la kibinafsi, alikuwa amesema kama nabii. Jambo hilolinapotafsiriwa kiroho na kwa upande wa Mungu, lina maana sana. Yesu atakufabadala ya Taifa la Israeli. Kiroho atakufa kwa ajili ya wenye dhambi wote,Wayahudi kwa WaMataifa, wote watakaomwamini baadaye. Yeye ni MchungajiMwema, aliye na kondoo wa zizi lingine ambao wataletwa ili liwe kundi moja naMchungaji mmoja. Kumbe, bila kutambua maana halisi ya yale aliyoyasemaKayafa alitoa unabii juu ya Kufa Kwake Yesu, unabii ambao hakuuelewa, hatahivyo, kwa upande mmoja ulikuwa unabii wa kweli. Ila taifa halikusalimika. Miaka40 baadaye, Warumi wakaja na kuuangamiza Yerusalemu na hekalu kwa kuwawalichoshwa na ukaidi wao, kama Yesu alivyotabiri (Mt.24:2).

k.53 Mwisho wa mazungumzo waliafikiana na maoni ya Kayafa na kukata shaurila kumwua Yesu. Tangu hapo walitafuta njia ya kumkamata, ila iliwabidiwajihadhari na umati wa watu ambao wangali wakimpenda. Shabaha yakumkamata Yesu haikuwa kufanya hukumu, maana walikuwa wameishaamuaauawe, ila ilikuwa kunyosha kesi ili liwali Pilato atoe hukumu hiyo waliyotaka.

MASWALI1. Katika kumfufua Lazaro Yesu alionyesha madaraka juu ya nini?2. Aliwasaidiaje Martha na Mariamu?3. Kwa jinsi alivyofanya alitaka watu wajifunze nini zaidi ya uwezo wake juu ya

mauti?4. Baada ya mwujiza huo wakuu walifanyaje?5. Wakuu walionyesha ujinga wao kwa njia gani?6. Kumfufua mfu wa siku nne kulikuwa ishara ya uwezo wa Yesu kufanya nini

kiroho?

UPEO WA MGOGORO 11:54 - 12:36Baada ya kumfufua Lazaro Yesu alifahamu kwamba mambo yameiva na yakwamba wakuu ambao hapo nyuma walikuwa wameishakata shauri lakumwondoa, waliendelea kuikamilisha mipango ya kumkamata. Kwa vyovyotehawataubadili uamuzi wao wa kumwondoa. Naye Yesu alijua hakika kwamba„Saa yake ya kuondoka ulimwenguni‟ inazidi kukaribia. Ni kwa ajili yake alikujaulimwenguni. Kwa hiyo alizidi kuwatayarisha wanafunzi kwa kuondolewakwake. Pia alijenga imani za wale waliomwamini kwa dhati ili wajitoe kabisakwake. Hakuwa tayari kuvumiliana na wale ambao bado hawajamwamini kwakweli, akawapo changamoto kwa kujitokeza wazi kuwa upande wake aukinyume chake. Baada ya kuingia Yerusalemu hadharani mwa watuhakuwashughulikia mikutano tena badala yake aliwahudumia wafuasi wakefaraghani.

11:54-57 Yesu alijitenga na kwenda EfraimuTwasoma kwamba Yesu alijitenga na kwenda mpaka mji wa Efraimu, nje yaYerusalemu, mashambani. Hapo alipata nafasi ya kutulia pamoja na

Page 100: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA589

wanafunzi wake na kuwaandaa kwa yote yatakayotokea pale Yerusalemu hivikaribuni. Yeye aliyajua hayo yote ila wao hawakuelewa ijapokuwa alikuwaamewaambia mara kwa mara ya kuwa atakamatwa na kuuawa. Bila shakakipindi hicho kilikuwa cha maana sana katika maisha yao. Wakati huo watuwengi walikuwa wakielekea Yerusalemu kwa Sikukuu ya Pasaka. Yesu alikuwaakitawala mawazo yao, wengine walikuwa wakimtazamia kwenye Sikukuu, hukubaadhi walidhani kwamba hatafika kwa sababu ya hatari iliyopo. Wakuu wamakuhani na Mafarisayo walitoa amri kwamba mtu akijua alipo awapashe habarikusudi wamkamate. Hivyo palikuwapo uvutano mkubwa na hali ya kusisimua,watu wakingoja jinsi mambo yatakayokuwa.

12:1-11 Yesu alirudi mpaka BethaniaYesu alirudi Bethania juma moja kabla ya Pasaka. Karamu kubwa iliandaliwakwa ajili ya kumshukuru Yesu kwa ufufuo wa Lazaro. Kama ilivyokuwa tabiayake Martha alishughulika sana na maandalizi. Mariamu alikuwapo pamoja naLazaro. Huenda Lazaro alikuwa ametulia nyumbani tangu alipofufuliwa asipendekutazamwa na watu. Yohana amesimulia habari hii kwa kuvuta mawazo yetukwa watu wawili hasa, ili tuzizingatie tabia zao zilizotofautiana sana. Mmoja niMariamu ambaye kwa tendo lake amekuwa kielelezo cha kujitoa, na wa pili niYuda Iskariote, ambaye alimwona kuwa kielelezo cha mtu wa kupenda fedha nakujipenda. Mariamu alionyesha upendo mwingi wa kujitoa katika kumpaka Yesumiguuni kwa marhamu ya ghali. Yuda alionyesha kujipenda kwake kwa manenoya kupiga kijembe. Mariamu alipoosha miguu ya Yesu alijinyenyekeza kamamtumwa. Ilikuwa desturi ya watumwa kufanya hivyo kwa mabwana zao. Hakujalijinsi watu walivyomwaza (makahaba walizoea kulegeza nywele zao). Kwa moyomkuu alimwonyesha Yesu upendo mwingi. Yuda Iskariote alijiinua kamamwamuzi akihukumu tendo jema la Mariamu.

k.3 Mariamu alikuwa na busara ya kushika nafasi hiyo maadamu ilikuwapo.Alisikia nafasini mwake kwamba muda wa Yesu kuwa pamoja nao ni mfupi, nanafasi hii haitamrudia. Hatujui ni kwa kiasi gani alielewa maana ya tendo lake, ilaYesu alilitafsiri kuwa tendo la kuutayarisha mwili wake kwa maziko. Ni tendoambalo Mariamu alikuwa ameliwaza siku nyingi, huenda kila wakati aliwekakando pesa za kununulia hiyo marhamu. Ni dhahiri kwamba hiyo marhamuilikuwa safi sana, ya ghali, tena alitumia nyingi kama ratli moja. Kwa ukarimumkubwa alimtolea Yesu bila mawazo yoyote ya kujistahilisha. Mara tatu katikaMaandiko tunaposoma habari za Mariamu, twamkuta miguuni pa Yesu (Lk.10:39akijifunza Kwake; Yn.11:32 akimtegemea; Yn.12:3 akimwabudu). Kwa hiyo, siajabu kwamba alikuwa na utambuzi juu ya wakati huo na hekima ya kuchukuanafasi hiyo, kwa sababu alikuwa amekaa miguuni pa Yesu na kujifunza Kwake,hivyo amekolea tabia ya kujitoa ya Bwana wake. Katika sura ifuatayo Yesualiwafundisha wanafunzi wake juu ya kuosha miguu ya wenzao alipowapakielelezo katika kuwatawadha miguu yao.

Page 101: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA590

„nyumba ikajaa harufu ya marhamu‟ Yesu alisema kwamba habari hiyo itatajwakila mahali Injili inapohubiriwa (Mk.14:9). Harufu ya tendo hilo imeenea sana nakugusa maisha ya waumini wengi na kuwavuta kujitoa kwa moyo kwa Yesu.Matokeo ya tendo hilo ni makubwa kupita tendo lenyewe.

k.4-6 Itikio la wanafunzi (Mt.26:8) pamoja na watu (Mk.14:4) na zaidi la Yudahalikuwa zuri. Waliwaza hasara ya fedha nyingi kutumiwa kwa marhamu hiyoambazo zingaliweza kutumiwa kwa kuwasaidia maskini. Kama tungalikuwepo,huenda na baadhi yetu tungaliwaza vivyo hivyo. Ila Yohana ameeleza kwambaYuda hakuwa mnyofu wa moyo alipotoa maoni yake. Yeye alishika mfuko wawanafunzi kama mtu aliyeaminika, kumbe alikuwa mwizi, kwa hiyo, alikuwaakiwaza faida yake mwenyewe, si ya maskini. Wanafunzi hawakuelewa tabiayake ya wizi, wala hawakujua kwamba atamsaliti Yesu. Jambo hilo la usalitilimetajwa juu ya Yuda kila anapotajwa katika Maandiko, kwa sababu, liliwashtuakabisa, hata kwa kumtaja tu, mara walikumbuka tendo hilo alilolifanya. Hivyotwaona mmoja (Mariamu) mtu wa nuru aliyezidi kuelekea kwenye nuru na mmoja(Yuda) mtu wa giza aliyezidi kuzama katika giza. Katika rafiki zake wote, Mariamuamekumbukwa kwa upendo na ukarimu na utiifu wake. Katika wanafunzi wakewote, Yuda amekumbukwa kwa usaliti wake. Yesu alitendewa mengi ya chuki ilaMariamu alimtendea tendo moja la upendo mwingi, bila shaka Yesu alifarijikasana na hilo tendo.

Kwa hiyo, katika habari hiyo, Yohana mwandishi ameendelea kutuonyeshamaendeleo katika kuamini na katika kutokuamini. Mariamu, mwanamke mpole,alijitokeza na kwa shauku alithubutu kuonyesha wazi upendo wake. Kufufuliwakwa ndugu yake Lazaro kuliamsha shukrani nyingi isiyofichika na imani ya ndaniilitokeza moyo wa ibada.

Ilikuwaje Yuda alidharau tendo hilo la Mariamu. Tangu mwanzo Yesu alikuwahakuonyesha tamaa yoyote ya kutaka kuwa mkubwa na kuwa Mfalme wa hapaduniani ingawa watu wengi walikuwa tayari kumfanya hivyo. Kwa miujiza yake nakwa mafundisho yake alikuwa amewavuta wengi kiasi cha wakuu kuwa na wivumkubwa juu yake, wivu wa kumwondoa. Yawezekana hii ndiyo sababuiliyomwongoza Yuda kumsaliti Yesu. Badala ya kuzungumza mambo ya Ufalmewa hapo duniani Yesu alitaja habari za Ufalme wa Mbinguni na Kuuawa Kwake.Kwa Yuda, ikiwa Yesu hatakuwa mfalme hapo duniani ni kazi bure kumfuata.Hatafaidi kitu huku amepoteza faida nyingi. Pengine aliogopa kwamba Yesuatakapouawa kama mhalifu yeye pia atashtakiwa kwa sababu alikuwa pamojanaye. Yuda ni kielelezo cha mtu ambaye hakumwamini Yesu kwa dhati, ndipoakateleza, kisha akamkana. Alikataa kujiunga na mpango wa Yesu. Yohanaaliyekuwa mwanafunzi pamoja naye, alimwona kama mtu asiyetulia, mwenyetamaa ya fedha, na mnafiki.

k.7 Ni vigumu kuelewa maana ya maneno hayo ya Yesu. Yesu alimteteaMariamu na kurekebisha mawazo ya Yuda aliyeificha choyo yake huku akidai

Page 102: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA591

kuwa na mzigo juu ya maskini. Yesu aliona Mariamu amewahi kumpaka mafutatayari kwa maziko yake, ambayo yatafanyika kwa haraka, kwa kuwahawakutazamia kwamba Yesu atauawa. Walikuwa hawajaandaa kwa habari hiyoila Mariamu alikuwa ameandaa, kama alifahamu hayo yote, au siyo, hatujui, ilatujuavyo ni kwamba ndivyo alivyomaanisha Yesu.

k.8 Yesu hakuwa na maana kwamba wafuasi wake wasiangalie mahitaji yamaskini. Walikuwa na mfuko ambao ulitumika kununua mahitaji yao pamoja nakuwapa wahitaji vipawa (13:29). Tukumbuke ya kuwa Yesu hakuwa na mali walahakuacha kitu chochote alipokufa ila mavazi aliyovaa, hata hivyo, aliwafundishawanafunzi wake kuwahurumia maskini. Kwa jinsi alivyosema ameonekana kamamwenye kujiona na kuwaza makuu juu ya nafsi yake, lakini siyo, ila budi Yeyeawe wa kwanza katika maisha ya wafuasi wake na bila shaka, kwa kumfuatabarabara, watakumbuka maskini.

k.9-11 Wayahudi wengi walikuja Bethania, si kama waalikwa kwa karamu, walasi kwa kumwona Yesu tu, bali hasa walitaka kumwona Lazaro. Baadhi yao wengi,walipomwona Lazaro yu hai, wakajitenga na wenzao, wakamwamini Yesu. Ila,ajabu ni kwamba, wakuu wa makuhani walikata shauri la kumwua Lazaro!!Jambo la Lazaro kuwa hai lilitoa ushuhuda mkali juu ya uwezo wa Yesu. Mwujizawa kumfufua haukufichika, na ulifuata mwujiza mkubwa wa mtu aliyezaliwakipofu kupewa uwezo wa kuona. Mambo hayo yataishia wapi? Atafanya nini zaidiwakimwacha kuendelea? Zaidi ya yote, Je! watabaki wangapi wasiomfuata? Niajabu kufikiri kwamba walitaka kumwua mtu ambaye majuzi tu amefufuliwakutoka wafu baada ya kuwa maiti siku nne? Wivu na chuki ni hatari sana,zinapofusha akili na mioyo ya watu kiasi cha kuwafanya wakose utambuzi wakweli na haki.

Kwa hiyo, wakati ulipokaribia wa Kuuawa Kwake Yesu alizidi kupata wafuasiwengi, huku wapinzani wake, ijapokuwa idadi yao ilipungua, walizidi kumkataa.Hivyo kuamini kwa wengine kulizidi na kutokuamini kwa wengine kulizidi, na hayoyote kwa sababu Yesu hakuogopa kuwakabili na kuwapa changamoto kwamaneno na matendo yake. Walisukumwa wakate shauri juu yake, amakumpokea, ama kumkataa.

12:12-19 Yesu aliingia Yerusalemu kwa shangweHabari hii imo katika Injili zote nne. Yohana hakutoa habari juu ya wanafunzikutumwa na kuleta punda n.k. Hakutaja jinsi Yesu Mwenyewe alivyojisikiaalipopewa sifa za watu. Hasa Yohana alisisitiza maitikio ya vikundi mbalimbalivya watu waliokuwapo pamoja na Yesu pale Bethania pamoja na wale waliotokaYerusalemu ili wamlaki. Tumeona imekuwa desturi ya Yohana kuonyeshamaitikio ya watu kwa maneno na matendo ya Yesu na kudhihirisha kuamini aukutokuamini kwao. Hapo alitaka kuonyesha maitikio ya watu kwa madai ya Yesukutawazwa kama Mfalme wa Israeli.

Page 103: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA592

Yohana ametaja mikutano miwili. Mmoja ni wa wageni waliokuwa wamekujaYerusalemu kwa Sikukuu, baadhi yao wengi walitoka sehemu za Galilaya.Walipashwa habari za Lazaro kufufuliwa na watu wa Bethania. Waliposikiakwamba Yesu anakuja mjini wakatoka nje kwenda kumlaki. Mkutano wa piliwalikuwa wenyeji wa Bethania (k.17).

Yesu aliondoka Bethania kama Mfalme aliyekwenda kutawazwa. Walewaliomlaki na kumshangilia njiani walikuwa na kusudi maalumu la kumpokeakama Masihi. Walikata mitende na kumfanyia kama Mfalme. Walitumia manenoya Zaburi 118:25, 26, ambayo ilikuwa baadhi ya Zaburi zilizotumika wakati waPasaka. „Binti Sayuni‟ ni watu wa Yerusalemu. Neno „Hosana‟ maana yake ni„okoa sasa‟. Maneno „Mfalme wa Israeli‟ hayapo katika Zaburi hiyo. Kwa hiyo,kwa maneno na matendo, ni dhahiri kwamba walimwaza Yesu kuwa Masihi,Mfalme wa Israeli, aliyekuja Yerusalemu kwa kusudi la kutawazwa. Kwa upandewa siasa wakati wa Pasaka ulikuwa wakati motomoto. Watu walipokumbuka jinsimababa zao walivyotolewa utumwani mwa Misri chini ya Musa, walikuwa nahamu sana ya kumpata „Musa mwingine‟ Masihi atakayewaokoa kutoka kwautawala wa Warumi.

Ni kama jaribio lao la kumfanya awe Mfalme, hapo nyuma walikuwa wamejaribukumshika (6:15). Kwa kupanda punda Yesu alikataza mambo ya kivita. Yeye nimfalme wa amani, mpole, wa kupokea, si Waisraeli tu, hata WaMtaifa pia kamanabii Zekaria alivyotabiri (Zek.9:9-11). Kwa hiyo, Yeye si yule wa kuwafukuzaWarumi kwa nguvu, wala Yeye si Yule wa kuusisitiza uteule wa Wayahudi; Yeyeni zaidi ya Mfalme wa Israeli, Yeye ni Mfalme wa Wafalme, Mkombozi waulimwengu. Zamani za kale Wafalme na Waamuzi walitumia punda walipoletaujumbe wa amani. Farasi alitumika hasa wakati wa vita. Yesu, kwa kusudi,alimpanda punda, dalili ya kuwa Mfalme wa Amani.

k.16 Yohana alieleza kwamba hata wanafunzi wake hawakuelewa hali yaUmasihi wake na maana yake, na ya kwamba ataingia Ufalme wake kwa njia yaKifo cha Msalaba. Wanafunzi walichanganyikiwa, walishindwa kupatanishamambo hayo mawili, utayari wa Yesu kutawazwa kuwa Mfalme na hali yake yakukataa kujichukulia mamlaka ya dunia ambayo walidhani kwamba mfalmealipaswa kuwa nayo. Hawakumwelewa vizuri mpaka baada ya Kufufuka Kwake(12:6 ling. na 2:22). Hivyo, Yesu aliingia Yerusalemu kama Mfalme aliye na kazimaalumu ya kuokoa.

k.19 Mafarisayo walipoona umati wa watu wakimpokea Yesu kama Mfalmewalikata tamaa, waliona kwamba jitahada zao zote zimekuwa bure. Imebakidawa moja, dawa ya kumwua. „ulimwengu umekwenda nyuma yake‟ ni manenoyatakayokuwa kweli, yatapata uwezekano wa kutimizwa Yesu atakapokufa kwadhambi za walimwengu wote. Ndipo mara twasikia habari za Wayunani kujawakitaka kumwona.

Page 104: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA593

12:20-36 Wayunani walitaka kumwona YesuHapo twapewa kwa mara ya kwanza habari ya kundi lingine la watuwaliokwenda Yerusalemu kwa shabaha ya kumwabudu Mungu katika Sikukuuhiyo ya Pasaka. Walikuwa WaMataifa, pengine walitoka Dekapoli au sehemu zakaskazini mashariki ya Palestina (si lazima tufikiri kwamba walitoka mbali kwanchi ya Uyunani). Hapo wengi walitumia lugha ya Kiyunani. Huenda walikuwawaongofu walioigeukia dini ya Kiyahudi wakivutwa na usafi wake na kuionakuwa bora kuliko dini zao za miungu mingi zilizokubali uchafu mwingi, zisizojalimaadili n.k. Wayahudi waliamini kuwa yuko Mungu mmoja tu, Mwumba wa kilakitu, Mtakatifu, Mungu mwenye mzigo wa maadili, aliyetoa mwongozo wa Toratikwa watu kuishi kwayo. Katika Matendo ya Mitume tumepewa habari zawaongofu waliogeuka kuwa Wakristo.

Hao Wayunani hawakumjia Yesu moja kwa moja ila walimwomba Filipo, mmojawa wanafunzi wa Yesu, awalete Kwake. Filipo alimwomba Andrea, mwanafunzimwenzake, awe pamoja naye, ndipo wote wawili wakawapeleka kwa Yesu.Hatujui kwa nini walimwomba Filipo. jina lake ni la Kiyunani, pia alitoka Bethsaidaambapo Wayunani wengi waliishi na lugha ya Kiyunani ilitumika katika sehemuzile. Haidhuru sababu ilikuwa nini tujualo ni kwamba walijihusisha na Filipoaliyewapokea vema. Kwa nini hawakumwendea Yesu moja kwa moja? hatujui,huenda hawakuona vema kumwendea mwalimu mashuhuri bila kuwa na mtu wakati.

k.23 Yesu aliwajibu kwa maneno ya ajabu. Kwa kufika kwao aliona amefikiaupeo wa Utume wake. Alisema „Saa imefika atukuzwe Mwana wa Adamu‟.Aliyasema maneno hayo kwa nani? kwa Wayunani? au kwa Filipo na Andrea?au vipi? Maana hatusikii lolote kuhusu hao Wayunani tena. Hatujui kamaaliwaona au siyo. Ombi lao lilimwongoza Yesu aseme mambo ya Nafsi Yake naUtume wake. Ila tusifikiri hao Wayunani hawakuhusika na mazungumo hayo yaYesu, ni kama wao wamekuwa sababu yake. Yesu alijua hakika kwambaWaMataifa hawataweza kuzishiriki baraka za Mungu mpaka Yeye atengenezeAgano Jipya lenye msingi tofauti na Agano alilolifanya Mungu zamani za kale.Katika Agano Jipya tofauti zote za wanadamu zinaondolewa. Kwa Kufa KwakeYesu atawaleta pamoja Wayahudi na Wayunani na kuwafanya kuwa sawa. Ndipoubaguzi wote utakwisha, wa kikabila, wa jinsia, wa tabaka, wa rangi n.k. Yesualitamka makuu kuhusu wakati huo na kazi ya upatanisho atakaofanya katikaKufa Kwake Msalabani. Kweli „saa yake imefika‟ saa iliyotajwa hapo nyuma kuwahaijafika bado (2:4; 7:6,30). Tena ni saa ya „kutukuzwa Kwake‟. Ni saa ya kufaMsalabani, saa ya kutoa nafsi yake kuwa fidia ya dhambi, saa ya kupambana naShetani na kumshinda, saa ya kumtii Baba kwa ukamilifu. Saa ya kuwaokoawanadamu wa kila aina, saa ya kubomoa kiambaza kati yao (Efe.2:13). Hafi kwabahati nasibu, wala kwa nia mbaya za adui zake tu, bali kwa kutimiza Mapenziya Baba yake.

Page 105: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA594

k.24 Alitumia maneno aliyoyazoea kuyatumia alipotaka kutilia mkazo tangazokubwa. Tangazo hilo lilihusu Yeye Mwenyewe, Yeye ndiye chembe ya ngano,kwa Kufa Kwake, uhai mpya utatokea. Msingi huo wa kufa ili uhai mpya utokeeumekuwa msingi wa upandaji katika dunia nzima tangu mwanzo wa uumbaji.Yeye atakapokufa ndipo mavuno yatapatikana, WaMataifa na Wayahudiwatakuja kumwamini na kuokolewa. Hasa neno hilo lilikuwa kubwa katikamwanga wa Wayahudi wengi kumkataa. Wakizidi kumkataa Mungu atawageukiaWaMataifa nao watampokea. Kihistoria imetokea hivyo.

k.25-26 Msingi huo haukumhusu Yesu tu, pia uliwahusu watumishi wake wote,tangu wale Mitume wa kwanza. Kila mtu amtumikiye Kristo apaswa ajikane nafsiyake ili amwishie Mungu, aseme „la‟ kwa mapenzi yake, na „ndiyo‟ kwa mapenziya Mungu. Mafanikio ya kazi ya wale watakaoachiwa huduma baada yakeyatategemea kujitoa kwao kama Bwana wao alivyojitoa. Wamewajibika kumfuataKristo na thawabu yao ni kushirikiana naye kwa ukaribu.

k.27 Katika Injili yake Yohana hakuandika habari za Gethsemane, ila katikahabari ya sehemu hiyo, ametuonyesha jinsi Yesu alivyojisikia alipokabili KufaKwake. Alipotaja habari ya chembe kuanguka nchini na kufa alisikia shida sanarohoni mwake, alifadhaika alipowaza zile dhiki zilizo mbele zake, dhiki za kimwili,kuuawa kwa ukatili sana, na dhiki za kiroho katika kuzibeba dhambi zaulimwengu wote na kuhukumiwa na kulaaniwa kwa ajili yake. Mbele yake zikonjia mbili. Ama amwombe Baba amwepushe na dhiki hizo, asiende Msalabani;ama akubali kufa kwa ajili ya dhambi. Katika ubinadamu wake Yesu hakupendakupata maumivu, kuchukiwa, kusutwa, na kufa. Hapo amefanana na wanadamuwote.

Hata hivyo, hakuruhusu ubinadamu wake utawale nia yake na kumwondoa katikashabaha ya Kuja Kwake. Alisimama imara sana juu ya Kusudi la Kuja Kwake,alimpenda Baba upeo, alimtii kabisa. Hapo nyuma aliwafundisha wanafunzikuomba „Mapenzi yako yatendeke‟ (Mt.6:9). Alitaka kumtukuza Baba zaidi yayote (k.28a). Hali yake ya utii ni hukumu juu ya uasi wa ulimwengu, kwa sababupale Msalabani utii wa Kristo ulidhihirika wazi kabisa ukawa kinyume cha uasiwote wa wanadamu. Shetani alishindwa. Kujitoa kwa Kristo kulishinda kabisakujipenda kwa wanadamu. Mwana wa Mungu awavuta watu wote Kwake kwa njiaya kujidhili kwake katika kushuka mpaka Kifo cha aibu kubwa na maumivu makaliya Msalaba. Yesu atatukuzwa Msalabani, si baada ya Kufa tu, na kwa njia hiyoBaba naye atatukuzwa. Pale Msalabani tabia zake zote njema zitadhihirika,upendo, utakatifu, haki, na rehemu.

k.29-30 Mkutano uliisikia sauti ya Baba ila hawakuelewa vema manenoyaliyosemwa; baadhi walifikiri ni sauti ya ngurumo na baadhi walifikiri malaikaamesema na Yesu. Yesu Mwenyewe alisema kwamba sauti hii ilikuja kwa ajiliyao, si kwa ajili yake. Kwa sauti hiyo waliweza kuelewa kwamba Baba na Mwanani umoja, wana uhusiano wa ukaribu kabisa, na Yesu aenda Msalabani

Page 106: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA595

kwa mapenzi na kibali cha Babake. Bila shaka wengi walitambua kwambamambo yanafikia kilele chake.

k.31 Yesu akaendelea kukisemea Kifo chake. Alisema ni wakati wa hukumu yaulimwengu huu, na wakati wa mkuu wake (Shetani) kutupwa nje, na ni wakati waYeye kuvuta watu wote Kwake. (wote si katika maana ya kila mtu, bali kila ainaya watu). Imekuwaje Shetani aitwe „mkuu wa ulimwengu huu‟ ni kwa sababualitawazwa na wanadamu walipomtii yeye na kumwasi Mungu. Wanadamuwaliamua kumpa yeye utiifu wao. Ila katika Yesu jambo jipya limetokea, kati yawanadamu wote Yesu amempa Mungu Baba yake utiifu wake wote, amemtiikatika maisha yake yote naye atafikia upeo wa utii atakapokufa kwa ajili yaKuukomboa ulimwengu. Pale Msalabani Yesu alilipindua Anguko na laana yakena yote yaliyotokana na uasi wa wanadamu.

k.32-33 „nami nikiinuliwa juu‟ Pale Msalabani Yesu atainuliwa juu, yaaniatasulibiwa. Kwa mawazo ya kibinadamu kusulibiwa ni kushushwa nakuaibishwa kabisa ila katika mawazo ya Mungu na ya Yesu ni kuadhimishwa nakutukuzwa.

k.34 Mkutano wakamjibu tena kwa kusema kwamba kutokana na ufahamu waowa Maandiko hayo aliyoyasema Yesu hayakumhusu Masihi. Akiuawa Yesuhawezi kuwa Masihi kwa sababu Torati ilisema kwamba amelaaniwa na Mungukila atundikwaye mtini. Pia Nabii Danieli alisema kwamba Mwana wa Adamuatakuja juu ya mawingu (Dan.7:13). Kutokana na maneno hayo ya MaandikoYesu awezaje kuwa Masihi? Ni mara ya mwisho Yohana kutaja mikutano wawatu. Mpaka mwisho watu walishindwa kumtambua Yesu vizuri.k.35-36 Yesu hakuendelea kuhojiana nao ila alisisitiza madai yake ya kuwaNuru na kuwaita waiamini hiyo Nuru, hivyo, kwa mara ya mwisho aliwasihiwamwamini. „Enendeni maadamu mnayo nuru, giza lisije likawameza.... iaminininuru hiyo‟. Sababu ni kwamba Yeye yu pamoja nao kwa muda mfupi tu (hapoamedokezea Kifo chake). Hapo Yohana amerudia jambo la „nuru‟ ambalo tangumwanzo wa Injili ni uzi mmojawapo alioutumia katika ufumaji wa Injili yake.Pamoja na kuwaita, Yesu aliwaonya juu ya matokeo ya kutokumwamini, matokeomazito ya kumezwa na giza kiasi cha kutokujua waendapo. Yeye alikujaulimwenguni ili amtie nuru kila mtu. Hawana budi wajiunge naye wasijewakajikwaa katika giza.

k.36b Yesu alifunga huduma yake kati ya watu na wito na onyo kali. Akaendaakajificha (8:59) akazidi kuwaandaa wanafunzi wake kwa kuondolewa kwake.Tangu hapo alizidi kukanyaga zile hatua za kumfikisha Msalabani. Katikakusema „lakini kwa ajili yake nilivyoifikia saa hii. Baba ulitukuze jina lako‟ alikuwaamekata shauri kabisa la kusogea mbele na kukaribisha magumu yote yaliyombele yake. Kuwaacha watu kuliashiria uhalisi wa onyo lake la kuachwa gizani.

Page 107: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA596

MASWALI1. Yesu alimpambanua Mariamu na tendo lake na Yuda na tendo lake.

Eleza tofauti zilizoonekana katika hao wawili2. Yesu alisemaje juu ya tendo la Mariamu?3. Eleza habari za Yesu kuingia Yerusalemu kwa kuonyesha shabaha yake

na mawazo na shabaha ya watu juu yake4. Yesu alikuwa na maana gani aliposema juu ya chembe ya ngano

kuanguka nchini? Alikuwa akisemea nini hasa?5. Ni nini iliyosababisha aseme habari hiyo na alikuwa akitazamia nini mbele

baada ya kufa kwake?6. „Nami nikiinuliwa juu nitawavuta wote kwangu‟ Kuinuliwa juu ni nini hasa?

12:37-17:26 MUDA WA MAONGEZI

12:37-43 Majumlisho ya huduma ya Yesu kati ya watuMabadiliko yalitokea katika huduma ya Yesu. Hapo nyuma alikuwaamewahudumia mikutano ya watu hadharani. Tango hapo alitumia nafasiiliyobakia kwa shabaha ya kuzungumza sirini na wafuasi wake nakuwatayarisha kwa kuondoka kwake. Kwa hiyo, kabla ya kuendelea na habarihizo za maandalio ya wanafunzi Yohana aliona vema ajumlishe mamboyaliyotangulia, akitaja jambo la kuamini na kutokuamini (k.37, 42).

k.37 Katika majumlisho hayo ilimbidi aseme juu ya kutokuamini kwa watu wengi.Kwa sababu gani hasa watu hawakumwamini Yesu ijapokuwa amefanya isharanyingi kubwa mbele yao? Kutokuamini kwao kulikuwa kinyume kabisa chaushuhuda mkali wa miujiza iliyolenga kuwasaidia watu wamwamini (k.37).Ilikuwa jambo la kustaajabia kwamba watu hawakumwamini Yesu ijapokuwaalifanya makuu mengi. Kutokuamini kwao ni kama jambo lisilosadikika. HalafuYohana alitumia Maandiko kwa kuonyesha kwamba kutokuamini kwaokulitabiriwa katika Agano la Kale (Isa.53:1) na kulipatana na mwenendo wao natabia yao ya tangu zamani. Waliteuliwa kumpokea Masihi, lakini walifanyakinyume cha shabaha ya uteule wao.

k.38ku „ili litimie lile neno la nabii Isaya‟ „ili litimie‟ ni maneno ya kuonyeshakwamba kutokuamini kwao kulisababishwa na unabii wa Isaya. Ni zaidi yakusema ni jambo lililoonekana kabla yake na kutabiriwa. Jambo la kutokuaminikwao kulitokana na Mungu kujifunua kwao (Isa.6:10). Nabii Isaya alitumwakuwahubiri watu wa Yuda wakati wa ufalme wao kurudi nyuma. Mungualipomwita Isaya alimwambia kwamba kwa kuzidi kuwahubiri watu watubu watuwatazidi kukataa. Ujumbe wenye lengo la kuwaleta kwenye toba utawafanyawazidi kuachana na Mungu. Kama ilivyokuwa wakati wa Isaya, hata wakati waYesu, watu wengi hawakuitika wito wa Mungu. Tabia ya moyo mgumu iliyokuwaikifanya kazi wakati wa Isaya imefanya kazi hata wakati wa Yesu. Hata hivyo,Mungu anayo madaraka juu ya hayo yote na makusudi yake hayataanguka chini.Madaraka ya Mungu husimama potelea mbali itikio la watu ni nini. Hata

Page 108: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA597

hivyo Yohana alitaja maitikio ya watu (k.37, 42). Katika madaraka yake Munguhutoa hukumu ya adhabu juu ya watu walio na hatia, atia muhuri kwenyeuchaguzi wao. Walikataa nuru, wakachagua giza, kwa hiyo, adhabu yao itakuwawakae katika giza. Ila, kwa sababu Mungu anayo madaraka, kuna matumaini,kwa sababu watu waweza kuomba rehema zake na msaada wake. Yohanaalitamka neno la ajabu aliposema kwamba Isaya aliuona utukufu wa Kristo nakutoa habari zake. Tukilinganisha na Isaya 6 twajua kwamba Isaya aliuonautukufu wa mkuu mmoja aliyekaa kati ya Maserafi na kuabudiwa. Kumbe huyoaliyeitwa na Isaya, Yehova, ni Yesu.

k.42-43 Yohana alisema kwamba hata katika wakuu, wengi walimwamini Yesuila kwa siri. Aliwalaumu sana kwa sababu walipenda sifa za wanadamu kuliko sifaya Mungu. Alijuaje wengi walimwamini kama walimwamini kwa siri? YafikiriwaNikodemo na Yusufu wa Arimathaya walikuwa wawili wao. Yawezekana haowalimpasha Yohana habari hizo, au pengine, alijulikana na wengi wao na kujuamawazo yao. Iliyotakiwa wakati huo wa mambo kuiva ni watu wawe na ujasiri wakuuonyesha msimamo wao, wasiwe waoga. Mafarisayo, kama kawaida yao,hawakuwa tayari kumpokea Yesu (7:48).

12:44-50 Muhtasari wa mafundisho ya YesuKama kwa mara ya mwisho Yesu aliwaita watu. Katika 12:37 tulisoma kwambaYesu aliwaacha watu, akaenda, akajificha. Kwa hiyo kabla ya kuwaacha, alitoawito huo kwao. Aliwaelezea uzuri wa kumwamini na hatari ya kutokumwamini.Kumwamini Yeye ni sawa na kumwamini Mungu, Baba yake aliyempeleka, kwahiyo, ahadi zake ni ahadi za Mungu. Kumwamini Yeye ni kutiwa nuru yamaisha, mwanga wa kumwishia Mungu kwa kushirikiana naye kibinafsi, nakuishi maisha ya maana na shabaha njema (k.46).

Kutokuamini ni zaidi ya kutokuwa tayari kumpokea Kristo, ni kukataa kwa kusudikumjali na kuusukumia mbali ukweli wake kwa njia ya kuyakataa madai yake(k.48). Hukumu itafuata kutokumwamini kwao. Neno lake, ambalo ni ile kwelialiyoitangaza, litawahukumu watu siku ya mwisho. Maana yake itadhihirika wazikwamba Yesu alikuwa Yule aliyejidai kuwa, Mwana wa Baba aliyetumwa naBaba, na kusema na kufanya yote aliyoamriwa na Baba. Hivyo, ujumbe waMungu uliofungamana katika Kristo ni tumaini la waumini na hukumu kwawasiomwamini (k.48, 50) kwa sababu Kristo alikuja ili kila muumini awe na uzimawa milele. Kwa hiyo, kama alivyofanya sikuzote, Yesu alisisitiza umoja wake naBaba. Anaposema Yeye na yale anayosema, ni Mungu anayesema, yeye simjumbe tu anayesema kwa niaba ya Baba, Yeye ni zaidi, Yeye ni Mungu Mwanaaliyefanyika mwili. Kwa hiyo, kusema kwake na kufanya kwake ni sawa na MunguBaba kusema na kufanya. Kwa muhtasari huo mfupi Yohana alijumlisha kiini chamafundisho ya Yesu.

Page 109: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA598

13:1-16:33 MAONGEZI NA WANAFUNZI13:1-20 Chakula cha MwishoTukilinganisha na Injili tatu (Mt.26:17ku. Mk.14:12ku. Lk.22: 7ku) Yohanaameandika mambo hayo kwa tofauti. Hasemi juu ya maandalio na mamboyaliyotokea wakati wa kula, wala hatoi habari za maelezo ya Yesu kuhusu AganoJipya na maana ya mkate na divai, wala hataji mabishano ya wanafunzi kuhusuni nani atakayekuwa mkubwa. Waandishi wa Injili zingine hawataji habari yakutawadha miguu na wametoa habari fupi juu ya maongezi ya Yesu kuhusukielelezo cha utumishi. Wote wametaja kwamba Yesu aliwapasha habari yamsaliti na kuondoka kwake.

k.1 Hapo Yohana ametaja kwamba Pasaka ilikuwa karibu na „saa yake‟ imefika,ile saa iliyotajwa mara kwa mara kuwa haijafika bado, sasa imefika. Ni saa ganihiyo? Ni saa ya Yesu kutoka katika ulimwengu huu na kurudi kwa Baba. Pia nisaa ya kuwapenda watu wake upeo. „watu wake‟ ni wale ambao amewavutaKwake ili wawe kundi jipya katika ulimwengu, ambao watakuwa „mwili wake‟Kanisa. „Kuwapenda upeo‟ maneno hayo yaweza kuwa na maana mbili: (a)aliwapenda mpaka mwisho kabisa wa maisha yake; (b) aliwapenda kabisa hataasingaliweza kuwapenda zaidi.

k.2 Yohana ametuambia kwamba haya yafuatayo yalitokea wakati wa chakulacha jioni, huenda chakula kilikuwa kimeandaliwa tayari, na Yesu na wanafunziwameanza kuketi mezani. Ila kabla ya kuendelea na mambo mengine aliingizahabari za mwanafunzi mmoja Yuda Iskariote. Alisemaje juu yake? Alisemakwamba Yuda amemruhusu Shetani amshawishi kumsaliti Yesu. Kwa hiyo Yudaalishiriki katika kula, pia Yesu aliosha miguu yake, huku moyo wake umeingiliwana Shetani, naye amekubali shauri lake.

k.3 Katika vifungu hivi vya kwanza Yohana amefanya maandalio ya uangalifusana. Alitaka tujue mambo kadhaa kumhusu Yesu Mwenyewe kabla ya kutoahabari ya tendo lake la kuwatawadha miguu wanafunzi. Jambo moja kubwa nikujua kwamba Yesu alifahamu barabara kwamba Baba amempa vyote mikononimwake, Jambo lingine alilojua kwa hakika lilikuwa kwamba alitoka kwa Mungu naanarudi kwa Mungu. Hivyo, alikuwa na ufahamu kamili wa uwezo wake mkuu nawa asili yake na uhusiano wake wa kipekee na Baba, na ni katika nuru yaufahamu huo alifanya tendo la ajabu sana, la unyenyekevu kabisa, la kutawadhamiguu wanafunzi wake. Pia, katika ufahamu huohuo alijinyenyekeza kabisaalipokwenda kusulibiwa. Kwa hiyo, kwa cheo chake na kwa uwezo wake,angaliweza kumzuia Yuda mara moja, asitende alivyokusudia, ila badala yakealijaribu kumvuta kwa kumwosha miguu sawa na wanafunzi wengine!! Yesualijua asili yake na mwenendo wake na mwisho wake.

k.4-5 Ndipo Yesu alifanya kinyume cha utamaduni wao na desturi zao,alipindua mtindo wa mawazo yao juu ya mambo yafaayo. Walipofika kwenye

Page 110: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA599

chakula, hakuna aliyekuwepo kufanya kazi ya kutawadha miguu. Kazi hiiilihesabiwa kuwa duni kabisa, ya kufanywa na mtumwa tu, hata Wayahudihawakupenda watumwa wao waifanye, waliona ifanywe na wanawake auwatumwa wa KiMataifa. Pengine kwa sababu walikutana kwa siri katika nyumbafulani mtumwa hakuwepo au walisahau kumpanga mtu. Wanafunzi walikuwawameshikwa na mawazo ya cheo wakidhani kwamba Yesu atausimamishaufalme wake pale Yerusalemu, basi hakuna aliyejitoa kufanya kazi hiyo.Waligombania cheo, hawakugombania kitambaa!!

Ndipo Yesu aliondoka chakulani, akaweka kando mavazi yake, akatwaakitambaa, akajifunga kiunoni, akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadhawanafunzi miguu, na kuifuta kwa kitambaa...‟ Ni msaada tukilinganisha habarihiyo na Wafilipi 2:5-8. Upendo wa upeo ni upendo kiutendaji, si upendo wahewani, wa mawazo tu. Tena unyenyekevu wa Yesu ni unyenyekevu kiutendaji,tazama maneno mengi ni ya kitenzi. Upendo na unyenyekevu wake utafikia upeokabisa pale Msalabani, atakapojidhili afe kifo cha mhalifu wa hali ya juu, chawenye dhambi, kifo cha aibu nyingi na maumivu mengi, akiachwa na wanadamu,na kwa muda mfupi, pia na Mungu Baba yake. Aliuonyesha Uungu wake haliamevikwa ubinadamu wetu, wakati wa udhaifu mwingi na utumishi mkubwa.(Tukumbuke Yesu alifanya hayo majira ya Pasaka, wakati Waisraeliwalipokumbuka jinsi walivyotolewa utumwani mwa Misri zamani za kale. Wakatihuo na katika Pasaka hiyo Yesu ataufanya Ukombozi mkubwa zaidi, wa kiroho,wa kuwaokoa watu na dhambi, Wayahudi na WaMataifa).

Alifanya kwa upendo usioweza kuzimwa na maovu. Alijua Yuda Iskarioteatamsaliti (k.11) alijua Petro atamkana (k.28) hata hivyo aliendelea kuwapendana kutoa maisha yake kwa ajili yao.

k.6-9 Hivyo Yesu akaja kwa Simoni Petro ili amtawadhe miguu, na kwa waziPetro akakataa. Bila shaka alisikia aibu, pamoja na wanafunzi wenzake, alionahaiwezekani Yesu, mkuu wao, afanye kazi hiyo. Iliwapasa wao wamtawadheYeye miguu na bila shaka wangalikubali bila shida ila inaonekana hawakuwatayari kutawadhana wao kwa wao, wala hawakukubali Yesu afanye. Yesuakamjibu Petro kwa kusema kwamba hawawezi kuelewa anavyofanya sasa ilabaadaye wataelewa (baada ya Kufa na Kufufuka Kwake, si baada ya Chakula).Ikiwa wameshindwa kuelewa „ishara‟ hiyo waliwezaje kuelewa „Msalaba‟ulioashiriwa katika tendo la kutawadha miguu? Walishtuka sana na tendo la Yesukuwatawadha miguu, lakini jambo hilo halikuwa hata nusu ya mshtuko wakuwaza Masihi atakayesulibiwa kama mbaya wa mwisho.Ndipo Petro alisisitiza kwamba haiwezekani Yesu amwoshe miguu, lakini Yesualimfunulia kwamba asipokubali kuoshwa hana ushirika naye. Kwa maneno hayoPetro akakubali, maana jambo alilotamani sana lilikuwa awe anashirikana naYesu. Kisha akamwomba Yesu amwoshe mikono na kichwa pia.k.10 Yesu alisema kwamba ilitosha awe ameoshwa mara moja sawa na jinsimtu anavyooga, ndipo inayotakiwa ni kuondolewa mavumbi ya njiani,

Page 111: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA600

kusamehewa makosa ya kila wakati. Kwa hiyo, tunapomjia Yesu kwa mara yakwanza, na kumpokea kama Mwokozi wetu, Yeye hutuosha, yaani anasamehedhambi zetu zote, twatakaswa na yote yaliyopita, ndipo katika maisha ya kilasiku, ijapokuwa tumekataa mabaya, tutakosa mara kwa mara, kwa hiyo,inatupasa kwenda kwake na kupata msamaha, hatuna haja ya kuanza upyakabisa, damu yake huendelea kutusafisha (1 Yoh.1:7). Haiwezekani tuishi bilakukosa, ila katika Kristo tumejaliwa nguvu ya kushinda dhambi, isitutawale.

Kwa hiyo, upendo wa Yesu ni upendo unaoosha na kutakasa. Twaona kwambatendo hilo la kutawadha miguu liliashiria tendo kuu la kuosha dhambilitakalofanyika pale Msalabani, masaa machache yanayokuja. Neno hilolimeonekana katika majibu ya Yesu kwa Petro alipokataa Yesu asimtawadhemiguu. Mtu asipokubali kuoshwa dhambi zake kwa damu ya Yesu iliyomwagikaMsalabani hana ushirika naye. Mtu hujihusisha na Yesu pale Msalabani (Tit.3:4-7).

„nanyi mmekuwa safi, lakini si nyote‟ (k.9b). Yuda Iskariote hakuwa safi moyonimwake. Alioshwa miguu, ila hakuoshwa moyoni kwa sababu hakuwa tayarikumpokea Yesu kama Mwokozi wa roho yake. Alitafuta mwokozi wa kimwili, wasiasa, wa kuwafukuza Warumi nchini. Alidhani Yesu ndiye huyo, kumbe, siyo.

Kwa upande mmoja Yesu alifanya tendo hilo katika mazingara mazito: wanafunziwalikuwa wakigombania cheo, Yuda alikuwa njiani kumsaliti, wakuu walikuwawakiikamilisha mipango ya kumkamata (wakisaidiwa sana na Yuda kujiunganao). Kwa upande wa pili Yesu alifanya tendo hilo katika ufahamu kamili wa asiliyake ya kuwa ametoka kwa Mungu na anarudi kwa Mungu, na kibinafsi alijua kwahakika kwamba Yeye ni Mwana pekee wa Baba na alielewa barabara Utumewake maalum ni kuukomboa ulimwengu. Alijua kwa hakika kwamba Babaamempa vitu vyote. Hivyo pande zote mbili ziliwiana na kumpeleka YesuMsalabani. Ni vema kukumbuka pande zote mbili tunapoendelea kutafakari hayoyajayo katika Injili hiyo.

k.12ku „akatwaa mavazi na kuketi tena‟ Tukilinganisha na Flp. 2:9-11 „kwa hiyoMungu alimwadhimisha mno na kumpa jina lipitalo kila jina...‟ na Ebr.1:3„alipokwisha kufanya utakaso wa dhambi aliketi mkono wa kuume wa Ukuu hukojuu‟. Yaliyotokea wakati wa kula yalikuwa malimbuko ya yale yatakayompataatakapokwisha kutoa fidia ya dhambi Msalabani, ataadhamishwa mno; kutwaamavazi ni sawa na kuutwaa tena Utukufu wake huko juu; na kuketi ni sawa nakuketishwa huko juu. Ndipo Yesu akazungumza nao ili waelewe maana ya tendolake. Yeye alikuwa Bwana na Mwalimu aliyepita marabi wote (Lk.6:46) hatahivyo, alikuwa amejidhili na kuwatumikia kama mtumwa, akithubutukuwatawadha miguu, kazi ambayo wao wenyewe hawakuwa tayari kufanya.Ilikuwa njia yake ya kuwafundisha aina ya „ukubwa‟ katika ufalme wake, alikuwaamewapa kielelezo kilichowapasa wakifuate baadaye watakapoishi kama jamiiyake. Hakuna sababu yoyote au zuio lolote la

Page 112: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA601

kuwafanya wasiishi kwa kunyenyekeana na kupendana. Kwa vyovyotewafanyiane kama Yeye alivyowafanyia. Heri ni katika kufanya. Tabia hizozatofautiana sana na tabia za wakuu na viongozi katika ulimwengu huu.

k.18 Ndipo Yesu, hali akijua mmoja wao yu mbali naye kwa tabia, na yu kinyumechake kwa hali, aliwajulisha wanafunzi habari kwamba miongoni mwao yumoatakayemfanyia vibaya na kumsaliti kwa wakuu na kurahisisha kazi yao yakumkamata. Aliona kwamba maneno ya Zaburi 41:9 yametimizwa, ingawa Zaburiyenyewe ilimhusu Daudi na shida zake. Ni vema tuone ya kuwa Yuda ni „mmojawao‟ tangu alipochaguliwa amekuwa katika kundi teule la Mitume, alikuwaameishi na Yesu na kumwangalia kwa ukaribu kabisa. Kwa tendo hilo alisukumiambali urafiki na upendo wa Yesu.

k.19 Alitaka wafahamu habari hiyo mapema, wasije wakashtuka kabisa jambohilo litakapotokea. Yeye hawezi kushtuka kwa sababu amefahamu hayo yotemapema. Yeye hudumu kuwa Bwana (k.3) hana budi kushindana na yule mwovu,na kumshinda kwa kufa kwake. Alitaka wafahamu kwamba katika hayo yote YeyeNdiye mwenye madaraka, ingawa kondoo mmoja amepokonywa mikononimwake (10:28) hasa hakuwa kondoo wake kwa kuwa hakuisikia sauti yake. Yesuatatumia maovu yote na kuyageuza kuwa njia ya kuleta wokovu.

k.20 Halafu kama ilivyokuwa desturi yake kwa tamko la maana alitia uzito kwamaneno „Amin, amin‟ ndipo aliwaunganisha kabisa na Yeye mwenyewe katikaUtume wake. Wao watashiriki kabisa katika Utume wake na kuuendeleza baadaya Yesu kuondoka. Yeye alikuwa Yule aliyetumwa na Baba, nao watakuwa walewaliotumwa na Yeye na Baba. Hao si wanafunzi au wafuasi tu, bali ni Mitume.Usia wote wa sura hizo 13 hadi 16 si mausia ya mtu anayekufa kitandani, bali nimaagizo ya Jemadari mkuu akiweka msingi wa kazi yao baada ya Yeyekuondoka. Kweli aliwatayarisha kwa kuondoka kwake, lakini ni matayarisho sikwa kuondoka kwake tu bali kwa kazi, yaani utume wao, utakaofuata kuondokakwake. Katika sura zilizotangulia Yohana ameandika habari za Utume wakwanza, wa Yesu Mwenyewe, sasa katika sehemu ya mwisho wa Injili alilengaule utume wa Mitume utakaofuata. Kwa hiyo, utume wa Yesu hautakomaatakapokufa Msalabani bali utaendelea katika Utume wa „walio wake‟. Saa yakuondoka kwake imefika, pia ni saa ya kuanza kazi kwa walio wake. Bila shakahawakuelewa mambo hayo wakati ule, ila baada ya Yesu Kufufuka na Rohokushuka juu yao walielewa kutokana na hayo aliyoyasema Yesu.

13:21-30 Kuagana na Msalitik.21 Lakini Yesu hana budi kumkabili huyo msaliti wake na kwa uzito sanaaliwaambia wanafunzi „Amin, Amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti‟Twasoma Yesu alisikia uzito na shida nafsini mwake, ingawa alifahamu hayoyote mapema aliguswa sana moyoni mwake. Lilikuwa jambo zito Kwake,hakuweza kulidharau na kusema basi tu, ndivyo ilivyo Ni dhahiri kwamba Yesu

Page 113: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA602

aliumizwa sana na hali ya Yuda, ni kama amekumbushwa mapema dhiki nyingizilizo mbele yake. Wanafunzi hawakuelewa ni yupi miongoni mwaoatakayemsaliti Bwana wao. Yuda alikuwa amejificha na Yesu alikuwaamemwacha bila kumdhihirisha kwa wenzake mpaka wakati huo. Bila shaka,kama wenzake wangalijua mapema wangalimshambulia vibaya. Tangu sikunyingi dalili za uasi wake zilikuwepo, ila Yesu alivumilia, akampa muda mwingiwa kurekebisha hali yake.k.22-23 Wanafunzi walishikwa na bumbuazi, wakakaa kimya, hukuwakitazamana, ndipo Petro, yule mwepesi wa kusema, akampungia mkono yulewa karibu na Yesu ili amwombe Yesu amtaje kwa jina huyo msalati. Kwa desturiya kula wakati wa karamu kubwa Wayahudi walizoea kujinyosha wakiegemeaupande wa kushoto na vichwa kuelekea mezani, wakitumia mkono wa kuumekwa kula. Meza ilikuwa fupi. Ilikuwa rahisi kwa yule aliyekuwa karibu upande wakulia kuegemea kifuani mwa Yesu na kumwuliza ni yupi. „mwanafunzi ambayeYesu alimpenda‟ Je! hayo si maneno ya kiburi kwa upande wa Yohana? Je! simaneno ya upendeleo kwa upande wa Yesu? La, siyo. Ni maneno ya mtualiyesikia deni sana kwa Yesu, aliyeonja nafsini mwake neema nyingi, ambayehakuchoka kuutaja upendo wa Mungu kwake. Labda wenzake walimtania kwamaneno hayo. Wengi hufikiri maneno hayo yamhusu Mtume Yohana aliyeandikakitabu hicho. Huenda Yuda alikuwa karibu na Yesu upande wa kushoto, mahalipa heshima. Yesu akajibu, kwa sauti ndogo, na bila kutamka jina, alitoa ishara yakumfunua, ndipo akampa Yuda tonge la chakula. Desturi hii ya kumpa mtu tongeilikuwa njia ya kuonyesha upendeleo wa kipekee na kwa kufanya hivyo Yesualikuwa akijaribu kwa mara ya mwisho kumvuta aache mpango wake,ajirekebishe na kurudi kwenye zizi. Ila Yuda alikataa, na katika kumkataa Yesualimkaribisha Shetani amshike na kutawala moyo wake. Nafasi ya toba ilipita.Ilikuwa saa ya kumbagua kuwa si mmojawao, saa ya hukumu yake. Kisha Yesu akamshauri aende na kufanya kwa upesiyale aliyokusudia. Bila shaka Yuda alitaka kuondoka, alihofu wenzakewatakavyofanya watakapomgundua. Asingalikuwa salama kama angalibaki pale.Tena hakuna faida kukaa kwa sababu Yesu ameishajua mpango wake, kwa hiyo,hakuna haja ya kuendelea kujificha.

k.29 Kwa sababu Yesu amesema kwa upole na kwa fumbo basi wenzakehawakuelewa sababu ya kuondoka kwake. Walidhani, ama amekwenda kununuamahitaji yao, ama amekwenda kutoa sadaka kwa maskini. Yesu akamwachaaondoke hali akijua kwamba anawaendea wakuu na kuikamilisha mipango yakumtia mikononi mwao.

k.30 Twaona hatua katika utelezi wa Yuda. Katika 6:70, 71, wakati Yesu alipotoanafasi kwa watu kumwacha (na wengi walimwacha) Yuda alibaki, na Yesualimtaja kuwa „ni shetani‟ yaani mpinzani. Katika 12:4-6 ameitwa „mwivi‟ na 13:2„Ibilisi amekwisha kumtia Yuda moyo wa kumsaliti‟ na 13:27 „Shetani alimwingia‟.Maisha yake yalikuwa kinyume cha upendo, alijipenda na mwishoni Shetanialipandikiza mawazo ya kumsaliti Yesu kwa fedha.

Page 114: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA603

k.30 Yohana mwandishi alijumlisha habari hiyo kwa maneno mafupi yenyemaana kubwa kiroho. „nako kulikuwa ni usiku‟. Ilikuwa usiku, kuhusu wakati,lakini zaidi ilikuwa usiku katika roho ya Yuda; na usiku katika historia yaulimwengu huu, maana Mwana wa Mungu yuaenda kusalitiwa kwa fedha, kishaakauawa. Yeye aliyempenda upeo alitendewa kwa chuki kubwa, Yeye aliyejitoakupenda alisalitiwa kwa tendo la kujipenda.

Yuda ni onyo kali sana kwa Wakristo, yawezekana tuwemo katika Kanisa, shirikala wafuasi wake, bila kuwa na imani ya dhati mioyoni mwetu. Twajifanya kuwawake, lakini, sio. Ni Wakristo wa bandia tu. Tena, inawezekana watu wamkataeKristo baada ya kuitwa naye mara kwa mara. Wasikie Injili kila wakati bila kuitikakwa kutubu na kumwamini Kristo. Ni vema tuone kwamba kuna wale ambao hataYesu hawezi kuwaokoa, kwa sababu wanakataa kuja Kwake.

Hapo tena Yohana ametuonyesha umuhimu wa kuamini na uzito wa kutokuamini.Ila katika hayo yote Yesu ameshika usukani na kutawala mwenendo wake.

13:31 - 38 Amri mpyaHapo tunayo hotuba ya Yesu kuagana na wanafunzi wake. Yesu alitaka sanakuwapa mausia yake kabla ya kukamatwa kwake. Alijua kwamba mamboyameiva, na ya kuwa mambo yatakwenda mbio. Alitamani sana nafasi yakusema nao. Aliwapenda upeo, badala ya kujiwaza na kujihurumia, na kutafutamapumziko n.k. alijitoa kuzungumza nao.

Baada ya Yuda kuondoka, Yesu alipumua vizuri, alisikia uhuru wa kusema wazina wanafunzi wake. Ijapokuwa hawakuelewa vizuri mambo mengi, hata hivyo,nia yao ilitofautiana na ile ya Yuda, kimsingi walimwamini kwa dhati nakumpenda. Kwa kuondoka kwa Yuda kwenda kwa wakuu mlango ulifunguka wazikwa utekelezaji wa mipango ya kumkamata. Yuda ni yule wa kuwekea mtegotayari kumnasa. Yesu alijua kwamba mambo yote ni tayari kwa Kukamatwa naKuhukumiwa na Kuuawa Kwake, kwa hiyo alitaka kuongea na wanafunzi kablaya matukio hayo kutokea ili awaandae kwa ajili yake. Inaonekana mazungumzohayo yalitokea katika kile chumba walimoila Pasaka, na kabla ya kwenda Bustaniya Gethsemane. Mara kwa mara wanafunzi walikatiza mazungumzo hayo kwakuuliza maswali, naye Yesu akawajibu, ndipo akaendelea na mazungumzo.

Tazama jinsi Yesu alivyorudia kusema mara saba maneno „hayo niliyowaambia..‟au maneno yanayofanana na hayo (14:25; 15:11; 16:1, 4, 6, 25, 33) akitoasababu za kusema nao, kama „ili mwe na furaha‟ „msije mkachukizwa‟ „ilimakusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambia‟ „mpatekuwa na amani‟ n.k.

Page 115: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA604

k.31 Alianza na tangazo „Sasa ametukuzwa Mwana wa Adamu, naye Munguametukuzwa ndani yake...‟. „Mwana wa Adamu‟ ni jina alilozoea kujiita(Dan.7:13). Kutukuzwa ni upeo wa makusudi makuu ya Mungu katika Utume waKristo. Maana ya „kutukuza‟ ni kuadhimisha, kupandisha penye heshima kuu.Mwandishi Yohana katika Injili yake amesisitiza kwamba Yesu na Baba yakehutukuzwa katika Mateso na Kifo cha Yesu (7:39; 12:16) kwa sababu utukufuwao ni udhihirisho wa tabia zao njema za upendo, utakatifu, haki, na rehema.Tabia hizo zitaonekana wazi Msalabani. Yesu alitamka neno hilo la kutukuzwaWayunani walipotaka kumwona (12:23). Ombi lake la mwisho kwa Babakelilikuwa „mtukuze Mwana wako‟. Kwa njia ya Mateso yake Baba atatukuzwa naYeye atainuliwa juu kuwa Mwokozi wa Ulimwengu. Kwa hiyo saa ya kudhiliwasana ni saa ya kuadhimishwa mno. Bila shaka hata Kufufuka na Kupaa kwakekumefungamana na Kufa Kwake kwa sababu kwafuatana kama ni jambo moja.

Ila wanafunzi hawakuwa tayari kupokea mawazo ya Yesu kuhusu Kifo Chake.Walishikwa sana na mawazo juu ya Masihi wa kimwili, wa siasa, hatawalishindwa kumwelewa Yesu. Alikuwa amewaambia wazi mara kwa mara,ametaja kukamatwa kwake, kuhukumiwa kwake, kushtumiwa kwake, na kufakwake, pamoja na kufufuka kwake. Mapema sana alisema habari ya Hekalu lamwili wake kuharibika (2:20-21). Alimwambia Nikodemo kwamba „kama nyokaalivyoinuliwa jangwani, ndivyo na Mwana wa Adamu atakavyoinuliwa juu ya mti‟(3:14); alisema Mchungaji wa kweli „hutoa maisha yake kwa ajili ya kondoo‟(10:11). Kwa hiyo katika mazungumzo hayo Yesu alijitahidi kwa mara ya mwishokuwaandaa kwa mshtuko mkubwa utakaowapata atakapokamatwa.

k.33-35 Aliwaonya kwamba yuko pamoja nao kwa muda mfupi na ya kuwaanakwenda mahali wasipoweza kumfuata kwa sasa ila baadaye watamfuata.Alikuwa amesema jambo hilo kwa Wayahudi hapo nyuma (7:33-34; 8:21).Aliwaita „watoto wadogo‟ walikuwa wamekula Pasaka pamoja kama familia yake(Pasaka iliadhimishwa kwa kula pamoja kifamilia). Kwa kutaja kuondoka kwakealiwajulisha kwamba kuuawa kwake sio mwisho, yeye ni Mtangulizi wa kupasuanjia ili wao wamfuate baadaye.

Jambo kubwa kwa upande wao ni kuwa na umoja. Ni watu tofauti tofauti, haponyuma wameoneana wivu na kugombana juu ya nani atakayekuwa mkubwa, kwahiyo walihitaji nguvu mpya ili washikamane vizuri kusudi waitimize shabaha yakuitwa na kutumwa kwao. Kwa hiyo Yesu aliwapa amri mpya „Mpendane, kamaMimi nilivyowapenda ninyi nanyi mpendane vivyo hivyo‟. Upendo ndio alama yaufuasi wao na msingi wa umoja wao. Ameishawapa kielelezo alipotawadhamiguu, na karibuni hivi atatoa kielelezo kikubwa sana atakapowafia Msalabani,kwa hiyo, kiutendaji wameonyeshwa ni upendo wa aina gani aliosema. Ni upendowa kujitoa, usio na ubaguzi wala mpaka. Ni upendo wa kina sana. Yesu alisemailikuwa amri mpya. Kwa upande mmoja haikuwa mpya, kwa sababu, hata katikaAgano la Kale Waisraeli walikuwa na

Page 116: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA605

amri juu ya upendo (Kum.6:5; Law.19:18; Mk.12:28) hasa upya wake ni katikakipimo chake „kama nilivyowapenda ninyi‟ katika kina chake; pia huandama naAgano Jipya, kama msingi wake, Agano ambalo Yesu atafanya kwa kumwagadamu yake.

k.36-38 Petro, aliyekuwa mwenye haraka wa kusema, hakuvutwa na habari yaamri mpya ila alishikwa na maneno ya Yesu juu ya kuondoka kwake. Alitakakujua Yesu anakwenda wapi na kwa nini hakuweza kumfuata mara moja. Kwanini asiweze kumfuata sasa? Bila shaka Yesu aliona ya kuwa Petro hakutambuaenzi za uovu zitakazofanya kazi kwa nguvu usiku ule, wala hakuwa tayari kukabilihatari iliyo mbele yake itakayosababishwa na enzi hizo. Petro alisisitiza utayariwake wa kuhatarisha maisha yake kwa ajili ya Yesu, ila Yesu alimfahamu Petrona udhaifu wake kuliko alivyojifahamu mwenyewe. Akamhoji juu ya ukweli waahadi yake ya kuutoa uhai wake, ndipo kwa upole akamfunua kwamba licha yakuhatarisha nafsi yake atamkana mara tatu usiku uleule. „atamfuata baadaye‟kihistoria maneno hayo yalitimizwa, mapokeo husema kwamba aliuawa paleRumi kama mwaka B.K.64, huenda pamoja na Mtume Paulo.

MASWALI1. Yesu aliwatawadha miguu wanafunzi wake katika hali ya kujua nini?2. Tendo hilo la Yesu liliashiria nini?3. „Kama nisipokutawadha huna shirika nami‟ Kwa maneno hayo Yesu alitaka

kumwonyesha Petro lazima gani kwa upande wa kiroho?4. Yesu aliwaambia kwamba tendo lake la kutawadha miguu lilikuwa kielelezo

ili wao wafanye nini wao kwa wao?5. Zungumza kama Wakristo wa leo wanafuata kielelezo cha Yesu katika

kuishi kwao kama wafuasi wake?6. Katika sehemu hiyo Yesu aliwafunulia mambo gani kuhusu baadhi yao?7. Alitoa amri gani kwao? Eleza hali ya upendo waliotakiwa kuwa nao?

14:1-14 ‘Mwisho’ wa wauminiKatika sehemu hiyo yote Yesu aliwaelezea wanafunzi baraka za kuondokakwake, ila kwanza ilimbidi akabili hali ya fadhaa zao zilizosababishwa na habarihiyo.

Ni Yesu anayekwenda kwa dhiki kuu za Msalaba na tumeona kwambaalifadhaika alipowaza yote yaliyokuwa mbele yake (12:27; 13:21) na katika usikuhuo wa kipekee ingalifaa kama wafuasi wake wangalimfariji na kumtia moyo.Lakini, badala yake, wao walifadhaika, si kwa sababu watasulibiwa, bali kwasababu wamekanganyika, wana mashaka juu ya maana ya maneno ya Yesu, piawameudhika na habari za kuondoka kwake, walisikia kama watakuwa yatima.Kwa miaka mitatu wameshirikiana naye kwa ukaribu, ilikuwa vigumu kuwazamaisha bila Yeye. Walikata tamaa waliposikia kwamba wataachwa.

Page 117: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA606

Itakuwaje? Huko Petro kiongozi na msemaji wao atamkana, nao watakimbia kwahofu, na Yesu hatakuwapo, basi watafanya nini? Si ajabu nyuso zaozilikunjamana na miili yao ililegea, na hofu ilijaa macho na mioyo yao, walijisikiakama wameishiwa nguvu kabisa.

k.1 Lakini Yesu, hali akielewa hayo yote alisema „msifadhaike mioyoni,mnamwamini Mungu, niaminini na mimi‟. Hapo nyuma aliwashauri wapendane iliwapate kuuhifadhi umoja wao; hapa anawashauri wamwamini Mungu nakumwamini Yeye pia. Dawa kwa fadhaa zao ni imani. Kwa kuwa Mungu yuko naYesu yuko pamoja naye, yapo matumaini kwa wanadamu baada ya kuishi hapaduniani. Tumaini la uzima wa milele limejengwa juu ya ukweli na uaminifu waYesu na kazi ya ukombozi atakayofanya. Aliwaomba wanafunzi wake wawe naimani katika Mungu na katika Yeye, na katika kusema hayo alijiweka sawa naMungu. Tena wamwamini hata atakapokufa. Yesu ni ufunguo wa mwisho wao,mwisho unaotegemea kabisa kazi atakayofanya Msalabani. Kwenda kwakekutatia muhuri kuhusu mwisho wao katika uzima wa milele. Ni tendo la nguvuambalo litawapatia uzima wa milele. Ili wasiwe yatima baadaye itawabidi waweyatima kwa muda sasa. Yesu alikuwa jasiri wa ajabu, aliwadai utiifu, haidhuruyatampata mambo gani hivi karibuni.

k.2 Aliendelea kwa kuwaelezea kwamba mwisho wao ni „nyumbani mwa Babayake, penye makao mengi‟. „nyumbani mwa Baba ni mbinguni, na makao mengini ishara ya nafasi tele, nafasi kwa wote watakaotaka kuingia. Yeye ndiyemwandilizi wake, na Yeye atawakaribisha Kwake. Alisisitiza mambo mawili,„nyumbani mwa Baba‟ yaani mbinguni na „mbinguni‟ maana yake ni nini? hasa niKuwako kwa Mungu, potelea mbali kuna mambo gani zaidi, kuwa pamoja naMungu ni mbinguni. Haidhuru tutamaanisha „mahali‟ kwa jinsi gani, iliyopo nikwamba, waumini watakuwa katika mazingara ya furaha sana. Pia watakuwapamoja na Kristo ambaye ni „utukufu‟ wa hayo mazingara. „Mwisho‟ ni Yeye nawaumini kuwa pamoja kwa ukaribu kabisa. Yesu alieleza jambo hilo kwa manenomepesi.

Yesu aliwahakikishia tumaini hilo kwa kusema kwamba kama angalikuwa namashaka asingaliwaambia habari hiyo. Ikiwa Yeye atapitia katika magumu yaMsalaba na kusumbuka sana ili awaandalie mahali, haiwaziki kwamba haohawatamfuata. Alijua Yeye atafaulu kuwakomboa na wao watahitimu maisha yaKikristo. Yesu alikuwa na ujasiri wa kuamini kwamba mwishowe watafika kwenyenyumba ya Baba yake. Alikuwa thabiti juu ya mwenendo wake, tazama maneno„naenda‟ „nitakuja tena‟ „niwakaribishe Kwangu‟ „nilipo Mimi nanyi mwepo‟.Usalama wao ni katika kumwamini Yeye, ijapokuwa kwa sasa hofu imejaamioyoni mwao.

k.3 Ina maana gani „nitakuja tena‟. Mawazo mbalimbali yametolewa kuelezamaneno hayo. Wazo moja ni kwamba alikuja tena alipofufuka na kuwatokeamara nyingi. Wazo lingine ni kwamba alikuja kwa njia ya Kushuka kwa Roho

Page 118: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA607

Mtakatifu; ndipo wazo lingine ni kwamba anakuja mara kwa mara kwa muuminiwake pengine wakati wa kushiriki Chakula cha Bwana, na kusoma Maandiko, nawakati wowote mtu anaposikia kwamba Yesu yu pamoja naye. Mawazo hayo nimazuri, ila yawezekana wazo la Kurudi kwake mara ya pili ni wazo lenye nguvu.Tunajua hakika kwamba atakuja kutuchukua Kwake.

k.4 Yesu aliwaambia kwamba walijua njia. Huenda alikuwa na maana kwambakwa sababu wamemfahamu Yeye haikosi wataifahamu njia. Lakini kumbe, sivyo.

k.5-6 Katika Injili hiyo Tomaso ameonekana kama mkweli, mwaminifu, hata jasiri,ila pia alikuwa mtu aliyesikia mashaka. Kwa jinsi alivyomjibu Bwana Yesuinaonekana alitaka kujua mahali, bila kujua mahali wanapokwenda watajuajenjia. Lakini katika kifungu cha kwanza Yesu alisisitiza umuhimu wa kumwaminina katika k.2 alitaja mahali pa kwenda „nyumbani mwa Baba yangu‟. Hivyo, kwaswali lake Tomaso amekiri kwamba yeye na wanafunzi wenzake badohawajaelewa vizuri maana ya maneno ya Yesu. Yesu hakumkemea kwakutokuelewa kwake, maana alijua kwamba wamechanganyikiwa sana na kujaahuzuni juu ya kuondoka kwake. Alimsaidia kwa kutamka tangazo maalum juu yaNafsi Yake, tangazo ambalo juu yake yeye Tomaso na wenzake wapaswakujenga maisha yao. Kwa uthabiti alisema „Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima;mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya Mimi‟. Tangazo hilo ni kubwa mno na la maanasana. Hakusema kwamba alijua njia, wala ya kuwa aliifundisha. Hakujitoa kuwamfasiri wa mpango mpya au taratibu mpya, la, ila alijitangaza Mwenyewe kuwaufunguo wa kufumbua mafumbo yote na siri zote za maisha ya wanadamu nakuwa mpasuaji wa njia ya kufika kwa Baba.

Yeye ni njia: Liko shimo refu kati ya ukosefu na upungufu wa wanadamu namwisho wa kuhitimu kwake. Ni kama shimo lisilopitika, lisilo na daraja la kulivukia.Tomaso alitambua neno hilo na kukata tamaa. Ila Yesu alimwambia „Mimi ndimiNjia‟ kwa njia ya Yesu Mwenyewe, Njia hai, mtu hupata daraja ya kumrudiaMungu na kuhitimu makusudi ya Mungu juu yake. Yesu aweza kuwa Njia kwasababu hiyo moja tu, ya kwamba, Yeye pia ni Kweli na Uzima (Mt.7:14).

Yesu ni kweli: Kweli ni adimu sana katika ulimwengu huu. Wanafalsafa huitafutabila kufanikiwa. Hakuna mwenye akili za kutosha kuipata, wala hakuna mwenyeusafi wa maisha wa kuipata kwa matendo yake. Kweli imekaa katika mmoja YesuKristo. Kwa mamlaka kuu Yesu aliwatangazia wanadamu kwa maneno ya wazi„Mimi ni kweli‟ (1:14).

Yesu ni uzima: Kwa uzima wake watu wapata uwezo wa kutimiza mapenzi yaMungu. Ni uzima unaoanzia katika Mungu na ni uzima unaowainua watu watokekatika dhambi na kumwishia Mungu katika haki (1:4: 3:15; 5:26; 11:25). Ukristosi mpango wa falsafa, wala mawazo makuu, wala taratibu za ibada,

Page 119: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA608

wala mkusanyo wa sheria, wala mpango wa maadili, bali ni upokeaji wa kipawacha uzima kitolewacho na Mungu.Bila njia hakuna kwenda:Bila kweli hakuna kujua:Bila uzima hakuna kuishi:

Wengi wametoa habari ya mipango ya kuvuka daraja kati ya wanadamu naMungu, ila hakuna ambaye amefaulu ila mmoja tu, Yesu Kristo, ambaye alitokakwa Baba, kisha akarudi kwa Baba, baada ya kufanya upatanisho kati ya Babana wanadamu. Bila wasiwasi, na kwa uthabiti, Yesu alitamka „mtu haji kwa Babaila kwa njia ya Mimi‟. Kwa nini ni hivyo, ni kwa sababu kwa Kuja kwa Yesu, ufunuokamili wa Mungu Baba umepatikana, kwa hiyo, kipimo cha kumpimia mtuanayedai kuwa anamjua Mungu ni itikio lake kwa Yesu. Bila watu kumpokeaKristo hata Ukristo umebaki kama dini moja nyingine. Ila maneno hayo hayanamaana kwamba kila dhana la wasio Wakristo halina maana yoyote. Twajuakwamba dhamiri hufanya kazi mioyoni mwa watu wote, na dhamiri huungamkono matendo yanayopatana na sheria ya Mungu iliyomo ndani (Rum.2:14) ilatwajua pia dhamiri humshtaki mtu kuwa na dhambi, na mpatanishi ni mmoja tu,Yesu Kristo (Rum.3:23; 1 Tim.2:5).

k.7 Yesu aliwaambia wanafunzi kwamba wameshindwa kumwelewa kwa sababuhawakumjua Baba. Kwa maneno hayo inaonekana kwamba hata mpaka wakatihuo wa mwisho ijapokuwa wamemfahamu vizuri kama mtu, kumfahamu alivyohasa, Nafsi yake na Utume wake, bado hawafahamu kwa usahihi umoja wake naBaba. Ijapokuwa wameishi naye kwa miaka mitatu wamemwelewa kwa kiasi tu,ila ufahamu wao utakamilika baada ya Yeye kufa na kufufuka. Hivyo, kuna faidakubwa katika kuondoka kwake, kwa kuondoka kwake Mungu atakuwaamejifunua kwa ukamilifu, ndipo wataufahamu umoja wa Baba na Mwana. KatikaMsalaba wa Yesu wataona upendo wa ajabu wa Mungu na uzito wa utakatifuwake na kujua kwa hakika kwamba Mungu ni Pendo na Mungu ni Mtakatifu,Msalaba ni mahali pa udhihirisho wa tabia hizo.

k.8-11 Filipo alitaka kumwona Baba moja kwa moja, yaani Baba ajidhihirishekwao kwa njia ya pekee. Labda wamwone kama ambavyo walikuwa wakimwonaYesu mwenyewe, kwa macho ya kimwili. Filipo alikuwa na tabia ya „utendaji‟hakuwa na maelekeo ya kuyashughulikia mambo ya mawazo na falsafa. Tulionahali yake Yesu alipomwuliza juu ya kuwalisha umati wa watu. Alimjibu kwa kutoa„hesabu‟ ya mikate iliyotakiwa (6:5-7). Siyo kusema kwamba hakuwa na nia yakujua mambo ya kiroho, hata swali lake linaonyesha kwamba alitaka kumjuaMungu. Wanadamu hutamani sana kuwa na Mungu anayeshikika,anayeonekana. Mungu amejibu hamu hiyo ya wanadamu kwa kumtuma YesuKristo Mwana wake na ni Yeye aliyemfunua Baba ili apate kujulikana nawanadamu.

Page 120: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA609

k.9 Huenda Yesu alisema kwa huzuni „Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizizote‟ ni kama kusema kwamba muda umetosha kabisa kwa hao wanafunzikumtambua. Hapo nyuma tumeona upofu wa wapinzani wa Yesu, lakini hatakatika wanafunzi waaminifu alikuta „upofu wa kiroho‟. Yesu akamwambia Filipo„yeye aliyeniona Mimi amemwona Baba‟. Mwana wa milele wa Baba, ni mng‟aowa utukufu wake na chapa ya Nafsi yake (Ebr.1:3). Yesu alikuwa na umoja naBaba hata kiasi cha kumdhihirisha kwa ukamilifu, tabia na hali na uhalisi wake.Kwa hiyo, kwa jinsi Filipo alivyomwona Yesu, ndivyo alivyoweza kuwa na uhakikawa uhalisi wa Baba na jinsi Alivyo.

Ila jambo hilo kubwa lilihitaji uthibitisho. Yesu alimwambia Filipo amwamini, siamwamini kibinafsi tu, bali ayaamini aliyosema, kwa sababu Yeye alijua hakikakwamba Baba yu pamoja naye wakati wote. Kibinafsi Yesu alijua hakika kwambaBaba yu ndani yake na Yeye yu ndani ya Baba. Kwa kuishi pamoja na Yesuwanafunzi wangaliweza kutambua neno hilo. Ndipo Yesu aliwaomba wamwaminikwa ajili ya maneno aliyoyasema (3:34;7:46). Maneno yake yalikuwa yenyemamlaka iliyotoka juu. Yalikuwa ya kipekee yakipita hekima na uwezo wa wenyehekima na watakatifu wengine wote. Yalikuwa maneno ya Baba hasa. Hata ikiwawameshindwa kuyapokea maneno yake basi, waziamini kazi zake, miujiza,ishara, na maajabu, vyote vilivyotia muhuri maneno yake na kuyathibitisha madaiyake kuwa umoja na Baba. Wakati wote Yesu alikataa kufanya jambo lolote kwanafsi yake Mwenyewe.

k.12-14 Yesu aliendelea kusisitiza kwamba wamwamini hali akiwaahidi kwambawao wenyewe wataushiriki uwezo wa Mungu sawa na Yeye. Katika kushirikishwaUtume wake watajaliwa nguvu za utumishi ndipo kazi watakazofanyazitaushuhudia ukweli wa Yeye kuwa na umoja na Baba. Shabaha ya Yesuilikuwa kumtukuza Baba kwa kazi alizozifanya, vivyo hivyo, na shabaha ya kazizao itakuwa ile ile ya kumtukuza Baba na Mwana. Watafanya zaidi, si kwasababu wao ni wakubwa kuliko Yeye, la, ila kwa sababu Yesu anakwenda kwaBaba. Hizo kazi kubwa kuliko zile alizofanya Yesu ni kazi zipi? Haina maanawatafanya zaidi ya Yesu, tukikumbuka ufufuo wa Lazaro, kuyageuza maji kuwadivai, na kuwalisha watu elfu tano n.k. La, siyo.

Katika Matendo ya Mitume, Mitume walijaliwa kuwafufua wafu na kuwaponyawagonjwa n.k. Hasa maana ya maneno ya Yesu ni kwamba kwa kuondokakwake, baada ya kufanya ukombozi, utaratibu mpya utakuwa umeingia, ufalmewa Mungu utakuwa kati ya watu na nguvu yake itagusa maisha ya watu wengizaidi, mashahidi wa Yesu watakwenda katika ulimwengu mzima na kwa mataifayote, ndipo wengi zaidi wataokolewa. Mambo yatakuwa wazi na habari za Kristozitaenezwa na kueleweka bila shida na wanadamu watamtambua Mungukutokana na ufunuo ulioletwa na Yesu. Wanafunzi watajibiwa maombi yaowanapolenga kuitimiza shabaha ya kuitwa kwao na kwa ajili hiyo Yesu aliwapaahadi kubwa sana „mkiomba neno lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya‟. Ahadi

Page 121: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA610

hiyo si ruhusa kuomba neno lolote walipendalo, bali kuomba yale tuyatakayoendeleza Utume waliopewa na Yesu. Vivyo hivyo neno hili linahusumaombi yetu pia.

14:15-31 Kuondoka kwa Yesu na Kuja kwa Roho Mtakatifuk.15-21 Twaona uhusiano na sehemu iliyotangulia. Yesu alisema kwambawanafunzi wake watafanya makubwa kuliko aliyoyafanya Yeye. Kama ni hivyowatahitaji nguvu mpya ya kuwawezesha na Mungu atadhihirika katika mambohayo kwa njia ya Roho Mtakatifu. Pia Yesu alisema kwamba wakiomba kwa Jinalake atayajibu maombi yao. Katika sehemu hiyo Yesu alisisitiza umuhimu wa utii,hawatazaa matunda bila kujihusisha naye na kumtii.

Baada ya kuwahakikishia kwamba hatoroki ila anakwenda kuwatayarishiamahali, Yesu aliwaomba wamtii. „Mkinipenda, mtazishika amri zangu‟. Kamawamefadhaishwa sana na habari za kuondoka kwake ina maana kwambawalimpenda kweli na ikiwa ni hivyo, budi wauonyeshe upendo wao katika utii.Kama upendo ndio msukumo wao mpya, utii ndio msimamo wao mpya. Yesualikuwa amewaonyesha jinsi alivyowapenda upeo alipowatawadha miguu(13:lku) aliwaambia wazi kwamba aliwapenda na aliwaamuru wapendane kamaYeye alivyowapenda (13:34). Hivyo aliunganisha mawili, kama mamboyaendayo pamoja, yasiyoweza kubadilishwa; kumpenda Kristo na kumtii Kristo.Katika amri zake, mojawapo kubwa ni kupendana, hata yawezekana alikuwa namaana ya wautii ule ufunuo wote wa Baba aliokuwa amewapa.

k.16-17 Kwa sababu mbele yao ni hali mpya ya maisha, maana Yesu hatakuwapamoja nao kimwili Yesu aliwaahidi mwingine, kama Yeye, mwenye nguvu, RohoMtakatifu. Huyo Roho ameitwa Msaidizi mwingine, maana ya neno Msaidizi nimtetezi, mwakilishi, mtu amshughulikiaye mwingine. Neno „mwingine‟ ina maanakwamba huyo atafanana na Yeye. Yesu alimwita „Roho wa kweli‟ Yuleatakayewajulisha kweli. Katika 14:6 Yesu alisema „Mimi ndimi njia, na kweli, nauzima‟ hivyo Roho atamshuhudia Yesu (16:13-14). Ndipo Yesu alisema juu yaRoho na ulimwengu, yaani wote walio kinyume cha Mungu hawamtambui, nakwa sababu hawamwoni itakuwa vigumu wampokee, hata wengi hawakumpokeaYesu alipoonekana. (Katika 16:7-11 Yesu alisema juu ya kazi za Roho kwa walewasio Wakristo). Katika kuzungumzia habari za Roho Yesu hakuwa na maanakwamba wanafunzi wamkiri Roho kama sharti moja ya Imani, bali wawe na ujuziwake maishani mwao, bila kuwa na ujuzi huo ahadi yake juu ya tiba kwa fadhaazake ilikuwa bure. Roho atafanya kazi ndani yao.

k.18-20 Wanafunzi bado wangali walijisikia kuwa kama yatima na Yesualiwaahidi „naja kwenu‟. Ingawa baadhi ya wataalamu hufikiri kwamba alikuwana maana kwamba atakuja kwao kwa njia ya Roho, huenda hiyo si maana yakehasa. Atakuja kwao Atakapofufuka kutoka wafu. Katika muda ule baada yaKufufuka Yesu hakutokea kwa wale ambao walikuwa wamemkataa, ila kwa waletu, ambao walimwamini. „kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa

Page 122: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA611

hai‟. Roho hawezi kuja mpaka Yesu amekufa na kufufuka, ndipo atamwombaBaba awape msaidizi mwingine. Kwa hiyo alikuja na kujihusisha nao tenakuanzia siku ya Kufufuka kwake. Ndipo Yesu alitaja „siku ile‟ yaani siku ya Ufufuokuwa siku ambayo watatambua kwa uhakika kwamba Yeye ni ndani ya Baba, nawao ni ndani yake na Yeye ndani yao. Yeye na Baba huwa na umoja, nakutokana na umoja huo yeyote ampendaye apendwa na Baba, na Yeye piaampenda.

k.21 Ndipo Yesu akarudia kusisitiza mambo ya upendo na utii. Kwa sababu Yesualitangulia kutupenda, ni wazi kwamba utii si sharti ya upendo wake, ila umuhimuwa utii ni katika kuwa njia ya kuuendeleza huo uhusiano. „na kujidhihirishakwake‟ kama Baba alivyomwonyesha mambo yote ndivyo Mwana atawafunuliawatu wake mambo hayo (3:35; 5:20). Ni msingi wa umoja, atajidhihirisha Siku yaUfufuo na siku zifuatazo, hata baadaye ataendelea kujidhihirisha kwao (Mt.28:20).

k.22 Mmoja wa wanafunzi wake aliyesikia hayo aliyosema Yesu juu yakujidhihirisha kwao wala si kwa ulimwengu, akashindwa kuona ni kwa jinsi ganijambo hilo litakavyowezekana. Pengine alikuwa akifikiri kwamba Ufalme waMungu utakuja kwa nguvu na utukufu, hata ulimwengu utashtuka kumwonaMasihi akija katika utukufu wake. Kama Yesu ni Masihi, bila shaka atajidhihirishakwa wote, si kwa wale wachache tu. Aliyemwuliza amedhaniwa kuwa Yuda waYakobo (Lk.6:16; Mdo.1:13) ila hatuna hakika kwa sababu mwingine pia aliitwaYuda. Yesu akamjibu kwa kufafanua kwamba udhihirisho wake hutokea katikajamii ya wale wampendao na kumtii. Hivyo, iwapo Yesu anajitayarisha kuwaachawanafunzi wake na kwenda kuwaandalia mahali katika „nyumba ya Baba yake‟wakati huohuo anajiunga na Baba (usawa wao) ili wafanye makao mioyoni mwawaumini wake. Hali hiyo mpya itakuwa malimbuko ya tarajio la baadaye wakatiMungu atakapokuwa pamoja na watu wake kabisa (Ufu.21:3,22). Ujuzi huo wa„undani‟ wa Baba na Mwana umejengwa juu ya upendo na utii wao. IjapokuwaYesu anawaacha, kwa njia nyingine, haachani nao. Ni upendo unaozalisha utii.Maneno ya Yesu yapaswa kushikwa, kwa sababu, pamoja na kuwa maneno yakeni maneno ya Baba pia. Hamna mawasiliano na ulimwengu kwa sababuulimwengu haumpendi wala haumtii.

k.25-26 Yesu aliwakumbusha kwamba ameishawaambia mambo hayo„nilipokuwa nikikaa kwenu‟, dokezo la kuondoka kwake ambalo ni neno kuu lasehemu hiyo yote. Ndipo akarudia kusema juu ya Roho. Baba atampeleka Rohokwao „kwa Jina langu‟ kwa sababu Yesu amemwomba Baba amtume k.16. Ikiwaanakuja katika Jina lake ina maana kwamba Roho ni kama mjumbe wake, sibadala wake tu, sawa na jinsi Yesu alivyokuja katika Jina la Baba (5:43; 10:25).Hivyo Roho atakuwa na mamlaka ya Baba na Mwana. Ni hapo tu katika AganoJipya ambapo Baba na Mwana wametajwa pamoja katika kuja kukaa ndani yawaumini.

Page 123: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA612

Halafu Yesu alitaja kazi mojawapo ya Roho iliyo kubwa sana kwa upande wawanafunzi. Hapo nyuma mara kwa mara walikuwa wameshindwa kumwelewaYesu na huduma na mafundisho yake. Baada ya Yesu kutukuzwa Rohoatawakumbusha na kuwafunulia maana halisi ya maneno na matendo ya Yesu(2:19-22; 12:16; 20:9). Kwa hiyo, maneno hayo yalihusu kizazi cha kwanza chawanafunzi kusudi wapate kuwa na ufahamu sahihi na kamili kumhusu Kristo. ilivizazi vya baadaye wakabidhiwe habari zake sahihi katika Maandiko.Hawatapewa ufunuo mpya bali ufunuo waliokuwa nao utaeleweka barabara.Katika Injili na Nyaraka tumejaliwa kupata habari hizo kutoka wenzetu wakwanza na kuamini kwamba hayo waliyoandika ni sahihi kwa sababu walikuwamashahidi na kwa msaada wa Roho waliweza kukumbuka na kutafsiri maanayake.

k.27 Kisha Yesu alisema „amani nawaachieni, amani yangu nawapa‟. Amaniilikuwa neno la salaam ambalo Wayahudi walizoea kulitumia wakati wa kuamkiana kuagana na mtu. Hapo Yesu amelitumia kama neno la kuagana na wanafunziwake, ila Alipofufuka lilikuwa neno la kuwaamkia (20:19,21,26). Ajabu ni kwambawakati huo Yesu Mwenyewe alikuwa akikabiliwa na dhiki kubwa, bado hajapitiakatika mateso ya Gethsamane na shutuma na dhiki za kuhukumiwa nakusulubiwa, hata hivyo, aliweza kutoa kipawa hicho cha kutoka KwakeMwenyewe „amani yangu nawapeni‟. Amani ni hali moja kimsingi ya Ufalmewake, utaratibu mpya ambao ameuingiza kwa Kuletwa kwa Ufalme wake ni„amani ya Mungu ulimwenguni‟. Kwa mtu mmoja mmoja ni utulivu kati ya shidana kuondolewa hofu yake. Amani hulinda moyo na nia (Flp.4.7) na kuwa kamafilimbi ya kuamua mambo moyoni ili watu wa Mungu waishi kwa amani wao kwawao (Kol.3:15).

Tena Yesu alisema kwamba anawapa sivyo kama ulimwengu utoavyo.Ulimwengu hauna uwezo wa kuitoa, kwa sababu amani asemayo Yesu ni YakeMwenyewe, ile iliyodhihirika saa ya kuuawa kwake. Kwa Kifo chake amemezachuki na dhambi za ulimwengu. Imepatikana kwa njia ya mtu asiyekuwa na hatiakuuawa kama mhalifu. Alifanya amani kwa Mungu, akatupatanisha na Mungu, ilituwe na amani ya Mungu. Kwa hiyo vipawa vyake vikubwa vilivyotajwa katikasehemu hiyo ni amani na Roho. Katika 15:9-10 Yesu ataja pendo langu, na katika15:11 ataja furaha yangu.

k.28 Yesu aliendelea kukabili hali yao ya fadhaa, wamehofu sana kwa sababuameendelea kutaja kuondoka kwake. Wamekosa kumfahamu, wamekosakumtegemea kwa mambo ya baadaye, wakiwa na wasiwasi sana kila alipotajaKuondoka kwake. Pia Yesu aliona hali yao inaonyesha kwamba wamepunguakatika upendo wao. Wametawaliwa na hali ya kujihurumia, wakiwaza hasara yakutokuwa na Yesu pamoja nao, wala hawajamwaza Yeye na faida kubwaatakayopata katika kurudi kwa Baba yake. Iliwabidi wafurahi sana kwa sababuhiyo. Tena kwa sababu anarudi kwa Baba kuna uhakika wa wao kuwa pamojanaye milele na milele. Yana maana gani maneno „kwa maana Baba ni mkuu

Page 124: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA613

kuliko mimi‟. Hoja moja kubwa ya Injili hiyo ni kwamba Yesu yu sawa na Baba(1:1,18; 5:16-18; 10:30; 20:28). Lakini pamoja na hoja hiyo tumeona kwambaYohana alisisitiza utii kamili wa Yesu kwa Baba na jinsi alivyomtegemea kwa yote(4:34; 5:19-30; 8:29; 12:48-49). Mambo hayo mawili ni sawa na yanawiana katikaYesu. Maana hupatikana katika kutazama mazingira ya maneno.

Hapo Yesu aliwaambia wanafunzi walipaswa kufurahi kwa sababu Yeye anarudipale ambapo ni pake hasa, kwenye utukufu aliokuwa nao hapo mwanzo (17:5)mahali ambapo utukufu haupungui wakati wo wote, ambapo ni tofauti sana nahali ya kuwa Mwana wa Baba hapa ulimwenguni. Baba ni mkuu, kwa kulinganana hali ya Mwana katika kuzaliwa mwanadamu na kuishi hapa duniani, si katikaasili yake. Wakirekebisha mawazo yao na kuona Yesu anarudi „nyumbani kwaBaba‟ bila shaka fadhaa zao zitapungua. Ni kwa sababu wamewaza ya kwao,bila kumwaza Yesu, wamezidi kuhuzunika. Mwana alikuwa chini ya Baba kwakazi ya ukombozi, Baba ni kama chemchemi ambapo Mwana na Roho hutokadaima. Katika kuuawa Yesu alifikia upeo na mwisho wa kujidhili kwake.

k.29 Hakuwaambia hayo ili awaaibishe, ila imani yao ijengwe, ndipo matukiohayo yatakapotokea watakumbuka kwamba Yesu alikuwa ameishawaambiahabari zake, kama alivyowaambia juu ya usaliti wa Yuda (13:19).

k.30-31 Yesu alikuwa jasiri, kwa jinsi alivyokaza nia yake kufanya mapenzi yaBaba yake, hakuwa na wasiwasi, alijua hakika kwamba Shetani hawezikumshawishi na kumwondoa kwa Baba, hata kama atajaribu kwa mara yamwisho kumpata wakati wa dhiki yake nyingi. Shetani alikuwa nyuma ya yoteyatakayotendeka (6:70; 13:21; 27) potelea mbali ni Yuda aliyemsaliti n.k.Ijapokuwa Shetani alidhani ni saa yake ya ushindi, ukweli ni kwamba ilikuwa saayake ya kushindwa; kwa sababu Yesu ataendelea kumtii Baba mpaka kufa.Shetani hakuweza kumdai lolote, kwa sababu Yesu hakuwa wa ulimwengu huu(8:23) wala hakufanya dhambi (8:46) hivyo hakuweza kuleta shtaka la haki juuyake.

k.31 Ulimwengu utajifunza kwamba amempenda Baba upeo na kumtii kabisa.Upendo ulio kiini cha mawasiliano yao katika Utatu ulitangulia upendo wa Mungukwa ulimwengu uliodhihirika kiutendaji katika kifo cha Yesu. Tumepewa mfanohalisi jinsi uhusiano wetu na Baba na Mwana unavyopasa kuwa; ni upendo wautii. Baada ya hapo Yesu alitambua kwamba mambo yameiva, hivyo wakatokachumbani na kwenda nje, akiendelea kuongea nao.

MASWALI1. Kwa nini wanafunzi walijaa huzuni na kufadhaika?2. Yesu alisema dawa ya fadhaa zao ni nini?3. Kwa nini sehemu hiyo inatumiwa sana wakati wa mazishi? inatoa msaada

gani?

Page 125: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA614

4. Maneno ya Yesu „Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima: Mtu haji kwa Babaila kwa njia ya mimi‟ ni makubwa na ya maana sana. Kwa nini, hasaukiwaza imani na dini zingine?Zungumza katika kikundi umuhimu wake?

5. Yesu alitoa ahadi gani kuhusu maombi? Eleza msingi wa maombi ya kweli.6. Ni mambo gani mawili yanayowiana na kuwa msingi wa maisha ya Kikristo?7. Eleza faida ya Yesu kuondoka ili Roho Mtakatifu aje8. Roho atafanya kazi ipi muhimu sana kwa Mitume ambayo imekuwa

msaada kwa Wakristo wote wa baadaye ambao hawakumjua walakumsikia Yesu alipokuwa hapo duniani?

15:1-27 Maongezi juu ya Uhusiano wao na Yeye Mzabibu wa kweliIjapokuwa ilionekana kwamba Yesu alikuwa amemaliza maongezi yake,aliendelea kusema na wanafunzi wake, pengine nje karibu na hekalu. Alitakakusisitiza umuhimu wa Utume wao na shabaha yake hasa katika kuzaamatunda. Kufuatana na shabaha hiyo aliwapa misingi ya uzalishaji bora. Katikasehemu iliyofuata aliwajulisha gharama ya utume, na katika sura 16aliwajulisha juu ya utekelezaji wake kwa msaada wa Roho. Hapo nyumaamewadokezea habari ya utume wao (13:20) ndipo akarudia kuutaja tenakatika 17:18; 20:21. Kwa hiyo, iwapo twaweza kuutumia mfano wa Mzibibu namatawi kama kielelezo cha kukaa ndani ya Yesu na kutulia ndani yake, hasaukaaji wetu katika mzabibu unahusu mwito wetu wa kwenda ulimwenguni.

Ilikuwa rahisi kudaka maana ya mfano wa Mzabibu kwa sababu ililimwa sananchini na wengi walijua ulimaji wake. Mashamba ya mizabibu yalionekana kilamahali. Pamoja na hayo, nembo ya taifa la Israeli ilikuwa mzabibu na milangomikubwa ya Hekalu ilipambwa juu na Mzabibu wa dhahabu iliyometameta juani.Katika Agano la Kale Israeli lilitajwa mara kwa mara kwa mfano wa mzabibu nakila mara lilipotajwa kosa lake la kutokutimiza utume wake wa kuwa nuru yaWaMataifa lilisemwa (Isa.49:6; Mwa.l1:1ku). Nabii Isaya (5:1-7) alitumia Zabibukwa kueleza kosa kubwa la Israeli katika kutokumpenda Mungu ijapokuwaMungu alikuwa amelishughulikia sana. (Taz. Yer.2:21; 12:10ku. Eze.15:1-8;17:1-21; 19:10-14; Hos.10:1-2 na hasa Zab.80). Katika Zaburi 80:8ku. mzabibuumechomwa moto na k.16 na k.17 vinataja „mtu wa mkono wako wa kuume‟mhusika na mzabibu huo ulio Israeli. Kosa la Israeli liliendelea katika historiayake yote likafikia upeo katika kumkataa Masihi, Mfalme wao (19:15). Hata hivyo,makusudi ya Mungu hayaanguki chini. Yashikwa na kuendelezwa katika Yulealiyechukua nafasi ya Israeli, Yesu na wanafunzi wake.

k.1 „Mimi ndimi mzabibu wa kweli‟ na Baba yangu ndiye mkulima‟. Hapo tunaomsemo wa mwisho wa aina hiyo wa Yesu, misemo hiyo imekuwa madai yake yakuwa vitu mbalimbali, kama nuru ya ulimwengu, mkate wa uzima, MchungajiMwema n.k. Ila ni hapo tu alipoweka nyongeza „Baba yangu ndiye mkulima‟.

Page 126: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA615

Yesu ni mzabibu wa kweli tofauti na mzabibu, Israeli, utakaoondolewa. Mzabibuni mti ambao kazi yake hasa ni kuzaa matunda. Maua yake ni madogo, ilayanazaa matunda mengi, nayo yakiiva, mti huwa na fahari kwa muda mfupi,ndipo matunda yachumwa, kisha matawi hukatwa mpaka chini. Matundayapatikana kwa uhai wa mzabibu kupitia katika matawi yake.

Yesu alitaja Baba yake na kazi yake muhimu kuhusu uzalishaji wa mzabibu.Zimetajwa kazi mbili. Majira ya baridi mkulima hukata na kuyaondoa matawiyasiyozaa, yale yaliyokauka au yaliyopatwa na ugonjwa, kusudi mengine yapatenafasi nzuri ya kuendelea kuzaa vizuri. (Pengine Yesu alikuwa akimwaza YudaIskariote). Majira ya kuchipua mkulima hushughulikia matawi yazaayo na kukatavitawi vidogovidogo vilivyozidi. Pia mkulima hutumia kisu kikali, na kulikata kilatawi lizaalo, ili lipate kuwa na nguvu zaidi na kuzaa zaidi. Kazi hiyo ya kupogoleani muhimu, lakini inaumiza. Jambo kubwa ni kwamba inafanywa kwa upendo nakisu kimo mkononi mwa mtaalamu afahamuye afanyayo. (Ebr.12:4-11). Pasipokukata na kuondoa matawi yasiyozaa mzabibu haustahili sifa ya kuwa Mzabibuwa kweli.

k.3 Wanafunzi wamekuwa safi kwa sababu uzima wa Mzabibu umewashika, kwakushirikiana na Yesu wamejaliwa kusikia na kupokea maneno yaliyomfunuaMungu Baba.

k.4 Hamna tawi ambalo lenyewe lina uhai ndani yake, kila tawi, yaani kilamuumini budi amtegemee kabisa mzabibu kwa uhai wake na kwa uzalishaji wamatunda. Ni jambo muhimu sana wakae ndani yake na Yeye ndani yao, na Yesuakarudia kusema neno hilo kwa nguvu „kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu‟.Ni juu ya matawi kukaa ndani yake.

k.5-6 Akasisitiza tena uhusiano kati ya kukaa ndani yake na kuzaa matunda„pasipo Mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote‟. Mbele yao ni mawili, wakaendani yake na kuzaa matunda, au wakauke, watupwe, na kuchomwa moto.

Neno linalotawala sehemu hiyo yote ni „kukaa‟ limetumika mara kumi katikamistari kumi ya kwanza. Maana ya kukaa ni kudumisha uhusiano na ushirikianona shina, yaani uhusiano na Bwana Yesu Kristo. Kukaa si kutulia tu, bali nikuushughulikia huo ushirikiano, yasije mambo mengine yakaingia kati na kuletashida. Ni sawa na uhusiano wetu kifamilia, kijamii, kikazi n.k. mtu budi aangaliejinsi asemavyo na atendavyo ili uhusiano wake na mwingine udumishwe nakukua na kuwa mzuri zaidi. Tunaona maendeleo katika kuzaa: k.2 „kila tawilizaalo‟ k.2b „hulisafisha, ili lizidi kuzaa‟ k.5 „huyo huzaa sana‟. Yaani, matunda;matunda zaidi; ndipo matunda mengi.

k.7-8 Hayo matunda ni ya namna gani? Matunda katika maisha ya kuomba„ombeni mtakalo nanyi mtatendewa‟ (k.7) maombi yaliyojengwa juu ya msingiwa utii kwa Neno lake. Matokeo ya kuzaa matunda ni Baba atukuzwe. Kwa

Page 127: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA616

hiyo, kama hatuzai matunda tunamnyima Mungu utukufu wake. Kuzaa ni dalili yakuwa wanafunzi halisi wa Bwana Yesu.

k.9-10 Kukaa ndani yake ni kukaa katika upendo, ila si upendo wa aina yoyote.Ni upendo uleule ulio kati ya Baba na Mwana, na upendo uleule wa Yesu kwawanafunzi wake. Upendo wa ajabu, upendo wa kujitoa mpaka kufa, upendo usiona kipimo. Upendo kati ya Baba na Yesu ni kielelezo cha upendo wa Yesu kwawanafunzi, na kama ambavyo tumeona hapo nyuma, upendo wa namna hiyohuzaa utii wa hiari, utii usiosikia shida, sawa na ule utii wa Yesu kwa Baba namapenzi yake. Kipimo cha upendo wetu ndicho utii wetu.

k.11-12 Je! hayo yote si mzigo kwa waumini? Je! watasikia kulemewa kwakudaiwa upendo na utii wa namna hiyo? La! siyo. Hayo yote ni njia ya kusikiafuraha kubwa, furaha ileile ambayo Bwana Yesu Mwenyewe alikuwa nayo.Furaha yake, kama pendo lake, itakuwa ndani yao na kufanya furaha yao itimie.Furaha ni katika kufanya mapenzi ya Mungu, ni njia ya kusikia uhuru, yaanikutokufungwa katika matakwa ya kibinafsi. Ndipo Yesu akawapa tena amri yakupendana kama Yeye alivyowapenda. Hapo tena twaona Yesu ameunganishapamoja utii na upendo.

k.13-17 Hapo Yesu alifafanua kiini cha upendo, ni upendo ulio tayari kufa kwaajili ya rafiki. Hakutaja kupenda adui kama alivyofanya katika Mathayo 5:43-47kwa sababu hapo alikuwa akiongea na wanafunzi wakati maalumu, karibu nakuondoka kwake. Maneno hayo kwa upande mmoja yalihusu kifo chake. Msingiwa urafiki wao na Yesu ni utii. Ni nini hasa ambayo imewafanya kuwa rafiki zake,ni kwa sababu amewashirikisha mapenzi ya Mungu na siri ya uhusiano wake naBaba, ili waelewe anayofanya. Ni kama upendeleo mkubwa mtu ajue Bwanawake anafanya nini, ni msaada katika kumtii bwana wake. Baadaye Rohoataendelea kuwaelewesha katika yale waliyoshindwa kufahamu Yesu alipokuwapamoja nao (14:26; 16:12-15). Kwa kadiri watakavyojulishwa, ndivyowatakavyosikia kuheshimiwa, na kadiri watakavyosikia kuheshimiwa ndivyowatakavyozidi kufahamu. Kwa kupambanisha na watumwa, mtumwa apaswaamtii bwana wake bila kufahamu shabaha na maana za shughuli zake, hatapengine bila kuelewa shughuli zenyewe.

k.16-17 Ili wasije wakajiona kuwa bora Yesu aliwakumbusha kwamba ni Yeyealiyewachagua si wao waliomchagua Yeye. Upendeleo huo wa kuitwa rafiki zakehauna msingi katika wao wenyewe bali katika Yeye aliyewachagua. Tena Yesualisisitiza kwamba alikuwa na shabaha katika kuwachagua. Ilikuwa waende nakuzaa matunda. Waliwekwa kwa kusudi hilo, hawakuwekwa kwa maisha yastarehe, wala kwa maisha ya kukaa pamoja na kupendana wao kwa wao tu,kama kundi la pekee. Lazima waende kwa watu na kuwatangazia Injili nakuwavuta kwa Kristo. Kazi zao zote zilenge kuwaleta wengine kwa Kristo, ndiyomatunda waliyopaswa kuzaa. Wala wasifanye kazi kwa juujuu, wafanye ilimatunda yapatikanayo yadumu. Matunda hayo yatatokana na maombi yao kwa

Page 128: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA617

Baba katika Jina la Yesu. Wanapolenga kutimiza shabaha hiyo ya kuzaamatunda Baba huwa tayari kabisa kuyajibu maombi yao. Pamoja na matundahayo, tusisahau kwamba tunda la Roho limetajwa katika Gal.5:22 kuwa „upendo,furaha, amani...nk.‟ pia katika Isaya 5:7 matunda ni haki za kijamii n.k. KishaYesu akasisitiza tena jambo la kupendana. Kwa hiyo, katika sehemu hiyo yoteYesu amewaonyesha wanafunzi wake uhusiano uliopasa uwepo kati yake nawao na kati yao wenyewe. Yesu alipokuwa pamoja nao hawakuwa imara,walioneana wivu juu ya yupi kuwa mkubwa miongoni mwao, waligombana waokwa wao, na kwa tabia walitofautiana sana, wengine wakali, wengine wapole,baadhi yao wasemaji, na baadhi wakimya, hivyo ilikuwa vigumu waishi kwaumoja na upendano. Yesu alijua kwamba wakitaka kumshuhudia kwa kweli nakwa nguvu itawapasa wawe na umoja wa kweli. Wataharibu kazi wakikosakufanya kwa moyo mmoja na kwa nia mmoja, yaani wote walipaswa kuvutamakasia kwa pamoja. Kwa hiyo aliwapa amri mpya ya kupendana kama yeyealivyowapenda.

k.18 Yesu aliendelea kuongea na wanafunzi juu ya uhusiano wao na ulimwengukwa sababu wataufanya utume wao katika ulimwengu kama Yesu alivyofanyautume wake ulimwenguni. Ulimwengu, maana yake, ni jumuiya ya wanadamuwaishio kinyume cha Mungu na makusudi yake kwa maisha yao. Yesu hakutakakuwadanganya juu ya matokeo ya kumfuata. Hakuwavuta kwa ahadi za uongo,hapo nyuma alitoboa wazi kwamba kuna gharama katika kumfuata (Lk.9:57-62;14:25-33). Hakutaka washtuke watakapoona watu wanawachukia na kuwapinga,wasije wakakata tamaa. Ni jambo lisiloepukika. Watu wengi walishindwakumpokea Yesu ijapokuwa walikuwa wameona wema na upendo wake, vivyohivyo, watu wengi hawatawapokea, potelea mbali maisha yao ni mazuri kiasi gani.

k.19 Kwa nini imekuwa hivyo? Twaona sababu tatu zimetolewa. Sababu yakwanza imetajwa katika k.19. „wao si wa ulimwengu huu‟ Tabia ya wanadamuwote ni uadui na Mungu (Rum.8:6-8) na hata wanafunzi kabla ya kuchaguliwa naYesu walikuwa sawa na wanadamu wote, ila si sasa. Wamehamishwa kutoka„ulimwengu huu‟ wamezaliwa upya, badala ya kuwa wana wa uasi (Efe.2:1ku.Kol.1:21ku.) wamekuwa „wana‟ na rafiki wa Mungu, wana wa nuru. Kwa hiyo,wamekuwa tofauti na wa-ulimwengu, na kwa sababu hiyo badala ya kupendwawatachukiwa, kama ni wageni si wenyeji.

k.20-21 Sababu nyingine imetajwa kuwa ushirikiano wao na Yesu. Kwa jinsiwalivyomtendea Yeye, ndivyo watakavyowatendea watu wake. Wajiandae kwamateso kama Bwana wao (13:16). Ila si wote watakaowakataa, kwa sababu siwote waliomkataa Yesu (wao ni baadhi yao). Faraja ni kwamba, wakiwakatalia nikwa sababu wamemtambua Yesu ndani yao, si kwa sababu hawakumtambuakuwa ndani yao. Kwa hiyo, kama utengano ulivyotokea kutokana na Yesu naujumbe wake, vivyo hivyo, watu wataendelea kutengana kutokana na wafuasi waYesu na ujumbe wao.

Page 129: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA618

k.22-24 Sababu nyingine imetajwa katika k.22-24 ambayo ni msingi wa sababuzingine zote. Yesu, kwa kuja kwake, alichokoza ile dhambi iliyomo moyoni mwawanadamu na ilionekana wazi kwamba wanadamu kwa jumla hupenda gizakuliko nuru. Watu walisikia maneno ya ajabu na kuona matendo makubwa yaYesu, hata hivyo hawakuwa tayari kutubu na kumfuata. Yesu, nuru yaulimwengu, alileta mwanga mkubwa ulioangaza kwenye maisha ya watu, iliwazione na kuzitubu dhambi zao, lakini itikio lao lilikuwa kuizima Nuru (3:19ku).Yesu alikuja „kumsimulia‟ yaani kumwelezea Mungu kwa wanadamu, kwa hiyokumchukia Yesu kulikuwa sawa na kumchukia Mungu (1:18). Shida kwa upandewa wanadamu ni kwamba wamebaki bila kisingizio kwa dhambi zao. Yesualifunua dhambi pamoja na kuleta tiba yake, ni kwa dawa ya ghali sana dhambiilifidiwa. Tangu kuja kwa Yesu watu hawawezi kujifariji na kujisingizia kwambahawaitambui dhambi wala hawana dawa ya kuitibu. Hamna sababu yoyote yakuwazuia wasitubu. Hakuna anayemlaumu mgonjwa, eti ni mgonjwa, ilamgonjwa akipatiwa dawa za uponyaji, ndipo akazikataa, basi ni haki alaumiwe.

k.25 Chuki ya ulimwengu haizuii makusudi ya Mungu, chuki yake ni bure, maanaYesu alifahamu mambo hayo yametajwa katika Zab.35:19; 69:4 na sasayanatimizwa. Hivyo ulimwengu utaendelea kukemewa na kuonywa na kupewanafasi ya uponyaji.

k.26-27 Lakini itakuwaje atakapoondoka? Wafuasi wake watawezaje kukabiliulimwengu na dhambi zake? Wataweza kwa sababu ni utume wao, wamewekwakuwa chumvi na nuru katika ulimwengu. (Mt.5:11-16). Roho Mtakatifu atajiunganao, na kwa pamoja, watatoa ushuhuda juu ya Yesu na ukombozi wake. Rohoanao utume wake wa kuendeleza utume wa Yesu, ni Roho wa kweli, ambayeYesu atamwomba Baba aje baada ya Yeye kuondoka, kama zawadi kwa Kanisakuliwezesha kuutimiza utume wake. Roho atawashuhudia watu pasipo msaadawa Wakristo. Pia atakuwa pamoja na Wakristo wanapomshuhudia Kristo, ilaWakristo hawatamshuhudia Kristo kweli bila msaada wa Roho. Wanafunziwastahili kumshuhudia Kristo kwa sababu wao wameandamana na Kristo tangualipoanza Huduma yake, watakuwa mashahidi wa kweli wa mambo yotealiyosema na kuyatenda. Sisi wa leo tunayo Roho pamoja na Agano Jipya yenyehabari sahihi za Yesu.

MASWALI1. Yesu alitaka kuwafundisha nini alipotoa mfano wa Yeye kuwa Zabibu wa

kweli, na Baba kuwa mkulima, na wao kuwa matawi?2. Yesu alikuwa na shabaha gani alipowachagua Mitume? na kwa nini

aliwaita rafiki?3. Watatimiza wito wao na kufanikiwa katika utume wao wakiwa watu wa

namna gani?

Page 130: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA619

4. Eleza uhusiano wa wanafunzi na ulimwengu kwa kulingana na Yesu nauhusiano wake na ulimwengu

5. Watasaidiwaje watakapoushuhudia ulimwengu habari za Yesu?

16:1-33 Maongezi juu ya shida watakazozipata na huduma ya RohoMtakatifuk.1 Yesu aliendelea kutoa tahadhari juu ya mateso kwa sababu alihofu kwambawatachukizwa kiasi cha kumkana wakati watakapoteswa vikali. Tukilinganisha nak.33 alitaka wakati wote wawe na amani mioyoni mwao, amani kati ya dhiki, siamani bila dhiki.

k.2 Ndipo Yesu aliwaambia aina ya mateso watakayopata. Mateso si mchezo,yatakuwa mazito sana, watatengwa na sinagogi, huenda watatolewa kwa nguvuna baadhi yao watauawa. Yatatoka wapi mateso hayo makali? Yatatoka kwawatu wa dini, watu waheshimiwa, si kwa wahuni. Tena yatafanywa na kundirasmi, si na mtu mmoja mmoja mlokole. Yatafanywa katika Jina la Mungu, kamaibada (ila vifo vyao ni ibada kwa Mungu). Kwa hiyo itakuwa vigumu kuyaelewakwa kuwa sababu za watesi ni njema machoni pao, lakini sababu hizo njemahazihalalishi matendo yao mabaya. Wafanyao wamedanganywa. Kamayangalifanywa na wabaya na wahuni, yangalieleweka na kuvumilika.(Tukumbuke kwamba mamilioni ya Wakristo wameuawa katika karne hii ya 20,katika Jina la Mungu, katika Jina la Marx, katika Jina la Allah, pamoja na sababuzingine nyingi).

k.3 Kwa nini yatokee kwa watu wa dini? Kwa sababu hawakumjua Yesu walaMungu, Baba yake (14:7). Wale wasiomjua Yesu na Baba huwachukia walewanaomjua na kumfuata (15:18-21). Kuwatesa Wakristo ni kumtesa Yeye,„mbona waniudhi Mimi‟ ni maneno ya Yesu kwa Sauli alipomtokea njiani kwendaDameski ili awakamate Wakristo (Mdo.9:4ku). Upinzani hasa ni juu ya Yesu.

k.4 Yesu hakutaka washtuke mambo hayo yatakapotokea, maanawatakapoteswa vikali, watajaribiwa kumkana. Ila wakikumbuka jinsialivyowaonya watasaidiwa kuamini kwamba Yeye anajua yanayowapata nahayawi nje ya ujuzi na utawala wake. Yesu alitaka wafahamu kwamba matesoyatakuwa kawaida ya maisha yao, si kitu kigeni, ambacho kitatokea mara chachetu.k.4b-7 Yesu hakuwaambia mengi juu ya mateso wakati wa nyuma, kwa sababualikuwa pamoja nao na kuwakinga na chuki za wapinzani kwa kuzipokeamwenyewe.

Inaonekana maneno „hakuna mmoja wenu aniulizaye, Unakwendapi?‟yanabishia maneno ya 13:36 na 14:5, kwa sababu Petro na Tomasowalimwuliza swali hilo. Huenda hapo nyuma walimwuliza kwa juujuu bilakutaka kujua hasa anakwenda wapi na maana yake Kwake na kwao.

Page 131: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA620

Wamemezwa kabisa katika huzuni kubwa juu ya hali ya kuachwa, bilakumtafakari Yesu na jinsi kuondoka kunavyomgusa Yeye. Ndipo Yesu akasemakwao neno la ajabu sana, ambalo ni kama mzaha kwao. „Yafaa ninyi miminiondoke‟. Kumbe ni faida kuachwa!! Kwa nini ni faida kwao? si hasara tupu tu!La, hata kidogo. Kwa kuondoka kwake watapata mwingine, Msaidizi, kuchukuamahali pake (14:16, 26; 15:26). Si kwamba Yeye na Roho hawawezi kufanyahuduma pamoja, ila katika Maandiko ilitabiriwa kwamba Roho ataleta nguvumpya za dahari mpya, yaani Ufalme wa Mungu utakuja kwa nguvu katikaulimwengu na watu watazionja nguvu zake (Isa.11:1-10; 32:14-18; 42:1-4; 44:1-5; Eze.11:17-20; 36:24-27; 37:1-14; Yoe.2:28-32; Mdo.2:17ku). Lakini hali hiyompya haitawezekana mpaka Yesu afe, na kufufuka, na kutukuzwa. Kwa hiyo,kuondoka kwa Yesu ni zaidi ya kuondoka mahali fulani, hasa ni jambo la kiroholiletalo uwezekano wa Huduma ya Roho. Mungu katika Utatu wa Baba, Mwana,Roho yuko wakati wote, ila kila mmoja wao amewekewa fungu lake la kufanya.Kwa hiyo Nyakati za Roho ni bora zaidi, wengi zaidi watavutwa kumwaminiKristo. Hali akijua hayo Yesu aliweza kusema bila wasiwasi kwamba ni afadhaliaondoke ili Roho aje, na bila shaka baadaye wanafunzi waliunga mkono manenohayo, ambayo wakati yaliposemwa yalionekana kama mzaha na dharau kwahuzuni zao. Huenda sisi wa leo twaweza kuwaza „eti ningalikuwepo Galilaya nakumwona Yesu akinyamazisha tufani, au ningalimsikia akitoa hotuba yamlimani...ningemwamini na kumfuata vizuri zaidi‟ ila maneno ya Yesu, yafaayafikiriwe kama ni kemeo kwa mawazo kama hayo.

k.8-11 Yesu aliendelea kuongea nao na kuwaeleza uhusiano wa Roho naulimwengu katika kuuhakikisha juu ya mambo makubwa matatu - dhambi, haki,na hukumu. Neno „kuhakikisha‟ lina maana kwamba Roho atauonyeshaulimwengu jinsi unavyokosa kuhusu dhambi yake, haki yake, na hukumu yake.Ni kama kuwaaibisha watu hata waitambue hatia yao, ili watakapofahamumakosa yao wayatubu. Huduma hiyo ni kwa wasiomwamini Kristo.

Kuhusu dhambi, Roho atawasaidia watu kutambua ni wenye dhambi, na ubayawa dhambi yao, na kiini chake ni uasi kwa Mungu. Kazi hiyo ya Roho ni kazi yaneema. Watu wakielewa dhambi ni nini machoni mwa Mungu, na jinsiilivyomgharimu Yesu maisha yake, basi, watasaidiwa sana wakimruhusu Rohoawafunulie hayo.

Kuhusu haki, Roho atawasaidia watu wa ulimwengu watambue kwamba hakiyao haitoshi machoni mwa Mungu. Yesu alidhihirisha utupu wa mambo mengiambayo waliyoyafanya katika hali ya kudhani kwamba wanafanya haki. KuhaniMkuu alidhani kwamba alishauri tendo la haki kabisa alipoongoza wakuu kumwuaYesu ili taifa lao na hekalu lao na torati yao vihifadhiwe (11:50). Kumbe hakihiyo ilikuwa kosa kubwa. Yesu atakapoondoka ni nani atakayewafunulia watuvisingizio vyao vya hila?. Ni kazi ya Roho, kwa sababu Yesu hatakuwepo. Maishaya haki ya wanafunzi pia yatagusa watu na kuwahakikishia juu ya udhalimu wao.Ni dhahiri kwamba haki ya Yesu ndiyo

Page 132: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA621

haki ya kweli ikubalikayo na Mungu, kwa sababu alirudi kwenye Utukufu wakepamoja na Baba.

Kuhusu hukumu: Mara nyingi uamuzi wa ulimwengu si wa kweli na hukumu zakezimepotoka, zahusika na Shetani aliye mwongo tangu mwanzo (8:42-47).Shetani ameishahukumiwa pale Msalabani (12:31; 14:30) Kristo amemshinda.Mfano wa hukumu iliyopotoka ni ile iliyompata Yesu Mwenyewe, Yeye asiyekuwana dhambi alihukumiwa kuwa mhalifu wa hali ya juu. Tumeishasoma hapo juukwamba wale watakapowaua wafuasi wa Yesu watadhani kwambawanamtendea Mungu ibada. Ni kwa njia gani ulimwengu utaweza kutambuamakosa yake katika hukumu? Roho atauhakikisha ulimwengu juu yake.

Kwa hiyo, yafaa Yesu aende ili Roho aje, kwa sababu Roho atafanya kazi hizozote katika dhamiri na mioyoni mwa wasioamini na kuwatayarisha kulipokeaNeno la Injili litakapohubiriwa.

k.12-15 Hapo tumepewa habari jinsi ufunuo wa Mungu ulioletwa na Yesuutakavyotimizwa katika huduma ya Roho Mtakatifu.

k.13 Katika 14:26 tumeambiwa huduma mojawapo ya Roho itakuwakuwakumbusha Mitume yote Yesu aliyowaambia na kuwaelimisha juu yake. Je!itakuwaje kwa yale ambayo Yesu alishindwa kuwaambia kwa sababu ya hali yaoya huzuni pamoja na hali yao ya kuwa wazito wa kuelewa kwamba ni lazimaMasihi auawe? Hali hizo zilimzuia Yesu asiwafunulie mengine wakati huo. NdipoYesu akasema kwamba huduma ya maana sana ya Roho ni kuwafunulia hayomengine baada ya Yeye kuondoka, wakati ambapo wataweza kuyapokea. Rohoaitwa Roho wa kweli, Yesu Mwenyewe alisema Mimi ni Njia, Kweli, na Uzima(14:6) kwa hiyo, Roho atanena mambo ya Yesu kwa hao Mitume. Kwa hiyo,hatawaongoza ili wapate ujuzi wa kipekee, ujuzi kwa wachache tu, la, ila ni ujuzikuhusu ufunuo wa Mungu ulioletwa na Yesu. Hamna ufunuo nje ya Yesu, ufunuowote humzungukia Yeye na Yeye huwa kiini chake na yote huishia Kwake(Ebr.1:1-4). Kwa hiyo Roho haleti ufunuo mpya ila ayapanua yale yaliyoletwa nakuwaelimisha Mitume maana yake. Kama ambavyo Yesu kamwe hakusema walahakutenda lolote kwa shauri lake mwenyewe, ila yale tu ya Baba (3:34-35;5:19-20; 7:16-18; 8:26-29, 42-43; 12:47-50; 14:10) vivyo hivyo na Roho, asemayale tu asikiayo kwa Yesu. Hutegemea kabisa Yesu na Baba yake, na kwa njiahiyo, umoja wa Mungu na ufunuo sahihi ulioletwa na Yesu, hulindwa.

„na mambo yajayo atawapasha habari zake‟ Mambo hayo ni mambo gani?Hayawezi kuwa kufa na kufufuka kwa Yesu, kwa sababu matukio hayo yatatokeahivi karibuni na kabla ya Kushuka kwa Roho. Ila mambo yajayo yaweza kuhusumaana na umuhimu wa matukio hayo, na yatakayofuata matukio hayo makubwa.Kutokana na huduma ya Roho Mitume na wenzao waliwezeshwa kuandikaAgano Jipya, ambalo ndani yake tumepewa habari za

Page 133: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA622

matukio yenyewe katika Injili nne pamoja na tafsiri yake katika Nyaraka. Hivyo,Agano Jipya laweza kutegemewa kabisa kuwa sahihi kwa pande zote mbili,habari zenyewe, pamoja na tafsiri ya maana ya matukio, na hivyo kuwa kanunikwa waumini wa vizazi vyote.

k.14-15 Roho atamtukuza Yesu kama Yesu alivyomtukuza Baba. Atayatwaa yaYesu na kuwapasha habari hayo yote ambayo Baba alikuwa amempa Yesu(5:19-23).Kwa hiyo, wale ambao watafaidi hiyo Huduma ya Roho ni Mitume kwa sababumaneno yalisemwa kwao hasa (k.12, 14:26; 15:27). Kwa upande wa sisi wa leohuduma ya Roho kama Mwalimu ni katika kutuongoza kuyafahamu Maandiko nakuyatafsiri kwa maisha yetu na mazingira ya wakati huo. Ni huduma ya maanasana kwa sababu kwa Neno la Mungu tunajengwa kiroho. Katika sehemu hiyotunaonywa juu ya wale ambao hutokea mara kwa mara na kudai kwambawamepewa ufunuo mpya. Tena Roho hajiinui wakati wowote, kazi zake nikumtukuza Yesu, si Yeye. Si vizuri kuyatukuza matukio fulani ya Roho kama nimakubwa kuliko matendo makuu ya Yesu katika Kufa, Kufufuka, na Kupaa Kwake.

k.16-22 Wanafunzi walitatizwa na maneno ya Yesu „bado kitambo kidogo nanyihamnioni; na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona‟. Katika mawazo yaohakuna nafasi kwa wazo la Masihi atakayekufa, na kufufuka, kwa hiyo, walibakiwakisemezana wakitafuta maana ya maneno „kitambo kidogo‟. Ndipo Yesuakajiingiza katika maulizano yao na kuwafasiria maana yake. Inaonekanaalikuwa akisema juu ya muda ule kati ya Kufa na Kufufuka Kwake. Alitaja huzuniyao na furaha ya ulimwengu katika ule muda wa Kufa Kwake na kabla yaKufufuka Kwake. Watu watafurahi sana kwa sababu wamefaulu kumwondoaYesu na kunyamazisha sauti yake iliyowashtaki kwa dhambi zao, huku wanafunziwatakuwa wamehuzunika sana kwa kufiwa naye. Ndipo alitaja furaha yaoatakapofufuka, furaha itakayoendelea baada ya kuwaacha kabisa wakati waKupaa. Alitoa mfano wa huzuni na furaha ya mwanamke katika kuzaa mtoto(Isa.26:16-21) na kusema „ninyi hivi sasa mna huzuni lakini....‟(k.22)

k.23-24 Jambo linalofungamana na Kufufuka Kwake ni hali mpya ya maombi.Maneno mawili tofauti yametumika; katika k.23a na 26b maana ya neno ni„kuuliza swali‟ na neno lingine katika 23b,24,26a lina maana ya „kuomba kitu aujambo‟ hasa kuhusu mdogo kumwomba mkubwa. Kwa hiyo, kwa ufunuo waRoho na kutokana na Ufufuo wa Yesu, wanafunzi hawatahitaji tena kuulizamaswali. Pia kwa sababu watamtambua Yesu kuwa Mwana Mpendwa wa Babawataomba katika Jina lake, yaani kwa Yule aliye sawa kabisa na Baba na katikamwanga wa kufahamu mapenzi yake. Hapo nyuma wamemwona kamamwanadamu na kumwomba kama ni mwanadamu. Yesu atakapofufukawatamwendea Baba katika Jina lake na kumtegemea kuwa mwombezi wao. Kwahali hizo mpya furaha yao itazidi.

Page 134: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA623

k.25-28 Hapo nyuma wanafunzi wake walishindwa kuelewa mengiyaliyoyasemwa na Yesu, haina maana kwamba kila wakati alitumia mithalialiposema nao, ila yalikuwa mafumbo kwao. Walishindwa kuelewa maana yakehalisi, walishindwa kuelewa maana ya „saa ile‟ ambayo tangu mwanzo alikuwaameitaja. Saa ile itakapowadia Yeye atakufa na kufufuka ndipo dahari mpyaitapambazuka, dahari ya huduma ya Roho Mtakatifu. Itakapopambazuka daharihiyo, baada ya Kufufuka Kwake, Yesu atasema nao waziwazi, naowatamwelewa, hasa anaposema juu ya Baba. Baada ya Kufufuka kwake nakabla ya Kupaa Kwake aliwazungumzia mambo kuhusu Ufalme wa Mungu(Mdo.1:3) tazama Mdo.1:1 „aliyoanza Yesu‟ ndipo atakapoondoka kabisa Rohoataendelea kuwafundisha kama ambavyo tuliambiwa (16:12-15).Jambo hilo litagusa maombi yao, wataweza kumwendea Mungu kama Baba, nakusema naye moja kwa moja, katika Jina la Yesu. Baba awapenda kwa sababuwamempenda Mwana wake na kuamini kwamba alitoka kwake. Heshima kubwakwa wafuasi wa Yesu ni kuwa na upendeleo huo wa kumwomba Baba. Hivyo,wanao uhusiano mpya na Baba.

k.28 Yesu alisema kwa uhakika wa kushinda, ijapokuwa bado hajakamatwa n.k.Alijua alipotoka na aendapo, ametoka kwa Baba na anarudi kwa Baba. Mamboyake yote humzungukia Baba.Katika k.27,28 na k.30 maneno „kutoka kwa Baba‟ yametumika. Katika k.27 Yesualisema kwamba wanafunzi wamesadiki kwamba Yeye alitoka kwa Baba nakatika k.30 wao walikiri kwamba walisadiki ya kuwa alitoka kwa Mungu. Ila kunamaana tatu katika maneno hayo: k.27 „nalitoka kwa Baba‟ kama yule aliyetumwana Baba mwenye mamlaka na utume wake. k.28 „alitoka kwa Baba‟ kama yulemwenye asili moja na Baba, aliyemfunua Baba; k.30 „alitoka kwa Baba‟ manenoya wanafunzi juu ya kutengwa kwake na Baba, maanaalipokuwa nao alitengwa na Baba, na kwa maneno hayo walikiri kwamba alikuwaameishi na Baba kabla ya hapo.

k.29-33 Wanafunzi walikuwa wametiwa moyo na hayo aliyoyasema Yesu,wamedhani kwamba sasa wanaelewa vizuri na kuamini kweli. Ila Yesualiwakemea kwa hali yao ya kujiamini, kujiamini ni hatari kubwa. Wamefanana naaskari wapya waliovaa nguo rasmi za kijeshi na kujua utaratibu wa kwata nagwaride ila bado hawajaingia vita yenyewe. Kuna tofauti sana kati ya askari mpyana yule ambaye ameisha kupigana vitani. Baada ya masaa machache imani yaoitatikiswa na wao wenyewe watatawanyika na kumwacha Yesu peke yake.

Ijapokuwa watamwacha Yesu atafahamu nafasini mwake kwamba Baba yupamoja naye na ya kwamba atampitisha katika saa za giza zito na taabu nyingi.Pamoja na hayo, alijua kwa uhakika kwamba atashinda. Neno la mwisho si kwaShetani, wala si kwa ulimwengu, bali ni kwa Baba na Yeye aliyetumwa na Baba.Kwa utii wake mauti itashindwa, na enzi zote za giza na uovu na dhambizitanyonywa nguvu zake.

Page 135: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA624

Baada ya kuteleza kwa muda mfupi wanafunzi nao wataushiriki ushindi wake,watamrudia Siku ya Ufufuo, ndipo atawatuma katika nguvu za Roho Mtakatifu iliwaendeleze Utume ambao ulikuwa wake na sasa ni wao wa kuitangaza Injilikotekote ulimwenguni. Hivyo, wajipe moyo, watajua amani yake mioyoni mwao,na Yeye atakuwa nao daima (Mt.28:20).

MASWALI1. Yesu aliwaonya wanafunzi wajiandae kwa kupata nini?2. Roho Mtakatifu anafanya kazi gani katika ulimwengu?3. Roho Mtakatifu alikuwa na kazi gani maalum kwa wanafunzi?4. Kwa nini twaweza kutegemea Injili na Nyaraka kuwa Maandiko ya kweli?5. Mara kwa mara watu hujitokeza na kusema kwamba wamefunuliwa jambo

fulani jipya? Utawapima kwa njia gani?6. Eleza ni kwa sababu gani maombi yao yatajibiwa baadaye?7. Waonaje uthabiti wa Yesu usiku ule kabla ya kukabili Kifo chake

Msalabani? Uthabiti huo ulitokana na nini hasa?

17:1-26 Maongezi ya Yesu na Baba yake

Maombi hayo yameitwa Maombi ya Kuhani wetu mkuu, ila tunaposema hivi, nimaombi yaliyoombwa na Yesu alipokuwa angali hapo duniani. Kwa kawaidawazo la Yesu kuwa Kuhani wetu mkuu lahusu kazi yake mbinguni kwa ajili yetusasa. Wengine wamependa kuyaita Maombi ya Yesu ya kujiweka wakfu kuwadhabihu ya dhambi. Pengine yatosha kuyaita Maombi ya Yesu. Katika maombihayo tumefikia kilele kimojawapo kikubwa katika ufunuo wa Yesu. Alikuwaameishaongea na wanafunzi wake, ndipo akamgeukia Baba na kuongea naye,kwa ajili yake Mwenyewe (1-5) kwa ajili ya wanafunzi wake (6-19) kisha kwa ajiliya waumini wote wa baadaye (20-26). Ni kama kuagana na wanafunzi wake kwanjia ya maombi. Pengine walipotoka nje wakasimama chini ya kivuli cha ukutawa Yerusalemu kabla ya kwenda bustani ya Gethsemane. Katika 16:33 alikuwaametamka neno la ushindi, na wakati huo alikuwa akitazamia kwa shaukukwenda kukabili Kifo chake na magumu yote kama kukamatwa, kuhukumiwa,kushutumiwa n.k. Ijapokuwa rohoni alisononeka kwa ajili ya hayo yote, ndanikabisa alijaa furaha ya kuyatimiza mapenzi ya Baba yake ya kuukomboaulimwengu, na katika maombi hayo twaona msingi wa mapenzi hayo ya Babani kuwapa wanadamu uzima wa milele kwa njia ya kumjua Yeye na kumwamini.Alijua kwamba matokeo ya baadaye kama mafanikio ya Injili kupelekwaulimwenguni, na watu kuletwa kwenye kumwamini, yamo mikononi mwawanafunzi wake, wale waliopo na wale watakaowafuata. Alijua kwamba watakatatamaa watakapomwona amekamatwa na kuuawa, watapata shida sana kwa sikuzile tatu kabla hajafufuka, kwa hiyo, alifanya jambo la maana sana, alijitoakuwaombea (ling. neno lake kwa Petro Lk.22:31-32). Ilikuwa saa ya pekee katikamaisha yake, na saa ya pekee katika maisha yao, na saa ya

Page 136: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA625

pekee katika maisha ya ulimwengu, saa ya ukombozi wake. Yesu alikaribishasaa hii kwa maombi. Kwa nini aliomba wakati huo, na kwa nini Roho Mtakatifualiona vema tupate habari zake? Twajifunza kwamba Yesu hakufanya mamboyake kama roboti, hakuweza kujifariji na kusema haidhuru mwisho utakuja tu.Kujitoa juzi na jana hakutoshi, Yesu alihitaji kujitoa upya kwa Baba ili atimizemapenzi yake kikamilifu, lilikuwa jambo jipya na utii wa kipekee kwa Yesu kujitoakufa kifo cha mwenye dhambi. Ilimbidi afanye juu chini ili akabili shida kubwa iliyombele yake, na kufaulu katika kutimiza shabaha yake, na kwa sababu hiyo,aliomba. Tena hakujiombea tu, katika mambo yake aliwakumbuka wanafunziwake, wala si hao tu, bali wote watakaowafuata na kumwamini baadaye, ambaobaadhi yao ni sisi wa leo. Kwa hiyo, hata wao, na hata sisi, tulikumbatiwa katikamaombi hayo ya Yesu kwa Babaake. Jambo hilo lingetutia moyo sana.Twawajibika kuitika wito wake ila ni vema kukumbuka kwamba hayo yoteyameingizwa katika makusudi makuu ya Mungu. Yesu ametuombea. Hivyo,utume wake utatimizwa na utume wetu pia. Tu wa thamani sana kwa Mungu.

k.1-5 Yesu alijiombea mwenyewek.1a Maneno ya kwanza yanaonyesha kwamba maombi hayo hayawi hewani,bali yahusika na yote yaliyotangulia katika Injili hiyo na hasa maongezi ya Yesuna wanafunzi wake ya Sura 14 mpaka Sura 16. Katika Injili tatu tunayo Maombiya Yesu pale Gethsemane. Je! maombi hayo na yale ya Gethsemane nimamoja? Huenda, siyo. Ni vigumu kufikiri kwamba Yesu aliomba mara moja tuwakati huo.Alianza na neno „Baba‟ neno rahisi lililotumika na watoto kwa baba zao. Ilikuwadesturi ya Yesu kutumia neno hilo na lilionyesha jinsi alivyousikia ukaribu sanawa kimapenzi na Baba (jambo lililosisitizwa katika Injili hiyo) na hali yakumtumaini na kumtegemea kabisa wakati huo mgumu. Katika k.11 alisema„Baba Mtakatifu‟ na katika k.25 „Baba mwenye haki‟.

Ndipo Yesu akaendelea „saa imekwisha kufika‟. Saa ambayo hapo nyuma ilikuwabado haijafika, sasa imefika kabisa. Ila Yesu hakukaribia saa hii katika hali yakufikiri yote ni ajali tu. Itikio lake kwa saa hii kufika lilikuwa kuomba, aliomba hasakwa sababu alijua saa hiyo imefika. Ni saa iliyowekwa na Mungu, saa ya mapenziya Mungu kufanywa, na katika saa hii ngumu twajifunza ni mambo ganiyaliyokuwemo moyoni mwake.

Alijiombea nini? Alimwomba Baba „Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako nayeakutukuze wewe‟ (k.1) tena „Baba unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu uleniliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako‟ (k.5). Alitaka Babaamtukuze na kumvika ule utukufu aliokuwa nao hapo mwanzo na kumrudishakwenye fahari yake ya asili. Alipofanyika mwili aliweka kando huo utukufu nakuiacha nyuma fahari yake, hata kabla ya kuishi hapo duniani alitoa gharamahiyo (Flp.2:5-8). Ila aliporudi kwa Baba si kwamba mambo yote ya kufanyikamwili yalibatalishwa, la, hakuuacha mwili wake kaburini, mwili ukafufuka kuwa

Page 137: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA626

mwili wa utukufu, mwili wenye uwezo mpya, na katika mwili huo wa utukufuakapaa na kurudi kwa Babaye. Yesu alijua kwamba anapotukuzwa Yeye, naBaba pia hutukuzwa, kwa kuwa ni umoja naye na ya kwamba Yeye ndiye ufunuohalisi wa Baba. Kutukuzwa kutatokea pale Msalabani, tabia zote njema za Babana Mwana zitadhihirika. Itaonekana wazi kwamba Mungu ni Mtakatifu, yukinyume kabisa cha dhambi, hawezi kamwe kuridhiana nayo. Itaonekana wazikwamba Mungu ni Pendo, kwa sababu alimtoa Mwana wake kuwa dhabihu yakufidia dhambi, na Mwana alijitoa maisha yake ili awe ile fidia ya dhambi.Itaonekana wazi kwamba Mungu ni wa haki, ambaye aliihukumu dhambi, hatailipowekwa juu ya Mwana wake, asiyekuwa na dhambi. Itaonekana wazi kwambaMungu ni mwenye Rehema, kwa sababu ya kuwarehemu wanadamu wenyedhambi, walio dhaifu, wasio na nguvu ya kujiokoa. Mungu alisikitikia hali yetuakamtuma Mwana wake mpendwa, na Mwana alijitoa maisha mpaka kufa, ilitutolewe katika shida zetu. Tukiuliza utukufu ni nini, jibu moja ni, kuangaza kwanje tabia njema zilizo ndani, za asili. Utukufu wa Mungu ni tabia zake za upendo,utakatifu, haki, na rehema. Tabia hizo zilidhihirika kabisa Yesu alipokufaMsalabani. Kwa njia ya kumtukuza Baba (12:28) Yeye naye atatukuzwa.

k.2 Yesu atamtukuza Baba kwa njia ya kuwapatia wanadamu uzima wa milele.Kwa pamoja Baba na Mwana walikuwa na mzigo wa kuwapatia wenye dhambimsamaha wa dhambi na uzima wa milele, kwa njia ya kifo cha Yesu kwa ajili yao.Ila kabla ya Yesu kuweza kutoa hicho kipawa cha uzima, Yeye, kabla ya kujaduniani, alipewa na Baba mamlaka juu ya wote wenye mwili kwa sababu ya utiiwake kwa mapenzi hayo ya Babake. Kwa mamlaka hiyo Yesu aliweza kuwatumawanafunzi wake ulimwenguni mwote ili wahubiri Injili ya msamaha wa dhambi naya uzima wa milele kwa wote wanaotubu na kumwamini Yesu (Mt.28:18-20). Kwasababu Yesu ni Bwana wa wote anayo mamlaka kutoa uzima kwa wote ila kwaukaidi wao wengine hawataupata. Sikitiko kubwa ni kwamba itikio la wengine kwarehema za Mungu si zuri, wachagua kutokuamini. Wanaoupokea wamejaliwakuamini. Hivyo, Yesu alifahamu kwamba hatoi maisha yake bure.

k.3 Huo uzima wa milele ni nini hasa? Yesu aliueleza hivi: „Ni kumjua Mungu wapekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma‟. Ni ujuzi wa kibinafsi, si ujuzi wakujua mambo kadhaa juu ya Yesu kama alizaliwa wapi, alifanya nini n.k. bali nikumjua kibinafsi kwa kujihusisha naye kama mtu amjuavyo rafiki yake (2Tim.1:12 „kwa maana namjua Yeye niliyemwamini‟). Kwa hiyo, ni ujuzi upatikanaokwa njia ya kushirikiana na Yesu na Baba yake kwa njia ya maombi, kwakuongozwa na Neno lake na kwa kumtii. Ni ujuzi unaokua kadiri mtu anavyozidikushirikiana naye katika uhusiano mwema wa kumpenda na kumtii. Kwa hiyo,uzima wa milele si kitu fulani, wala hauhusu muda wa kuishi na kuendelea kuishibaada ya kufa tu. Hasa uzima wa milele ni hali bora ya kuishi, ni maisha mapyaambayo mtu anaanza kuishi wakati huu wa sasa (1 Yoh.5:12). Kwa sababu Yesuyu hai uhusiano haukatiki wakati wa Kufa bali unaendelea na

Page 138: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA627

mtu huzidi kushirikiana naye hata baada ya kufa. Zaidi ni kumjua na kushirikianana Yule wa Umilele kuliko kuwa na maisha yanayoendelea tu. Yahusu uborakuliko kitambo cha maisha. Kuishi maisha ya namna hiyo ndiyo shabaha yakuishi hapa duniani. Kumjua Mungu hakuwezi kutengwa na kumjua Mwana, kwasababu ni Mwana aliyemfunua Mungu. Ujuzi huo si wa kiakili wala si wa habaritu. Ni ujuzi tuupatao kwa njia ya ushirikiano.

k.4 Yesu alishuhudia kwamba alikuwa ameimaliza ile kazi ambayo Baba yakealikuwa amempa kuifanya. Ilikuwa kazi bayana ya kuwapatia watu uzima wamilele (Yn.3:16) na kwa ajili yake alikubali mipaka iliyowekwa. Hakwenda kwanchi nyingine, hakuoa, hakuwa mzazi na kujua ulezi wa watoto, hakujua hali zakuishi miaka ya kati au ya uzee. Hakuwahudumia watu wengi. Hata hivyo,aliimaliza ile kazi aliyopewa na Baba, na kwa sababu hiyo kazi yake ilikuwanjema, kamili, na timilifu. Ndiyo sababu Msalabani alitoa tangazo rasmi„Imekwisha‟ ila kuimaliza kulimgharimia maisha yake.

k.5 Akarudia kumwomba Baba amtukuze kwa kumrudisha pale alipokuwapokabla ya kuja duniani, awe ndani yake, pale alipotoka, ndipo atakuwaametukuzwa, wote watafahamu kwamba alitoka kwa Baba naye anarudi kwaBaba. Alikuwa na uthabiti kwamba atapitishwa salama katika dhoruba kali iliyombele yake na kufika ng‟ambo ya pili kwa Babake. Uthabiti huo ulitokana na Yeyekukaza nia yake kufanya yote aliyopangiwa na Baba. Msukumo wake ulikuwakufanya mapenzi ya Baba na kumtukuza.

k.6-19 Yesu aliwaombea wanafunzi wakeHao wanafunzi ni dhihirisho kwamba kazi yake imetimizwa na ni kwa ajili yaoalijiweka wakfu, ili wao nao watakaswe (k.19). Makusudi ya Mungu katikaukombozi yalilenga shirika hilo dogo ambalo hivi karibuni watamwacha nakumkana na kutawanyika kama kondoo walioshtushwa. Ila Yesu alifahamukwamba hayo si mwisho wa mambo, makusudi ya Mungu yataendelezwa na hao,wao watakuwa mbegu itakayosababisha mavuno makubwa yatakayoonekanasiku ya mwisho. Yesu amemaliza kazi yake katika kutokeza kundi hiloulimwenguni, kundi la wanafunzi waaminifu wa Masihi. Yesu ameunda shirikahilo, Kanisa, kutoka ulimwenguni.

Kwa nini anawaombea? Maombi hayo yanatuonyesha mzigo wake kwa ajili yao.Yana sehemu mbili (1) k.6-10 iliyo na maelezo juu ya hao wanafunzi ambaoanawaombea (2) k.11-19 iliyo na maombi mbalimbali kwa ajili yao.

k.6 Katika maelezo yake amewataja kuwa mali ya Babake „walikuwa wako‟ (k.2;6:37) hata kabla ya huduma ya Yesu. Tena ni mali yake „ukanipa Mimi‟ (k.6) nakatika k.10 „na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu‟ (5:23). Babana Mwana wamewiana katika jambo hilo. Yesu amewafunulia yote yamhusuyoMungu, tabia na mapenzi yake. Baba amewatoa katika ulimwengu na kumpaMwanawe. Walikuwa katika ulimwengu wa uasi, hawakuwa na uzuri

Page 139: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA628

au hali njema ndani yao iliyosababisha Baba awatoe katika ulimwengu, ilaalipenda kufanya hivyo, hata hivyo, walikuwa wamelishika neno lake, wamejitoakwa Yesu Masihi, si kwamba wamekuwa bila kosa ila wamemwamini na kumtiikinyume cha walimwengu waliokataa kumwamini na kumtii.

k.7-8 Hao wanafunzi wamejua nini? Iwapo walikuwa na upungufu mwingi katikaufahamu wao kumhusu Yesu, hata bado hawajaelewa Yesu ni Masihiatakayekufa kwa dhambi za ulimwengu, hata hivyo walishika kweli moja yamsingi ya kuwa Yesu haelezwi mbali na Baba yake. Walijua hakika ametoka kwaBaba na ya kwamba alitumwa na Baba. Waliyapokea maneno ya Yesu kuwamaneno ya Mungu, kwa sababu Yesu alisema yale tu ambayo Baba alimpakuyasema. Kwa hiyo, hata ikiwa walijaliwa neema ya Mungu kwa kuwawezeshakumwamini Kristo, wao wenyewe waliyapokea na kuyasadiki maneno yake.

k.9 Iwapo upendo wa Baba ni mpana sana na alipenda sana ulimwenguuokolewe, kiasi cha kumtuma Mwana wake kuwa Mwokozi wake (3:16; 4:42)hata hivyo, katika maombi Yesu aliwabainisha wanafunzi na walimwengu, ilakubainishwa huku si kwa namna ya udikteta. Sababu ya kuwatofautisha nawalimwengu ni kwamba wanafunzi ni mali ya Baba „kwa kuwa hao ni wako‟.

k.10 Walio wa Baba ni mali ya Yesu pia (5:23). Yesu alikiri kwamba Yeyeamepata kutukuzwa kwa njia yao. Ni neno la ajabu tukifikiri jinsi ambavyo mpakahapa wamekosa kuyaelewa mengi na ufahamu wao hautapanuka mpakabaadaye Atakapofufuka na Kupaa na Roho kuwaelewesha. TunapomwaminiKristo kuwa Mwokozi wetu twathibitisha ukweli wa matendo yake makuu na Yeyehuadhimishwa. Yeye asiye na haja ya kitu chochote aweza kutukuzwa kwa utiina utumishi wetu.

k.11-17 Yesu aliwaombea wanafunzi mambo kadhaHivi karibuni yatatokea mabadiliko makubwa katika uhusiano wao na Yeye. Yeyealisema „simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami najakwako‟. Yeye hatakuwapo ulimwenguni, wao watakuwapo ulimwenguni, namabadiliko hayo yatawaleta kwenye upeo wa hatari. Hatakuwapo kwa mudamfupi kati ya Siku ya Kusulibiwa hadi Siku ya Kufufuka ndipo baada ya Kupaahataonekana tena.

k.11-12 Alimwomba „Baba Mtakatifu‟ akitayarisha njia kwa maneno yake yak.17-20 juu ya Yeye kujiweka wakfu na wanafunzi kutakaswa. Msingi wa mambohayo ni katika Utakatifu wa Baba (Law.11:44; 1 Pet.1:16; Mt.5:48).

k.11-12 Jambo la kwanza aliomba walindwe. Walindwe kwa sababu ya maaduiwawili wakubwa. Adui wa kwanza ni ulimwengu. Ulimwengu umewachukia(15:18-25) na chuki hiyo ni kwa sababu ulimwengu umetambua kwa kwelikwamba wamekuwa si wa ulimwengu na kutokana na neno hilo wanaihukumu.

Page 140: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA629

Adui wa pili ni Shetani. Ijapokuwa mara kwa mara Yesu alitaja kushindwa kwaYule Mwovu Yesu hakupuuza upinzani wake kama si kitu. Alimtaja Yuda Iskariotekuwa shahidi wa nguvu zake. Katika huduma yake Yesu aliwalinda wanafunziwake, ila si Yuda, ambaye alikuwa amemchagua kuwa miongoni mwa wale kumina wawili. Hata hivyo, alichaguliwa na Yesu hali akijua yatakayotokea (6:64,70;13:10-11; 18:21-22) alionyesha kwamba Yuda hakumzuia asitimize mapenzi yaBaba na ya kwamba neno hilo lilitabiriwa katika Maandiko. Alikuwa „mwana waupotevu‟ ama kwa sababu ya tabia yake au mwisho wake au kwa sababu zotembili. Kwa hiyo, Yesu alikuwa mwaminifu katika wajibu wake kuwalindawanafunzi wake, hata ikiwa mmojawapo Yuda alimwasi. Maandiko yalitimizwa,kuanguka kwake kuliandikwa katika Maandiko, hivyo si haki kusema kwambaYesu alishindwa kuwalinda. Aliwatahadharisha wanafunzi kwamba Shetani nimpinzani mkuu wa kweli. Baadaye Petro alimwita „simba ang‟urumaye‟ (1Pet.5:8) na Paulo alisema juu ya kupiga vita na hila za Shetani (Efe.6:12ku). Kwasababu ya maadui hao wawili, ulimwengu na Shetani, Yesu alikuwa machoakawaombea wanafunzi wake walindwe.

Ni kitu gani kitakachowalinda? „kwa Jina lako ulilonipa uwalinde hawa‟. Yanamaana gani maneno „Jina lako‟? Yesu amewajulisha juu ya Baba, hali na tabiana makusudi yake. Katika Agano la Kale Mungu alijulikana kwa majinambalimbali, kila jina lilieleza jambo fulani juu yake. Sasa Yesu ameleta ufahamumpya na ombi lake kwa Babake ni kwamba walindwe katika ufahamu huo mpya,wawe watiifu kwa ukweli wake, wauruhusu huo ukweli kuongoza maisha yao, iliwaendelee katika Jina lake (Mit.18:10).

Jambo mojawapo kubwa ni umoja wao. Wakidumu katika Jina lake, wakiendeleakuwa waaminifu kwa ufunuo waliopewa, watakuwa na umoja, umojautakaowasaidia kuyakabili mashambulio ya Shetani na ya ulimwengu. Umojawao utakuwa dalili ya kumshinda Shetani kwa sababu silaha mojawapo yaShetani ni kuleta mafarakano. Kwa umoja watakuwa na silaha kali ya kumshinda,wataonyesha uwezo wa Jina la Mungu, yaani ule ufunuo wa hali na tabia yaMungu wa kweli. Umoja wao ni mfano wa umoja wa Baba na Mwana. Shabahaya kulindwa ni umoja wao.

k.13 Yesu aliendelea na maombi yake kwa ajili ya wanafunzi wake kwakumwomba Baba kwamba waijue furaha yake (14:27; 15:11). Haidhuruwamezungukwa na maadui wakubwa, ulimwengu, na Shetani, alitaka wawe nafuraha, kama Yeye aliyokuwa nayo. Ni ajabu kwamba wakati huo wa kukabiliwana dhiki kubwa Yesu alitaja furaha yake. Furaha yake haikutawaliwa na matokeoya nje, kama uadui wa ulimwengu, wala kwa mambo ya ndani, kama uasi waYuda. Furaha ya Yesu haikuzimwa na mambo hayo, na hakuna sababu furahayao izimwe na mambo kama hayo. Furaha ya Yesu ilitokana na moyo uliotuliakwa Baba na mapenzi yake. Furaha iliyotokana na utii wake kwa Baba. Yesualiamini kabisa kwamba Baba atamshika katika yote, hakuwa na wasiwasiwowote juu ya utunzaji wake. Vivyo hivyo, na wao waweza kuijua furaha hiyo

Page 141: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA630

kama wakifuata nyayo zake na kuishi katika mwanga wa ufunuo wa Babaaliokuwa amewapa (15:11). Baadaye watastaajabu watakapotambua uhalisi waukuu wa Yesu na kuwa na hakika kwamba amerudi kifuani mwa Baba, kwenyeenzi kuu, akiwa na mamlaka juu ya mambo yote.

k.14 Yesu alirudia kutaja kwa Babake ule uadui wa ulimwengu juu yake ambaowanafunzi hurithi. Ni kwa sababu amewapa „neno lako‟ yaani ufunuo halisi juuyake; katika ujuzi huo wa kumjua Mungu wamepata uzima wa milele (17:3;20:31). Ameishataja sababu ya chuki hiyo ya ulimwengu. Walikuwa waulimwengu ndipo Mungu akawachagua watoke katika ulimwengu kwa shabahaya kulitii Neno la Mungu. Katika kufungamana na ufunuo huo wanaukasirishaulimwengu, kwa sababu wanaufunua uovu wake (3:19-21; 7:7).

k.15-16 Ni katika nuru ya uadui huo Yesu aliwaombea walio wake. Aliombakwamba Baba yake asiwatoe katika ulimwengu (Yeye anaondoka karibuni hivi)bali awalinde na yule mwovu. Wakristo wamewajibika wakae ulimwenguni nakumshuhudia Kristo kwa msaada wa Roho Mtakatifu (15:26; 16:27) waumezeuadui wake. Hawaruhusiwi kuachana na ulimwengu wala kuafikiana nao.Usalama wao utatoka kwa Mungu peke yake na katika kuwaombea kwa Babakwamba walindwe Yesu aliwahakikishia kuwa Baba atamjibu.

k.17-19 Halafu Yesu aliwaombea wanafunzi kwamba Baba awatakase kwa ilekweli. Wawe watakatifu, wafanye yote Mungu anayotaka na kuyachukia yoteambayo Mungu huyachukia (Law. 11:44-45; 1 Pet.1:16). Makusudi ya Mungu niwakae ulimwenguni, ila wasijifanye kuwa „ngome‟ ndani yake bali wauendeeulimwengu. Baba alimtenga Mwana wake kwa makusudi ya kuukomboaulimwengu, akamtuma ulimwenguni ili ulimwengu upate kuokolewa naye (10:36).Mwana alijiweka wakfu na kujitenga na mambo mengine yote ili ayatimizemapenzi hayo ya Mungu ya kuuokoa ulimwengu. Vivyo hivyo, na wanafunzi wakewamepaswa kujiweka wakfu ili wao pia waende ulimwenguni na kuushuhudiahabari za Yesu. Ni kwa njia gani watatakaswa? Ni kwa „ile kweli‟ wamefunuliwajinsi Baba alivyo, wameandamana na Yesu na kujua kwa usahihi habari zake naRoho atawajia na kuwafahamisha yale ambayo wameshindwa kuyaelewa wakatihuo. Wapaswa wajitoe kwa kuishi na kuueneza huo ufunuo waliopewa na kuwawaaminifu kwake kinyume cha ulimwengu unaozikandamiza na kuzikana kwelizimhusuzo Mungu na Kristo wake. Kwa hiyo, shabaha ya kutakaswa kwao nikuuendeleza huo Utume wa Yesu, utume Yesu alioupata kwa Baba. Utakatifu waBaba ni msingi wa Utume wa Yesu, Yesu alijitenga na dhambi na kujitoa kufanyahaki na wanafunzi wanadaiwa kufanya vivyo hivyo, wawe wana wa nuru, watuwasiotembea gizani (8:12; Rum.1:1). Kwa hiyo kazi ya Yesu ya kuupatanishaulimwengu na Baba itakwisha pale Msalabani ila kazi yake itatimilizwa kabisawanafunzi watakapotimiza huduma yao (2 Kor.5:15) kwa hiyo ni wajibu waokujitoa kwa utumishi wa Injili. Mwanafunzi hana budi kuwa mpelekwa. Ila ipotofauti moja kati ya Yesu na wanafunzi wake. Yesu alikuwa nje ya ulimwengu,akafanyika

Page 142: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA631

mwili, akaja ulimwenguni. Wanafunzi walikuwa ndani ya ulimwengu, hawakuhitajikufanyika mwili, nao walitolewa katika ulimwengu ili wafanye mapenzi ya Mungu.„najiweka wakfu mwenyewe‟ Wakati ulipokaribia wa kukamatwa Yesu alikazanakufanya mapenzi ya Mungu katika kuitoa nafsi yake kuwa dhabihu kwa ajili yadhambi za ulimwengu (Kum.15:19, 21). Alisema „kwa ajili yao...‟ ili maisha yaopia yawe dhabihu kwa ajili ya utume wao unaohusu wokovu wa wanadamu, ilasiyo kusema kwamba itawalazimu kila mmoja auawe kwa ajili yake.

Katika sehemu hiyo tumeona kwamba Yesu aliwaombea wanafunzi wakewalindwe, wawe na umoja, wawe na furaha yake, watakaswe katika kweli.Mambo hayo yalikuwa muhimu mawazoni mwa Yesu alipomwomba Baba usikuule kabla ya Kufa Kwake. Bila shaka Yesu angali anamwomba Baba mambohayo kwa ajili yetu sisi wa leo.

k.20-26 Yesu aliwaombea Waumini wa baadayeMwishowe Yesu aliinua mawazo yake na kuona matukio ya baadaye, wale wotewatakaomwamini kwa ushuhuda wa hao wanafunzi wa kwanza, na wale wotewatakaomshuhudia kizazi kwa kizazi. Ni dalili ya mafanikio ya ushuhuda wao. Nijambo la faraja kubwa kujua kwamba sisi nasi tulikuwa mawazoni mwake naalitukumbatia sisi katika maombi yake.

Aliwaombea nini, hao Wakristo wote wa baadaye? Kwanza aliomba wawe naumoja sawa na ombi lake kwa wale wa kwanza. Umoja huo ni wa namna gani?Hauwi tu umoja wa mapenzi au upendo, zaidi ni umoja uliojengwa juu ya kukubaliufunuo wa Baba ulioletwa kwa njia ya Yesu kwa wale wa kwanza na kupokelewanao (k.6,8). Gundi la umoja wao ni „neno lile Yesu alilowafunulia wanafunzi wakwanza‟ (k.20). Tena umoja huo unalingana na umoja wa Baba na Mwana.Wanie mamoja na kupendana na kunyenyekeana chini ya ufunuo waliopewa, siumoja usiojali kweli bali ni umoja ulio na msingi katika kweli ya ufunuo wa Yesu.Umoja wao ni zaidi ya kufanana na umoja wa Baba na Mwana ni umojaulioingizwa katika huo umoja wa Baba na Mwana. Jambo hilo ni la ajabu, ni kamakuishi maisha Mungu wa Utatu aishiyo. Kwa hiyo ni umoja wa kipekee, wakimwujiza, ambao utashurutisha watu wakubali kwamba Baba alimtuma Mwanawake, kwa sababu ni umoja usioelezwa kwa njia nyingine.

Ni umoja waliopewa, uliozalishwa na Roho Mtakatifu. Kwa Roho wamezaliwakatika familia ya Mungu (1:12: 3:1ku). Wajibu wao ni kuudumisha (Efe.4:3) nakuuonyesha katika ubora wa maisha yao ya pamoja. Ijapokuwa umoja huo ni wakipekee, hata hivyo, ni umoja unaoonekana, si wa hewani tu. Kwa jinsi wafuasiwake watakavyoishi kwa upendo na umoja ndivyo watu watakavyotambuakwamba Baba anawapenda kama Alivyompenda Yesu. Yesu anatamani sanaKanisa liwe na umoja ili ulimwengu upate kusadiki kwamba alitumwa na Baba.Kwa hiyo, umoja wao ni silaha mojawapo katika uinjilisti. Maneno yao, tangazola Injili ni silaha moja, na umoja wao wa kupendana ni

Page 143: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA632

silaha nyingine (13:34-35). Mara nyingi, umoja wa kupendana wa Wakristo nijambo lisilotiwa maanani kwa upande wa uinjilisti, lakini ni silaha kali. Ubora waushirikiano wetu unavuta watu, na kinyume chake, udhaifu wa ushirikiano wetuunadhoofisha ushuhuda wetu.

k.22 Ule utukufu Yesu aliokuwa nao kabla ya Kuja ulimwenguni, ambaoamemwomba Baba amvike atakaporudi Kwake (k.5) amewapa wafuasi wake, iliwatu wake wote wawe na umoja. Utukufu ni udhihirisho wa tabia zote njema zaMungu, upendo, utakatifu, haki, rehema zake n.k.

k.23 Yesu aliomba wakamilike katika umoja, kwa hiyo, ina maana kwamba,iwapo wanao umoja kiasi fulani, bado haujakamilika. Hayo yote, si kwa sababuulimwengu ujue Baba alimtuma tu bali pia ujue kwamba Baba anawapendawanafunzi wake sawa na anavyompenda Yeye. Yaani wanafunzi washikwe naupendo uleule alio nao Baba kwa Mwana.

k.24-26 Kwa jinsi gani utume wa Yesu utatimizwa? Kweli utatimizwa paleMsalabani katika ukombozi wa ulimwengu ila utatimizwa mbeleni katikawanafunzi wake. Yesu alimwomba Baba kwa hao walio wake kwamba wawepamoja naye na wauone utukufu wake, ni ombi la mapenzi. Hao ni wale wotewalioteuliwa kumwamini. Yohana alikiri kwamba alikuwa ameuona utukufu waMwana (1:14; ling. na 1 Yoh.3:2; 2 Kor.3:18)

k.25 Hapo Yesu aliomba kwa „Baba mwenye haki‟ tabia yake mojawapo kubwa.Yesu hakuhesabu kwamba utume wake haukufaulu kwa sababu ulimwenguhaukumjua Baba, kwa sababu Yeye, pamoja na wanafunzi wake wamemjua.Tena, wanafunzi wataendelea kumjua kwa huduma ya Roho Mtakatifu.Watamjua katika ujuzi wa maisha, ujuzi ulio hai, si ujuzi wa jambo la kihistoria tu(14:23). Kiini cha ujuzi huo ni upendo, watajua ndani yao na kati yao ule upendoambao Baba anao kwa Mwana wake. Ni ajabu kwamba upendo wanaojifunzawanapojitahidi kupendana wao kwa wao ni uleule wa Mungu wa Utatu, Baba,Mwana, Roho. Mafuta yanayoendesha Utatu ndiyo mafuta yatakayowaendeshawao.

18:1 - 21:25 MUDA WA MATIMIZO

Ni muda wa kutimia mambo mawili, kuamini na kutokuamini. Tangu mwanzoYohana ameonyesha mvutano kati ya hayo mawili. Kutokuamini kulifikia upeo waubaya katika Yesu kukamatwa na kusulibiwa. Kuamini kulifikia upeo wa uzurikatika wanafunzi kumwamini Yesu alipofufuka na katika kujitoa kutekeleza utumewake baadaye.

Yesu aliitimiza kazi aliyopewa na Baba kutokana na mambo hayo mawili. Katika17:4 alisema „nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye‟ na katika 19:30 alipokuwaMsalabani alisema „Imekwisha‟. Kwa Kufa Kwake Yesu alifikia upeo wa maisha

Page 144: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA633

yake na matimizo ya Utume wake. Tukilinganisha mashtaka ya makuhani„alijifanya kuwa Mwana wa Mungu‟ (19:7) na ukiri wa Tomaso „Bwana wangu naMungu wangu‟ (20:28) twaona upeo wa kutokuamini kwa wakuu na wenzao nakuamini kwa wanafunzi.

Katika kuandika habari hizo Yohana ameingiza habari zisizoonekana katika Injilizingine tatu pamoja na kuacha habari zingine. Aliingiza hukumu ya kwanzambele za Anasi (18:12ku); Sehemu ya mazungumzo na Pilato isiyotajwa katikaInjili tatu; Yesu kumkabidhi mama yake kwa Yohana (19:25ku); Misemo yamwisho ya Yesu alipokuwa Msalabani (19:26, 28, 30); Petro na Yohana kwendakaburini (20:1ku); Yesu kukutana na Mariamu Magdalene (20:11ku); Yesukumtokea Tomaso (20:24ku); Yesu kutokea wanafunzi saba ziwani (21:1ku).Yohana hakutaja habari za maombi ya Yesu katika Bustani ya Gethsemane; walapazia la Hekalu kupasuka kutoka juu; wala kundi la wanawake kwenda mapemakaburini; wala habari za wawili waliokwenda Emau na kukutana na Yesu njiani;wala hakutaja Agizo Kuu la Yesu kwa Mitume wake, wala habari za KupaaKwake. Hatujui kwa nini habari hizo hazikutajwa wala sababu ya kuchagua zilezingine.MASWALI1. Yesu alieleza uzima wa milele kuwa nini hasa? Eleza kwa maneno yako

mwenyewe2. Katika sehemu ya kwanza Yesu alijiombea. Aliomba mambo gani?3. Katika kuwaombea wanafunzi, wale wa kwanza, aliomba nini?4. Katika kuwaombea waumini wa baadaye, aliomba nini?5. Umejifunza nini kuhusu maombi kutokana na maombi ya Yesu?6. Ikiwa wewe ni pasta au kiongozi katika shirika fulani umejifunza nini juu ya

kuwaombea watu wako kutokana na maombi ya Yesu?

18:1-11 Yesu kusalitiwa na kukamatwaYohana ameziandika habari hizo kwa kuonyesha kwamba Yesu aliyafahamuyatakayotokea. Alitoka kwa Baba na kuja ulimwenguni, sasa atoka ulimwengunina kurudi kwa Baba. Mambo yatakayotokea hayazuiliki. Machoni mwaulimwengu utume wake haumaliziki katika furaha na ushindi ila Yesualiyakaribisha matukio hayo. Uovu na uasi wa ulimwengu ulifikia upeo wakekatika kumkataa Yesu na madai yake kwa kumwua Mwana wa Mungu. Ni kwanjia hiyo tu giza lashindwa na upendo wa Baba kwa ulimwengu hudhihirishwa.Yohana alisisitiza ujasiri na utawala wa Yesu katika mambo hayo. IjapokuwaYuda alikuwa amerahisisha njia ya wakuu si Yuda aliyetawala mambo hayo.Yesu alikwenda mahali ambapo alipenda kwenda na wanafunzi wake na Yudaalijua hivyo na kwa kuzoea kwenda alijua njia. Tena Yesu alikwenda usiku,wakati wa utulivu, tukumbuke kwamba Yerusalemu ulijaa wageni wengi, kwahiyo, waliweza kumkamata bila fujo nyingi. Yesu alijua hatakuwa na mikutano yawatu kumsaidia. Kwa hiyo, yote yalikuwa kama mtego wa kumleta Yuda palebustanini, ili akamate chambo chake. Kama angalitoroka Yuda angaliachwamahali pafinyu na wakuu wangalimkasirikia sana.

Page 145: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA634

k.1 „Alipokwisha kusema hayo‟ neno „hayo‟ ama ni maombi yake ya sura ya 17au sehemu yote kuanzia sura 14 hadi 17. Yesu na wanafunzi walitoka mjini nakupitia bonde la Kidroni mpaka bustani ya Gethsemane, kama maili moja tu. Kwasheria, iliwapasa watu wakae mjini au kando yake, usiku wa Pasaka, kwa hiyo,waliweza kwenda mpaka Gethsemane, hawakuweza kwenda Bethania, kamawalivyofanya siku zilizotangulia. Pengine bustani ilizungukwa na ukuta kwasababu Yohana alitaja „akaingia‟ halafu „akatoka‟ k.4. Huenda mfadhili mmojaalimruhusu kufika hapo na wanafunzi wake. Katika Injili nyingine tumepashwahabari ya masononeko yake na uzito wa hali yake na maombi yake (Mt.26:36ku.Mk.14:32ku. Lk.22:39ku).

Kwa hiyo, tumeona kwamba Yesu kwa hiari yake mwenyewe alikwenda bustaninina pale aliomba. Masaa kadha yalikuwa yamepita tangu Yuda alipoondokachumbani, kwa hiyo, Yesu, kama angalipenda, alikuwa na muda wa kutoshakutoroka na kwenda mbali. Yohana hakueleza habari ya maombi hayo ilaametupasha habari ya maombi kabla ya kwenda bustanini. Bila shaka Yesualisikia haja ya kuomba tena.

k.2 Ni Yohana tu ambaye ametueleza kwamba Yesu alizoea kwenda pale, naYuda alipajua mahali pale. Kwa hiyo, Yesu hakubadili desturi yake, kwa sababuamekwisha kujiweka wakfu kufanya mapenzi ya Babake.

k.3 Ndipo akaja Yuda akiongoza kikosi cha askari wa Kirumi waliotoka katikangome yao pale Kaisaria na kuja Yerusalemu wakati wa Sikukuu ili waulindeYerusalemu. Wakati wa Sikukuu, hasa ile ya Pasaka, watu walikuwa katika haliya msisimuko, wakitamani sana kuupata uhuru mbali na Warumi. Walikumbukazamani za kale na jinsi walivyookolewa utumwani mwa Misri chini ya uongozi waMusa. Hivyo ilikuwa rahisi kwa wanasiasa kuuvuta usikivu wa watu na kwaMasihi wa uongo kujitokeza. Warumi walikuwa macho sana nao walikuwa tayarikuzuia fujo na ghasia zikitokea. Pamoja na askari walikuwapo kikundi chawatumishi wa wakuu waliokuwa na amri ya kumkamata Yesu. Iwapo Sikukuuilifanyika wakati wa mwezi mpevu, hata hivyo, watu walikuja na taa na mienge nasilaha, ili wasiparuzwe au kuteleza njiani. Warumi na Wayahudi walijiungapamoja ili wamkamate Yesu na neno hilo linaashiria uadui wa ulimwengu mzimajuu yake.

k.4 Kifungu hicho ni muhimu „Yesu, hali akijua yote yatakayompata, akatokea,akawaambia, Ni nani mnayemtafuta?‟ Yesu katika hali ya kujua yatakayotokea(pengine bustani ilikuwa na ukuta na lango) akaenda mpaka langoni. Nanialiyetawala mambo hayo? ni Yesu. Akawauliza „ni nani mnayemtafuta?‟. Yesuhakuwa mtu wa kuhurumiwa kama mtu aliyekamatwa kinyume cha mapenziyake. La! hata kidogo. Ni Yeye aliyejitokeza na kuwakabili.

k.5-6 Yesu alijitambulisha kwao. Pengine wakati huo Yuda alimbusu (Mt.26:48-49). „Ni Mimi‟ Maneno hayo ni ukumbusho wa 6:20; 8:24, 28, 58; 13:10 kuhusu

Page 146: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA635

Yesu kuwa Mungu Mwana, ila itakuwa vigumu kufikiri kwamba hao waliokuwepowaliyaelewa hivyo. Pengine walikumbuka makuu aliyoyafanya hapo nyuma nakushikwa na wasiwasi. Kwa vyovyote hali ya Yesu iliwashtusha na kwa mudamfupi wakasita, wakarudi nyuma na kuanguka chini. Wengine hufikiri kwambaYesu alivaa utukufu wake wa asili kwa dakika chache, ila si lazima tufikiri hivyo.Tukumbuke kwamba wamekuja na silaha ili wamkamate mhalifu, kumbe, huyo„mhalifu‟ hakimbii, wala hatumii mabavu, bali akubali kukamatwa.

k.8-9 Halafu Yesu alionyesha madaraka yake katika haya yote, akawauliza tena„Mnamtafuta nani?‟ Ndipo wakasema tena „Yesu wa Nazareti‟. Halafu Yesuakajitia mikononi mwao akiomba wawaachilie wanafunzi wake. Alijitoa kwa haliya kuwaokoa wanafunzi wake. Hakuna haja ya wao kuingizwa katika jambo hilo,kwa sababu ni Yeye, peke yake, astahiliye kutoa dhabihu ya nafsi yake kwadhambi za ulimwengu mzima. Alivuta chuki zote Kwake na kuwaepusha waowasizipate. Kama alivyowaambia hapo nyuma, Yeye ni Mchungaji mwema,atunzaye kondoo zake, aonapo mbwa mwitu anakuja hukaa pale na kuwatunza(Yn.10:11-12).

k.10-11 Ila Petro hakuweza kukubali Bwana wake akamatwe na kwa ujasirimkubwa akaufuta upanga na kumpiga mtumishi mmoja wa Kuhani Mkuu nakukata sikio lake la kuume, jina lake Malko.Ulikuwa ujasiri wa bure, ujasiri uliokana mapenzi ya Baba kwa Yesu, ambayoYesu Mwenyewe alikuwa amejiweka wakfu kuyatimiza. Katika kumponya mtumishi(Lk.22:51) na katika kuwasalimisha wanafunzi, Yesu alitoa kielelezo cha kaziatakayofanya Msalabani, kazi ya kuwaokoa wanadamu na dhambi zao. Jambola lazima ni Yeye kukinywea „kikombe cha Baba yake‟, ni njiailiyowekwa ili uovu ushindwe, Shetani ashindwe, mauti ishindwe, na dhambiishindwe. Katika Agano la Kale „kikombe‟ kilishuhudia ghadhabu ya haki yaMungu (Isa.51:17-23; Yer.25:15-28; Zek.12:2) kumbe kikombe hicho Munguhawapi adui zake bali Mwana wake mpendwa. Ni kikombe alichopewa kukinyweana Baba (Mk.14:36). Wala hakumsuta Yuda kwa usaliti mbaya mno wa kumsalitirafiki aliyekula naye, pengine alikuwa akimwachia nafasi ya toba.

Tukilinganisha Petro na Yuda twaona.Yuda alikuja na wenye silaha ili wamkamate Yesu.Petro aliufuta upanga ili amlinde Yesu.Yuda alifanya kwa hila; Petro alifanya kwa wazi. Yudaalifanya kwa kusudi; Petro alifanya bila kufikiri.Yuda hakumwamini Yesu ijapokuwa aliishi naye miaka mitatu.Petro alimwamini Yesu ijapokuwa mara kwa mara aliteleza.Yuda hakuwa mnyofu moyoni.Petro alikuwa mnyofu moyoni.

Page 147: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA636

Yuda na askari ni wajumbe wa ulimwengu huu wakitegemea silaha na nguvu zakimwili. Yesu ni mjumbe wa ulimwengu wa kiroho, hakutegemea silaha walanguvu za kimwili. Msaada wake ulikuwa katika ushirikiano wake na Baba nakatika kutii mapenzi yake.

18:12-27 Kuhukumiwa na Anasi na Petro kumkanaTukumbuke ya kuwa makuhani walikuwa wametoa fedha kwa Yuda ili wampateYesu bila shida.k.12-14 Yesu mbele ya AnasiHapo tunazo habari za mambo yaliyotokea mara baada ya Yesu kukamatwa.Katika sehemu hiyo yote twaona umuhimu wa yote kwenda kwa haraka kwasababu lazima wapitishe kesi juu ya Yesu kwa Anasi, ndipo kwa Kayafa naBaraza Kuu la Sanhedrin, kisha kwa Pilato, liwali wa Kirumi, hatimaye Yesuasulibiwe, awe amekufa na kutolewa msalabani kabla ya jua kuchwa na kuanzakwa Sabato kuu ya Sikukuu, au itawabidi wangoje mpaka zipite Sikukuu na Sikuza Mkate usiotiwa chache. Hapo nyuma ilionekana wameamua kungoja mpakasiku hizo zimepita (Mt.26:3-5) ila Yuda alipotokea na kuahidi kwambaatawajulisha mahali pa kumpata, basi wakaamua kutekeleza mipango yao maramoja. Kwa hiyo, mara baada ya kumkamata Yesu wakamwendea Anasi palenyumbani kwake na kuanza kesi juu ya Yesu. Ilikuwa usiku na baadhi yawajumbe wa Baraza walikuwapo, wengi wao walifika baadaye, asubuhi namapema, ndipo Baraza kuu lilikutana.

(Maelezo kuhusu Anasi na Kayafa ambao wote wawili wameitwa Kuhani Mkuu.Anasi alikuwa Kuhani Mkuu B.K.6-15 ndipo akaondolewa na liwali aliyemtanguliaPilato. Wayahudi walichukizwa na jambo hilo la Warumi kujiingiza katika dini yaona kuchagua Kuhani Mkuu. Katika Agano la Kale Kuhani Mkuu aliwekwa kwamaisha yake yote. Baada ya Anasi, wana wake wanne walimfuata na wakati huoni mkwewe Kayafa aliyekuwa Kuhani Mkuu (11:49). Katika Luka 3:2 na Matendo4:6 wamewekwa pamoja. Inaonekana Anasi alikuwa na sauti na nguvu ingawaKayafa hasa alikuwa Kuhani Mkuu, hivyo, walimpeleka Yesu kwake kwanza).

k.15-16 Hapo mwandishi Yohana ameingiza habari ya Petro kumkana Yesu kwamara ya kwanza. Alipata nafasi ya kuingia behewa la Kuhani Mkuu kwa sababu„mwanafunzi mwingine‟ aliyejulikana na Kuhani Mkuu aliruhusiwa kuingia,akaomba ruhusa kwa Petro kuingia pamoja naye. Behewa la Kuhani Mkuu, niwapi? Je! ni behewa la Anasi au Kayafa. Huenda lilikuwa moja, wote wawiliwakiishi kwa ukaribu. Ni vigumu kufikiri ni pale hekaluni kwa sababu mngojamlango angalikuwa wa kiume si wa kike. Huyo „mwanafunzi mwingine‟ alikuwanani? Yafikiriwa kuwa Yohana. Ilikuwaje ajulikane na mtu maarufu kama KuhaniMkuu na yeye ni mvuvi wa Galilaya? Inaonekana babake alikuwa tajiri mwenyevyombo na uwezo wa kuajiri watu (Mk.1:19-20) pengine alikuwa na biashara yasamaki mjini Yerusalemu. Mara nyingine Petro na Yohana wametajwa kuwapamoja (13:23-24; 20:2-10; 21:20-24). Kama si yeye huenda alikuwamwanafunzi wa Yesu aliyeishi Yerusalemu.

Page 148: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA637

Ilikuwa usiku na watumishi walikuwa wamewasha moto wa makaa kwa sababuya baridi na Petro akasimama karibu, huku Yesu yu ndani, akihojiwa na Anasi.Basi yule mngoja mlango wa kike akamwuliza Petro „Wewe nawe, je! humwanafunzi mmojawapo wa mtu huyu?‟ Kwa jinsi swali lilivyotungwa jibulililotazamiwa lilikuwa „la‟ haikuwa rahisi kujibu moja kwa moja, „ndiyo‟. Lilikuwaswali lenye dharau kama ni jambo lisilosadikika kwamba mtu amfuate mtu huyo.Petro alitishwa na mazingira yake pamoja na kujua kwamba ni yeye aliyemkatasikio mtumishi wa Kuhani Mkuu akaanza kuteleza, akakana kuwa mfuasi wa Yesu.

k.19-24 Anasi alimhoji Yesuk.19-20 Kutokana na maneno ya k.24 hapo Kuhani Mkuu ni Anasi. Yesu aliulizwajuu ya mambo mawili, wanafunzi wake na mafundisho yake. Bila shaka aliulizwajuu ya wafuasi wake kwa sababu alikuwa na wafuasi wengi. Wengi waliotokaGalilaya kwa Sikukuu, walikuwa wamemsindikiza mpaka mjini kwa shangwekubwa. Yesu hakumjibu Anasi kuhusu hao wafuasi wake. Jambo kubwa hasalilihusu Yesu na mafundisho yake, jambo la theologia si jambo la siasa, ilawalipompeleka kwa Pilato walisisitiza mambo ya siasa (19:7,12). Hasa kiini chachuki yao kilikuwa madai yake kuwa Mwana wa Mungu mwenye umoja na Baba.Hapo nyuma walimshtaki Yesu kwamba alikuwa akiwadanganya watu (7:12,47)kama anawaongoza kumwasi Mungu wa baba zao. Yesu akamjibu Anasi kwakusema kwamba mafundisho yake yametolewa hadharani mwa watu,masinagogini na hekaluni, tena hakusema neno lolote sirini. Hakuwa na maanakwamba kwa wanafunzi wake hakusema nao walipokuwa peke yao, la, ilaaliyoyasema kwao hayakuwa tofauti na yale aliyosema wazi, sirinihakuwachochea na kuwafundisha kinyume cha alivyosema kwa wazi.

k.21 Hapo Yesu aliwapa changamoto ya kuwauliza wale waliomsikia ili haowatoe habari za mafundisho yake. Kwa sheria ya Kiyahudi haikuwa halalimshtakiwa aulizwe maswali na kujitetea, ilipaswa mashahidi wahojiwe na kamawawili wao wakipatana ndipo mshtakiwa hakuwa na nguvu ya kujitetea.

k.22-23 Kwa kusikia hayo mtumishi fulani alimpiga Yesu kofi na kusema„Wamjibu hivi Kuhani Mkuu?‟ Yesu akasimama imara na kumkabili ana kwa anana kumpa changamoto aseme ni ubaya gani aliofanya, na kama hakusemavibaya, mbona amempiga? Yesu alitaka kunyosha kanuni za hukumu ili wafuatesheria za halali wanapomhukumu. Yesu alikuwa na haki ya kumjibu hivyo. HasaYesu alikuwa akiomba ahukumiwe kwa halali. Si haki ageuze shavu lake nakunyamaza kama ni neno lihusulo kweli, Yesu hakuwa mwoga.(Tukilinganisha habari hii na itikio la Paulo alipopigwa wakati wa kuhukumiwa,mambo ni tofauti. Paulo alikuwa mbele ya Sanhedrin, Baraza Kuu la nchi.Alimwita Kuhani Mkuu „ukuta uliopakwa chokaa‟ na katika Maandikohaikuruhusiwa mtu aseme neno baya juu ya Kuhani Mkuu, na ndiyo sababuPaulo aliomba msamaha (Mdo. 23:2-5). Yesu hakusema neno baya juu ya mtuyeyote na hakuwa mbele ya Sanhedrin).

Page 149: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA638

k.24 Anasi alitambua kwamba itakuwa vigumu kumlazimisha Yesu aseme nenolitakalofaulu mbele ya liwali. Hivyo akaona vema ampeleke kwa Kayafa, kwasababu bila kupitia kwa Kuhani Mkuu aliyeko, liwali wa Kirumi, Pilato, atakataakuwasikiliza. Imewabakia kazi kubwa ya kunyosha mashtaka ili yapate kibali chaPilato.

Yesu alikuwa mpole na mnyenyekevu ila upole wake si upole wa kutokujali haki.Shida yao kubwa ilikuwa kwamba hawakumwamini wala hawakutaka kumwaminina kwa sababu hiyo wameisha kumhukumu kuwa na hatia hata kabla yakuanzisha kesi.

k.25-27 Petro kumkana YesuYohana ameturudisha kwenye mambo yaliyokuwa yakitokea behewani penyemoto uliowashwa. Petro alikuwa amesogea karibu na moto na wenginewaliokuwapo. Ni kama amejiweka mahali pa kujaribiwa tena. Yesu alikuwaamesimama imara mbele za Anasi huko Petro ameteleza na kukana kuwamwanafunzi mbele ya mjakazi. Halafu Petro akaulizwa tena swali kama lile lakwanza na kwa mara ya pili akakana kuwa mfuasi wa Yesu.

Kisha akaulizwa kwa mara ya tatu, na aliyemwuliza wakati huo alikuwa ndugu wayule aliyekatwa sikio. Huenda alikuwa amemtambua Petro katika mwanga wa ulemoto. Hapo tena Petro akateleza zaidi na kukana tena kuwa mwanafunzi waYesu. Yohana hakutaja kwamba alilaani na kuapiza kama Marko alivyosema(Mk.14:71ku). Kisha jogoo akawika, na Petro akakumbuka maneno ya Yesu(13:38) akatoka na kulia machozi ya uchungu. Petro hakuweza kumfuata Yesubarabara mpaka Yesu amekufa kwa ajili yake (13:36). (Ling. na Luka 22:62maneno ya matumaini). Hayo yote yaliingizwa katika mipango ya Mungu nabaadaye kwa neema kubwa ya Mungu Petro atarudishwa na kuwa kiongozihodari wa wenzake.

Jambo hilo lilikuwa mojawapo katika fungu zima la mambo yaliyomwudhi Yesu.Alisalitiwa na Yuda, alikanwa na Petro, aliachwa na wanafunzi; alishtakiwa nawatu wake wenyewe; Yeye asiye na dhambi alihukimiwa na wenye dhambi akinaAnasi, Pilato, Herode, Kayafa n.k. Yeye aliye Mungu alinyenyekezwa na kusutwana wanadamu aliowaumba!! Ila Petro hakukusudia kumkana. Alitegemea nguvuna ujasiri wake wa kimwili, na kwa sababu hiyo, alipobanwa hakuweza kusimamaimara. Vilevile wanafunzi walimwacha na kumkimbia kwa sababu ya hofu yakukamatwa. Bila kukusudia Ila Yuda na wakuu walifanya kwa kusudi, kwa sababuhawakumwamini.

18:28-40 Kuhojiwa na PilatoYohana ameandika mengi juu ya hukumu ya Yesu mbele ya Pilato, liwali waKirumi, na machache kwa hukumu mbele ya Sanhedrin na wakuu wa Kiyahudi.Hakutaja mashtaka ya kwanza (Lk.23:2); wala mashtaka yaliyoletwa namakuhani (Mt.27:12; Mk.15:3) wala habari ya kupelekwa kwa Mfalme Herode

Page 150: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA639

(Lk.23:4-12) wala makuhani kumwomba wapewe Baraba (Mt.27:20, Mk.15:11).Inaonekana Yohana alitaka kupambanua hali na tabia za Pilato na hali na tabiaza Yesu na kuonyesha tofauti kati ya falme za dunia hiyo na Ufalme wa Mungu.Mkazo wake ulikuwa juu ya Ufalme na mamlaka ya Yesu (18:36; 19:11,14).Ijapokuwa Pilato alikuwa akimhukumu Yesu kwa upande mwingine Yesu alikuwaakimhukumu Pilato. Ni vema kulinganisha Mt.26:57-27:2 na Mk.14:53- 65 kwahabari za Yesu mbele ya Sanhedrin. Mashahidi walioitwa walikosa kuletaushuhuda wa kumtia hatiani na mwishowe Kuhani Mkuu alimwapiza Yesu asemewazi kama alikuwa Masihi au siyo. Jambo la kumwapiza mtu ajishuhudiemwenyewe kwa kiapo halikuwa halali, ila kwa sababu mambo yalishindikanawalikuwa hawana njia nyingine. Alipoulizwa Yesu akakiri kwa wazi kuwa NdiyeMasihi (Mimi Ndiye Mk.14:62) naye akaendelea na kusisitiza madai ya kuwaMwana wa Adamu mwenye kuushiriki utukufu wa Mzee wa siku na kupewamamlaka n.k. (Dan.7-13-14). Waliposikia hayo wajumbe wa Baraza walichukizwasana, wakaona kwamba Yesu amekufuru sana, hakuna haja tena ya kupatamashahidi, waliamua amestahili kuuawa, wakaanza kumshutumu (Mt.26:64ku)ndipo wakampeleka kwa Pilato ili yeye atekeleze uamuzi wao.

k.28 Yohana hakuandika habari hizo, alianza na neno „kisha‟ kama kuendeleana habari baada ya zile za Injili tatu kuhusu hukumu mbele ya Sanhedrin naWayahudi.

Mambo yaanza katika nyumba ya Liwali. Ilikuwa desturi ya liwali kuja Yerusalemukutoka Kaisaria wakati wa Sikukuu za Kiyahudi, ili awepo karibu na kukabili fujoikitokea. Liwali alikuwa Pilato, alikuwa liwali tangu B.K.26-37. Wayahudihawakumpenda (Lk.13:1) alikuwa mkatili, mara kwa mara aliwaonyesha dharau.Hakuwa mtu imara, hakuwa na msimamo, na jambo hilo laonekana wazi katikahukumu za Yesu. Ilikuwa asubuhi na mapema, na Wayahudi hawakuingia ndaniya nyumba yake, nyumba ya Mmtaifa wasije wakanajisika na kuzuiliwa wasiilePasaka kwa sababu hiyo. Ajabu ni kwamba walitaka kuwa safi mbele za Munguhuku wanapanga na kufanya juu chini ili wamwue Mwana wake mpendwa.Walikuwa tayari kutumia hila na werevu katika hukumu ili wafaulu kumvuta Pilatoatoe hukumu ya hatia. Ila hayo yote yatatimiza mapenzi ya Mungu, kwa kutakaYesu auawe walitimiza makusudi ya Mungu ya Yesu kuwa Mwana Kondoo,dhabihu ya dhambi, kama Yesu alivyotabiri (12:32-33). Twaona hatari yakushikilia taratibu za dini na kupoza dhamiri, taratibu ambazo zenyewe haziokoimtu.

k.29 Pilato aliridhiana nao na kutoka nje na kuwauliza kuhusu mashitaka yao.Yawezekana ameishajua kwamba Wayahudi watamleta kwake kwa sababuaskari za Kirumi walitumiwa alipokamatwa.

k.30 Wakamjibu Pilato kwa ufidhuli. Walidhani kwamba Pilato atathibitishahukumu yao na kutoa amri Yesu asulibiwe, na badala yake, alianza kwa upyakesi juu yake.

Page 151: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA640

k.31 Pilato hakupendezwa na jinsi walivyomjibu akawaambia wamtwae Yesu nakumhukumu kwa sheria yao, hali akijua kwamba hawana ruhusa kumwua mtu.Kwa kutawaliwa walikuwa wamenyimwa haki hiyo. Bila shaka Pilato alifahamu nikitu gani walichotaka, lakini hakuwa tayari kupokea mashtaka ya hewani„asingekuwa mtenda mabaya, tusingemleta kwako‟. Lazima watamke wazimashtaka na kumhakikishia ukweli wake. Alijua hawawezi kuendelea kufanyalolote kwa halali bila yeye (twajua kwamba baadaye walimwua Stefano (Mdo.6-7)ila jambo hilo lilifanyika ghafula kutokana na ghasia ya kundi fulani. Bila shaka,mara kwa mara, Warumi walifumba macho kwa mambo hayo). Tena ilikubalikakwamba kama kosa lilihusu mambo ya hekalu walikuwa na haki ya kuchukuahatua, huenda hii ni sababu walitafuta kumbana Yesu juu ya mambo ya hekalu(Mk.14:57-59). Ingawa mara ya kwanza hawakutaja mashtaka baadayewaliyataja na kuyageuza yawe ya kisiasa si ya kidini, ijapokuwa hasa ni mamboya dini yaliyowachukiza (Lk.23:1ku). Walifanya hivyo kwa sababu walijuakwamba Pilato hatayajali mambo ya dini yao.

k.32 Katika hayo yote mwandishi aliona Mungu ni nyuma yake, Yesu atakufakwa kusulibiwa si kwa kupigwa mawe. Katika kutundikwa mtini atakufa chini yalaana ya Mungu hivyo maneno ya Yesu na Neno la Mungu yalitimizwa(Yn.12:32-33; Kum.21:23).Masihi aliyesulibiwa ni kikwazo kwa Wayahudi na kwa WaMataifa ni upuzi mtupu,ila kwa wote wanaompokea Yesu kama Masihi ni njia ya wokovu (1 Kor.1:18ku).

k.33-38a Pilato alirudi ndani na kuzungumza na Yesu. Swali lake lilikuwa „Je!Wewe ni Mfalme wa Wayahudi?‟ Swali hilo limetajwa katika Injili zote nne nalinashuhudia jinsi Baraza la Kiyahudi walivyofanya juu chini ya kumwonyeshaPilato kwamba Yesu alikuwa hatari kwa Dola ya Kirumi. Pengine Pilato alionashida kufikiri kwamba huyo aliyekuwa mbele yake aweza kuwa Mfalme, maanaalionekana kuwa mpole, alikamatwa bila shida, hata akamkemea mfuasi wakealiyeufuta upanga, hata akamrudishia sikio yule aliyejeruhiwa. Awezaje kuwaMfalme?

k.34 Yesu hakumwogopa Pilato, akamkabili kama mtu aliyehitaji neema yaMungu si kama yule wa kuamua auawe. Alijibu swali lake kwa kumwuliza ni kwajinsi gani alivyotumia na kuwaza neno „Mfalme‟ pia aliuliza kwa kutaka kujuazaidi au kwa kurudia shtaka la Wayahudi. Hivyo ilikuwa vigumu Yesu ajibu „ndiyo‟au „siyo‟ mpaka amefahamu haya, kama Pilato anataka kujua zaidi awezakumsaidia.

k.35 Pilato akamjibu Yesu kwa dharau, ila bado alitatanishwa na sababu yaWayahudi kumchukia Yesu kiasi cha kutaka auawe. Ni kama alitambua kwambakuna kitu fulani kinachowaudhi ambacho bado hawajakiweka wazi, hivyo Pilatoakamwuliza „Umefanya nini?‟

Page 152: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA641

k.36 Ndipo Yesu akamfafanua Pilato habari za Ufalme wake. Ni ufalme usio naasili katika ulimwengu huu, hauhusu maeneo ya kijiografia, kama nchi yaUyahudi. Wala hali yake haifanani na zile za ulimwengu huu. Wafalme wa duniahutumia silaha na nguvu na mabavu ili wazilinde falme zao, sivyo ilivyo kwaufalme wake. Ni wazi kwamba hakuwa na askari na majeshi wala silaha, kwahiyo Yeye si hatari kwa Pilato na utawala wake. „Ufalme wangu si wa ulimwenguhuu‟ maneno hayo yasimaanishwe kwamba ufalme wa Yesu hauhusiki naulimwengu huu, la sivyo. Unagusa maisha yote ya wanadamu ambayo sehemumojawapo ni siasa na haki yake hupaswa kuongoza mipango yote ya wanadamuambayo sehemu moja ni serikali. Tofauti ni katika silaha za Ufalme ambazo niupendo, rehema, haki, na utakatifu. Ufalme wa Yesu hasa huhusu ushirikiano wamtu na Mungu (17:3) na uhuru wa kweli (8:32).

k.37 Pengine Pilato alifahamu machache tu ya hayo maelezo ya Yesu, akarudiakumwuliza „Wewe u Mfalme basi? Ndipo Yesu akamjibu „Wewe wasema, kwakuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya hayo, na kwa ajili ya hayomimi nalikuja ulimwenguni‟ Yesu alikubali kuwa Mfalme, na ya kuwa alizaliwa nakuja ulimwenguni kwa kusudi hilo, hata hivyo, hasa ufalme wake wahusu kweli,alikuja ila aishuhudie kweli. Kweli gani? ile kweli ya ufunuo wake juu ya MunguBaba. Ni wale tu wenye uhusiano mwema na Mungu ambao wanaingia katikaUfalme huo (3:16-21; 10:3,16,26; 14:6). „kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sautiyangu‟ ni kama mwito kwa Pilato kuwa mfuasi wake.

k.38 Pilato akamwuliza Yesu „Kweli ni nini‟ Ni vigumu kujua kama Pilato alitakakujua zaidi juu ya kweli; au kama ni swali la kejeli kutokana na maisha yakimwanasiasa na maridhiano mengi aliyofanya ili ahifadhi uliwali wake. Penginehakutaka kujua, pengine alisikia kama Yesu anamsumbua. Hayo yote hatuyajui,ila tujualo ni kwamba hakukaa ili azungumze zaidi na Yesu, dakika za nafasinjema ya kukata shauri la kumfuata Yesu zilipita.

k.38b-40 Kumchagua Baraba badala ya YesuPilato akawaendea Wayahudi tena, hali amekuwa na hakika kwamba hamnamsingi wo wote katika mashtaka yao. Akawaambia wazi „Mimi sioni hatia yoyotekwake‟. Kama ni hivyo ilikuwa haki aifunge kesi hiyo na kumwachilia Yesu marana kuwaondosha Wayahudi. Ila alisita kufanya hayo. Akaona vema awape nafasiya kumpokea Mfalme wao Yesu. Alitumia maneno yaliyo na uhasama masikionimwao „niwafungulie Mfalme wa Wayahudi?‟ jinsi ambavyo kamwe hawakutakaYesu aitwe. Akawakumbusha desturi ya kumfungulia mfungwa mmoja wakati waPasaka, hivyo, Je! walitaka amfungulie Yesu au Baraba. (Baraba alikuwa mtumwenye sifa mbaya; gaidi, mnyang‟anyi, pia alikuwa amemwua mtu.Ameishahukumiwa kuwa na hatia, alikuwa akisubiri kusulibiwa).

Wakuu pamoja na wengine waliojiunga nao wakaanza kupiga kelele nakumwomba wapewe Baraba si Yesu. Ijapokuwa hawakupenda huyo gaidi

Page 153: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA642

katika chuki yao na wivu wao walimchagua gaidi badala ya Yesu. Ni vigumu kujuasababu ya Pilato kuingiza jambo hilo, pengine aliogopa kumruhusu Yesu maramoja (19:12) ila ilikuwa hatua kubwa katika utelezi wake wa kufanya hukumu yahaki. Maana uchaguzi ulikuwa kati ya mmoja aliyeishahukumiwa kuwa na hatiana mmoja ambaye alimtangaza kuwa „sioni hatia yoyote kwake‟. Hakuna usawakati yao hata kidogo. Ila mapenzi yao yalilingana na haja yetu kubwa ya kumpatayule asiyekuwa na dhambi wala hatia abebe dhambi na hatia zetu mwilini mwakepale Msalabani (1 Pet.2:24; 3:18). Ni juu ya kila mwanadamu kuamua ni nanianayemtaka kuwa „mfalme‟ wake. Twamtaka nani?

MASWALI1. Umejifunza nini kuhusu madaraka ya Mungu Yesu alipokamatwa?2. Kwani Mungu aliwaruhusu kumkamata Yesu? na kwa nini Yesu

hakutoroka?3. Kwa nini Yesu alipelekwa kwa Anasi kwanza?4. Unaonaje jambo la Petro kumkana? ilitokeaje mwanafunzi huyu

aliyempenda sana amkane?5. Onyesha tofauti kati ya Petro na Yuda Iskariote, wote wawili walikosa, ila

mmoja tu alitubu na kurudishwa.

19:1-16 Pilato alitoa hukumu Yesu afe

k.1 Hapo twaona jinsi Pilato alivyozidi kuteleza. Alitafuta njia ya kumwachiliaYesu huku akitafuta kuwaridhisha washtaki wake. Akamtwaa Yesu na kumpigamijeledi na kuwaruhusu askari wamvike taji ya miiba na kumdhihaki kufuatana nashtaka lake la kuwa Mfalme. Katika k.4 twaona sababu ya Pilato kufanya hivyo(Lk.23:16, 22) alikusudia kuridhisha Wayahudi akidhani kwamba wakimwonaYesu katika hali hiyo ya unyonge watamhurumia, wataacha kudai auawe. Niajabu kuona kwamba alimpiga yule aliyemtangaza kuwa hana hatia. Ni haki ganihiyo? Warumi walisifiwa sana kuwa watu wa kuhukumu kwa haki.

Warumi walitumia aina tatu za kuwapiga watu mijeledi: walimpiga mtu kidogokama kosa lake lilikuwa dogo. Kwa mtu aliyekosa zaidi walimpiga zaidi; na kwamtu aliyefanya jambo baya sana walimpiga sana sana. Kwa kawaida wahalifuwalipigwa mijeledi kabla ya kusulibiwa kwa shabaha ya kuwadhoofisha iliwatakapotundikwa mtini wasikawie kufa, baadhi yao walikufa kabla yakutundikwa msalabani kwa kuwa walijeruhiwa vibaya. Yafikiriwa Yesu alipigwa,si mapigo makali, kama onyo kwake na kwa kutuliza Wayahudi, huenda alipigwavikali sana baada ya hapo, wakati Pilato alitoa hukumu afe, kwa sababualishindwa kuubeba mti wa msalaba. Ni vigumu kufikiri angalipigwa sana kablaya Pilato kutoa hukumu ya kufa.

Page 154: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA643

k.2-3 Yesu alitolewa kwa askari nao walimfanyia dhihaka kufuatana na shtaka lakudai kuwa Mfalme wa Wayahudi. Ni kama walimsimika kitini na kumvika taji (yamiiba) na kumpigia magoti, na kumsuta, na kumpiga usoni n.k. Tukumbuke yakuwa walimpiga na kumdhihaki huyu aliye Mungu Mwana, Muumba na Mhifadhiwa wanadamu wote. Ila hayo hawakutambua, walikuwa wakimsuta kulingana namashtaka ya Wayahudi waliomleta.

k.4 Askari walimrudisha kwa Pilato naye akamleta Yesu nje hali damu inatiririkakutoka majeraha yake na alionekana mnyonge kabisa.

k.5 Ndipo Yesu akatokea hali amevaa ile taji ya miiba na kuvikwa vazi lazambarau, kisha Pilato akatangaza „Tazama, mtu huyu!‟ akadhani kwambawakimwona hivyo watamhurumia na watashawishiwa wasiendelee kumtakaasulibishwe. Katika maneno hayo twaona uhakika wa Yesu kufanyika mwili kweli(1:14). Labda Pilato alikuwa akimdhihaki Yesu na wayahudi kwa kuwawalithubutu kafikiri kwamba huyo aweza kuwa Mfalme.

k.6 Lakini kila njia aliyotumia ili amwachilie Yesu haikufaulu, makuhani nawenzao walikazana kabisa, walipiga kelele „asulibishwe‟. Walimsukuma Pilatokufanya kinyume cha mapenzi yake. Alikuwa amefikia mwisho wa kuchukuliananao, na kwa kusikia ameshindwa, akajibizana nao „mtwaeni ninyi basi,mkamsulibishe, kwa maana mimi sioni hatia kwake‟. Alitaka kujiondoa katikakesi hiyo na kuwatwisha Wayahudi wajibu wa kutekeleza ile hukumu waliyotaka,hali akijua hawaruhusiwi kufanya. Katika kusema hivyo alikusudia kuwaudhi kwakuwakumbusha jinsi walivyokuwa chini ya utawala wa Kirumi na kwa sababu hiyohawakuwa na madaraka ya kumsulibisha Yesu. Ni kama kuwalipiza kisasa. Waowakambana na yeye akawabana.

k.7 Ndipo mwishowe Wayahudi wakataja kosa lililokuwa kubwa machoni mwao,ambalo lilisababisha chuki yao, Yesu kujifanya kuwa Mwana wa Mungu na sawana Mungu. Kumbe! shida yao ilikuwa hiyo, ilizidi ile ya Yesu kudai kuwa Masihi.Hili lilikuwa kufuru kuu kabisa. Mwishowe kabisa walitoboa wazi ni niniiliyowaghadhabisha. Wakaacha kusisitiza upande wa siasa na kukaza upandewa dini. Walianza na upande wa siasa kwa sababu walidhani kwamba Pilatohatayajali mambo ya dini. Mara nyingi Pilato amesema kwamba hakuona hatiakwa upande wa siasa. Kwa sheria yao walifikiri Yesu alikuwa na hatia (Law.24:16).

k.8 Pilato aliposikia maneno „Mwana wa Mungu‟ aliogopa sana. Kwa Pilato hayomaneno yalikuwa na maana tofauti na maana yake kwa Wayahudi. KwaWayahudi ni maneno ya kufuru. Sivyo ilivyokuwa kwa Pilato. Katika malezi yakeya Kirumi alikuwa amezoea kuamini kuwepo kwa miungu mingi, na hiyo miungu,mara kwa mara, walizaa „wana‟ na wana hao waliweza kuja duniani na kufanyamakubwa. Je! Yesu ni mmojawapo wa hao „wana‟ kama nusu mwanadamu nanusu Mungu? Itakuwaje kama anao uwezo wa kimungu nami

Page 155: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA644

nimempiga mijeledi? Tangu mwanzo Yesu amekuwa fumbo kwake na kwamaneno hayo Pilato akazidi kukanganyikiwa. Wasiwasi ulizidi na hofu ikamshika.Wapagani walishikwa na ushirikina na Yesu alimtia wasiwasi.

k.9 Akarudi ndani tena ili amchunguze Yesu zaidi juu ya neno hilo. Akamwulizamoja kwa moja „Wewe umetoka wapi?‟. Yesu akanyamaza, hakumjibu hata nenomoja; hapo nyuma mbele ya Wayahudi hakuwajibu (Mk.14:60-61; 15:5). Haponyuma Pilato hakuonyesha mzigo juu ya kweli, kwa hiyo Yesu hakuona vemaaseme naye tena. Ametelezateleza katika kufanya haki na kutokumfungua hukuamemtangaza kuwa bila hatia. Basi, akakaa kimya. Hali thabiti ya Yesuilimsumbua na kumwudhi. Kwa kiburi Pilato akamjibu kwa ukali na kwakumkemea akimkumbusha kwamba hukumu yake ilikuwa mikononi mwake,alikuwa na uwezo wa kumruhusu na uwezo wa kumsulibisha. Ila maneno yake nimaneno ya kejeli. Mbona basi, hakumfungua ikiwa alikuwa na madaraka yakufanya hivyo? Kweli, kinadharia alikuwa na mamlaka, ila kiutendaji hakuwa nauwezo kutokana na udhaifu wake wa kibinafsi na vibano vya siasa, nakumbukumbu za mambo yaliyotokea nyuma kuhusu uhusiano wake mbaya naWayahudi. Pilato alikuwa mfungwa wa mambo hayo iwapo yu huru, Yesu ingawani mfungwa alikuwa huru, alijitawala, hakutiishwa na liwali, akawa thabiti katikamsimamo wake. Alikuwa na uwezo zaidi ya Pilato (Yn.10:18) Alijua ni mapenziya Babake asulibiwe kwa dhambi za ulimwengu, si kwa kosa lake mwenyewe.Pengine ni wakati huo ambapo Pilato alipata ujumbe wa mkewe „usiwe na nenojuu ya yule mwenye haki; kwa sababu nimeteswa mengi leo katika ndoto kwa ajiliyake‟ (Mt.27:19).

k.11 Yesu akamjibu kwa huruma na kwa kumkemea. Alijua ilikuwa si kosa laPilato kuwa liwali wakati ule. „yeye aliyenitia mikononi mwako‟ huyu ni nani hasa?Yafikiriwa maneno hayo yamhusu Kayafa pamoja na wenzake waliomkamataYesu na kumleta kwa Pilato na kumsukuma afanye kinyume cha alivyotaka nakinyume cha haki. Nyuma ya yote ni Mungu Baba na mapenzi yake ya kuokoaulimwengu. Hata hivyo, walikuwa na hatia ya uovu huo wa kumtia hatiani mtuasiyekuwa na kosa. Pilato naye alikuwa na hatia, ila haikulingana na ile yaWayahudi. Ijapokuwa mambo hayo yote yalitimiza mapenzi ya Mungu kilamhusika aliwajibika kwa sehemu yake.

k.12 Pilato akazidi kutafuta njia ya kumfungua ila Wayahudi hawakuwa tayariYesu aponyoke mikononi mwake. Walipiku turufu inayoshinda kama silaha yamwisho. Walimkumbusha hatari ya kukipoteza cheo chake, kwa hiyo, achague,ama atoe hukumu Yesu afe ama amwachilie nao watapeleka ripoti mbaya kwaKaisari huko Rumi. Pia aliogopa ghasia itatokea mjini wakati wa Pasaka ambapowatu waliwaka moto wa kutamani uhuru mbali na Warumi.

k.13-16 Kwa maneno yao Wayahudi wakafaulu. Pilato alipoyasikia waliyosemaakaona hana njia ya kujisalimisha na cheo chake isipokuwa kutoa hukumukwamba Yesu afe. Alikuwa amewakinai, ila hakuwa na nguvu ya kufanya haki.

Page 156: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA645

Akaketi juu ya kiti cha hukumu tayari kutoa hukumu yake. Kwa uchungu sanaakamtoa Yesu kwao akitumia maneno ya kuwalipiza kisasa. Alisema „TazamaMfalme wenu‟ maneno ya dhihaka, maneno ya dharau, ndipo akawashurutishawaseme maneno magumu sana „sisi hatuna mfalme ila Kaisari‟. Walilazimishwakukiri kwamba walikuwako chini ya utawala wa Dola ya Kirumi, jambo lililowaudhisana. Bila shaka walisema hayo kwa shida sana, ila walikubali kusema ili Yesuasulibishwe. Jambo hilo lilidhihirisha kiasi cha chuki yao kwa Yesu. Kwa kusema„hatuna Mfalme ila Kaisari‟ walikuwa wamekufuru (Amu.8:23; 1 Sam.8:7)wameacha tumaini la kupata Masihi na msingi wa Agano lao na Mungu. KatikaAgano hilo Mungu alikuwa Mfalme wao na wafalme wao walitawala katika kukirikwamba walifanya kwa niaba ya Mungu. Tokeo lake lilikuwa Kanisa lilishikamahali pa Israeli na tangu hapo makusudi ya Mungu yatekelezwa kwa njia yaKanisa si Israeli (ling.1:11; 12:37ku). Kisha akamtoa Yesu kwa askari iliwamtayarishe kwa kusulibishwa.

Katika habari hiyo yote twaona jinsi Pilato alivyoanza kwa hali ya kutokujali, kamamtu asiyetaka kuhusika. Ndipo akashikwa na udadisi juu ya Yesu, akazidikuvutwa na msimamo wake na kwa muda aliongea naye uso kwa uso. Ndipoalianza kuwa na wasiwasi na hofu, tazama jinsi alivyotoka nje mara kwa mara iliazungumze na Wayahudi:

18:29 Pilato akawatokea nje, akasema, „Ni mashtaka gani.....?‟18:33 Akarudi ndani na kumwita Yesu aongee naye18:38 Akawatokea Wayahudi tena, akawaambia „Mimi sioni hatia.....‟19:1 Alimtwaa Yesu, akampiga mijeledi...19:4 Pilato akatokea tena nje, akawaambia „sioni hatia....‟19:9 Akarudi ndani tena ili aongee na Yesu zaidi19:13 Akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti cha hukumu...

Kwenda nje na kurudi ndani mara nyingi ilikuwa dalili ya wasiwasi. Alikosa amanirohoni kwa sababu alikuwa na uhakika kwamba Yesu hakuwa mkosaji. Hali hiyoya kusita haikuwa kawaida yake jinsi anavyokumbukwa kihistoria.Udhaifu wake ulidhihirika wazi kwa jinsi alivyokawia kumfungua Yesu ijapokuwaalimtangaza mara nyingi kuwa bila hatia. Alitafuta kuridhiana na Wayahudi nakuwatuliza, huku alitaka kumwachilia Yesu, alitafuta asiwakwaze Wayahudi,mambo hayo hayakuwiana. Mwishowe tuliona kiburi chake na hasira yake katikakubishana na Wayahudi na kuwalipiza kisasa na kwa dhihaka kusema „Je!nimsulibishe Mfalme wenu?‟ Huenda dhihaka hiyo haikuwa kwa Yesu kibinafsibali kwa Wayahudi na kwa tumaini lao la kupata Masihi wa kuwaokoa na Warumi.Hivyo Yesu aliuawa kwa siasa ya Kiyahudi pamoja na siasa ya Kirumi, ingawazilipishana zilikutana na kusababisha kifo chake.

Page 157: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA646

19:17-37 Kusulibishwa kwa Bwana YesuKatika sehemu hiyo tuna habari ya tendo la kumsulibisha Yesu; anwaniiliyoandikwa na kuwekwa juu yake; kugawa mavazi; wanawake kuwepo pale naYesu kumkabidhi mama yake kwa Yohana, mwanafunzi wake; na vilio vyamwisho.

k.17-18 Tendo la kumsulibishaPilato alimkabidhi Yesu kwa askari na iwapo Yohana hakutaja jambo hiloyafikiriwa Yesu alipigwa mijeledi kwa ukali kwa desturi yao ya kuwadhoofishawahalifu kabla ya kuwasulibisha. Yesu alipelekwa nje ya mji wa Yerusalemu(Ebr.13:12) mpaka mahali palipoitwa „Fuvu la Kichwa‟ kwa Kiebrania „Golgotha‟na kwa Kilatini Kalvari; kutokana na sura ya mahali pale ambapo palikuwamwinuko. Alibeba mwenyewe mti wa msalaba. Katika Injili zingine tunajuaalishindwa njiani na Warumi walimshurutisha mtu ambebee. Katika wanafunziwote ni Yohana tu aliyekuwepo naye ameandika habari hiyo kwa manenomachache sana. Alitaja tu tendo lenyewe na mahali na wengine wawiliwaliosulibiwa pamoja na Yesu, wala hakusema zaidi. Hakutaka kusisitizamaumivu yake ya kimwili, alijua watu walikuwa wamezoea kuona jambo hilo, nalilikuwa la kutisha sana hata hakuona vema alielezee zaidi. Wahalifuwalitembezwa kwa njia ndefu hali wamevaa kadi au ubao wa kuonyesha kosalao, kusudi wengine wapate onyo kali. Twajua walikuwa na haraka ili Yesuasulibiwe kabla ya kuchwa, kwa hiyo, hatujui kama walikwenda moja kwa mojampaka mahali pa kusulibiwa au walizunguka mjini.

(Kusulibishwa kulitisha sana. Kulifanywa hadharani mwa watu. Ubao wa wimaulikuwa umewekwa tayari ardhini, ndipo ubao wa kukingama uliwekwa chini namhalifu alilazwa juu yake, na misumari ya chuma ilipitishwa katika vifundo vyamikono yake, ndipo wakainua ubao wenye mtu na kuufunga kwenye ubao wawima, kisha wakafunga miguu ama kwa kamba au kwa misumari kwenye ubao.Mtu akaachwa kwenye jua kali ya mchana na katika baridi ya usiku ili afepolepole. Pengine mtu alichukua muda wa siku mbili au zaidi hata juma kufa.Alitaabika sana, akaishiwa maji mwilini, na alipumua kwa shida sana. Kifo hichokilikuwa kibaya mno hata Warumi hawakukitumia kwa watu wao hata ikiwawalikuwa wabaya sana na kama mmoja wao alisulibiwa ilihitaji idhini ya Kaisari).

k.18 Yesu aliwekwa kati ya wahalifu wawili waliosulibiwa pamoja naye.Yawezekana Baraba angalikuwa pale kama watu wangalimchagua Yesu badalayake. Huenda hao wahalifu walikuwa washiriki wa Baraba. (katika Luka 23:40-43tuna habari ya mmoja kumwamini Yesu). Kumweka Yesu katikati kulikuwa daliliya Yeye kuwa mbaya zaidi na kwa kufanya hivyo Pilato alizidi kuonyesha dharaukubwa kwa Wayahudi. Ila kwa Mungu Yesu kuwa katikati ya wahalifu iliashiriaheshima yake kuu ya kuwa Mwokozi wa Ulimwengu na kazi yake maalum yakuwa mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu. Alikuja ulimwenguni ili awaokoewenye dhambi (Isa.53:12). Katika Kufa Kwake

Page 158: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA647

alitimiza makusudi makuu ya ajabu ya Mungu yaliyokusudiwa hata kabla yakuumbwa kwa ulimwengu (1 Pet.1:18-20; Ufu.38:8). Yeye aliyeishi katika faharina utukufu na raha ya mbinguni alifanyika mwili akafika duniani kisha akashukampaka pande za chini kabisa na kuonja maudhi, aibu, dharua na shida na kutoanafsi yake kuwa fidia ya dhambi. Kutundikwa msalabani kulihesabiwa kufa chiniya laana ya Mungu kama Torati ilivyosema (Kum.21:23; Gal.3:13).

Yesu alisulibiwa

Page 159: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA648

k.19-22 Anwani iliyowekwa juu ya msalabaKwa kawaida wahalifu walitembezwa mjini kwanza, hali wakibeba tangazo lamakosa yao ili watu waelewe sababu za kusulibiwa kwao na kuonywa. Ndipotangazo liliwekwa juu ya msalaba ili iwe dhahiri kwa wote ni kwa kosa gani yulemtu alitundikwa pale. Ila ugomvi ulitokea baina ya wakuu wa makuhani na liwaliPilato kuhusu maneno ya anwani iliyowekwa juu ya msalaba wa Yesu. Pilatoalitawala yaliyoandikwa na maneno yalilingana na mashtaka ya kwanzayaliyoletwa na wakuu juu ya Yesu kudai kuwa Mfalme wa Wayahudi. Wakuuwalitaka ayabadili maneno ili yasomwe kwamba Yesu alidai kuwa Mfalme waWayahudi si kwamba Yeye ndiye Mfalme wa Wayahudi. Pilato, ambayealitangatanga wakati wa hukumu hakuwa tayari kuridhiana nao tena, akakazamsimamo wake na kusema kwa ufupi na kwa mkato na kwa mamlaka„Niliyoandika, nimeyaandika‟. Tena iliandikwa kwa lugha tatu, kama kuonyeshakwamba Yesu anahusika na ulimwengu mzima. Yawezekana Pilato alitaka kwamara ya mwisho kuonyesha dharau kwa Wayahudi kwa maneno ya kejeli. Nikama kusema „ikiwa huyo ni mfalme wenu, inasema nini juu yenu na taifa lenu?Wakuu wa Wayahudi walikuwa wamemfedhehesha yeye, yeye naye aliwalipizakisasi na kuwafedhehesha zaidi. Huenda Pilato kwa kutumia maneno hayoalikuwa akidokezea kwamba aliamini Yesu kuwa mfalme. Zaidi ya yote manenohayo yalitangaza ukweli wa Yesu kuwa Mfalme ambaye anatawala kutokaMsalaba na kwa njia ya kufa ni mshindi bila vita na kutumia mabavu.

k.23-25a Kugawa mavazi yakeIlikuwa desturi askari waruhusiwe kuchukua mavazi ya msulibiwa kama zawadiyao kwa kazi hii ngumu. Inaonekana askari wanne walishughulikia jambo hilo namavazi ya Yesu yaligawiwa kati yao, kanzu, viatu, kitambaa cha kichwa na mshipina kila askari alipata moja moja. Lilibaki vazi lililofumwa moja kwa moja bilakufumwa kipande kwa kipande na waliona vema wasilirarue bali wapige kura ilimmoja wao apate vazi zima. Katika jambo hilo Yohana aliona Maandikoyalitimizwa (Zab.22:18). Katika sehemu hiyo alitaja Maandiko kutimizwa maratatu (k.24,28,36,37; Ling.na Zab.22:14ku). Kwa kutaja Maandiko mwandishiYohana alitaka tuone ya kuwa mapenzi ya Mungu yalitendeka, ijapokuwa askarihawakutambua jambo hilo, hayo waliyofanya kwa hiari na kwa kufuata desturiyao yalilingana na mapenzi ya Mungu.

k.25b-27 Uaminifu wa Wanawake waliofuatana na YesuKatika masaa hayo yote ya mwisho mambo yametawaliwa na adui zake Yesu ilapale Msalabani walikuwapo baadhi ya wanawake waliomfuata tangu Galilayawakimhudumia kwa mahitaji ya kimwili. Hao walithubutu kukaa karibu naMsalaba wakimfariji kwa kuwepo kwa ukaribu na kushiriki masaa yake yamwisho. Pia walitaka kuwa pamoja na Mariamu mamaye katika kipindi hichokigumu cha kumwona Mwana wake akifa kwa maumivu makali na katika aibukubwa. Hao walikuwa wangapi na akina nani? Yohana ametaja wanne, huendawalikuwapo wengine pia (Ling. Mk.15:40, Mt.27:56). Walikuwa waaminifu kwaYesu mpaka mwisho, tofauti na wanafunzi wa kiume ambao wameishakimbia

Page 160: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA649

na kujificha. Bila shaka Yesu aliumizwa sana alipomtazama mama yake haliamejaa majonzi rohoni wala hakuweza kumsaidia. Yohana hakutoa habari yandugu zake, huenda hawakuwapo, maana hawakumwamini mpaka baada yaKufufuka Kwake (7:5). Tena waliishi kaskazini, huko Kapernaumu. Katikamaneno aliyoyasema katika saa yake ya mwisho Yesu alifunua yaliyokuwamomoyoni mwake. Jambo kubwa lilihusu utunzaji wa mama yake, akamkabidhi kwaYohana, yule mwanafunzi aliyebaki pale. Aliposema na mama hakutumia nenola kawaida la mama bali lile la „mwanamke‟. Hakutaka kumwongezea shida kwakumkumbusha uhusiano wa kipekee ya „mama‟ na „mwana‟. Kimwili, ndiouhusiano wao, ila kiroho Yeye ni Bwana wake na Mwokozi wake, na kwa kifochake cha ukombozi huzuni zake na zote za kibinadamu zitatibiwa. InaonekanaYohana na Yesu walikuwa binamu kwa upande wa mama. Yesu alikuwa akiunda„jamii mpya ya wanadamu‟ familia mpya ya watu wa Mungu, ya wale wotewanaomkubali na kumpenda na kumtii (Mt.12:47-50). Yohana akaitika mara nakumchukua Mama nyumbani kwake. Yawezekana alimwondoa Mariamumapema kabla ya mwisho ndipo akarudi ili atazame mambo ya mwisho ili awe nahabari kamili ya kumpasha Mariamu. Kwa jambo hilo twajifunza kwamba Yohanaalijitwika wajibu wa kumtunza Mariamu.

k.28-30 Kifo cha Yesuk.28 Yohana ameeleza mazingira ya matukio hayo ya mwisho „Yesu hali akijuaya kuwa yote yamekwisha kumalizika‟ (ling. na 13:1ku. na 17:1 na „saa yakekufika‟). Alijua halijabaki neno lolote limpasalo kufanya katika kutimiza mapenziya Babake. Hatua zote zilizomfikisha kwenye maumivu yake makali na kufakwake zilikuwemo katika mpango wa Baba na wa utii wake mpaka kufa. Kwahiyo, alipotambua hayo alitamka maneno „naona kiu‟. Hakuna haja ya kuendeleana kutaabika ikiwa ameishafanya ule ukombozi wa ulimwenguuliokusudiwa. Taabu moja kubwa ya kusulibiwa ilikuwa kuishiwa maji mwilini nakusikia kiu kali, na maneno hayo ni ishara ya ukweli wa maumivu yake na ya Yesukufanyika mwili. Askari walitumia kinywaji cha divai iliyochanganywa na siki yabei rahisi na waliosulibiwa walipewa kunywa ikiwa walikiomba. Ni ajabu kuonakwamba Yeye aliyetoa Maji ya Uzima (4:14; 7:37,38) na kuita yeyote mwenye kiuaje kwake hapo alikufa katika hali ya kusikia kiu kali. Ni vema tutafsiri maneno„naona kiu‟ kuwa yanahusu maumivu ya kimwili. Hata hivyo twaweza kuongezakwa kusema Yesu alikufa katika hali ya kusikia kiu ya kuwaokoa watu, alitamanisana kuokoa roho za watu, hii ndiyo sababu kuu ya kutundikwa pale. Pamoja nahayo alikuwa na kiu ya kumtii Baba na kufanya mapenzi yake. Alitamani sanakurudi kwa Babaake. Kwa kiu yake watu watapata uzima wa milele, atakata kiuza wanadamu na Kwake watapata raha na amani, furaha, na utoshelevu wa kweliwa maisha. (Mwanzoni mwa kusulibiwa wahalifu walipewa kinywaji chakuyapunguza maumivu yao na Yesu alikikataa kwa sababu alitaka kuwa na akilitimamu ili afahamu anayofanya katika kuwa dhabihu ya dhambi, hachukuliwikama mnyama asiyefahamu sababu ya kuuawa kwake (Mk.15:23; Ebr.10:4ku).

Page 161: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA650

k.30 Baada ya kuinywa ile divai Yesu alipata nguvu ya kusema tena neno mojala maana sana „Imekwisha‟. Ni ushuhuda wa ushindi wake. Ametimiza yale yoteyaliyomleta hapa duniani, yote ambayo Baba alimtuma ayafanye, yaaniukombozi wa ulimwengu. Katika udhaifu wa kukaribia kukata roho alikuwa naufahamu wa kutosha kujua kwamba ameutimiza kabisa utume wake (17:4).Alikuwa mshindi, si mshindwa. Bila shaka kinywaji alichopokea kilimsaidia kupatasauti ya kutoa tangazo hilo. Kumbe! kwa kifo chake ulimwengu umekombolewa,ametoa dhabihu itoshayo kusamehe na kuondoa dhambi zote za watu wote wawakati wote. Katika kufa kwake amefanya kazi kubwa mno, udhaifu waMungu-Mwana ulikuwa na nguvu kupita uwezo wote wa kibindamu. Imekwisha -itikio lake kwa utume wa Baba; ufunuo wa kumfunua Baba; na ukombozi waulimwengu ulioumbwa na Baba.

Akainamisha kichwa, neno sawa na lile la Mt.8:20; Lk.9:58 kueleza mtu kwendakulala, alikufa katika amani na hali ya kumtegemea Baba, alikufa katika utii wakumkabidhi Baba roho yake (Lk.23:46). Alikufa kwa hiari ya kuisalimu roho yake(10:11) alikuwa na madaraka mpaka mwisho kabisa. Neno lililotumika halikuwalile la kawaida kwa kufa, uhusiano wake na mauti si kama yetu.

k.31-37 Pigo la mkuki ubavuni na mazikoIjapokuwa Yesu ameishauawa viongozi wa Wayahudi hawakuwa na amani kwasababu ya uangalifu wao wa kutimiza hata masharti madogo ya dini yao. Haowaliosababisha kifo cha Yesu walikuwa watu walioshika sana dini yao. Sheriayao ilisema kwamba miili ya waliosulubiwa isikae misalabani baada ya jioni ileiliyoamkia Sabato hasa ikiwa ilikuwa Sabato ya Sikukuu. (Walijali mambo hayomadogo huku wamemwua mtu asiyekuwa na hatia, tena yule aliyedai kuwaMasihi wao na Mwana wa Mungu - hali hii ya kufuata madogo na kuachamakuu Yesu alikuwa amewashtaki hapo nyuma Mt.23:23). Hivyo Maandikoyalitimizwa, Kut.12:46; Hes. 9:12 kuhusu kondoo wa Pasaka; Zab,34:20 juu yamwenye haki. Ilikuwa desturi ya Warumi kuvunja miguu ya wahalifu. Lilikuwatendo la ukatili pamoja na tendo la huruma ya kuharakisha kifo. Walianza kwawale wa upande wa kulia na wa kushoto ndipo wakaja kwa Yesu aliyekuwa katinao wakamkuta amekwisha kufa. Kwa mazoea yao kikazi askari walielewakabisa ikiwa mtu amekufa au amezimia tu. Habari hiyo inashuhudia ukweli waYesu kuwa amekufa.

k.34-35 Walipomkuta ameishakufa basi askari mmoja akamchoma ubavuni namkuki na maji na damu vilitoka. Ushuhuda tena wa ukweli wa kufa kwake, maanaikiwa ni damu tu iliyotoka iliwezekana awe angali hai ila kwa sababu maji piayalitoka ni ushuhuda wa kuthibitisha ukweli wa kufa na ya kwamba alikuwa namwili kweli sawa na wanadamu wengine, hakuwa njozi tu. Yohana mwandishindiye aliyeona jambo hilo na kusisitiza ukweli wa hayo aliyoyaona, kusudi watuwaamini kabisa kwamba Yesu alikufa kweli. Kwa hiyo ijapokuwa ni mwanafunzimmoja aliyetoa ushuhuda juu ya jambo hilo vilevile ushuhuda ni katika tendo laaskari waliomchoma mkuki.

Page 162: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA651

Wengi wametoa mawazo kuhusu maji na damu wakihisi juu ya maana yake. Kwawengine ni ishara ya uzima na utakaso ulio matokeo ya Kifo cha Yesu, Yesualisema kwamba Roho haji mpaka amekufa na ikiwa damu ni ishara ya ukombozindipo maji ni ishara ya Roho na uzima unaoletwa na Roho, wakilinganisha namaneno kwa Nikodemo (3:1ku) na Mwanamke Msamaria (4:1ku) na manenoyake wakati wa Sikukuu ya Vibanda (7:50ku). Wengine wameona kwamba niishara ya Yesu kuvunjika moyo, si kwamba alikufa kwa ajili ya maumivu ya kimwilihasa bali kwa ajili ya masononeko ya roho, au kwamba moyo ulishtuka kwa ajiliya uzito wa moyo. Haidhuru tumaanishe jambo hilo kwa njia fulani hasa linamaana ya kuwa Yesu alikuwa amekufa kweli. Hilo ni jambo kubwa kwa sababuwapinzani wa Ukristo husema kwamba Yesu hakufa kweli, bali alizimia, ndipokatika baridi ya kaburi alipata nafuu.

k.36-37 Katika hayo yote Yohana aliona kwamba Maandiko yametimizwa naYesu hakufa kwa bahati nasibu bali katika mapenzi ya Mungu yaliyotabiriwazamani zaidi ya miaka elfu.

19:38-42 Kuzikwa kwa Bwana YesuNdipo Yusufu wa Arimathaya alionekana kwa mara ya kwanza kuwa mhusikakatika maziko ya Yesu. Injili zote nne zimemtaja. Alikuwa mjumbe wa Sanhedrin(Mk.15:43; tajiri (Mt.27:57) na mwanafunzi wa siri wa Yesu (Mt.27:57; Lk.23:5).Alijitoa kwa wazi, alithubutu kwenda kwa Pilato na kumwomba apewe mwili waYesu. Miili ya waliosulibiwa ilikuwa mali ya Warumi na kwa kawaida amawaliiacha misalabani ili ndege waile au walitoa kwa jamaa ikiwa walihukumiwamakosa fulani ila kwa kosa la mapinduzi serikali haikukubali kuitoa. Wayahudiwaliwazika mahali pa pekee nje ya mji ili wasiyanajisi makaburi yao ya kawaidi.Pilato, katika kumruhusu Yusufu auchukue mwili wa Yesu alifanya kinyume chadesturi yao, maana Yesu alisulibiwa kama mwana mpinduzi.

k.39 Nikodemo alijiunga na Yusufu na kumsaidia katika maziko. Nikodemoalikuwa ametajwa hapo nyuma katika Injili hiyo. Ni yule aliyemjia Yesu usiku(3:1ku) halafu akajaribu kumtetea Yesu barazani (7:50ku). Yusufu alishughulikiamambo ya ruhusa n.k. huku Nikodemo alishughulika mambo ya dawa na sandan.k. Kwa kazi hiyo kubwa ya haraka huenda walisaidiwa na watumishi wao,maana uzito wa manemane na uudi ulikuwa kama ratli mia pamoja na uzito wamaiti. Hao walikuwa wapi Yesu alipohukumiwa? Pengine kwa sababu Barazaliliitishwa haraka usiku huenda hao hawakuitwa au walishindwa kufika.Tukumbuke walijitokeza huku hawana habari kwamba Yesu atafufuka kutokawafu. Waliona wamewajibika kuonyesha utiifu wao, iwapo wamechelewa sanakufanya hivyo. Manemane na uudi ni manukato yaliyotajwa katika Zab.45:8;Mk.2:11. Yawezekana walitumia dawa hiyo kupunguza mnuko mbaya wa kuozakuliko kuihifadhi maiti isioze kama desturi ya WaMisri. Walitia dawa katikati yavipande vya vitambaa kisha wakaiweka maiti katika kaburi jipya ambalohalijatumiwa bado, lililokuwapo katika bustani iliyokuwa karibu.

Page 163: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA652

Yafikiriwa kaburi hilo lilikuwa mali ya Yusufu. Hayo yote ni dalili ya Yesu kuzikwakama Mfalme. Kiasi cha dawa kilichotumiwa ni kile kilichotumiwa kwa wafalme,tena kaburi lilikuwa jipya bila kutumiwa, tena lilikuwa mahali pazuri, katikabustani. Yesu alikuwa amedhiliwa sana sana pale Msalabani, tangu hapoatainuliwa na kupewa jina lipitalo kila jina (Flp.2:5-11). Kwa kuwa ni yeye tualiyewekwa kaburini ni maiti moja tu ambayo haitaonekana siku ya tatu (Isa.53:9).Ni ajabu kwa mambo hayo yote kufanyika kabla ya kuanza Sabato kuu yaPasaka, kwa sababu tangu jioni ile wasingaliruhusiwa kufanya kazi hiyo.

MASWALI1. Umejifunza nini kuhusu kielelezo cha Bwana wakati wote wa kuhukumiwa

kwake?2. Umejifunza nini kwa hali ya liwali Pilato, mhukumu wake?3. Je! Kanisa lifanye nini linapobanwa na mambo ya siasa? Zungumza habari

hiyo katika vikundi4. Katika Kufa kwake Yesu alikuwa akifanya nini zaidi ya Kufa? Eleza maana

na umuhimu wa Kifo chake kwa waumini wote?5. Ni mambo gani yanayoonyesha kwamba Yesu alikuwa na mwili wa kweli

wa kibinadamu?Ni mambo gani yanayoonyesha kwamba Yesu alikuwa amekufa kweli?

6. Kwa nini Nikodemo na Yusufu wa Arimathaya walijitokeza na kufanyashughuli nzuri ya kumzika Yesu? Je! wadhani kwamba walikuwawameandaa kufanya jinsi walivyofanya? Je! wadhani kwamba walikuwawamekumbuka jinsi Yesu alivyosema kwamba atafufuka? Wafikirije?

7. Onyesha jinsi utawala wa Mungu ulivyoonekana katika Kufa na Kuzikwakwa Yesu?

20:1-29 Kufufuka kwa Bwana YesuYohana ametoa habari ya Ufufuo kwa kutaja wafuasi mbalimbali wa Yesuwaliokuwa wa kwanza kujua habari hiyo kwa njia mbalimbali. Pamoja na hayoametumia ushuhuda wa vitu kadhaa kama kaburi kuwa wazi na vitambaakuachwa mle ndani.

Kwa upande wa wanafunzi Yohana ameandika kwa kukumbuka hali zao ndipoalionyesha mabadiliko yaliyotokea katika hali hizo. Mariamu Magdalenealishikwa na huzuni kubwa; wanafunzi walishikwa na hofu nyingi; Tomasoalishikwa na mashaka. Mariamu aligeuzwa kuwa mjumbe wa ufufuo kwawenzake. Hofu za wanafunzi ziligeuzwa kuwa furaha, na mashaka ya Tomasoyaligeuzwa kuwa imani. Kwa hiyo, jambo kubwa kwa Yohana, si katika Yesukuonyesha nguvu ya ufufuo bali katika Yesu kuonyesha upendo wa ajabu nakuwatokea wanafunzi kwa lengo la kuwajenga, akimsaidia mmoja mmojakufuatana na hali na mahitaji yake, ili kwa pamoja waanze maisha mapya.

Page 164: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA653

k.1-2 Mapema sana baada ya Sabato kuu kupita wanawake waliamka mapemana kwenda kaburini ili waipake maiti ya Yesu kwa mara ya mwisho na kumalizakazi iliyofanywa kwa haraka jioni ya kufa kwake. Kulinganisha na Injili zingineinaonekana kundi fulani la wanawake waliondoka wakishikwa na hamu yakuishughulikia maiti ya Yesu huku wamesahau kwamba jiwe lilikuwa limewekwamdomoni mwa kaburi. Yohana ameandika kama Mariamu Magdalene alikuwapeke yake, huenda hakwenda peke yake, maana katika k.2b alisema „hatujuiwalikomweka‟. Alipofika alikuta nini? „akaliona lile jiwe limeondolewa‟. Kwakawaida jiwe zito liliwekwa katika mfuo, kwa hiyo, haikuwa kazi ngumu sanakuliweka, ila ilihitaji kundi la watu kulitoa katika mfuo na kuliondoa. Kumbe!limekwisha kuondolewa. Na nani? Wanawake hawakutazamia kuwa litakuwalimeondolewa. Wenyewe hawakuwa na nguvu za kutosha kuliondoa. Kamawanafunzi wamefanya, hawakuwaambia wanawake wala akina Petro naYohana. Yohana na Petro walikuja mbio, kama ni mara ya kwanza kufika. Aduizake Yesu hawakuwa na sababu yoyote ya kuwavuta pale, wao walitaka mwiliwa Yesu ukae humo daima. Inaonekana jiwe liliondolewa na nguvu za Mungu tu.Mariamu alifanya nini alipoona jiwe limeondolewa? Hakubaki pale ila mara mojaakaenda mbio na kumwambia Petro na Yohana. Hakuchungulia ndani, akaamuamara moja kwamba mwili wa Yesu umeondolewa.

Halafu Yohana alisisitiza ushuhuda mwingine, ushuhuda wa vitambaa na jinsivilivyolala mle kaburini.

Walipoambiwa habari ya jiwe kuondolewa Petro na Yohana wakaja mbiokaburini. Mmoja, Yohana, alikuwa wa kwanza kufika, naye akainama nakuchungulia ndani. Ijapokuwa lilikuwa giza mle ndani akaweza kuviona vitambaavimelala (vingekuwa vyeupe). Huenda alidhani kwamba mwili umo. Petroalipofika, akaingia mara moja, naye akaviona vitambaa na jinsi vilivyolala, pialeso peke yake mahali ambapo kichwa cha Yesu kilikuwa kimelala. Kisha Yohanaakaingia, na twasoma kwamba akaona na kuamini. Katika muda wa kukaa nje,alikuwa na nafasi ya kuzingatia mambo hayo ya vitambaa. Ndipo alipoona mwilihaupo akatambua maana ya vitambaa kulala jinsi vilivyolala, ushuhuda wa Yesukuwa amevipitia, mfano wa nyoka kuambua ngozi yake au kipepeo kutoka buulake, hata kuvua hakuvivulia. Yohana alikuwa na uhakika kwamba hakunaaliyemwondoa Yesu, maana ingalikuwa vigumu sana mtu afungue vitambaa nakuviacha na manukato yangalianguka chini. Tena ni nani ambaye angalipotezamuda wa kufanya hivyo? tena atapata faida gani? Kwa kawaida wezi hufanyaharaka ili waondoke mapema iwezekanavyo. Kumbe, Yesu katika upendo wakemkuu, alifahamu hali ya utambuzi wa kiroho wa Yohana, akamwachia vitu vyakuuvutia usikivu wake wa kiroho na yeye na Petro waliachiwa ushuhuda wa vilevitambaa. Hawakuona dalili zozote za kaburi kuvamiwa hivyo twasoma wakarudinyumbani kwao, jambo la ajabu kufuatana na jinsi walivyokuta mambo kaburini.Huenda sababu ilikuwa kumjulisha mama yake Yesu jinsi mambo yalivyokuwa,maana walipoondoka

Page 165: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA654

kwa haraka yeye angalibaki na mashaka mengi. Pia, wasubiri kuona yatatokeanini mchana ule.Mmoja ameandika kwamba jiwe liliondolewa si kwa Yesu kutoka bali kwawanafunzi kuingia na kuushuhudia utupu wake isipokuwa kwa vile vitambaa.(Ilikuwa desturi kutia muhuri kwenye kaburi kwa sababu mara kwa mara weziwaliyavamia makaburi, hata hali hiyo ilipozidi Kaisari Klaudio (B.K.41-44) aliagizaadhabu iwe ya kuuawa kwa wale waliokamatwa).Twaona Yesu alisema kwamba imani inayotegemea Maandiko ni bora(Zab.16:9-11).

Mariamu Magdalene, Petro na Yohana, walijaliwa kufika kaburini mapemaasubuhi ile, na kupata ushuhuda wa kaburi kuwa wazi na vitambaa kuwemo halivimelala, ili waone mambo hayo kabla wengine hawajapata habari hizo na kablaya kaburi kuvamiwa.

k.11-18 Yesu alimtokea Mariamu MagdaleneYesu alimtokea Mariamu kabla ya Mitume. Hatuna habari yoyote kama alimtokeamama yake mwenyewe au siyo. Inaonekana Mariamu alirudi kaburini hali akiliana kuinama na kuchungulia ndani. Petro na Yohana wameishaondoka. Vitambaahavitajwi, ila malaika wametajwa nao walikuwamo ndani kama walinzi wa mahalipale. Mariamu hakushtuka alipowaona. Wakamwuliza sababu ya kulia kwake?Swali la ajabu kwa yule aliyefiwa na rafiki yake mpendwa, ila lilikuwa swali kamakumkemea kwa sababu uhalisi wa mambo hayo ni kwamba Yesu yu hai. Ilikuwawakati wa kufurahi si wa kulia, na swali lao si mzaha bali lilidokezea uhalisi huo.Akajibu kwamba analia kwa sababu hakujua mwili wa Yesu umewekwa wapi.Mawazo yake yote yalitawaliwa na haja ya kuupata mwili wa Yesu. Kwa hiyofaraja yake ni katikakujua mahali ulipowekwa. Ndipo lilitokea jambo ambalo lilimfanya ageukenyuma. Pengine malaika walielekeza nyuso zao nje, au pengine alisikia kishindonyuma yake kama mtu yuko. Hatujui lilikuwa nini ila twajua Mariamu akageukaakamwona mtu aliyemdhani kuwa mtunza bustani. Mawazoni mwake alidhanikwamba huenda ni yeye aliyeuondoa mwili au yeye atapajua mahali ulipo. Niayake yote ni kuupata mwili wa Yesu na kuuhudumia. Kumbe! yule mtu ni YesuMwenyewe katika hali ya kutokutambulika mara. Yesu ameingia utaratibu mpya,hakuhuishwa na kurudishwa kwenye hali yake ya hapo nyuma. Huyo Yesualimwuliza swali lilelile la malaika „Mama unalilia nini?‟ ndipo akaendelea kwakuuliza „Unamtafuta nani?‟ swali la kumpa changamoto, amwaze kwa upya yulealiyemfahamu hapo nyuma. Mariamu akamjibu kwamba kama anapajua mahaliulipo mwili wake amwambie. Ndipo Yesu akajifunua kwake kwa neno moja tu,akatamka jina lake kama alivyozoea kulitamka siku zote za hapo nyuma. Nenomoja lilitosha kabisa kupenya machozi ya Mariamu na kugeuza huzuni yakekuwa furaha, kumbe, Bwana wake yu hai, Yesu mwenyewe alikuwa amesimamambele yake na kusema naye. Akaitika kwa kusema „Raboni‟. Kwa upole sana nakwa upendo mwingi Yesu alijitambulisha kwake. Mchungaji mwema ajua kilakondoo wake na kumwita kwa jina lake na

Page 166: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA655

kondoo waitambua sauti yake. Yesu hakujifunua na kuwatisha walewaliosababisha kuuawa kwake, ila kwa wafuasi wake kibinafsi tu.

Katika furaha yake alitaka kumshika Yesu, hakutaka kuachana naye, ila Yesuhakumruhusu. Alitoa sababu kwamba „sijapaa kwenda kwa Baba‟. Maneno hayoyamewatatanisha wataalamu kuhusu maana yake hasa kwa sababualimkaribisha Tomaso amguse. Huenda maana yake ni kwamba Mariamu hanahaja ya kumshika sana sasa kwa sababu ataendelea kuwa nao kwa muda nanafasi zitapatikana mpaka atakapopaa ndipo ataachana nao. Wakati huo niwakati wa kufurahi na kushirikisha wengine habari njema ya kufufuka kwake.Mariamu amekosa kuelewa mambo mawili, jambo la kwanza, Yesu haondokimara moja, na pili, Yesu ataondoka baada ya muda. Pamoja na hayoyawezekana Yesu alisema maneno hayo kwa busara akimwelekeza kwa jambomoja kubwa la mbele, kwa wakati atakapowaacha kabisa. Muda wa siku arobainiatawatokea na kutoweka ili wahakikishiwe ukweli wa kufufuka kwake, na ya kuwaYeye yu hai, wala hafi tena. Yalikuwa maneno ya hekima sana kwa Mariamu,yalimfaa, yalimwelekeza atafakari mambo ya mbele, wakati Yesuatakapowaacha kabisa. Kufufuka na kupaa kumefungamana. Pamoja namaneno hayo Yesu akampa jambo la kufanya, kwa upendo akampa kazi yaheshima, kazi ya maana sana, kazi ya kuwajulisha wanafunzi wake kwambaYeye yu hai, naye atapaa na kurudi kwa Babaye. Njia za Mungu si za wanadamu,wa kwanza kupewa kazi ya kuwaambia wanafunzi, alikuwa mwanamke. Nimwanamke mlei aliyewajulisha Mitume habari za Yesu kufufuka. Yesu aliwaitawanafunzi „ndugu zangu‟ ijapokuwa walikuwa wamemwacha alijuahawakukusudia kufanya hivyo, ila katika udhaifu wa kimwili ilitokea hivyo.Anaunda jamii mpya ya wanadamu, ya wale waliokombelewa na kumtumaini kwawokovu. Alipotaja Baba, hakusema „narudi kwa Baba yetu‟ bali kwa „Baba yanguna Baba yenu‟. Ni Baba yake kwa asili moja, yu umoja naye. Ni Baba yetu kwaneema na kufanywa mwana kutokana na ukombozi wa Yesu. Kwa kifo chakeupatanisho umefanyika na uhusiano mpya umepatikana, Yesu ni Mwana pekeewa Baba na wamwaminio waushirikishwa uana wake.

k.18 Mariamu akaondoka, akatimiza wajibu wake, akawaendea wanafunzi wakena kuwaambia wazi „nimemwona Bwana‟ na ya kwamba ametumwa kuwaambiakwamba Yeye yu hai.

Jambo la Ufufuo wa Yesu, si jambo la dhana, ni jambo lililotokea kweli, kaburimoja lililokuwapo, la Yusufu wa Arimathaya, lilitunza maiti ya Yesu kwa mudamfupi, ndipo katika siku moja, yaani, siku ya kwanza ya juma iliyofuata Pasakaya kama B.K.33 Yesu alitoka kaburini hali yu hai, akawatokea watu binafsiwaliojulikana na jamaa na jirani zao.

(Jambo la Yesu kutokutambulika mara: Wawili waliokwenda Emauhawakumtambua mpaka baadaye (Lk.24:26) Wanafunzi waliokwenda kuvuasamaki hawakumtambua mara (Yn.21:4) na hapo juu tumeona ya kuwa

Page 167: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA656

Mariamu hakumtambua mara. Katika Marko 16:12 tunayo maneno „ana suranyingine‟. Ila pia tunayo maneno ya kuonyesha ni Yesu yuleyule aliyewatokea.Mwili wake uliguswa (k.27; Lk.24:39; ulikuwa na jeraha (Yn.20:20,25,27) alipikasamaki (21:9) akala (Lk. 24:41-43). Kwa upande wa pili alifufuka kwa kupitiavitambaa vya maziko na kuta za kaburi; akatokea chumbani hali milangoimefungwa (20:19,26). Kuendelea kulikuwepo kati ya mwili wa Yesu kabla yakufa na mwili wake baada ya kufufuka. (Taz.1 Kor.15:35ku. 1 The.4:13-18).

20:19-23 Yesu aliwatokea mitumeHabari hii inalingana na Luka 24:36ku. ila Yohana ameeleza mengine kwatofauti. Kama ilivyokuwa desturi yake Yohana ametaja wakati; ilikuwa „jioni‟ yasiku ya kwanza. Mitume na wanafunzi wengine walikuwa wamekutana pamojachumbani, pengine kile walichotumia wakati wa kula Pasaka siku tatuzilizotangulia. Mchana kutwa walikuwa wamesikia mambo yaliyowashtusha.Mpaka hapo Yohana ameamini, Mariamu Magdalene ameshuhudia kwambaamemwona Yesu, ila wanafunzi wengine walikuwa bado hawajapata kuaminikwamba Yesu yu hai. Waliogopa kwamba Wayahudi watawatafuta, nakuwashtaki kwamba wameuiba mwili wa Yesu kwa sababu ya kaburi alilowekwalilikuwa wazi na tupu. Walijificha mle ndani hali wamefunga milango.

„akaja Yesu, akasimama katikati‟. Inaonekana Yesu alipitia milango na ukuta, kwakuwa tumeambiwa kwamba milango ilikuwa imefungwa na hatuambiwi kwambaYesu aliifungua. Ndipo akawasalimu kwa neno „amani‟ kama desturi ya Kiyahudi.Alirudia kulitumia tena (k.21). Neno kwa Kiebrania lilikuwa na maana zaidi yakutokuwepo kwa matatizo, lilikuwa na maana ya afya bora na maisha mazima.Kila Waraka wa Agano Jipya unaanza na salaam za neema na amani. Kipawahicho cha amani ya kweli ni cha kwanza katika historia ya ulimwengu. Katikakuwasalimia kwa jinsi hiyo Yesu aliwathibitishia msamaha wake kwa udhaifu waowa kumwacha wakati wa dhiki zake kuu; hakuwalaumu wala kuwakemea. Ndipoakawaonyesha mikono yake na ubavu wake, vilivyokuwa na majeraha yamisumari na mkuki. Alama hizo ziliwahakikishia kabisa kwamba ni YeyeMwenyewe. Wengine walikuwa na alama za misumari ila ni Yeye tu aliye najeraha la kuchomwa mkuki (19:32-35). Hayo majeraha yaliashiria gharama yakifo chake. Amani aliyowapatia imetokana na kifo chake cha upatanisho.Amewapatanisha na Mungu, amesamehe dhambi zao, na sasa awapa amaniyake. Aliendelea pale alipoachia mazungumzo yake kabla ya kukamatwa (16:33).Mara huzuni yao iligeuzwa kuwa furaha kama alivyowaahidi hapo nyuma (14:18;16:20-22).

k.21 Yesu akarudia kusema „amani iwe kwenu‟ ndipo aliwaelekeza kuhusumambo yaliyo mbele yao, yaani utume wao unaotokana na Utume wake. KamaBaba alivyomtuma Yeye, Yeye, Yesu aliyefufuka, awatuma wao. Katika Injili hiyoyote Yohana amesisitiza uhusiano wa umoja na wa ukaribu kati ya Yesu na Babayake. Yesu ni Yule aliyetumwa (5:36; 7:29; 8:42; 10:36; 13:20; 20:21) na Babandiye aliyemtuma (3:17; 4:34; 5:23; 6:44; 7:18; 8:29; 11:42; 12:44ku.

Page 168: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA657

13:15; 14:24; 15:21; 17:8). Hoja hiyo ni kama uzi unaopitia kila sura. Kwa hiyo,kufanana na Yesu ni kuwa mpelekwa. Si kwamba wafuasi wake wanamshikiabali Utume ni ule mmoja; wa Mwana katika maisha yake hapo duniani, na waMwana katika maisha yake ya Ufufuo katika maisha ya watu wake. Kwa sababuhiyo wanaotumwa wameshirikishwa mamlaka yake (Mt.28:18-20). Msingi wautume wao ni utii kama ulivyokuwa msingi wa utume wa Yesu. Yesu ataendeleakuwa kiongozi wao kutoka mbinguni naye ataendelea kuwaombea kwa Baba(17:18). Hivyo Utume wake na utume wao umefungamana.

k.22 „akiisha kusema hayo, akawavuvia‟ Neno „vuvia‟ ni lile lililotumika katikaMwa.2:7 na Eze.37:9, lahusu uumbaji mpya, uzima kutolewa kwa „wafu katikadhambi‟ watakapohuishwa na Neno la Injili (Mt.16:19; 18:18). Kwa tendo hiloYesu aliashiria ule uwezo watakaopewa, siku ya Pentekoste, uwezo wa RohoMtakatifu, nao watautekeleza utume wao katika nguvu zake. Ni uwezo uleuleuliomfufua Yesu na kumpandisha mpaka mkono wa kuume wa Baba (Efe.1:18).Alipovuvia (tafsiri nzuri ni alivuvia si aliwavuvia) hakutoa kipawa cha Rohopalepale. Kipawa cha Roho kilitolewa siku ya Pentekoste, ila alitoa ishara yakuwajulisha kwamba ile ahadi ya Roho waliyopewa, itatimizwa hivi karibuni naowatapata Roho. Wakati ule hawakubadilika sana, waliendelea kushikwa na hofu(k.26) baadhi walirudia kuvua samaki (21:1ku) ila kuanzia Siku ya Pentekoste halizao zilibadilika kabisa. Kwa ajili ya huo utume watapewa nguvu mpya, RohoMtakatifu. Yeye atawaongoza na kuwajaza, kama Yeye naye alivyojaliwa kuwanaye kwa utume wake (Yn.1:31ku; Mt.3:13ku).

k.23 Katika sura zilizotangulia tumeona kwamba Yesu alisema mengi kuhusuRoho na kazi zake. Utume wao unahusu Injili ya msamaha. Ni kipawa kwaKanisa Zima, si kwa watu kadha tu walio maofisa wa Kanisa. Injili inapotangazwawatu wapewe nafasi ya kutubu na kumwamini Kristo, kusamehewa dhambi nakuupata uzima wa milele. Ila Injili inapohubiriwa na watu wanaikataa, basiwanakataliwa uzima kwa kuwa wamekataa kutubu na kuamini; hivyo,wamefungiwa nje, ndio maana ya kufungiwa dhambi. Dhambi haina msamahanje ya Kristo na Kifo chake cha upatanisho. Kwa wale wanaoikataa Injiliimewabakia hukumu ya Mungu (3:19-21; 9:39). Ni wajibu wa Kanisa kuitangazaInjili ya msamaha na ni katika Injili kuhubiriwa mtu mmoja mmoja binafsihufunguliwa au kufungiwa dhambi zake. Jambo hilo halimo mikononi mwa watukadha nje ya kuhubiriwa kwa Injili.

Kwa mambo hayo Yesu aliwarudisha Mitume na wenzao katika familia yake, tenaaliwapa kazi ile ambayo tangu mwanzo alikusudia waifanye, ambayo, haponyuma, waliposhirikiana naye walijifunza kwake na kupata mazoezi.

k.24-29 Bwana Yesu alimtokea TomasoHatujui sababu ya Tomaso kutokuwapo pamoja na wenzake Yesu alipowatokeajioni ile siku ya kwanza ya juma. Tomaso ametajwa mara mbili katika Injili hiyo(11:16; 15:5). Alikuwa mzito wa kuamini maneno ya wenzake walipomwambia

Page 169: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA658

kwamba wamemwona Bwana Yesu, na ya kuwa amesema nao. Kamaangalikuwapo pamoja nao bila shaka angaliamini. Kwa tabia, Tomaso alikuwamsorajua, mzito, akiona mambo yote ni mabaya. Yesu alipokufa tumaini lake lotelilikwisha, wala hakudhani kwamba mambo ya baadaye yaweza kuwa memakama yale ya kwanza. Alimpenda Yesu sana, alikuwa mtiifu kwake, tayari kufapamoja naye (11:16). Kwa hiyo, itikio lake kwa ushuhuda wa wenzake lilikuwakujiwekea masharti ya kutimiziwa kwa kuamini kwake. La kwanza lilikuwakuziona kovu za misumari mikononi mwake na kutia kidole mahali pake...na la pilililikuwa kutia mkono katika ubavu wake. Yaani amwone uso kwa uso na kumgusakweli hata kiasi cha kutia kidole na mkono katika majeraha yake. Ilikuwa siku yakwanza ya juma, na juma moja limepita tangu wale wanafunzi wake kuwemochumbani na kumwona Yesu. Twaona kwamba Yesu hakufanya haraka kumpaTomaso nafasi ya kumwona na kumgusa. Wanafunzi walikuwa wakiwaogopaWayahudi, milango ilifungwa na Yesu akawatokea tena na kusimama katikati nakusema maneno yaleyale „amani iwe kwenu‟. Kisha akamwita Tomaso afanyekufuatana na masharti aliyojiwekea. Kumbe! Maajabu mawili yalifanyika kwaTomaso. Yesu yu hai kweli, yu mbele yake, karibu kabisa. Pia Yesu alikuwaameyasikia aliyosema kwa wenzake. Yesu, Mchungaji mwema, alijua kondoowake, alijinyenyekeza kabisa kwa Tomaso, alimwachia nafasi ya kutimizamasharti yake. „Tomaso, lete hapa...ulete na mkono wako...wala usiweasiyeamini, bali aaminiye‟. Ilitosha kabisa. Tomaso akaitika mara moja na kumkiri„Bwana wangu, na Mungu wangu!‟ Tomaso hakuwa na mashaka kiasialichojidhania, hakuhitaji kutimiziwa masharti yake. Yesu ni yule yulealiyemfahamu hapo nyuma, mpole, mnyenyekevu, wa upendo mwingi, mvumilivuwa kuchukuliana na udhaifu wake. Yesu aliyesulibiwa na Yesu aliyefufuliwa nimmoja. Tomaso alimwabudu kwa moyo mkuu, akawa wa kwanza kumkiri kuwaMungu. Tomaso alitambua kwa ndani kwamba katika ufufuo wake Yesuamefunuliwa kuwa sawa na Mungu. Hivyo alimpa Yesu heshima ile impasayoBaba (5:23). Yesu akapokea ibada hiyo bila wasiwasi wowote. Mwanzo kabisawa Injili Yesu alitangazwa kuwa na asili moja na Baba (1:1) na mwishoni mwenyedhambi amemkiri vivyo hivyo (1 Pet.1:18).

k.29 Kwa sehemu Yesu alimkemea Tomaso, katika 4:48 alihukumu tabia ya walewaliotaka ishara ili wamwamini. Hapo nyuma kwa kuishi na Yesu alikuwaamepewa kuona mambo ya kutosha kumsaidia ammwamini. Ndipo Yesualikumbuka wale wote ambao baadaye hawatamwona kwa sababu atarudi kwaBaba. Wao watakuwa heri, watabarikiwa. Imani yao ni imani safi, nao watajuakwa hakika kwamba Yesu yu hai kwa kushirikiana naye nafsini mwao. Si rahisikuamini, wengine kwa tabia, ni wazito, pia twaona Tomaso hakusaidiwaalipokosa kuwapo mara ya kwanza Yesu alipowatokea wanafunzi. Mara nyingineimani yetu hupoa kwa sababu hatujali ushirikiano wetu na waumini wenzetu,katika ibada, na mikutano ya faragha n.k. Matumaini yote ya Tomaso yalilazwachini Yesu aliposulibishwa, ila kwa kumwona Yesu alishinda mashaka yake naalikuwa mhubiri hodari wa Injili. Katika mapokeo ya historia

Page 170: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA659

inasemekana kwamba alikwenda Bara India na kuihubiri Injili na ya kuwa aliuawakwa ushuhuda wake.

k.30-31 Kusudi la Yohana katika kuandika Injili lilitimizwa katika ukiri wa Tomasowa Yesu kuwa Mungu wake na Bwana wake. Ishara hiyo ya mwisho ya ufufuoilitimiza lengo la ishara zote alizozifanya Yesu, zilizotajwa katika Injili hiyo,pamoja na zile zote zingine, nyingi, zisizotajwa humo. Yohana alizichagua hizo iliwatu wapate kumwamini Yesu kuwa Mwana wa Mungu na kwa kumwamini wawena uzima wa milele. Tangu mwanzo alipambanua wale wa kuamini na wale wakutokuamini. Upeo wa kutokuamini ulifikiwa na wale waliosababisha kifo chaYesu na upeo wa kumwamini ulifikiwa na Tomaso na wenzake. Mambo hayoyalitokea kweli, hayakuwa hadithi tu (2 Pet.1:8-9,16), hivyo iliyo mbele yetu nikuyaamini au kutokuyaamini, ila hatuna haki ya kukataa eti! hayakutokea. Mpakaleo twaweza kukutana na Yesu aliye hai nafsini mwetu na kujua uheri wakumwamini. Twaitwa na maneno hayo ya Yohana kumwamini Kristo, imani yetuinakuja kwa kusikia neno la Injili (Rum.10:17).

MASWALI1. Kwa nini Petro na Yohana waliamini kwamba Yesu amefufuka bila

kumwona Mwenyewe?2. Yesu alionekana kuwa Mchungaji Mwema kwa jinsi alivyomtokea Mariamu

Magdalene. Kwa njia zipi alionekana hivyo?3. Katika habari hizo zote uwezo mkuu wa Yesu ulitawaliwa na nini? Kwa

nini Yesu hakutokea wakuu na wapinzani wake waliosababisha kifochake? Kwa nini hakuwastusha na kuwaogofya?

4. Alipokutana na Mitume Yesu aliwaelekeza kwenye jambo gani?5. Eleza hali zote za Tomaso katika mwenendo wake wa kutokuwaamini

wenzake juu ya kumwona Yesu mpaka alipokutana na Yesu Mwenyewe6. Sisi wa leo twawezaje kujua kwamba Yesu yu hai?

21:1-23 Mambo ya mwisho kuhusu Utume wa wanafunziBaadhi ya wataalamu wameona sura hii kuwa kama kiambatanisho kwa sababumwishoni mwa sura 20 ilionekana Yohana ameifunga Injili yake (20:30-31). Kwahiyo wafikiri kwamba sura hii iliandikwa baadaye, ama na yeye, au na mwingine.Ila jambo kubwa ni kwamba hakuna nakala yoyote ya Injili isiyo na sura hiyo.

Sura hii ina mambo ya maana sana. Utume wa wanafunzi kuwa wavuvi wa watuumesisitizwa. Yesu aliwafundisha siri za mafanikio ya utume wao wa kuleta watukwenye kumwamini. Petro alirudishwa rasmi kazini na Yesu na kupewa jukumula kuwachunga na kuwalisha kondoo wa Bwana. Uhusiano kati ya Petro naYohana ulifafanuliwa. Pamoja na hayo yawezekana Yohana alitaka kurekebishamawazo ya watu waliofikiri kwamba „mwanafunzi mpendwa‟ (Mtume Yohana)atakuwa hai mpaka Bwana atakaporudi, huku muda

Page 171: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA660

unaendelea na inaonekana atakufa kabla hajaja Bwana. Yafikiriwa kwambawakati wa Injili kuandikwa Petro alikuwa ameishakufa na Yohana alikuwaamezeeka. Hivyo, sura hii inafaa sana kuwa sura ya hitimisho. Badala ya Injilikumalizika na Yesu hai akikutana na wanafunzi wake inakamilika na habari yaYesu kuwaongoza katika uvuvi, ishara ya kazi watakayofanya hivi karibuni, kaziya kuvua watu. Wataifanya chini ya mamlaka yake na katika ushirika wa Yeyekuwa pamoja nao kiroho. Kwa hiyo sura hii ni kama daraja kati ya Yesukujidhihirisha kwa wanafunzi kuwa amefufuka na Yesu kuwaandaa kwa mamboyaliyo mbele yao.

Ni vigumu kwetu sisi kujiweka mahali pao kwa sababu tunajua habari za matukiohayo, lakini kwao ilikuwa vigumu kutambua mara moja maana ya tukio hilo kubwala ajabu la Yesu kufufuka kutoka kwa wafu. Walikuwa wamepita katika magumumengi ya kuwapima yaliyowachanganya. Yesu alikuwa amewapa mafundishomengi kuliko walivyoweza kuyapokea. Matumaini yao ya Yesu kuusimamiaufalme wake hapo duniani yalibomolewa kabisa. Katika siku chache hali yaoilibadilika kutoka kuwa wanafunzi wa mwalimu mheshimiwa aliyependwa nawengi kuwa watu waliowindwa kwa sababu ya kumfuata aliyehukumiwa kuwamkosaji, mdanganyifu na mwongo. Walikuwa wamemsindikiza Yesu kwashangwe mpaka Yerusalemu, ndipo baada ya siku chache walifika pande za chinisana Yesu aliposulibiwa, kisha baada ya siku tatu mioyo yao ilifurahi tena, Yesualifufuka na kuwatokea. Sasa, nini? Basi, wakaondoka Yerusalemu, mahalipageni kwao, mahali pa adui za Bwana wao, wakaenda Galilaya, mahali pamazoea yao, wakarudi kwa kazi waliyozoea hapo nyuma, kwa vyombo, nyavu,na samaki.

k.1-2 Bahari ya Tiberia ni jina lingine kwa Bahari ya Galilaya. Wametajwawanafunzi saba, watano kwa majina na wawili bila kutaja majina. Tomasoalikuwa miongoni mwao.

Katika Injili zingine twaona kwamba Yesu aliwaagiza waende Galilaya (Mt.28:7;Mk.16:7). Ila kwa nini walienda kuvua samaki? Jambo hilo laweza kuelezwa kuwawameweka kando wito wao. Ila pengine ni kwa sababu walikuwa kama hewani,ni afadhali wafanye kazi badala ya kukaa tu, au, walihitaji riziki. Kwa hiyo, si vemakuwalaamu. Hawakwenda Galilaya ili wavue samaki, bali ilitokea hivi, mpakawaagizwe kuanza kazi. Mpaka hapo Roho Mtakatifu hajawashukia kwa hiyohawakusikia msukumo wa kwenda kuhubiri ijapokuwa walijua kwa hakikakwamba Yesu amefufuka. Petro alikuwa bado hajarudishwa rasmi mbele yawenzake baada ya kumkana Yesu.

k.3 Petro aonekana kama kiongozi wao, akawaambia „Naenda kuvua samaki‟nao wakajiunga naye. Wakaenda kuvua samaki, ila usiku ule walikosa kupatakitu, na asubuhi iliwakuta hali wamechoka, walijisikia kushindwa, njaa iliwauma,nao hawakuwa na chochote cha kuonyesha kwa juhudi yao. Huendawalikumbuka wakati wa zamani ilipotokea vivyo hivyo (Lk.5:1)

Page 172: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA661

k.4b-8 Ila walipotazama walimwona mtu wasiyemtambua amesimama ufuoni. NiYesu, hatuambiwi alifikaje, wala hatujui kwa nini hawakumtambua mara. Yesuakawauliza „Wanangu, mna kitoweo?‟ na kwa ufupi sana wakamjibu „La!‟. NdipoYesu akawaagiza walitupe jarife upande wa kuume wa chombo, nao watapata.Kuvua samaki saa za mchana kulikuwa kinyume cha kanuni ya uvuvi. Ni vigumukujua kwa nini walikubali shauri la huyo mgeni, maana mpaka hapo hawakujuani Yesu. Si rahisi kwa mabingwa wa kazi fulani kupokea mashauri kutoka kwawageni. Ila kwa sababu walikuwa wameshindwa wakawa tayari kujaribu njiayoyote mradi wafaulu kupata samaki. Utii wao ulifanikiwa, wakapata samakiwengi mno. Hatuna haja ya kuwaza kama iko maana fulani kwa jarife kutupwaupande wa kuume, Yesu alijua samaki wengi walikuwapo upande ule, ndiosababu alisema hivi. Ndipo Yohana alipoona wingi wa samaki na jarifehalikukatika kwa uzito wake alitambua maana yake na ya kwamba ni Yesuambaye amesimama ufuoni na kusema nao (twakumbuka ni Yohanaaliyetambua maana ya vitambaa na jinsi vilivyolala kaburini). Yesu alijifunuakwao na kuonyesha uwezo wake wakiwa Galilaya, mahali pa mazoea yao nakatika kazi waliyozoea. Kila jambo lilithibitisha kwamba ni Yesu ambaye kwauwezo ameingia katika maisha yao ya kawaida. Petro alifanya kulingana na tabiayake ya kuwa mwepesi wa kutenda, tofauti na Yohana aliyekuwa mwepesi wakutambua (20:3ku).

Walijifunza nini kutokana na habari hiyo? Walijifunza kuwa itawapasa kufanyakazi ya „kuvua watu‟ chini ya uongozi wake na kwa mamlaka yake (15:5b).

k.9-14 Yesu aliwaalika waje karibu na kushirikiana naye katika mlo. Alikuwaamewaandalia chakula na pamoja na kile alichopika aliwaomba walete baadhi yasamaki waliovua, huku Petro alikuwa akishughulikia jarife na kulivuta mpakapwani. Walishangazwa na wingi wa samaki waliokamatwa na ya kwamba jarifehalikupasuka kwa uzito wake. Yohana alipenda kutaja mambo madogo kamaumbali na hesabu ya samaki. Hatuna haja ya kutafuta maana ya hesabu hiyo ya153, iliashiria wingi wa samaki waliovua, mafanikio katika kumtii Yesu.Yawezekana walihesabu ili wawagawe kati yao. Uvuvi ni mfano mzuri wa utumewao na kazi watakayofanya mbeleni. Pengine walikuwa karibu na mahali ambapobaadhi yao walikuwapo walipoitwa kwa mara ya kwanza (Mk.1:16-17; Lk.5:1-11).Walijifunza kwamba Yesu atawatangulia na kuwajalia kupata mahitaji yao. Wotewalijua ni Yesu ila hakuna aliyethubutu kumwuliza. Ilichukua muda kuzoea halihiyo mpya. Yohana alitaja kwamba ilikuwa mara ya tatu kwa Yesu kuwatokeakundi la wanafunzi wake baada ya Kufufuka kwake. Ni mara tatu katika Injili hiyo,na kwa wanafunzi wake, ila Yohana hakuingiza katika mara hizo Yesu kutokeakwa Mariamu Magdalene wala habari za jinsi alivyowatokea wengine, habari hizoni katika Injili zingine.

k.15-25 Yesu, Petro, na YohanaYesu alikuwa amemtokea Petro peke yake siku ile alipofufuka (Mk.16:7;Lk.24:34; 1 Kor.15:5). Petro alisikia aibu na huzuni kwa jinsi alivyomkana

Page 173: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA662

Bwana wake na Yesu alimwona mchana ule wa siku ya kufufuka kwake, na kwasiri alimsamehe na kumrudisha kwenye ushirika wake. Ila haikutosha Yesuamsamehe ilimpasa amrudishe rasmi hadharani mwa wanafunzi wenzake. Haponyuma alikuwa amejiweka mbele ya wenzake kama yule atakayekuwamwaminifu kuliko wao (13:8; 37-38; 18:17ku). Jambo hilo lilihitaji matengenezokwa upande wa Yesu na kwa upande wa wanafunzi. Mpaka litakapotengenezwaPetro hataweza kuutimiza utume wake. Msamaha na kurudishwa wazi kulifunguamlango kwa yeye kushika mahali pake kama kiongozi wao tena. Yesu si pekeyake, anaye „bibi arusi‟ (Kanisa lake) mtu hawezi kumpenda Yesu bilakuwapenda walio wake pia, wala mtu hawezi kutumika bila kujihusisha vema nawenzake. Mwanzoni Kanisa lilikuwa kama mmea dhaifu, watu wachache tu, bilaraslimali yoyote ila Roho Mtakatifu, kwa hiyo, lazima washikamane wao kwa wao,bila kunyosheana vidole kwa makosa ya hapo nyuma. Umoja wao ni nenomuhimu kama Yesu alivyoomba (17:21).

Petro alionyesha nia ya kumwona Yesu kwa kufanya haraka ya kutoka chombonina kumwendea. Lakini budi Petro akiri wazi upendo wake. Hivyo Yesu alimwulizaswali la kumchunguza na kumpa nafasi ya kusema wazi. Yesu alitumia jina lakela asili si lile alilompa (1:42) (bado hajawa mwamba). Alimwuliza „wewewanipenda kuliko hawa?‟ Yesu alitumia neno kwa „penda‟ lililotumika katikaYn.3:16 „kwa jinsi hii Mungu aliupenda.‟ Ni nini maana ya maneno „kuliko hawa‟Je! hawa ni wanafunzi wenzake? au Je! ni samaki? au Je! unanipenda kuliko haowanafunzi wanavyonipenda? Ni vigumu kujua, labda Yesu alimchunguza kuonakwamba kama bado angali anajifikiria kwamba anampenda kuliko wenzake.Kama ni wenzake, haina maana kwamba Yesu anamtaka yeye azidi wenzakekatika kumpenda, maana ataka wote wampenda mia kwa mia, ila alikuwaamejivuna kwamba „hata wote wakikuacha mimi siyo‟. Kama ina maana yasamaki ni kama kumwuliza utayari wake wa kuvunja kabisa uhusiano wake namaisha yaliyotangulia na kazi ya kuvua samaki. Petro alipojibu akatumia nenolingine kwa penda, neno la kuhusu kupenda rafiki. Ni kama ameachakujitegemea, na kujivuna, alijua yeye mwenyewe yu dhaifu na alitegemea ujuziwa Bwana juu yake. Ndipo Yesu akampa kazi ya maana sana, kazi ya kulishawana-kondoo wake, akamthibitishia wito wake. Ni vema tuone kwamba Yesuhakusema „uwe mchungaji/pasta, kama anampa cheo, bali akampa „kazi‟ yauchungaji (ling. 1 Tim.3:1: mtu akitaka kazi ya askofu si cheo).

Halafu kwa mara ya pili Yesu akamwuliza tena swali lile lile na Petro akamjibukwamba „Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda‟ akilitumia neno lilelile la „penda‟kama alivyolitumia kwa jibu lake la kwanza. Yesu akampa kazi ya kuchungakondoo zake.

Halafu kwa mara ya tatu Yesu akamwuliza tena swali lile lile ila alilitumia nenoambalo Petro alikuwa amelitumia kwa „penda‟. Hapo Petro alihuzunika. Kwa ninialihuzunika? Pengine kwa sababu Yesu alirudia kumwuliza kwa mara ya

Page 174: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA663

tatu, au pengine kwa sababu Yesu alibadili lile neno „penda‟ na kulitumia lilealilolitumia Petro, kama alikuwa na wasiwasi juu ya ukweli wake. Yesu akampakazi namna ileile, ya kulisha kondoo zake. Petro alikuwa amemkana Yesu maratatu, na Yesu alimpa nafasi ya kutengeneza kwa kumwuliza mara tatu kukiriupendo wake. Alitaka kumfahamisha yeye na wenzake kwamba msingi wautumishi ni upendo, wawe wanamtumikia hasa kwa sababu ya kumpenda. Kwahiyo Yesu hakuwakemea kwa kurudia kazi ya uvuvi ila kazi hii haitakuwashughuli yao maalumu tangu hapo. Waanze kufanya kazi ya kulisha na kutunzakondoo zake wa hali zote, wadogo kwa wakubwa, wakifuata kielelezo chake chaMchungaji Mwema (10:11ku. 1 Pet.5:2-4). Hivyo, Petro alirudishwa rasmi,hadharani mwa wenzake, kama kiongozi wao (Mt.16:13-20).

k.18-23 Yesu alitabiri mambo ya mbele kuhusu Petro na Yohana. Alitabirikwamba atakapokuwa mzee Petro atatendewa asivyotaka, atauawa kwa kifokitakachomtukuza Mungu. Katika historia upo ushuhuda wa Paulo na Petrokuuawa huko Rumi, Petro kwa kusulibiwa. Ila kwa wakati huo ilimpasa Petroamfuate Yesu. Kwa hiyo Petro aliishi na kutumika maisha yake yote, kama miakathelathini hivi, hali akijua unabii huo utatimizwa baadaye. Hivyo, kumfuata Yesukutamgharimia maisha yake, sawa na Yesu alivyowaambia mara kwa mara haponyuma. Wakati wa kuandika Injili yake watu walifahamu habari hizo kuhusuPetro, maana alikuwa ameishauawa, ila hawakujua mwisho wa Yohana utakuwanini.

k.20 Kwa kifungu hicho twapata kujua kwamba „mwanafunzi mpendwa‟ niYohana. Alikuwa mtu kweli, si kama wengine wanavyodhani kwamba lugha hiyoilitumika kama mfano wa kumwelezea mwanafunzi bora. Kwa sababu Petroalipomwona Yohana anafuata alimwuliza Bwana Yesu juu yake. Kwa vilealivyoambiwa habari zake mwenyewe alitaka kujua habari za mwenzake, kamatabia yetu ya kibinadamu ilivyo. Yesu akamjibu kwa maneno ya mkato „Ikiwanataka huyu akae hata nijapo, imekupasaje wewe?‟ „Wewe unifuate mimi‟. Petroalikuwa na wajibu wake haidhuru itampata nini Yohana mwenzake. Wajibu wakumfuata. Ila kwa maneno hayo watu walifikiri kwamba huyo Yohana hatakufa,waliyatafsiri kinyume cha alivyosema Yesu na uvumi ulienea kwamba Yohanaatadumu kuwa hai hata ajapo Yesu tena, hasa kwa sababu Yohana aliendeleakuishi baada ya Mitume wote wengine kuwa wamefariki dunia. Ila sivyoalivyosema Yesu, wala sivyo alivyoelewa Yohana. Kila mmoja alipewa wajibuwake, na kila mmoja alipaswa autimize, aliopewa mwenzake haukumhusu yeye,asijilinganishe na mwingine. Katika kalendari ya Mungu jambo moja kubwalimebaki nalo ni Kurudi kwa Bwana Yesu. Mwanzoni Wakristo walitazamiakwamba Yesu atarudi mapema, na maadamu Yohana yu hai tumaini lingaliko ilabila shaka wengine walianza kuwa na mashaka walipoona hata Petroameishauawa na Yohana amezeeka na iliwabidi wayarekebishe mawazo yao (1The.4:13ku). Walipewa changamoto ya kuitafsiri imani yao katika maisha nautendaji wa kila siku. Zipo tofauti za huduma; zipo tofauti za kazi; kila mmojaapaswa atimize ya kwake, ndipo atapata thawabu

Page 175: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Yohana - African Pastors Fellowship · 2017-01-10 · mmoja wa wafuasi wake aliyeandika chini ya uongozi wake. Wanafikiri huyo pia aliitwa Yohana. (b) Walioandikiwa

YOHANA664

yake. Katika Waraka kwa Korintho twaona hali ya waumini kugawanyikakufuatana na watumishi mbalimbali, na Yohana hakutaka watu waseme „mimi niwa Petro‟ au „mimi ni wa Yohana‟ n.k. (1 Kor.1:10ku).

21:24-25 Yohana afunga Injili yakeYohana alitia sahihi yake kwenye yote aliyoandika katika Injili hiyo nakuuthibitisha ukweli wake. Mwenyewe alikuwa shahidi aliyeyaona na kuyasikiahayo. Ila yaliyoandikwa yalikuwa baadhi tu ya mengi aliyofanya Yesu, ila hayomachache aliyoyachagua yalitosha kwa watu kumwamini Yesu kuwa Kristo,Mwana na Mungu, na kwa kumwamini wawe na uzima wa milele.

MASWALI1. Wanafunzi waliokwenda kuvua samaki walijifunza neno gani muhimu

kufuatana na jinsi mambo yalivyokwenda siku ile?2. Hayo waliyojifunza yalilenga nini?3. Msingi wa kumtumikia Kristo ni upendo. Tumepataje kufikiri kwamba

upendo ndio msingi wa utumishi kutokana na habari za mazungumzo katiya Yesu na Petro?

4. Yesu alisema mwisho wa Petro utakuwa nini? na mwisho wa Yohanautakuwa nini? Twajifunza nini kuhusu kujilinganisha na mwingine katikakumtumikia Kristo?

5. Mwisho wa sura 20 mwandishi Yohana alieleza wazi shabaha ya kuandikaInjili yake na mwisho wa sura 21 alithibitisha ukweli wa yale aliyoandika.

6. Eleza shabaha yake na thibitisho la ukweli wa Injili hiyo?

MASWALI JUU YA INJILI NZIMA

1. Umejifunza mambo makubwa gani kumuhusu Yesu Kristo?2. Andika insha juu ya jinsi Injili hiyo imekuwa msaada kwako